Rais Magufuli afuta safari ya UN General Assembly

Rais Magufuli afuta safari ya UN General Assembly

Chige

JF-Expert Member
Joined
Dec 20, 2008
Posts
13,493
Reaction score
29,888
Kutokana na janga la tetemeko la ardhi, kwa mara nyingine Mheshimiwa Rais wetu, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania analazimika "kuvunja" safari ya kwenda kuhudhuria Mkutano wa 71 wa Umoja Mataifa ambao unaanza kesho tarehe 20.09.2016 hadi 30.09.2016

Kwa mujibu wa Ms. Mindi Kasiga aliyehojiwa na gazeti la The Citizen Mheshimiwa Rais amelazimika kutoenda kuhudhuria mkutano huo ili kushughulika na matokeo ya maafa ya tetemeko hilo lililochukua maisha ya Watanzania wenzetu takribani 19 huku wengine takribani 200 wakiachwa majeruhi.

NOTE: Mada mbalimbali zitajadiliwa kwenye mkutano huo lakini moja ya mada ambayo inatarajiwa kuwa na msisimko ni ile itakayozungumzia wimbi la Wakimbizi na Wahamiaji duniani. Kwa mujibu wa tovuti ya Umoja wa Mataifa, hii ni mara ya kwanza Mkutano Mkuu wa UN kukutanisha wakuu wa nchi kujadili suala hilo.

Pamoja na hilo la Wakimbizi na Wahamiaji, pia kutakuwa na kikao muhimu sana ambacho kitachukua takribani 70% ya mkutano wote kutokana na umuhimu wake. Huu ni mdahalo unaolenga kuzungumzia malengo ya maendeleo endelevu na nafasi yetu katika kusukuma mabadiliko ya kufikia malengo hayo.

United Nations

JPM.png


Huyu hapa chini bila shaka ni mmoja wa Marais walioona umuhimu wa UN General Assembly. Ni Rais wa Msumbiji akizungumzia umuhimu huo:
 
Back
Top Bottom