Jamani naomba nimtetee Mtalii wetu maarufu.
Hii Safari ilipangwa na Wachina kumkaribisha kwenye mkutano fulani mkubwa kuhusu msuala ya biashara na maendeleo na mahusiano kati ya China na Africa. Kama sijakosea sana Kikwete ndio mgeni rasmi na atafungua huo mkutano.
Labda mjiulize Wachina wameona nini kwa Tanzania watupe heshima kubwa kiasi hicho? je wamegundua kuwa viongozi wetu na watendaji wa Serikali ni wepesi wa kulewa mvinyo na kusaini mikataba harakaharaka ambayo ni bei poa kwa wawekezaji?
Kingine ambacho najiuliza kwa ziara hii, ni kusikia kuwa Musharaf na jamaa wa Chile watakuwapo huko. Je China wanajenga hoja gani ya kimataifa?
Jamani tunataka Tanzania itangazwe kwa ari, kasi na nguvu mpya. Nendeni Galilaya Karpenaumu na pande zote za dunia mtangaze Tanzania ni kichwa cha mwendawazimu, njoo danganya unauwezo na pesa kuwa mwekezaji, tutakupa mkataba wa kudumu na kukulipa capacity charge nono, tutakusamehe kodi na ushuru jinsi upendavyo!
Angalia sana mradi mipya ya uwekezaji utasikia Pakistan na Chile ndio wawekezaji wapya!