Rais kaishiwa pumzi, karudi square one

Rais kaishiwa pumzi, karudi square one

Hivi tuungemkono kitugani kuyaacha majizi yakipete mtaani nawewe unatushauli tuungemkono majitu yaliyokula pesa za esikulo mpakaleo yakoyanatesa mtaani nafamilia zao zinakulabata kwapesa yauma nawewe unashauli tuunge mkono huu upuuzi .. wanaokamatwa niwanyonge namajizi yabaki.. Leo unaseme tuunge mkono aunewewe nimmojawa yawaliofaidi fedha za uma
 
Vibaka wamenyooka hivi haowalionyooka wameshaludisha mabilioni waliogawana na lug
 
Kutawala si sawa na kuongoza, kutawala ni rahisi kwa sababu kunahitajika kitu kimoja tu...nguvu
kulazimisha matakwa.

Kuongoza ni kugumu zaidi kwani kunahitajika vitu vitatu...ushawishi, busara na hekima, vitu adimu sana kwa baadhi ya watu.

Watawala hushindwa, viongozi hufaulu. Tulicheza pata potea kumchagua mtawala na sasa tunaonja ladha ya kosa letu.
 
Ndege sita isije kuwa hela za rambirambi zimetumika, bomba la mafuta kwani tunajenga sisi, reli ya standard gauge hivi imefika wapi vile, meli mpya isije kuwa kama ahadi ya Kigoma kuwa Dubai.
Hovyo! Ishukuru demokrasia.
 
Kila kitu alichodhani atakirekebisha kimeanza kurudia hali yake ya zamani.

Moto wa kupambana na mafisadi ni kama umezimika baada ya kuambiwa mahakama ya mafisadi imekosa kesi, tumerudi palepale.

Wakati anaingia alikuta TRA inakusanya bn 900 hadi tn1, yakaongezeka hadi tn1.5 leo yamerudi kule kule bn 900 sijui ya Nov inawezekana yameshuka zaidi.

Spidi ya kubomoa nyumba zilizojengwa mabondeni na kinyume cha sheria ulianza kwa mkwara ukapiga breki kwa mama Lwakatare, leo tumerudi kule kule.

Machinga ni vurugu mechi, ondoa rudisha ondoa, tatizo halijatatuliwa limebaki palepale.

Tumbua tengua teua mwisho tumeishia kuteua walewale tuliowatumbua hatuja solve kitu tumerudi kule kule.

Mikopo ya wanafunzi sio tu tumerudi tulipokuwa yaani square one bali hata uwezo wa serikali kulipa umepungua kulinganisha na serikali iliyopita.

Serikali imeshindwa hata kuajiri na kupandisha madaraja watumishi wake, ni kama tumerudi square one.

Alipoingia alizuia safari za nje akazuia sikukuu za kitaifa, leo watumishi wanasafiri kama kawaida na juzi tumesherehekea sikukuu ya Uhuru aliyoikataa mwaka jana, mambo yamekuwa business as usual.

Mapigano kati ya wakulima na wafugaji ni kama ndiyo yamezidi, pamoja na ahadi ya serikali yake kutatua kadhia hiyo ni kama tumerudi kule kule.

Kuna mengi ambayo alidhani rahisi kuyafanya yameanza kumshinda mfano, sukari ya Bharesa, pembe za ndovu, madawa ya kulevya, majangili. Nina uhakika anaweza kumaliza muda wake akayacha kama alivyoyakuta.

Naomba kutoa hoja.

Quinine.
Safari zikizuiwa kelele,watu wameanza kusafiri tena kelele,hivi sisi tunataka nini hasa?
 
Anapambana na kina Lema sasa...


[HASHTAG]#justiceforLema[/HASHTAG].
[HASHTAG]#bringbackBenalive[/HASHTAG]
[HASHTAG]#RestInPeaceDena[/HASHTAG].
 
  • Thanks
Reactions: BAK
Ni kwa waliopungukiwa maarifa tu ndo wanaoweza kuunga mkono hoja hii ya hovyo. Ka una maarifa timamu huwezi kuleta hoja hii ukafikiri ndo jambo jema kwa nchi na kwamba tulishabikie hapa JF. Sisi kama watu waungwana yatupasa kumuunga mkono mheshimiwa raisi kuhakikisha nchi inakaa kwenye mstari na inakuwa na maendeleo chanya na si kumdhihaki na kuonyesha juhudi zake ni bure na kwamba nchi iendelee kuendeshwa hovyohovyo kwa kuendekeza wahujumu uchumi, wauza madawa ya kulevya, mafisadi na majanga mengineyo ktk nchi.
tumuunge mkono kwa lipi sasa ??? Looh hakuna kiongozi mpumbavu kama huyo
 
  • Thanks
Reactions: BAK
Ukwapuzi wa bilioni 16 za wahanga, utoaji rushwa wa milioni 10 kwa Wabunge wa MACCM ili kuminya uhuru wa habari nchini, kuangusha uchumi wa nchi na kufanya Watanzania kuishi kama mashetani.

Ebu nitajie moja lililofanikiwa labda kujenga Airport Chato.
 
Ni kwa waliopungukiwa maarifa tu ndo wanaoweza kuunga mkono hoja hii ya hovyo. Ka una maarifa timamu huwezi kuleta hoja hii ukafikiri ndo jambo jema kwa nchi na kwamba tulishabikie hapa JF. Sisi kama watu waungwana yatupasa kumuunga mkono mheshimiwa raisi kuhakikisha nchi inakaa kwenye mstari na inakuwa na maendeleo chanya na si kumdhihaki na kuonyesha juhudi zake ni bure na kwamba nchi iendelee kuendeshwa hovyohovyo kwa kuendekeza wahujumu uchumi, wauza madawa ya kulevya, mafisadi na majanga mengineyo ktk nchi.
Kwani Ilipinda?na kama ilipinda nani aliipindisha?kama aliipindisha au waliipindisha wamechukuliwa hatua gani?na tunahakikishiwa vipi kama haitapinda tena?
 
  1. Kanunua ndege sita
  2. Ujenzi wa Reli ya Kati kwq Standard Gauge
  3. Ujenzi wa Bomba la Mafuta toka Uganda hadi Tanga
  4. Kudhibiti ufisadi na matumizi mabaya ya fedha za umma
  5. Ujenzi wq Hostel pale UDSM
  6. Nyumba za Magomeni Kota
  7. Kupandisha bei ya korosho kutoka shilingi 1000 hado 4000
  8. Ujenzi wq Barabara ya Mwenge hadi Morocco
  9. Ununuzi wa Meli mpya Ziwa Tanganyika na Victoria
  10. Umeme wa uhakika. Hakuna mgawo kwa sasa
  11. Nk nk
[emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] ndio vipaumbele??? Hivi mbona mnadandia mambo Bomba ni la Sizonje?? Reli gani imejengwa?? Ndege sita ziko wapi mi najua mbili tuu
 
Huu ni utawala uliofitinika na kulaanika
Mkuu hata wazee wanasema kuwa ukiona utawala mwaka wa kwanza tuu hakuna mvua hizo ni salaam toka juu kuwa kuna laana ya aina fulani imewashukia.
 
Back
Top Bottom