Rais kaishiwa pumzi, karudi square one

Rais kaishiwa pumzi, karudi square one

Kila kitu alichodhani atakirekebisha kimeanza kurudia hali yake ya zamani.

Moto wa kupambana na mafisadi ni kama umezimika baada ya kuambiwa mahakama ya mafisadi imekosa kesi, tumerudi palepale.

Wakati anaingia alikuta TRA inakusanya bn 900 hadi tn1, yakaongezeka hadi tn1.5 leo yamerudi kule kule bn 900 sijui ya Nov inawezekana yameshuka zaidi.

Spidi ya kubomoa nyumba zilizojengwa mabondeni na kinyume cha sheria ulianza kwa mkwara ukapiga breki kwa mama Lwakatare, leo tumerudi kule kule.

Machinga ni vurugu mechi, ondoa rudisha ondoa, tatizo halijatatuliwa limebaki palepale.

Tumbua tengua teua mwisho tumeishia kuteua walewale tuliowatumbua hatuja solve kitu tumerudi kule kule.

Mikopo ya wanafunzi sio tu tumerudi tulipokuwa yaani square one bali hata uwezo wa serikali kulipa umepungua kulinganisha na serikali iliyopita.

Serikali imeshindwa hata kuajiri na kupandisha madaraja watumishi wake, ni kama tumerudi square one.

Alipoingia alizuia safari za nje akazuia sikukuu za kitaifa, leo watumishi wanasafiri kama kawaida na juzi tumesherehekea sikukuu ya Uhuru aliyoikataa mwaka jana, mambo yamekuwa business as usual.

Mapigano kati ya wakulima na wafugaji ni kama ndiyo yamezidi, pamoja na ahadi ya serikali yake kutatua kadhia hiyo ni kama tumerudi kule kule.

Kuna mengi ambayo alidhani rahisi kuyafanya yameanza kumshinda mfano, sukari ya Bharesa, pembe za ndovu, madawa ya kulevya, majangili. Nina uhakika anaweza kumaliza muda wake akayacha kama alivyoyakuta.

Naomba kutoa hoja.

Quinine.
Wenyewe ha2pendi kusikia maneno kama hayo, subiri msemaji wa chama atakuja kukujibu kupitia mkutano na waandishi wa habari

Sent from my TECNO-L5 using JamiiForums mobile app
 
Mahakama ya mafisadi itafanyaje kazi wakati vibaka wote mmenyooka? Thats the whole point....unapaswa kulalamika ikiwa ufisadi unaendelea huku watuhumiwa hawafikishwi mahakamani
Kununua madege bila kuwa kwenye bajeti na kuforce kuhamisha kwenye pesa ya shughuli nyingine nao ni ufisadi; Kutumia mabilioni kuhamia Dodoma nje ya idihini ya Bunge nao ni ufisadi. Inaelekea umejikita kwenye narrow definition ya ufisadi. Kutumia madaraka kutoa maamuzi ya matumizi ya pesa nje ya mfumo rasmi nao ni ufisadi...etc.etc. Grow up!
 
Tumebaki tunakimbizana kuuliza kaburi la mnyama! As if ndo changamoto zetu za maendeleo
 
Ni kwa waliopungukiwa maarifa tu ndo wanaoweza kuunga mkono hoja hii ya hovyo. Ka una maarifa timamu huwezi kuleta hoja hii ukafikiri ndo jambo jema kwa nchi na kwamba tulishabikie hapa JF. Sisi kama watu waungwana yatupasa kumuunga mkono mheshimiwa raisi kuhakikisha nchi inakaa kwenye mstari na inakuwa na maendeleo chanya na si kumdhihaki na kuonyesha juhudi zake ni bure na kwamba nchi iendelee kuendeshwa hovyohovyo kwa kuendekeza wahujumu uchumi, wauza madawa ya kulevya, mafisadi na majanga mengineyo ktk nchi.
wewe unapinga hoja, haya nakuuliza hivyo vyoooooote vilivyoeelezwa hapo na quinine ni uwongo? au kazusha tu
 
Wachochezi mnazidi kuongezeka tu .
Mtoa mada unamaanisha ile spidi ya mukulu wa bendi ikuwa ni honey moon tu ! Mana alianza kwa sspeed ya ajabu uku akituaminisha kuwa mtangulizi wake aliwabeba wapiga dili.
Mukulu ameanza kuwateua wale aliowatumbua !
Quinine mungu anakuona ...lol
 
Ni kwa waliopungukiwa maarifa tu ndo wanaoweza kuunga mkono hoja hii ya hovyo. Ka una maarifa timamu huwezi kuleta hoja hii ukafikiri ndo jambo jema kwa nchi na kwamba tulishabikie hapa JF. Sisi kama watu waungwana yatupasa kumuunga mkono mheshimiwa raisi kuhakikisha nchi inakaa kwenye mstari na inakuwa na maendeleo chanya na si kumdhihaki na kuonyesha juhudi zake ni bure na kwamba nchi iendelee kuendeshwa hovyohovyo kwa kuendekeza wahujumu uchumi, wauza madawa ya kulevya, mafisadi na majanga mengineyo ktk nchi.
Kuna watu zaidi ya milioni 20 kaamua kuwatenga. Unadhani ataongoza kirahisi? Unadhani hao milioni 20 hawana mchango wowote kwenye maendeleo? Ndo ajifunze uungwana. Sio ubabe ubabe kama vile taifa ni familia yake
 
  1. Kanunua ndege sita
  2. Ujenzi wa Reli ya Kati kwq Standard Gauge
  3. Ujenzi wa Bomba la Mafuta toka Uganda hadi Tanga
  4. Kudhibiti ufisadi na matumizi mabaya ya fedha za umma
  5. Ujenzi wq Hostel pale UDSM
  6. Nyumba za Magomeni Kota
  7. Kupandisha bei ya korosho kutoka shilingi 1000 hado 4000
  8. Ujenzi wq Barabara ya Mwenge hadi Morocco
  9. Ununuzi wa Meli mpya Ziwa Tanganyika na Victoria
  10. Umeme wa uhakika. Hakuna mgawo kwa sasa
  11. Nk nk
Njoo na improvements bro, sio uje na majukumu ya kila siku ya serikali.... hata likikaaa jiwe pale magogoni lazima barabara zijengwe, miundo mbinu iimarishwe, sasa pure government responsibilities tunaoma ni neema? Are we serious?
 
