Rais kaishiwa pumzi, karudi square one

Rais kaishiwa pumzi, karudi square one

Ni Bora Basi Mambo Yamerudi Vile Vile Mlivyokuwa Mnaomba Iwe, Nadhani Sasa Vilio, Laana Na Matusi Humu Vitapungua, Mambo Kama Kawaida. Fanyeni Na Sherehe Kabisa

gsam Enzi Za Kikwete Zimerudi, Enjoy
Mbona kila siku wanalialia humu hamna hela leo wanasema tumerud kulekule....
 
Kila kitu alichodhani atakirekebisha kimeanza kurudia hali yake ya zamani.

Moto wa kupambana na mafisadi ni kama umezimika baada ya kuambiwa mahakama ya mafisadi imekosa kesi, tumerudi palepale.

Wakati anaingia alikuta TRA inakusanya bn 900 hadi tn1, yakaongezeka hadi tn1.5 leo yamerudi kule kule bn 900 sijui ya Nov inawezekana yameshuka zaidi.

Spidi ya kubomoa nyumba zilizojengwa mabondeni na kinyume cha sheria ulianza kwa mkwara ukapiga breki kwa mama Lwakatare, leo tumerudi kule kule.

Machinga ni vurugu mechi, ondoa rudisha ondoa, tatizo halijatatuliwa limebaki palepale.

Tumbua tengua teua mwisho tumeishia kuteua walewale tuliowatumbua hatuja solve kitu tumerudi kule kule.

Mikopo ya wanafunzi sio tu tumerudi tulipokuwa yaani square one bali hata uwezo wa serikali kulipa umepungua kulinganisha na serikali iliyopita.

Serikali imeshindwa hata kuajiri na kupandisha madaraja watumishi wake, ni kama tumerudi square one.

Alipoingia alizuia safari za nje akazuia sikukuu za kitaifa, leo watumishi wanasafiri kama kawaida na juzi tumesherehekea sikukuu ya Uhuru aliyoikataa mwaka jana, mambo yamekuwa business as usual.

Mapigano kati ya wakulima na wafugaji ni kama ndiyo yamezidi, pamoja na ahadi ya serikali yake kutatua kadhia hiyo ni kama tumerudi kule kule.

Kuna mengi ambayo alidhani rahisi kuyafanya yameanza kumshinda mfano, sukari ya Bharesa, pembe za ndovu, madawa ya kulevya, majangili. Nina uhakika anaweza kumaliza muda wake akayacha kama alivyoyakuta.

Naomba kutoa hoja.

Quinine.
asante sana mheshimiwa....alitukumbusha tumuombee sana.Mungu anawezesha kwa kila aliye na good planning na good strategies.kama anazo tutazidi kumuombea uhai na waache papara wafanye kazi kwa weledi na ache kutumbua tumbua.watu hawana matatizo bali SYSTEM NZIMA ina matatizo
 
Kila kitu alichodhani atakirekebisha kimeanza kurudia hali yake ya zamani.

Moto wa kupambana na mafisadi ni kama umezimika baada ya kuambiwa mahakama ya mafisadi imekosa kesi, tumerudi palepale.

Wakati anaingia alikuta TRA inakusanya bn 900 hadi tn1, yakaongezeka hadi tn1.5 leo yamerudi kule kule bn 900 sijui ya Nov inawezekana yameshuka zaidi.

Spidi ya kubomoa nyumba zilizojengwa mabondeni na kinyume cha sheria ulianza kwa mkwara ukapiga breki kwa mama Lwakatare, leo tumerudi kule kule.

Machinga ni vurugu mechi, ondoa rudisha ondoa, tatizo halijatatuliwa limebaki palepale.

Tumbua tengua teua mwisho tumeishia kuteua walewale tuliowatumbua hatuja solve kitu tumerudi kule kule.

Mikopo ya wanafunzi sio tu tumerudi tulipokuwa yaani square one bali hata uwezo wa serikali kulipa umepungua kulinganisha na serikali iliyopita.

Serikali imeshindwa hata kuajiri na kupandisha madaraja watumishi wake, ni kama tumerudi square one.

Alipoingia alizuia safari za nje akazuia sikukuu za kitaifa, leo watumishi wanasafiri kama kawaida na juzi tumesherehekea sikukuu ya Uhuru aliyoikataa mwaka jana, mambo yamekuwa business as usual.

Mapigano kati ya wakulima na wafugaji ni kama ndiyo yamezidi, pamoja na ahadi ya serikali yake kutatua kadhia hiyo ni kama tumerudi kule kule.

