Rais kaishiwa pumzi, karudi square one

Quinine

JF-Expert Member
Jul 26, 2010
21,803
48,957
Kila kitu alichodhani atakirekebisha kimeanza kurudia hali yake ya zamani.

Moto wa kupambana na mafisadi ni kama umezimika baada ya kuambiwa mahakama ya mafisadi imekosa kesi, tumerudi palepale.

Wakati anaingia alikuta TRA inakusanya bn 900 hadi tn1, yakaongezeka hadi tn1.5 leo yamerudi kule kule bn 900 sijui ya Nov inawezekana yameshuka zaidi.

Spidi ya kubomoa nyumba zilizojengwa mabondeni na kinyume cha sheria ulianza kwa mkwara ukapiga breki kwa mama Lwakatare, leo tumerudi kule kule.

Machinga ni vurugu mechi, ondoa rudisha ondoa, tatizo halijatatuliwa limebaki palepale.

Tumbua tengua teua mwisho tumeishia kuteua walewale tuliowatumbua hatuja solve kitu tumerudi kule kule.

Mikopo ya wanafunzi sio tu tumerudi tulipokuwa yaani square one bali hata uwezo wa serikali kulipa umepungua kulinganisha na serikali iliyopita.

Serikali imeshindwa hata kuajiri na kupandisha madaraja watumishi wake, ni kama tumerudi square one.

Alipoingia alizuia safari za nje akazuia sikukuu za kitaifa, leo watumishi wanasafiri kama kawaida na juzi tumesherehekea sikukuu ya Uhuru aliyoikataa mwaka jana, mambo yamekuwa business as usual.

Mapigano kati ya wakulima na wafugaji ni kama ndiyo yamezidi, pamoja na ahadi ya serikali yake kutatua kadhia hiyo ni kama tumerudi kule kule.

Kuna mengi ambayo alidhani rahisi kuyafanya yameanza kumshinda mfano, sukari ya Bharesa, pembe za ndovu, madawa ya kulevya, majangili. Nina uhakika anaweza kumaliza muda wake akayacha kama alivyoyakuta.

Naomba kutoa hoja.

Quinine.
 
Ni kwa waliopungukiwa maarifa tu ndo wanaoweza kuunga mkono hoja hii ya hovyo. Ka una maarifa timamu huwezi kuleta hoja hii ukafikiri ndo jambo jema kwa nchi na kwamba tulishabikie hapa JF. Sisi kama watu waungwana yatupasa kumuunga mkono mheshimiwa raisi kuhakikisha nchi inakaa kwenye mstari na inakuwa na maendeleo chanya na si kumdhihaki na kuonyesha juhudi zake ni bure na kwamba nchi iendelee kuendeshwa hovyohovyo kwa kuendekeza wahujumu uchumi, wauza madawa ya kulevya, mafisadi na majanga mengineyo ktk nchi.
 
Jibu hoja madawa ya kulevya yameisha au kamfunga nani? fisadi yupi kafikishwa mahakamani nk nk.
 
Back
Top Bottom