Rais Magufuli ataja sababu kusitisha ujenzi bandari ya Bagamoyo kwa Mkopo wa Dola Bilioni 10

Viongozi wa hii nchi hivi hawaoni umuhim au ni ushenzi tuu kula like umemaliza uzi
 
Kwanini isijengwe mtwara
 
Mimi ndio maana mbunge yeyote wa CCM namchukia nakumuombea laana kwanin hawazungumzi na wapi kwa niaba ya wananchi? Kwann wasipiganie Mali zetu na rasilimali ewe mbunge utae ona hii post usiposimamia majukumu yako ipasavyo na ulaaniwe.. nakizazi chako ndio kiteseke kwa upuuzi wako
 
Mkuu, ndiyo maana nimesema awali kuwa sisi tuwepesi sana kusahau na tunazowea maumivu kirahisi sana. Wengine tunapojaribu to raise alarm kuhusu michezo inayoendelea tunaambiwa ni MATAGA na SUKUMA GAN.
Imefika mahala tunaokosoa huu ufedhuli unaofanyika tunaambiwa tuna wivu kwa kuwa tulinufaika na utawala uliopita though sisi wengine tulikuwa tunaukosoa hata huo utawala wanaotunasibisha nao.
Ndiyo maana nimesema ngoja tusubiri tuone jinsi meli inavyotuzamisha pamoja.
Lakini as we will be sinking down tutakuwa tunakumbushana kuhusu hii collective foolishness of the majority
 
Ume usoma mkataba? Mara nyingi kama huna taarifa za kutosha hakuna haja ya kupinga kitu

1.Mkuu wewe Umeusoma?
2.Unajua Nikupe mfano mdogo tuu,Kampuni hata kwenye mambo ya Tenda kama Kampuni inayoomba tenda ina Historia Mbaya,Hata Kama Ina uwezo wa Kushinda tenda Inapigwa chini!(Ethics) sasa Binafsi Nimefanya Kazi kwa Waarabu,Wahindi,Wazungu na Wachina!
Aiseee Wachina duuu acha tuuu sema Umaskininwetu na Kuhitaji hela na Sio UTU!
MUNGU atusaidie...Mi Nimeanza Kupiga Goti tuu sio tuu Kuomba Mvua,Hapana Pamoja na Mambo mengine ya Nchi kama hilo la Uwekezaji ili Maingilie kati afanye Kama Itakavyompendeza Mna Sio Mimi!
Sio Busara Kupinga Kitu Usichokijua Nakubaliana na wewe 100%!
Ndio Maana Mimi sijapinga Mkuu Ila Nimeeleza Upande wa pili Kaka!
 

Ni Muhimu kweli!
Sasa nasema Kwa mfano tuu akaoewa Mchina wewe una Mawazo gani?
Regardless Hujui Kilichomo kwenye Mkataba
Mi nakuuliza tuu kama Kapewa Mchina una Mawazo gani kuhusu Kupewa mchina Hilo tuuu hayo mengine mi sijui!
 

China unayoisema iliwapa Waingereza miaka 200 kumiliki Hong Kong na ndio ikawa insipiration ya China unayoiona leo. Dubai Bandari yao kubwa ya Kwanza waliwapa wamarekani wajenge na waendeshe kwa miaka 50, leo hii wanashirika linaitwa Dubai Port World na sasa linaendesha Bandari Mbalimbali duniani ikiwemo Marekani mara baada ya kupata uzoefu mkubwa kwa Wamarekani. Ukiwa na mawazo ya kuibiwa kila siku utashindwa hata kufungua genge. Master plan ya Bandari tuandae sisi, wachina watoe hela kulalamike tuanze sisi. Maajabu sana!!
 
Cha msingi mambo yawe hadharani kwa wabunge na sisi raia.

Tuambiwe kwa lugha rahisi wachina watapata ABC.

Tuambiwe sisi tutapata XYZ.

Na kwamba hiyo ndio njia iliyo bora na sababu zake.

Na kwamba kitu gani hatupaswi kukiuka na madhara yake.

Maana tumeshasikia kilichowapata Zambia.

Kurudia ya Chifu Mangungo ni fedheha kubwa.

Wabunge mpo?
 
cc Chige a.k.a .........
Point niliyoiona mimi, kwa kuzingatia mada zangu ni pale aliposema kulipa mabilion ya pesa kwamba Wachina wanataka kujenga viwanda Kigamboni, lakini hapo hapo akazungumzia suala la kujenga Bandari Kigamboni...

