Rais kaishiwa pumzi, karudi square one

Rais kaishiwa pumzi, karudi square one

Quinine Rais amepewa na wanancchi mandate ya miaka mitano kuongoza nchi na kutekeleza Ilani ya Uchaguzi ya CCM. Ndio kwanza tumemaliza mwaka mmoja, kutoa hukumu kwamba Rais atamaliza muda wake akayaacha kama alivyoyakuta ni upotoshaji or rather wishful thinking.

wakati ni muamuzi sahihi wa kufanikiwa kwa Rais...na wakati huo ni miaka mitano na sio mwaka mmoja. Lakini hata ukiamua kumpima kwa mwaka mmoja, umechagua kuyaacha mambo ya msingi yaliyokwishafanyika yenye manufaa kwa wananchi wengi.

Jambo la kwanza na kubwa lililofanyika ni kutoa ELIMU BURE kuanzia msingi hadi sekondari. usipoangalia jambo hili kwa upana,waweza kudhani ni jambo dogo,lakini ukweli ni kwamba familia zote mijini na vijijini zenye watoto wenye umri wa kwenda shule, sasa wana uhakika wa elimu ya watoto wao katika ngazi hiyo ya msingi.

Eneo jingine ambalo Serikali inachukua hatua ambalo watu wengi hawalizungumzi ni kulipa madeni. Tunaposoma habari kwamba serikali imekopa fedha kujenga barabara, hospitali n.k maana yake ipo siku tutatakiwa kulipa. Serikali ya Awamu ya tano imeingia madarakani katika kipindi ambacho madeni yaliyokopwa miaka ya nyuma yamemature na yanatakiwa kulipwa. Kwa kuweza kulipa madeni hayo ndiko kunakoifanyTanzania iendelee kuaminiwa na mashirika ya fedha ya kimataifa kuendelea kukopeshwa fedha kwa ajiili ya kutekeleza miradi mipya ambayo itawagusa wanachi walio wengi

Kuanza hatua za Kutekeleza miradi yenye tija kwa wananchi wengi. hivi sasa Serikali ipo kwenye hatua ya kupata mkandarasi wa kujenga Reli ya Kati katika Kiwango cha kimataifa. Mradi huu utafungua upya fursa za uchumi kwa wananchi wa dar es salaam, Morogoro, Dodoma, Singida, Tabora, Kigoma, Mwanza.....Reli itakapojengwa itatoa ajira kwa maelfu ya wanannchi, na itakapokamilika itarahisisha usafirishaji wa mizigo na kupunguza gharama za kufannya biashara kutokana na urahisi iwa usafiri...lakini sio hivyo tu ikikamilika itapungusa kasi ya uharibifu wa barabara zetu ambazo zimejengwa kwa pesa nyingi za walipakodi na mikopo tunayoendelea kuilipia

Kupunguza mianya ya upotevu wa fedha za umma kwa njia ya ukwepaji kodi, malipo hewa (mishahara hewa, wanafunzi hewa, zabuni hewa) pamoja na overpricing/overcharging zilizokuwa zinafanywa kwenye manunuzi ya umma ambayo mwisho wake mzigo ulikuwa unabebwa na walipakodi. Juhudi zilizokwishafanyika zinastahili kuungwa mkono,lakini zaidi ushirikiano wa wananchi wazalendo, wenye nia njema ya kuona maovu yanatoweka unahitajika sana....Rais hawezi kujua kila kitu kinachotokea kila mahala.....anahitaji ushirikiano wa wananchi, anahitaji utendaji bora wa vyombo vyake.....


Mnyonge mnyongeni,haki yake mpeni.....ndani ya muda mfupi tumeona ndege yetu iliyokuwa inachechemea miaka nennda rudi inaruka.....tena ikiwa na ndege mbili mpya tunazomiliki wenyewe. Wapo watu wanabeza mafanikio hayo....pengine ni kwakuwa tumesahau tulikotoka......hivi mnajua ATCL iliwahi kukodikukodisha ndege ya zamani na kulipia mabilioni ya shilingi? leo hii tunamiliki ndege,hatudaiwi na mtu...si jambo la kubeza.


