Rais Kikwete na safari za nje

Rais Kikwete na safari za nje

Yaani hiyo sh bilioni 2.4 kwa miaka minne ndiyo iliyokausha hazina? Ndio maana waandishi wa habari hamumpendi Ben Mkapa, alikuwa anawapa ukweli wenu kuwa ni WAVIVU.
 
Hii habari nilikuwa tunaijadili wiki iliyopita kuhusu kwanini Hazina inashindwa kulipa malimbikizo ya waalimu na kuongeza mishahara ya wafanyakazi Tanzania tukaipata kuwa moja ya vikwazo ni hili swala. Uvascodagama wa Mkuu wa kaya na vimwana anaowabeba unaligharimu Taifa ile mbaya sijui na watu wa wizara ya mambo ya nje na wizara ya fedha wanalijua hilo ila wanaogopa kulisema kwakuhofia kupoteza ajira.

Wakati serikali za ulaya zinajaribu kupunguza fiscal budget Tanzania inapaa budget yake sasa sijui hizo pesa watazitoa maana wafadhili wameliona hili wameamua kukata panga sijui watazitoa wapi pesa zengine
 
Naomba kujua faida ya safari zote za JK kwa Taifa la TANZANIA??? mpaka sasa Si serikali wa Msemaji mkuu wa IKULU ameisha twambia tumefaidika vipi na safari za mweshima nje ya nchi mpaka sasa maana zote ni ahadi tuu za wawekezaji kuja nchi na je tumejipanga vipi kuhakikisha wawekezaji wajapo ni watanzania watafaidika??
 
Tatizo la watu kama nyinyi hampendi fikra na mawazo tofauti na mliyokuwa nayo na itokeapo hivyo huanza kuzungumza jamvini kama tupo kwenye kipindi cha leo tena cha clouds

No hard feelings BUT hapo utakuwa umekosea.

Unataka kuniambia mtu akipata mafanikio ataacha kujisifia kuwa ameleta mafanikio?Ni kweli haileti mantiki kuona Rais akifanya safari za US mara nane na UK mara nne.Tumepata mafanikio gani kutokana na hizi safari?Kuna mtu amesema mkonga wa mawasiliano...Huu mkonga umewa kuwasaidiaje Watanzania so far?Rates za mawasiliano zimeshuka au kupanda?Hayo maisha bora yamewezekana?Hizo ni baadhi ya hizo cost benefit analysis unazotaka wewe ziwekwe hapa jamvini?

Ukweli ni kuwa mambo yanakwenda kiholelaholela.Watu Morogoro wamepata maafa,Serikali imewasaidiaje?Ingekuwa umeme wa kuaminika umepatikana ndani ya kipindi hichi tungeweza kusema kweli haya ni baadhi ya matunda ya safari hizi.

Mwingine amesema 2.(something)bn sio nyingi....Akafananisha za safari za nchi za G8(Note tofauti-'Developed World')Sasa kweli utafananisha na pesa wanazotanga nchi tajiri kwa safari za marais wao?Kweli leo hii rais wa US anafanya safari nyingi kwa mwaka kuliko rais wetu pamoja na kuwa ni nchi tajiri?Are we exporting more to these countries kutokana na safari hizi?Uchumi umekua kwa kiasi gani?Sometimes inabidi kuangalia mwenyewe na usidhani kila mtu ana ill-feeling na Mhe.Rais.

Ukweli unabaki kuwa sio kila mtu ameumbwa aje kuwa kiongozi.Kuna wale wameumbwa kuwa watawala na wamekirimiwa vipaji vya kuongoza na kuna wengine wapo katikati na kundi lingine la mwisho-wananchi.Pale unajifananya wewe ni kiongozo na kuwahadaa wananchi wakakupa hiyo dhamana,matokeo yake ndiyo haya.I know we can do better than this!!

Nawasilisha!
 
Taito imenifurahisha sana..Hazina imekauka duu basi Tz hatuna tu masikini sana kama Rais tu anamaliza hela
 
Sasa tunapewa Faru na kwa majivuno tunasema tutaoa ulinzi sawa na Rais wa nchi.

Inakuwaje hatuwezi kuwalinda Albino?
 
Ninavyofahamu, safari za kujitambulisha hazina tija kabisa. Hazina hata chembe ya tija. Maana anachofanya ni kwenda kuongea na Rais mwenzie na kumwambia amsahau Rais alietangulia kwa kuwa yeye ndie Rais sasa.

Naamini kuwa kama safari zake zingekuwa na tija, na kama kweli kuna wawekezaji waliopatikana tungewaona. Haiwezekani Rais afunge safari kwenda kushawishi mwekezaji mmoja kuja nchini. Changamoto hiyo ingeweza kuchukuliwa na watu wa chini sana kwenye serikali.