Kuna mengi ambayo alidhani rahisi kuyafanya yameanza kumshinda mfano, sukari ya Bharesa, pembe za ndovu, madawa ya kulevya, majangili. Nina uhakika anaweza kumaliza muda wake akayacha kama alivyoyakuta.

Naomba kutoa hoja.

Quinine.
Akili yako ni ya tope.
Yaani mahakama kukosa kesi huoni kama uadilifu umeongezeka wewe unaona ni tatizo.

Kitakwimu utajivunia kuongezeka kwa makosa au kupungua kwa makosa??!!
 
Hebu kuwa mkweli kwa nafsi yako na useme ni mhujumu uchumi aliyeshughulikiwa, ni muuzaji gani wa madawa ya kulevya aliyeshughulikiwa, au labda ni fisadi gani kesi yake inanguruma mahakama ya mafisadi? Watu wengi waliweka matumaini makubwa kwa utawala wa awamu hii pale mwanzoni, ila sasa matumaini hayo yanayeyuka kila kukicha na kila kukichwa na wanajisikia kusalitiwa!
Punguza upuuzi nyie ndo mnakua wa kwanza kusema raisi haongozi nchi vzr...afu unatuletea pumba zako hapa eti ameshindwa....kwa hiyo mliomba ashindwe ili mpate cha kuongea....nyie msio jielewa ndo mnaona tumerudi kulekule....lakin kwa wenye timamu wanajua nidhamu iliyopo kwa taasisi za serikali...na huduma zinavotolewa bila ubaguzi...sasa nyie kazeni kuomba ashindwe...mwisho mtashindwa nyie...maana hadi 2025 mtakua mmenyooka..
 
Tatzo letu watanzania ni wajamaa tumelazimishwa tu na huu mfumo huu, huu mfumo tulonao hata utakapopevuka na kumea vizuri, matunda yake machungu yatapaza sauti kali kuliko hizi (akina Malema South).

Kibaya zaidi watu hatuna elimu wala ujuzi wa siasa hizi za vyama vingi na demokrasia yake ya kizushi. Uchaguzi ktk udemokrasia wa vyama vingi ni kumpata kiongozi kupitia sera za chama chake, atakayepewa term ya miaka 5 kuzitekeleza.

Wapaswao kuhoji haya tunayoyafanya ni wenye chama chao, kupitia vikao vyao. Juu ya utekelezaji wa ilani yao. Kwasasa wengine wote jukumu letu ni kutekeleza kikamilifu yote tutakayoagizwa na kupewa maelekezo, sheria, kanuni na ilani ya chama kilichoshinda.

Kama wananchi hatuzuiwi kukosoa, kushauri na kupendekeza mengine, kupokea ni jukumu la wenye chama tu, ndo demokrasia.
Kufaulu au kufeli kwa sarikali kutapimwa tena na wale wote waliompa ridhaa baada ya miaka mitano na si vinginevyo. Ndo demokrasia hii.
Taarifa : Kila baada ya miezi kadhaa, siikumbuki vyema, vikao vya chama hukaa kuanzia ngazi ya kata,halmashauri wilaya kupitia ilani na utekelezaji wake. Kuna wataalamu washauri humo ktk nyanja mbalimbali.
Kwahyo, wenye sera wanajua nn wanafanya, na labda wana uhakika nacho.
Ushauri kwa wapinzani, wasikazie tu kukosoa serikali iliyopo madarakani, bali nayo ijizatiti kichama chao kuhakikisha mnaingia madarakani, ndo demokrasia hiyo.
Hadi mwaka 2020 Tanzania itaongozwa na Dr. Magufuli. Kipimo chake si kelele zetu, bali uchaguzi ujao. Atajitetea hoja zote mnazompa leo, kama hali ikibaki hivi atasema kwanini aliamua kununua ndege na si kutoa mikopo, wakimuelewa atarejea tena magogoni, ndo demokrasia hii.
Sio Vita hii, ni kuangalia sera tu, zipi zinatufaa, basi. Kwa sasa, tuna jukumu kuzitii zote tunazopewa, tulishampa ridhaa.
 
