Rais Magufuli afuta safari ya UN General Assembly

Rais Magufuli afuta safari ya UN General Assembly

Hana wasaidizi? Mwisho watatusahau na waache kutualika matokeo yake mtu ukienda ulaya wazungu wanakuuliza umetokea Nigeria au South Africa? Maana tz hawaijui

Mkuu hapo logic ni hipi, unataka kusema Wazungu hawana somo la Jografia mashuleni mwao?
 
Pamoja na hilo la Wakimbizi na Wahamiaji, pia kutakuwa na kikao muhimu sana ambacho kitachukua takribani 70% ya mkutano wote kutokana na umuhimu wake. Huu ni mdahalo unaolenga kuzungumzia malengo ya maendeleo endelevu na nafasi yetu katika kusukuma mabadiliko ya kufikia malengo hayo.

Ebo yaani 70% ya mkutano wote ni mdahalo!!! (debate) !!!! Tunarudi kule kule sekondary kwenye debates (midahalo)!!! Yaani Raisi mzima aende safari yote na gharama zote aende kuhudhuria mdahalo (debate)???
Hata watu wazima UN huwa wanafanya midahalo (debates) nilifikiri vitu hivyo ni kwa ajili ya watoto wa sekondari tu.Hata maraisi MWEEEE!!! Hivi Raisi anaweza shuka uwanja wa ndege wa nchi yake bila aibu akasema nilikuwa umoja wa mataifa kwenye mdahalo!!!! LOOOOO.Magufuli heri haendi yuko sahihi.
 
Sasa huo usalama wa taifa hawataki watu watoe mawazo yao?

Utawala wa leo hautaki mawazo hata kidogo. Kama uko nje unaweza saidia toa mawazo huku tutangolewa kucha na kulazwa kuwa ni majambazi ka ya Zombe na Bageni
 
Tuzoeee tu..mpaka 2020.... Kuna nini huko UN si kuongea tu na kurudi home. Bora hizo pesa za safari ajenge skuli bukoba
hizo pesa za safari kile ki gulf stream kinajazwa wese halafu yule maza anaenda na kurudi!!!!! hamna matumizi yaliyobanwa hapo!!!! jason bourne aliwahi kusema hapa ili ndege ya rais iende irudi kadirio la chini la mafuta ni milioni 250 mpaka milioni 300 maximum!!! sasa hapo angeenda baba mwenye nyumba angepungukiwa nini?
 
Huo mkutano una faida gani kwa Tanzania ? UNAIINGIZIA nchi pato la shilingi ngapi mwisho wa mkutano?
Toka nje ya box la ujinga. Hiyo mikopo mnayochukua kila siku kutoka IMF na World Bank unadhani inadondoka hewani? Ngoja wavute handbrakes kidogo ndo utaelewa kilichomtoa kanga manyoya.
 
Mnamlaumu bure Mzee wetu , ana haki ya kutenda Kile anachoona yeye kina manufaa kwake na kwa Taifa lakini cha ajabu sana mmeshindwa kung'amua kuwa kuna key people ambao wametufikisha hapa. Hao ndo wanastahili lawama zote, msimuonee mzee wetu, wang'amueni hao kwanza ndo muwatupie lawama au pongezi. JF home of Greater Thinkers [emoji125][emoji125][emoji125]
 
Sio kweli kabisa tetemeko linatumika kama sababu tuu
Mshana jr NINAKUUNGA mkono, awamu hii tuna tatizo kubwa sana katika mahusiano ya kimataifa, unajua mikutano kama hii huzaa matunda kwani maraisi hutumia kuonana na wenzao kando ya mikutano na kuzungumzia mahusiano ya kibiasha na yenye tija kwa nchi zao.
Naona raisi wetu anaendeleza visingizio visivyo na mashiko.
AMEKIRI
1. Haendi bukoba anawatu wa
kushughulikia tetemeko
2. Amesema wabukoba wachape
kazi, kwnn naye asichape enda
po wahanga wanachapa analipi
la kuomboleza?

Afundwe ktk hili, mbahili hapigagi hatua sawa na aliyepewa talanta moja akaificha mchangani
 
Jamani naomba kuuliza, kuna video inasambaa kwenye mitandao ikionyeshaa majengo pacha ya bank kuu yakiungua. Je, kuna ukweli wowote, au ndio kutafutiana jela huku?
 
Tatizo sio kwenda au kutokwenda tatizo ni sababu iliyotolewa.

UN Sio lazima kwenda ila ni muhimu kwenda, Tanzania sio kisiwa.

Tunaanza kupata shaka kile kinachosemwa mitandaoni kuwa 'Kirengesa' tatizo, Waumini wa hili la Lugha tunazidi kuongezeka.
Ninamshaka na kilichopo kichwani mwako, unafikiri kila anaekwenda UN anazungumza kiingereza?

Obama hamkumzika Mohamed Ali kisa mwanae ana graduate. Marais kutoka sehem mbalimbali walikwenda kumzika..?

Ulimwengu wa diplomasia sio wa kishabiki wa kisiasa kama unavyodhani.
 
Aliyekuwa anaenda bila kukosa mahudhurio mlimuita Vasco Dagama. Anayebana matumizi....mnamponda humu. WaTanzania tunataka nini?

By the way UN New York.....ni kitu gani kipya anahitaji kwenda kufanya? maana maximum time ya kuongea kwa kila Kiongozi ni dakika tano! Na mara nyingi kumbi zinakuwa empty! wakubwa wameshaondoka.

WATANZANIA tuamke...Tanzania ya Magufuli ni ukurasa mwingine. You either adapt or perish!
UN hatuendi, AU hatuendi, SADC hatuendi .... Hivi ni mkutano gani wenye faida kwa Tanzania!!? Au ni mikutano ya CCM tu ndiyo yenye faida kwa Taifa hili? Wajuzi mtueleweshe!!
 
Toka nje ya box la ujinga. Hiyo mikopo mayochukua kila siku kutoka IMF na World Bank unadhani inadondoka hewani? Ngoja wavute handbrakes kidogo ndo utaelewa kilichomtoa kanga manyoya.

Hao IMF na WORLD bank ofisi zao ziko kwenye majengo ya umoja wa mataifa? na hiyo mikopo ma-teller wao huwa wanaitolea kwenye madirisha ya majengo ya umoja wa mataifa? Au wao ni idara zilizo chini ya Umoja wa mataifa?
 
sasa hivyo kujifungia ikulu na kusubiri ripoti eti za maafa ndio ushuhulikiaji wenyewe ?
kwa hilo tu hata makamo anaweza kulisimamia..
basi angeenda hata kuwapa pole wahanga..kashindwa !
mwisho anatupa vijembe kutoka Magogoni kwamba wahanga waanze kujisaidia wenyewe wasikae tu na kusubiri hela ya serikali..
hili ni jipu..
 
Ebo yaani 70% ya mkutano wote ni mdahalo!!! (debate) !!!! Tunarudi kule kule sekondary kwenye debates (midahalo)!!! Yaani Raisi mzima aende safari yote na gharama zote aende kuhudhuria mdahalo (debate)???
Hata watu wazima UN huwa wanafanya midahalo (debates) nilifikiri vitu hivyo ni kwa ajili ya watoto wa sekondari tu.Hata maraisi MWEEEE!!! Hivi Raisi anaweza shuka uwanja wa ndege wa nchi yake bila aibu akasema nilikuwa umoja wa mataifa kwenye mdahalo!!!! LOOOOO.Magufuli heri haendi yuko sahihi.
Kwahiyo haendi kisa mdahalo au anashughulikia wahanga wa tetemeko?
 
Back
Top Bottom