Ben Saanane
JF-Expert Member
- Jan 18, 2007
- 14,580
- 18,157
Upatu wa DECI, Babu wa Loliondo na mkumbo wa Rais Magufuli
Na: Ben Saanane
RaiaMwema Toleo la 456
4 May 2016
UTAFITI uliofanywa na wasomi wa Chuo Kikuu cha Nottingham nchini Uingereza ulibaini kuwa Watanzania ndio watu wanafiki zaidi duniani. Nilisikitika na kujihisi fedheha niliposoma utangulizi wa ripoti hiyo kwa lugha ya kimombo; “The British and Dutch are the most honest in the world, while people in Tanzania are the least and it’s all down to how corrupt their politicians are (Waingereza na Waholanzi ndio vinara wa kuwa wakweli, wakati Watanzania ndio watu wa mwisho na hii inadhihirisha kwa jinsi wanasiasa wake walivyo mafisadi)”
Niliposoma ripoti hiyo ya utafiti nilifedheheka lakini nikashindwa kuipinga kwani sikuwa nimefanya utafiti sambamba kwa kuwa maadili ya kitaaluma yanaelekeza kuwa utafiti unapaswa upingwe kwa kufanya utafiti mwingine wenye matokeo tofauti na sio kwa maneno tu bila utafiti.
Utafiti huu ni mchungu kama ule uliofanywa na shirika moja la nchini Marekani la PEW Research, ulioeleza kuwa Watanzania ndio vinara wa kuamini katika ushirikina zaidi tukiongoza kwa alama 93 huku tukiwabwaga kwa mbali Congo DRC na Nigeria.
Kisaikolojia ukitafakari kwa mbali utaona kuwa haya mawili ya unafiki (kutokuwa wakweli) na kuamini katika ushirikina yanaweza yakatuweka katika ramani nyingine ya juu ya kutufanya kuwa taifa la watu wasiojiamini zaidi na vilevile tusiofikiri kwa kina.
Ni katika hali hii sasa tumejikuta kuwa taifa la watu wa kufuata mkumbo, kutojishughulisha kufikiri na kugeuka kuwa mashabiki wa matukio na wakati wa mwisho kabisa tunageuzwa kuwa ‘majeruhi’ wa mkumbo wenyewe.
Katika jamii ambayo raia wake hawaamini kama wanaweza kufanikiwa kwa kutumia elimu, sayansi, utafiti, bidii na maarifa bila kutafuta miujiza ya kuamini katika ndumba au muujiza unaofanywa na kiongozi mmoja ni jamii ambayo inapiga hatua nyuma kwa kasi na inayojiandalia maangamizi kwa vizazi vijavyo.
Mwaka 2011 aliibuka Mchungaji Mwasapile maarufu kama Babu wa Loliondo, aliyetangaza kugundua (kupitia ndoto) dawa ya kuponya magonjwa sugu. Maelfu ya wananchi wakiwemo wasomi wakiwamo viongozi mashuhuri nchini wakamfuata kupewa uponyaji huo wa kikombe, baadhi ya vyombo vya habari vikashabikia.
Hakuna aliyejiuliza kama dawa husika imepimwa na kufanyiwa utafiti wa kisayansi. Serikali nayo ikazidi kudhihirisha udhaifu wetu kama taifa kwa kuweka miundombinu ya kuwafikisha watu huko. Serikali ikakumbwa na mkumbo wa kuamini katika miujiza. Baada ya hapo tumejinyamazia kama vile Babu wa Loliondo hajawahi kuwapo. Aibu, tulijifedhehesha kitaifa.
Watu waliliwa hela zao, wengine wakafanya biashara,wengine wakafia njiani baada ya kuachana na matibabu ya kisayansi hospitalini.
Miaka michache kabla ya hapo ni Watanzania hawa hawa waliokumbwa na mkumbo wa Pyramid Scheme (Upatu) ya DECI. Wakaaminishwa kwamba ukiweka fedha yako shilingi 10,000 utavuna 100,000 ndani ya muda mfupi. Hawakujiuliza na kutafakari sana kwamba hiyo fedha inayopatikana bila kufanya kazi inapatikanaje? Wao walichofikiria tu ni hela za chapchap.
Mlolongo wa matukio haya na mengine yote yaliyopita hasa yale ya “..maisha bora kwa kila Mtanzania” yaliyosukumwa kwa upepo mkali na kuwafanya Watanzania washindwe kufikiri sawa sawa yamenipa jibu kuwa tuna safari ndefu kama taifa. Tumekuwa wasahaulifu wa haraka, tumekuwa watu wa subira za miujiza na matamanio bila jitihada za kifikra.
