Missile of the Nation
JF-Expert Member
- May 24, 2018
- 13,602
- 51,500
Misri katika ule mtaa mkuu kutoka uwanja wa ndege kuna msikiti upo karibu kabisa na kanisa na hali imekuwa hivyo miaka na miaka.
Mada yako imekosa mizania inayotokana na tafiti za kiulimwengu.
Msikiti kuwa karibu na kanisa siyo tatizo hata kidogo, ipo misikiti mingi tu duniani imejengwa na inapakana na makanisa
Tatizo ni Rais wa nchi, tena wa imani nyingine, kwenda katika nyumba yake ya ibada na kisha kutaka sadaka za waumini wenzie kanisani zikajenge msikiti.
Kama waislamu wenyewe wangemuomba aendeshe harambee ya kuchangia ujenzi wa msikiti wangeweza kumualika msikitini au kwenye uwanja wa wazi akapewa muongozo na waislamu wa namna ya kuendesha zoezi hilo!
La sivyo alivyofanya Magufuli ni kujivisha jambo ambalo si la dini yake kwa malengo yake binafsi (naamini ni ya kisiasa)