Rais kaishiwa pumzi, karudi square one

Rais kaishiwa pumzi, karudi square one

Pole sana. Utakuwa unaumwa ugonjwa wa upungufu wa lishe maana hufikiri chochote katika uchumi. Uliza usaidiwe usikurupuke
Mjinga tu unajidai wala hujui. Elimu kwa cheti feki ndio inakupeni confidence za kijinga
 
Ni kwa waliopungukiwa maarifa tu ndo wanaoweza kuunga mkono hoja hii ya hovyo. Ka una maarifa timamu huwezi kuleta hoja hii ukafikiri ndo jambo jema kwa nchi na kwamba tulishabikie hapa JF. Sisi kama watu waungwana yatupasa kumuunga mkono mheshimiwa raisi kuhakikisha nchi inakaa kwenye mstari na inakuwa na maendeleo chanya na si kumdhihaki na kuonyesha juhudi zake ni bure na kwamba nchi iendelee kuendeshwa hovyohovyo kwa kuendekeza wahujumu uchumi, wauza madawa ya kulevya, mafisadi na majanga mengineyo ktk nchi.
Wakati mwingine mkaage kimya, huyu jamaa yenu hasafishiki anadamu za watu mwili mzima. Piga kimya mtu wangu
 
Kuongoza nchi ni kazi kwa sababu kuna wanafiki wa kila Aina. Kuna wakwamishaji kama wewe. Na kuna wasiokuwa na uzalendo na nchi yao kama wewe.

Ndio nyie mkishindwa kuwapa wake zenu mimba mnaanza kusingizia bia na majirani.
 
alikuwepo miaka 20 kabla sasa mlitaka jipya lipi? mwacheni mtotoo wa watu ale raha form alichukua mwenyewe , na tunampigia kura tena hivyo hivyo tulimpenda tutampenda
 
Kila kitu alichodhani atakirekebisha kimeanza kurudia hali yake ya zamani.

Moto wa kupambana na mafisadi ni kama umezimika baada ya kuambiwa mahakama ya mafisadi imekosa kesi, tumerudi palepale.

Wakati anaingia alikuta TRA inakusanya bn 900 hadi tn1, yakaongezeka hadi tn1.5 leo yamerudi kule kule bn 900 sijui ya Nov inawezekana yameshuka zaidi.

Spidi ya kubomoa nyumba zilizojengwa mabondeni na kinyume cha sheria ulianza kwa mkwara ukapiga breki kwa mama Lwakatare, leo tumerudi kule kule.

Machinga ni vurugu mechi, ondoa rudisha ondoa, tatizo halijatatuliwa limebaki palepale.

Tumbua tengua teua mwisho tumeishia kuteua walewale tuliowatumbua hatuja solve kitu tumerudi kule kule.

Mikopo ya wanafunzi sio tu tumerudi tulipokuwa yaani square one bali hata uwezo wa serikali kulipa umepungua kulinganisha na serikali iliyopita.

Serikali imeshindwa hata kuajiri na kupandisha madaraja watumishi wake, ni kama tumerudi square one.

Alipoingia alizuia safari za nje akazuia sikukuu za kitaifa, leo watumishi wanasafiri kama kawaida na juzi tumesherehekea sikukuu ya Uhuru aliyoikataa mwaka jana, mambo yamekuwa business as usual.

Mapigano kati ya wakulima na wafugaji ni kama ndiyo yamezidi, pamoja na ahadi ya serikali yake kutatua kadhia hiyo ni kama tumerudi kule kule.

Kuna mengi ambayo alidhani rahisi kuyafanya yameanza kumshinda mfano, sukari ya Bharesa, pembe za ndovu, madawa ya kulevya, majangili. Nina uhakika anaweza kumaliza muda wake akayacha kama alivyoyakuta.

Naomba kutoa hoja.

Quinine.
Dua la kuku halimpati mwewe!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
1.2016_Baa mwisho SAA 5, 2019 baa 24hrs

2.2017 marufuku kulima kwenye 60m kutoka MTO, 2019 ruksa kulima mtoni

3. 2017 Nyumba holela zitabomolewa, 2019 nyumba holela hazibomolewi, zitsrasimishwa
 
Mahakama ya mafisadi itafanyaje kazi wakati vibaka wote mmenyooka? Thats the whole point....unapaswa kulalamika ikiwa ufisadi unaendelea huku watuhumiwa hawafikishwi mahakamani
Siku tutakapowafikisha mahakamani mafisadi wa 1.5t, nitajua kweli tumedhamiria kupambana na ufisadi kwa nguvu zetu zote

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Atakayechangisha mzazi atafukuzwa kazi leo tunachangishwa 5000 kukamilisha madarasa
 
1.2016_Baa mwisho SAA 5, 2019 baa 24hrs

2.2017 marufuku kulima kwenye 60m kutoka MTO, 2019 ruksa kulima mtoni

3. 2017 Nyumba holela zitabomolewa, 2019 nyumba holela hazibomolewi, zitsrasimishwa
4. Nyumba zilizojengwa kwenye hifadhi ya taifa zisiondolewe zithaminishwe.
 
Rais akiungwa mkono tu nchi Itakaa kwenye mtari
Ni kwa waliopungukiwa maarifa tu ndo wanaoweza kuunga mkono hoja hii ya hovyo. Ka una maarifa timamu huwezi kuleta hoja hii ukafikiri ndo jambo jema kwa nchi na kwamba tulishabikie hapa JF. Sisi kama watu waungwana yatupasa kumuunga mkono mheshimiwa raisi kuhakikisha nchi inakaa kwenye mstari na inakuwa na maendeleo chanya na si kumdhihaki na kuonyesha juhudi zake ni bure na kwamba nchi iendelee kuendeshwa hovyohovyo kwa kuendekeza wahujumu uchumi, wauza madawa ya kulevya, mafisadi na majanga mengineyo ktk nchi.
Kama Ndo hvo bas sawa sawa
 
Back
Top Bottom