Kwa vyovyote vile, yapo mapungufu na changamoto mbalimbali zilizojitokeza ndani ya mwaka mmoja, lakini hazitoshi kutoa hukumu ya kushindwa kazi wakati kuna mafanikio mengi na muda wa miaka minnne wa kutekeleza zaidi. Tumpe nafasi Rais wetu atekeleze wajibu aliopewa na wananchi ili tutoe verdict yetu vizuri baada ya miaka mitano. pale penye mapungufu tuwe wazalendo kutoa solutions zifanyiwe kazi na sio kupinga tu maana nchi hii ni yetu sote.
Mbona unajibu kama una cheo pale magogoni
humu tunapigana vikumbo na mawaziri kadha wa kadha .Hila miaka 5 sio mingi!!
 
Kila kitu alichodhani atakirekebisha kimeanza kurudia hali yake ya zamani.

Moto wa kupambana na mafisadi ni kama umezimika baada ya kuambiwa mahakama ya mafisadi imekosa kesi, tumerudi palepale.

Wakati anaingia alikuta TRA inakusanya bn 900 hadi tn1, yakaongezeka hadi tn1.5 leo yamerudi kule kule bn 900 sijui ya Nov inawezekana yameshuka zaidi.

Spidi ya kubomoa nyumba zilizojengwa mabondeni na kinyume cha sheria ulianza kwa mkwara ukapiga breki kwa mama Lwakatare, leo tumerudi kule kule.

Machinga ni vurugu mechi, ondoa rudisha ondoa, tatizo halijatatuliwa limebaki palepale.

Tumbua tengua teua mwisho tumeishia kuteua walewale tuliowatumbua hatuja solve kitu tumerudi kule kule.

Mikopo ya wanafunzi sio tu tumerudi tulipokuwa yaani square one bali hata uwezo wa serikali kulipa umepungua kulinganisha na serikali iliyopita.

Serikali imeshindwa hata kuajiri na kupandisha madaraja watumishi wake, ni kama tumerudi square one.

Alipoingia alizuia safari za nje akazuia sikukuu za kitaifa, leo watumishi wanasafiri kama kawaida na juzi tumesherehekea sikukuu ya Uhuru aliyoikataa mwaka jana, mambo yamekuwa business as usual.

Mapigano kati ya wakulima na wafugaji ni kama ndiyo yamezidi, pamoja na ahadi ya serikali yake kutatua kadhia hiyo ni kama tumerudi kule kule.

Kuna mengi ambayo alidhani rahisi kuyafanya yameanza kumshinda mfano, sukari ya Bharesa, pembe za ndovu, madawa ya kulevya, majangili. Nina uhakika anaweza kumaliza muda wake akayacha kama alivyoyakuta.

Naomba kutoa hoja.

Quinine.
Umesahau kelele za kuhamia Dodoma
Sasa ziko wap
 
MOJA MMEKOSA UZALENDO,LAKIN PILI HUENDA UNA UGONJWA WA MDONDO.MAANA MTANZANIA TIMAMU HAWEZI KUWA KAMA WEWE.
 
Sikuungi mkono na wala sitakaa nikuunge mkono. Hii tabia ya kumsema hovyo rais halaf huonyeshi njia ni mbaya kuliko upofu. Mwambiye afanye nini sio kafanya nini. Urais hauna shule yakhee. Urais ni kuelekezana, tusibaki kulaumu tu na kusimangana humu jf. Toa wazo lako sio masimango yako nadhani rais ni msikivu atasikia. Hata kama hatakupongeza lakini ukimpa ushauri mzuri, naamini huufuata kimya kimya
 
Ni kwa waliopungukiwa maarifa tu ndo wanaoweza kuunga mkono hoja hii ya hovyo. Ka una maarifa timamu huwezi kuleta hoja hii ukafikiri ndo jambo jema kwa nchi na kwamba tulishabikie hapa JF. Sisi kama watu waungwana yatupasa kumuunga mkono mheshimiwa raisi kuhakikisha nchi inakaa kwenye mstari na inakuwa na maendeleo chanya na si kumdhihaki na kuonyesha juhudi zake ni bure na kwamba nchi iendelee kuendeshwa hovyohovyo kwa kuendekeza wahujumu uchumi, wauza madawa ya kulevya, mafisadi na majanga mengineyo ktk nchi.
kwa hiyo, hayo ulioyataja hapo chini ameyasolve?
 