Now tell me: NI Wachina gani walitaka kujenga Bandari Kigamboni?!

Au tuseme alikusudia kusema Bagamoyo, na hivyo viwanda of course, ilikuwa ni huko huko Bagamoyo kwenye Bagamoyo Special Economic Zone!!

Kwa mfuatiliaji anafahamu Bagamoyo Special Econmic Zone iliyokuwa inatarajiwa kujengwa viwanda, ni mradi uliokuwa uende pamoja na Ujenzi wa Bandari!! Sasa alitarajia aone viwanda gani wakati Mradi wa Bandari ulipigwa stop?!

On top of that, JPM anasema Wajenzi walitoa masharti ya kipumbavu kwamba:-

Huyo ndo JPM mmoja, but another version of JPM is here:-


Hivi yule aliyesema ni "ni mambo ya kipumbavu kabisa yamefanyika ndo huyo huyo hapo juu, au ni watu wawili tofauti?

Lakini kwa upande mwingine nao, Deusdedit Kakoko, aliyekuwa Mkurugenzi wa Bandari nae anasema kuanzia dakika ya 4 kwamba:-

Sasa nijuze wewe! Kumbe Bandari ya Bagamoyo ilikuwa iwe export port na sio competitor wa bandari zilizopo, na ndo maana hapo hapo palitakiwa kujengwa viwanda!!

Sasa how come tena unatoa masharti ya kutojenga bandari ingine ambazo zisingekuwa competitor?!

Na msikilize hata huyo Kakoko mwenyewe alivyo mwongo! Eti kule Sri Lanka hadi ikatokea vita! Na wengi wamekuwa wakihusisha Bandari ya Hambantonta (ya Sri Lanka) na umafia wa Wachina!!

Sasa ni lini Sri Lanka ilitokea vita inayohusishwa na hiyo bandari?!

Kila anayefuatilia mambo anafahamu vita ambavyo vilidumu Sri Lanka ni vile kati ya Serikali na Tamil Tiger!! Kama nawe ni mfuatiliaji... hivyo vita vilipiganwa lini hadi lini na Bandari ya Hambantonta ilijengwa lini?!

Na miongoni mwa propaganda ambazo zilisambazwa sana Tanzania na wale wale mliokuwa mnawashingilia, ni suala la Wachina kuichukua hiyo Bandari ya Sri Lanka ili kujilipa deni lao! Watu tukasema hapa hizo ni habari za uongo zilizoanzishwa na Trump Administration ili ku-discredit Belt & Road Initiative!!

Mkasema tumenunuliwa!

Hata Wamarekani nao waliingizwa chaka na propaganda za Trump Administration hadi pale Wasomi wa Harvard na John Hopkins University walivyoanza kutilia wasiwasi habari hizo! Ili kupata ukweli wa kile wanachoambiwa na serikali yao, wakaamua kupeleka watu field kufanya research ili kufahamu ukweli!

Abstract ya research husika inasema:-


Hivi mlikuwa mnaambiwaje vile kuhusu Wachina na Bandari ya Sri Lanka?!
 
Tatizo nikuweka mkataba wazi watu wajue nakama jpm nimuhongo mbona wazungu walimpiga sana vita mpaka akakata motoo
 
🤣🤣 🤣 🤣 🤣 🤣 🤣 🤣 🤣 Zitto alikuwa anasema jamani tukikataa tutakuwa tumepoteza bahati kubwa na wanakwenda kujenga sehemu nyingine. Mimi nilidhani walishakwenda huko kwingine zamani lakini kila nikisikia bado wanapambana kwa nguvu zote ili ''watusaidie'' ndipo nabaki hoi.
 
Hoja hujibiwa kwa hoja!

He unaona masharti hayo kwa dunia ya Sasa Yana umaana wowote wa kunufaisha hili taifa saiz Kama dunia kijiji.

Kwa miaka 99 tusikusanye chochote hao wenzetu walipewa 50yrs kutokana na maelezo yako but kulikuwa na condition za kubadilika hayo maandiko nasio hili la Tanzania hata iweje haiwezekani kubadilika hvyo ukuaji wa teknolojia, mawasiliano in next 10yrs unafikiri tutadhindwa sisi wenyewe kuanzia?

Kama sisi wenyewe hatunufaiki kwa lolote bado gharama za kulipa huo mradi xipo pale pale na faida juu, Nani anaumia kwenye huu mradi Kama sio Mimi, mwanangu, mjukuu wangu na kitukuu changu na wakimaliza sio wanakuwa mbele ndo wanarudi pale walipoishia 2021 wakati huo n 2120.