Katika Uchaguzi Mkuu 2010 na 2015 Chama Kikuu cha Upinzani, Chadema na hata ACT-Wazalendo vimekuwa mstari wa mbele kupigania ukombozi wa kifikra kwa Watanzania kupitia elimu. Elimu ilipewa kipaumbele cha kwanza ili kujenga taifa adilifu, lenye raia wenye ujuzi, weledi, maarifa na linalojiamini mbele ya jamii nyingine ya kimataifa.
Taifa lenye raia wenye elimu bora haliwezi kuyumbishwa kwa matukio ya ajabu, haliwezi kuwa na raia wengi wanaowaza kuendelea kwa nguvu za kishirikina wala miujiza, haliwezi kuwa na raia wasiojiamini katika kusema ukweli (Wanafiki) na haliwezi kuwavumilia viongozi wala rushwa.
Taifa la aina hii haliwezi kuwa na viongozi wa kutunga na kuongoza kwa matukio ya mtu mmoja mmoja (one man show) bila kuwa falsafa, itikadi, sera na dira madhubuti katika uongozi. Ni lazima taifa makini (serious) liongozwe na viongozi makini na mifumo imara kitaasisi. Kiongozi asiyeamini katika mifumo imara kitaasisi katika uongozi anaweza kuwa hatari sana kwa taifa na kama tutafikiri kwa kina, atakuwa hatendi tofauti na mtu anayecheza sarakasi sokoni na kurudi palepale.
Kwa bahati mbaya katika sifa nilizoeleza hapo mwanzo za kutokuwa wakweli na za kuamini katika miujiza zimewanufaisha viongozi na wahusika wanaoandaa matukio yanayowaumiza wananchi.
Kwa mfano, mara kadhaa kabla na hata baada ya kuapishwa kwa Rais John Magufuli nimewahi kuandika hapa kwamba yeye na chama chake hawana dira thabiti ya kuweza kuliongoza taifa kukabili changamoto za sasa. Kuna baadhi ya wasomi hawakutaka kufikiri kwa kina zaidi ya kuimba nyimbo za sifa na mapambio tu na kuona kwamba tunaomkosoa Rais Magufuli tuna hila mbaya tu dhidi yake.
Aliposema kuwa amemfukuza kazi Mkurugenzi wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) eti kwa kuwa haendani na kasi yake nilimkosoa kwamba tatizo sio la mkurugenzi huyo bali la kimfumo. Nikamshauri kuwa abadili sheria na kuruhusu Takukuru kupeleka kesi mahakamani bila kupitia kwa DPP. Nikamshauri akipe meno chombo hiki kiwe kinawajibika bungeni.
Nilikosoa utendaji wake usiozingatia sheria kwake yeye binafsi na watendaji walioko chini yake. Tulimpa changamoto kuwa yeye kama raia namba moja awe mstari wa mbele kuonyesha mfano katika kupambana na ufisadi.
Tulimshauri Rais ataje mshahara wake, marupurupu na alipe kodi na kama tatizo ni kifungu cha Katiba ibara ya 43(2) kilichoiwekwa na watangulizi wake kuzuia mshahara wa rais kupunguzwa, basi aonyeshe mfano wa kuchukia rushwa aanzishe mchakato wa kukibadili kifungu hicho au kwa uaminifu kabisa arejeshe rasimu ya Katiba ya wananchi ili tuanze upya kama taifa kwani kwa kufanya hivyo atakuwa ameliponya taifa kwa kusimika mifumo imara ya kitaasisi katika kupambana na maradhi, ujinga, umasikini na adui mkubwa ufisadi.
Rais alitaja mshahara wake, hakutaja marupurupu yake. Aliahidi ataweka hadharani vielelezo vya malipo ya mshahara wake baada ya mapumziko mafupi ya Pasaka hadi sasa kimya. Bado tunaendelea kusimamia maudhui ya makala moja kati ya matoleo yaliyopita; “Mfumo unadhamini ufisadi”.
Rais asipofanya hivyo halisaidii taifa na matukio yote anayofanya hayajengi misingi ya kiuwajibikaji. Kwa hatua ambayo taifa limefikia, raia wengi wamepigika. Wana hasira na kila mtu na wanapenda kusikia matukio ya kimiujiza. Vinara wa mchezo wa upatu wa DECI na hata wa kikombe cha Babu wa Loliondo waliona hali hii, kwao ikawa fursa.
Sasa ni makosa makubwa kwa rais kutumia hali hiyo hiyo na fursa ile ile kwa wananchi wale wale waliopigika kweli kweli chini ya sera za chama chake kujijenga binafsi kisiasa bila ajenda madhubuti ya kulijenga taifa. Taifa linaendelea kuangamia.