  1. Kanunua ndege sita
  2. Ujenzi wa Reli ya Kati kwq Standard Gauge
  3. Ujenzi wa Bomba la Mafuta toka Uganda hadi Tanga
  4. Kudhibiti ufisadi na matumizi mabaya ya fedha za umma
  5. Ujenzi wq Hostel pale UDSM
  6. Nyumba za Magomeni Kota
  7. Kupandisha bei ya korosho kutoka shilingi 1000 hado 4000
  8. Ujenzi wq Barabara ya Mwenge hadi Morocco
  9. Ununuzi wa Meli mpya Ziwa Tanganyika na Victoria
  10. Umeme wa uhakika. Hakuna mgawo kwa sasa
  11. Nk nk

Ni kweli kafanya hayo, ila swali la msingi DIRA ya uchumi wetu ni ipi? Je ni viwanda kama wanavyosema? Na mkakati wa kufika huko kwenye viwanda ni upi?

Bilashaka tunahitaji mijadala mipana hasa wakati wa kuwachagua hawa viongozi. Kwa ufupi hatuendelei kwa sababu hatuna scientific approach ktk mambo yetu. Ni kama mtoto ukimpa hela ataishia kula bagia na chops mpaka anamaliza pesa bila jambo la msingi
 
Mahakama ya mafisadi itafanyaje kazi wakati vibaka wote mmenyooka? Thats the whole point....unapaswa kulalamika ikiwa ufisadi unaendelea huku watuhumiwa hawafikishwi mahakamani
Lugumi Chenge Lowassa Karamagi Escrow Epa nani aliwasafisha? Mahakama ianze na hizo kabla ya kutafuta mpya.
 
Wengi nchi hii hamuijui. Anayeongoza nchi sio Rais. Rais ni nembo tu. Hata hivyo kuwa na negative mind ni kitu hatari sana. Maana siku zote kitu ambacho ni hakika lazima kitokee ni kifo peke yake. Mengine yote ni yamkini. Ila ni afya zaidi kuangalia mazuri na kumpa nguvu yaimarishwe. Sio kulalamika. Anayeleta maendeleo sio Rais!!! Hapa ndipo ujinga wa wengi ulipo.
 
Mu
Ni kwa waliopungukiwa maarifa tu ndo wanaoweza kuunga mkono hoja hii ya hovyo. Ka una maarifa timamu huwezi kuleta hoja hii ukafikiri ndo jambo jema kwa nchi na kwamba tulishabikie hapa JF. Sisi kama watu waungwana yatupasa kumuunga mkono mheshimiwa raisi kuhakikisha nchi inakaa kwenye mstari na inakuwa na maendeleo chanya na si kumdhihaki na kuonyesha juhudi zake ni bure na kwamba nchi iendelee kuendeshwa hovyohovyo kwa kuendekeza wahujumu uchumi, wauza madawa ya kulevya, mafisadi na majanga mengineyo ktk nchi.
muulize kwanini alikingia kifua lugumi kampuni ya rafiki yake kwa kutupiga changa la macho kumtumbua ili asiumbuke
 
Ni humu humu mlikuwa mnalalamika na issue za bandari na kwengine, leo wametumbuliwa wale tulokuwa tunalalamika bado mnalaumu, Nadhani kuna wengine wametumbuliwa kihaki hasa hata mwanzoni mlikuwa mna msifu, iweje sasa mnakuwa na kigeugeu.
He don't have road map, plan, control, lead, excute, staff, implement etc.siyo kwenda kwenda tu.
 
  1. Kanunua ndege sita
  2. Ujenzi wa Reli ya Kati kwq Standard Gauge
  3. Ujenzi wa Bomba la Mafuta toka Uganda hadi Tanga
  4. Kudhibiti ufisadi na matumizi mabaya ya fedha za umma
  5. Ujenzi wq Hostel pale UDSM
  6. Nyumba za Magomeni Kota
  7. Kupandisha bei ya korosho kutoka shilingi 1000 hado 4000
  8. Ujenzi wq Barabara ya Mwenge hadi Morocco
  9. Ununuzi wa Meli mpya Ziwa Tanganyika na Victoria
  10. Umeme wa uhakika. Hakuna mgawo kwa sasa
  11. Nk nk
[emoji134] [emoji134] [emoji134]
 
Na kama ha2sikilizi je!!!!?, kila analoshauriwa halichukui ya ndo mwamuzi wa mwisho...tufanyeje hapo mkuu!!?
Naamini kila mtanzania anatamani kuona nchi ye2 inaendelea lakini tatizo ni kwamba huyu mkulu hashauriki, anadhani anaweza kuifikisha nchi anapotamani yeye (kwenye mafanikio nadhani/uchumi imara + maendeleo) kwa nguvu zake binafsi pasina kuwashirikisha wenza wake.
Wenzake wapi?Chadema?utakuwa umechanganyikiwa,kama unamaanisha watanzania mbona anawashirikisha kupitia wabunge wao ambao wengi ni CCM
 
Back
Top Bottom