Je una akili wewe?
 
Bagamoyo ikijengwa bandari ya dar ndo itakuwa By By iwe kwa lazima au kwa hilari
 
Mkuu, unazungumzia miaka 200 na miaka 50 kwa Hong Kong na Dubai mtawalia. Je, unaweza kutueleza covenants/ terms ambazo zilikuwemo kwenye mikataba ya uwekezaji huko Hong Kong na Dubai?
 
Ndo unavyojidanganya kwamba wanapambana, sio?!

Hivi una habari pamoja na porooooooojo zote wanazopiga mbele ya kamera lakini behind the curtain wanaendelea na mazungumzo?!

Yaani sawa sawa na wanavyopiga porojo mbele ya kamera kuhusu gesi ili waonekane ni wapambania maslahi kumbe behind the curtain wanaendelea na maandalizi!

Ambacho kilitokea ni kitu kimoja:

Gesi na Bandari vilikuwa priority kwa JK but not to JPM!

Lakini kutokuwa priority sio kwamba eti walikuwa hawaendelei na mazungumzo!

That's one but two, kama unadhani wanashindwa kujenga hizo sehemu zingine kwa sababu wanabembeleza Bagamoyo, look here:-

Je, baada ya hapo Mchina ametulia kuisubiria your "Blessed Tanzanian Land" kama unavyojidanganya?! Jibu wanalo The Diplomat kwamba:-

Na hiyo bandari Mmarekani na Mfaransa waliipinga kweli kweli huku wakitumia Western Media kusambaza propaganda zao! Hapa ndipo walipoanza kusambaza propaganda kwa njia ya kutisha kwamba Mchina anataka kutumia bandari za Afrika kwa masuala ya kijeshi!

Wakaanza kuwaasa Wazalendo wa Kiafrika aina yenu kwamba wawe makini na mpango huo wa Wachina kwa sababu itakuwa ni hatari sana kiusalama kwenye nchi zao!!

Mkameza hizo propaganda na kuzihamishia Bagamoyo!

And YES. Mchina akaweka military base pale Djibout!!

But the question is: Ni kweli concern ya US na France ni usalama wetu or something else? Jibu wanalo The New York Times:-


Yaani Mchina alivyo fala, akaenda kujenga military base pua na mdomo na ilipo US Military Base!! Na kwavile US wanajiona ni yeye na Wazungu wenzao wa West ndio wenye haki ya kujenga military bases thousands of miles from their own lands, basi wakiona mwingine anataka kufanya kama anavyofanya yeye kwa miongo kadhaa sasa... nongwa ndo inaanza!

Again, endelea kujidanganya kwamba you're BLESSED LAND na watu hawana alternatives!! Media ya Kibeberu, tena ya Serikali, yaani Deutsche Welle, wanakujuza Mr. Blessed Land, who'll always people beg to you kwamba:-


So, you're NOT that special! U-special wako ni kwavile tu upo kwenye strategic position!!!

Ikiwa China ameamua kujenga reli kutoka China hadi Pakistan ili kupunguza utegemezi wa Mfereji wa Malaca ambao USA wana ushawishi wao pale (Singapore), hivi unaamini kabisa atashindwa kuiunganisha Bandari ya Djibouti kwa reli kutoka Ethiopia (ambayo Mchina kajenga) hadi Kenya kisha kuja kutokeza Central Corridor na hatimae mizigo ya East and Central Africa ikawa inashushwa Djibouti Port na kusafirishwa kwa the said possible railway route?

the University of Berkeley kwamba:-

Endeleeni kupiga porojo huku ukijikita kwenye kutaja watu kila wakati... mara Zitto, mara January! Like you've more of personal stuff kuliko issues zenyewe!

Hivi ni mara ngapi umemtaja Zitto na Makamba kila tunapokutana kwenye hii mijadala?

Man, jadili mada badala ya watu, especially kama watu wenyewe hawapo kwenye nafasi ya kufanya maamuzi!! Bandari au Gas Projects vikijengwa, au Bwawa la Nyerere likipigwa chini, KATU "adui" yako hatakuwa Zitto wala January Makamba kwa sababu wote hao hawana uwezo wa kufanya jambo ambalo Rais wa nchi HATAKI!!!

Binafsi huwa namtaja sana JPM kwa sababu yeye ndo alikuwa Alpha na Omega!! He was at the center of everything... alichotaka kilifanyika, na ambacho hakutaka hakikufanyika!!

Na huyo ndo Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania... AMEPEWA MAGUVU YOTE!!!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…