Ni kwa waliopungukiwa maarifa tu ndo wanaoweza kuunga mkono hoja hii ya hovyo. Ka una maarifa timamu huwezi kuleta hoja hii ukafikiri ndo jambo jema kwa nchi na kwamba tulishabikie hapa JF. Sisi kama watu waungwana yatupasa kumuunga mkono mheshimiwa raisi kuhakikisha nchi inakaa kwenye mstari na inakuwa na maendeleo chanya na si kumdhihaki na kuonyesha juhudi zake ni bure na kwamba nchi iendelee kuendeshwa hovyohovyo kwa kuendekeza wahujumu uchumi, wauza madawa ya kulevya, mafisadi na majanga mengineyo ktk nchi.
Acha kukurupuka wewe tulia u reply vizur Mzee Wa buku 7
 
Mahakama ya mafisadi itafanyaje kazi wakati vibaka wote mmenyooka? Thats the whole point....unapaswa kulalamika ikiwa ufisadi unaendelea huku watuhumiwa hawafikishwi mahakamani
Sasa hapa unanichanganya:
Hivi hii mahakama ilianzishwa kwa ajili ya kuwashughulikia mafisadi ambao tayari walikuwepo au watu wanaotarajia kuwa mafisadi baada ya mahakama kuanzishwa?
 
Sikuungi mkono na wala sitakaa nikuunge mkono. Hii tabia ya kumsema hovyo rais halaf huonyeshi njia ni mbaya kuliko upofu. Mwambiye afanye nini sio kafanya nini. Urais hauna shule yakhee. Urais ni kuelekezana, tusibaki kulaumu tu na kusimangana humu jf. Toa wazo lako sio masimango yako nadhani rais ni msikivu atasikia. Hata kama hatakupongeza lakini ukimpa ushauri mzuri, naamini huufuata kimya kimya
mmhh... yaani umwelekeze au umshauri? leo leo utatenguliwa na kupangiwa kwingine
 
Anatumia hadi hela za maafa wa kagera!,mbaya zaid wanyonge wanazid kuwa wanyonge.
 
Kutawala si sawa na kuongoza, kutawala ni rahisi kwa sababu kunahitajika kitu kimoja tu...nguvu
kulazimisha matakwa.

Kuongoza ni kugumu zaidi kwani kunahitajika vitu vitatu...ushawishi, busara na hekima, vitu adimu sana kwa baadhi ya watu.

Watawala hushindwa, viongozi hufaulu. Tulicheza pata potea kumchagua mtawala na sasa tunaonja ladha ya kosa letu.
Simple kulaumu!
Wewe jiulize ungekuwa raisi wa Tanzania leo kuna kitu gani ambacho kingekufanya uendelee kuchapa kazi!
Mtu yeyote anategemea malipo kwa anayoyatenda.
Hivi wewe huoni kuwa kama raisi anachanganyikiwa?
jamani Magufuli alikuwepo Tanzania miaka Zaidi ya 50, hajaja mwaka huu!
sorry kwa ku-shout (bold)!
wote kwa umoja (at least wengi) tulimlaumu Kikwete kuwa legelege, tulisema serikali imeingia ubia na matajiri wachache, tunataka kiongozi mkali na sio huyu wa kuchekacheka, tukasema wezi waondolewe serikali, tulitaka wanaokwepa kodi waadhibiwe! the guy was here na alikuwa anasikia tunachotaka! sasa amekuja na package ambayo ndio tuliokuwa tunaihitaji at least ktk maneno yetu!
leo tunaanza kulilia demokrasia, uhuru wa kuchonga, kupunguziwa kodi, kupindisha taratibu na sharia za nchi! Je haya si ndio tuliyakataa kwa Kikwete?
Raisi amezidiwa kwa sasa, nadhani yupo ktk wakati mgumu, hajui atende anayofikiri ni sahihi au asikilize makelele yetu!
kumbuka naye yupo kazini, anatamani apate matokeo chanya ktk kazi anazozifanya kwa hapa kuwatumikia watanzania, ila shida tumebadili adidu za rejea tulizomkabidhi! yale tuliyomuwekea kama vigezo hapo mwanzo tumeamua kubadilisha!
 
Unafikiria sana ila hakuna gazeti ata moja lakuandi nakuanika usanii wa magu na serkl yake.
 