Lakini vile vile, kama amefanya safari zenye mafanikio, kwanini wahisani wapunguze misaada kwa budget ya nchi? Inawezekana kuwa safari zake ndizo zilizopunguza mafanikio ya nchi kwa kiasi kikubwa. Maana, nani atakaesaidia nchi kupata pesa za safari?

Nadhani angefanya jambo la maana zaidi kufunga safari ya kutembelea TRA na kuomba kuongeza bidii ya kukusanya mapato. Labda hata hiyo isingetosha. Angehamia kabisa kwenye ofisi zao ili kuongeza tija. Naamini angepata pesa nyingi kuliko anazokwenda kuomba na kudhalilisha Taifa baada ya kulimaliza kiuchumi.
 
:angry::target::yuck:tik tok tik tok 2015 sijui itakuwaje,:A S clock: nahisi kama wanajeshi wanakuja ....... roho inaniuma sana.hivi na huu mkopo wa benki kwa ajili bajeti ya 2010-2011 utalipwa lini,na Je atakopa tena 2011/12...........😛ainkiller:
 
hizo safari zingejenga hospitali ngapi na kununua madawati ya shule au ujenzi wa shule ngapi? ni nyingi tu. nafikiri hapa mkuu anahitaji kuleta maelezo ya kutosha hawa kwa watz waliojaa uchungu wa maisha magumu kama kipindi hiki. Mungu atusaidie kwenye uchaguzi wa mwaka huu.
 
I think we need a system kama Mexico where the President's foreign trips have to be approved by the senate....like this story...are some of those trips really necessary? Should the people know the costs of each trip? I think it should be open to debate.


Mexican president is forbidden to travel

By E. Eduardo Castillo
Associated Press

MEXICO CITY - President Vicente Fox's press secretary Wednesday urged constitutional reform to let Mexican leaders travel abroad without congressional approval, a day after lawmakers irked Fox by blocking his planned trip to Australia and Vietnam.

Fox's press secretary Rubén Aguilar harshly criticized the legislators for their decision, which came amid rumors that Fox was going to Australia to visit his daughter. Aguilar decried ``the pettiness of Mexican political life,'' marked by ``childish positions that speak of a low level of discussion.''


``This administration believes that this article of the constitution has to be reformed because it causes unwarranted tension between the executive and legislative branches,'' Aguilar said.


The lower house of Congress voted 258-187, with six abstentions, to deny Fox permission for an official visit to Australia on Nov. 12-16. From there, he was to have traveled to Vietnam for the Nov. 18-19 Asia-Pacific Economic Cooperation summit.


The Senate approved the trip, but either chamber can block it.


The trip would have been Fox's last international trip. He leaves office Dec. 1.


Legislators said they were upset that Fox wanted to travel abroad as a political conflict in the southern state of Oaxaca continued to smolder and small bombs presumably planted by guerrilla groups exploded Monday in Mexico City.


Fox went on national television Tuesday night to express his disappointment in the lower house's vote, saying it ``goes against Mexico's interests'' and was ``clearly partisan.''


Fox singled out Mexico's opposition parties for criticism, particularly the Institutional Revolutionary Party, or PRI: ``I regret that lawmakers from the PRI refuse to listen to the voice of the people and aren't capable of acting responsibly to resolve local conflicts.''


That was an apparent reference to the refusal of the PRI governor of Oaxaca to heed calls to step down. Protesters have demanded the governor step down for months, sparking unrest that has left nine dead and driven tourists away from one of Mexico's top tourist destinations.


The PRI leadership called Fox's accusations ``offensive and baseless.''


Fox's statement ``constitutes an unacceptable discourtesy and an unforgivable challenge to the powers'' of the lower house of Congress, the PRI's national executive committee said.


It was the second time Congress has exercised its constitutional power to block one of Fox's trips. In April 2002, the lower house denied Fox permission to travel to the United States and Canada, saying he was focusing too much attention on international events.
This' impossible for our country... Labda tubadili system nzima
 
Kiukweli awamu hii tumepata kiongozi mwenye uchungu na nchi hii. Yule mwingine alikuwa anatupeleka chakavu.
 
Pamoja na kufurahi kumuona Rais wetu akisafiri katika mikutano ya kimataifa, nimefuatilia na kuona kuwa rais wetu anasafiri sana na kuhudhuria mikutano mingine ambayo ingeweza kuwakilishwa na makamu wake, waziri mkuu au mawaziri maalum wa wizara husika.

Mfano mkutano wa juzi wa Afrika Kusini kukutana na Bill gate angeweza kuhudhuria waziri anayehusika na technology. Hii itampa muda wa kutosha raisi kukaa ofisini kwake na kutoa mwongozo wa taifa.

Anyway ni small observation. Nahisi kuna baadhi ya watu huenda pia mmeiona.
Mbona mnamlaum wa sasa?? CHADEMA buana
 
Back
Top Bottom