Ni kwa waliopungukiwa maarifa tu ndo wanaoweza kuunga mkono hoja hii ya hovyo. Ka una maarifa timamu huwezi kuleta hoja hii ukafikiri ndo jambo jema kwa nchi na kwamba tulishabikie hapa JF. Sisi kama watu waungwana yatupasa kumuunga mkono mheshimiwa raisi kuhakikisha nchi inakaa kwenye mstari na inakuwa na maendeleo chanya na si kumdhihaki na kuonyesha juhudi zake ni bure na kwamba nchi iendelee kuendeshwa hovyohovyo kwa kuendekeza wahujumu uchumi, wauza madawa ya kulevya, mafisadi na majanga mengineyo ktk nchi.
Mtoa hoja amemdhihaki nani? Naona kama wewe ndo unajiaibisha. Labda tugeuze hizo hoja kuwa mafanikio ili usikwazike tena
 
Jibu hoja madawa ya kulevya yameisha au kamfunga nani? fisadi yupi kafikishwa mahakamani nk nk.
Huelewi kitu kuhusu madawa ya kulevya na sababu huwajui magodfather wa hiyo biashara ila nakuhakikishia wengi wako keko au waliwahi wakatoroka ila 70% wametolewa uraini. Tatizo unafikiri kila kitu lazima kiandikwe kwenye magazeti
 
Mstsri gani huku unaumiza wasiohusika na unajisifia?? Umesimamisha maswala ya ajira ambalo ni tegemeo kubwa la wanyonge wa nchi hii maana hawana hata MTU wa kuwapa laki mbili za mtaji,umesimamisha ongezeko la mishahara ambalo huwasaidia sana wanyonge wenye kipato kidogo kuliko hao wenye mishahara mikubwa,mikopo ya chuo imekuwa shida kuliko awamu zote,sasa hakuna vigezo vya wazi tofauti na awamu zilizopita,ni wanyonge gani anaowatetea huyu mzee?? Mbona wanyonge ndo tunaoumia zaidi??
Point mkuu
 
Sikuungi mkono na wala sitakaa nikuunge mkono. Hii tabia ya kumsema hovyo rais halaf huonyeshi njia ni mbaya kuliko upofu. Mwambiye afanye nini sio kafanya nini. Urais hauna shule yakhee. Urais ni kuelekezana, tusibaki kulaumu tu na kusimangana humu jf. Toa wazo lako sio masimango yako nadhani rais ni msikivu atasikia. Hata kama hatakupongeza lakini ukimpa ushauri mzuri, naamini huufuata kimya kimya
Mara ngapi anashauriwa tena na wataalamu waliobobea wanaishia kutumbuliwa refer Mafuru, wapinzani wameshauri mangapi wanaishia kubezwa, mimi ni nani hadi nisikilizwe.

Kama hapendi kushauriwa watu walichobakiza ni kusubiri akosee wamkosoe.
 
  1. Kanunua ndege sita
  2. Ujenzi wa Reli ya Kati kwq Standard Gauge
  3. Ujenzi wa Bomba la Mafuta toka Uganda hadi Tanga
  4. Kudhibiti ufisadi na matumizi mabaya ya fedha za umma
  5. Ujenzi wq Hostel pale UDSM
  6. Nyumba za Magomeni Kota
  7. Kupandisha bei ya korosho kutoka shilingi 1000 hado 4000
  8. Ujenzi wq Barabara ya Mwenge hadi Morocco
  9. Ununuzi wa Meli mpya Ziwa Tanganyika na Victoria
  10. Umeme wa uhakika. Hakuna mgawo kwa sasa
  11. Nk nk
10 ni uongo
 
Ni kwa waliopungukiwa maarifa tu ndo wanaoweza kuunga mkono hoja hii ya hovyo. Ka una maarifa timamu huwezi kuleta hoja hii ukafikiri ndo jambo jema kwa nchi na kwamba tulishabikie hapa JF. Sisi kama watu waungwana yatupasa kumuunga mkono mheshimiwa raisi kuhakikisha nchi inakaa kwenye mstari na inakuwa na maendeleo chanya na si kumdhihaki na kuonyesha juhudi zake ni bure na kwamba nchi iendelee kuendeshwa hovyohovyo kwa kuendekeza wahujumu uchumi, wauza madawa ya kulevya, mafisadi na majanga mengineyo ktk nchi.
Jaribu kuepuka kutoa majibu ya jumla jumla yasiyo na vielelezo (generalization) kama ulivyofanya. Kwa mtizamo wa harakaharaka unapinga hoja ya mtoa hoja bila hoja.

Ungejitendea haki kwa kuorodhesha mafanikio, ambayo wote tunajua ni mengi, ya mhe rais JPM katika kipindi chake cha mwaka mmoja akiwa madarakani.
 
Mahakama ya mafisadi itafanyaje kazi wakati vibaka wote mmenyooka? Thats the whole point....unapaswa kulalamika ikiwa ufisadi unaendelea huku watuhumiwa hawafikishwi mahakamani
Lowassa siyo fisadi tena? Kwanini hiyo mahakama isianze naye awe demo?
 
Back
Top Bottom