Haya matukio ya mfululizo kama vile tupo kwenye mashindano ya Olimpiki ambako msimu wa mashindano ukiisha na matukio yanatoweka haulisaidii taifa. Rais arudishe mchakato wa Katiba Mpya, atangaze vipaumbele vyake kwa mtiririko sahihi kifalsafa, kiitikadi na kisera ili aweze kuipambanua sawia dira yake kwa taifa hili kuendana na Dira ya Taifa 2025.
Alhamisi, wiki hii, rais anatimiza miezi sita tangu ashike madaraka ya nchi. Hakuna jambo lolote la kimfumo alilofanya zaidi ya kuimba “majipu”. Inashangaza sana kwamba anaweza kuwa na ujasiri wa kuita wengine ni majipu wakati yeye binafsi ni mnufaika wa mfumo huu kupitia sheria mbovu kama inayounda Takukuru, sheria inayounda Sekretarieti ya Maadili ya Umma na ibara ya 43(2) ya Katiba ya nchi.
Watanzania tulishayaona ya DECI, ya Babu wa Loliondo na sasa tusikubali haya ya Magufuli. Yale mema tuyaunge mkono lakini anapovunja sheria na kukiuka taratibu tumkosoe bila kumuogopa. Anapoingilia mhimili kama Bunge na kujaribu kupoka madaraka ya Bunge tumkemee.
Tusikubali nchi kuongozwa kikomunisti. Nchi ambayo uhuru wa vyombo vya habari unaminywa na wananchi kukosa haki yao ya kikatiba ya kupata habari kama ilivyo kwenye Katiba Ibara ya 18 ambayo rais aliapa kuilinda. Rais huyo huyo amevumilia kwa serikali kuminya haki ya wananchi kuonyeshwa mjadala wa Bunge moja kwa moja.
Bunge ndio kipaza sauti cha wananchi. Serikali ya Magufuli ilichofanya ni shambulizi dhidi ya haki za kiraia na demokrasia (assault on democracy). Tumkatalie katakata na kumkemea.
Hata anapotangaza kushusha kiwango cha kodi kwa wafanyakazi kutoka asilimia 11 hadi asilimia 9, hatupaswi kumshangilia bila kutafakari kwa kina. Mwaka 2012 Kambi ya Upinzani Bungeni, kupitia kwa msemaji wake wa Wizara kivuli ya Fedha, Zitto Kabwe, ilisoma bajeti yake na kutoa mapendekezo ya kupunguza kiwango cha kodi hadi asilimia 9.
Ni suala la miaka minne iliyopita. Wakati huo, sarafu yetu haikuwa imeporomoka kwa kiwango cha kutisha kama sasa na mfumuko wa bei za vyakula ulikuwa wa kiwango cha kuridhisha kidogo. Leo Rais anasoma upepo anakuja anawahadaa Watanzania tena wale wanaolipwa mshahara kuanzia Sh.171,000 hadi 360,000 tu, kuwa atawapunguzia kodi hadi asilimia tisa wakati wale wanaolipwa kuanzia 361,000 hadi 540,000 wakiendelea kulipa kodi asilimia 20 huku wanaolipwa mshahara Sh. 541,000 hadi 720,000 wakikatwa asilimia 25 na wale wanaolipwa zaidi ya 720,000 wakikatwa asilimia 30.
Katika sera yetu ya uchumi na pia sera ajira tumeelekeza kwamba ni lazima madaraja ya mshahara na viwango vyake (income brackets) yaongezeke. Kwa mfano hali ilivyo sasa hivi ni kuwa anayelipwa 721,000 atalipa kodi asilimia 30 ya mshahara wake sawa na anayelipwa milioni tano au 15 kwa mwezi. Kwa hiyo ili kutengeneza mfumo sawia (progressive) wa kulipa kodi kwa wafanyakazi ni vyema madaraja yakaongezeka sambamba na kupunguza viwango vya kodi kadiri daraja linapoongezeka.
Alichojinasibu nacho juzi ni ongezeko (au unafuu) la kiasi cha shilingi 3,800 katika mishahara ya wafanyakazi kwa mwezi tu.
Watanzania tusikubali kuwa washabiki, tujitafakari kwa kina kwanza ili tuziaibishe tafiti zile za Chuo Kikuu cha Nottingham na asasi ya PEW Research ya kule Washington DC. Tumzuie rais wetu kupita njia ile ile ya DECI na Babu wa Loliondo na kikombe chake.
Mwandishi wa makala hii, Ben Saanane, ni Mkuu wa Idara ya Sera na Utafiti – Chadema. Anapatikana simu 0768078523.
- See more at: Raia Mwema - Upatu wa DECI, Babu wa Loliondo na mkumbo wa Rais Magufuli