Kununua madege bila kuwa kwenye bajeti na kuforce kuhamisha kwenye pesa ya shughuli nyingine nao ni ufisadi; Kutumia mabilioni kuhamia Dodoma nje ya idihini ya Bunge nao ni ufisadi. Inaelekea umejikita kwenye narrow definition ya ufisadi. Kutumia madaraka kutoa maamuzi ya matumizi ya pesa nje ya mfumo rasmi nao ni ufisadi...etc.etc. Grow up!
Hapana! Hiyo haiwezi kukubalika kuwa ni tafsiri ya ufisadi, labda kwa kuzingatia asili ya neno ambayo mi siijui, kwa asili ni kosa la kiuasherati. Maana mpya, ni ujinai. Jinai lina sehemu kuu mbili, vitendo na ubongo. Ubongo linathibitishwa na NIA. Jinai ktk ubongo lazima to prove nia OVU.

Haya, unaweza kuonesha nia ovu ktk kuamia Dom tulifanye tendo kuwa ufisadi? Inaweza kuwa uzembe, ingawa mi siuoni lakin si ufisadi. Nia ilikuwa njema na bado ni njema sana, itekelezwe.
 
Ni zaidi ya kule , makontena matano kwa mwezi si mchezo .

Walalamikaji mtashindwa na hamtaona kinachoendelea.Tunaotenda tutashinda mtabakia kushangaa imekuwaje.Faiza Foxy ana swali zuri sana japo jina alilochagua kulitumia silipendi"foxy" anauliza mlienda shule kujifunza ujinga? Ukienda shule akili yako yote ni ajira tu nje ya ajira hoooi,je ni kweli umeelimika?
 
Mambo yamekuwa magumu hadi misaada ya maafa ya tetemeko imegeuzwa mali ya serikali! Mi nasubiria nione kama kweli atarudia hapo Chato bila kufika Bk kutoa pole pamoja na kuwa misaada iliyokusudiwa waathirika imechepushwa
 
Mahakama ya mafisadi itafanyaje kazi wakati vibaka wote mmenyooka? Thats the whole point....unapaswa kulalamika ikiwa ufisadi unaendelea huku watuhumiwa hawafikishwi mahakamani
Tulitegemea esrow, lugumi, epa, rada, richmond, kuwaona kwenye hiyo mahakama. Watu wanapiga kelele kila siku Edo fisadi wameunda mahskama lakini hawamshitaki kwanini?
 
Ni Bora Basi Mambo Yamerudi Vile Vile Mlivyokuwa Mnaomba Iwe, Nadhani Sasa Vilio, Laana Na Matusi Humu Vitapungua, Mambo Kama Kawaida. Fanyeni Na Sherehe Kabisa

gsam Enzi Za Kikwete Zimerudi, Enjoy
Lini maisha ya mlalahoi na mdanganyika yalikuwa "maisha bora" chini ya siri-kali ya ccm?

CCM ya "Maisha bora" kwa ari, kasi na nguvu ya soda?

Au wananchi na wafanyabiashara wameficha sera bora za uchumi wa viwanda?
Hawa wananchi na wafanya biashara wanaficha sukari, fedha, umeme, kodi, ajira, majipu, zika...ahhh wamezidisha domo-krasia.
serikali imevuruga uchumi wa tanzania
"Katika utawala wa serikali yangu, sikubali wachache waishi kama malaika na wengi waishi kishetani. Niwahakikishieni kuanzia bunge lijalo, tutaanza kufanya kazi hiyo ili nao waishi kama shetani," alisema Rais Pombe Magufuli.

Angalizo: kuishi kishetani ni kuishi "maisha bora" kwa mwendokasi.
Siri-kali na CCM wana utaalamu na uzoefu wa kuwagawia wadanganyika "maisha bora" kwa miaka 40

Link Magufuli asema wanaoishi kama malaika wataishi kama shetani - MUUNGWANA BLOG

Mambo yamekuwa magumu hadi misaada ya maafa ya tetemeko imegeuzwa mali ya serikali! Mi nasubiria nione kama kweli atarudia hapo Chato bila kufika Bk kutoa pole pamoja na kuwa misaada iliyokusudiwa waathirika imechepushwa
 
Walalamikaji mtashindwa na hamtaona kinachoendelea.Tunaotenda tutashinda mtabakia kushangaa imekuwaje.Faiza Foxy ana swali zuri sana japo jina alilochagua kulitumia silipendi"foxy" anauliza mlienda shule kujifunza ujinga? Ukienda shule akili yako yote ni ajira tu nje ya ajira hoooi,je ni kweli umeelimika?
Bila shaka wewe ni mgeni hapa , mimi nimeajili zaidi ya watanzania wenzako 300 , sikuja jf kutafuta ajira .
 
Back
Top Bottom