Ilebayee
Senior Member
- Aug 3, 2020
- 141
- 694
Hii imenichekesha sana alooh🤣🤣Na wewe unavyoona Kagame anaweza kumuogopa Mama kweli?
Hii imenichekesha sana alooh🤣🤣Na wewe unavyoona Kagame anaweza kumuogopa Mama kweli?
Kuna yule mkuu wa majeshi ya SA alihojiwa akiwa Ethiopia nadhani wali attack sasa sijui kwa bahati mbaya au walipanga wakafa warwanda almost 20Nini kimelipata jeshi la SADC huko DRC mashariki walipokumbana na M23 yenye support ya Rwanda??
Mkuu wa majeshi alishasema,TZ kuna wageni wengi mno serikalini na kwenye vyombo vya usalama,nadhani ndio uhamiaji ikaja na operesheni mjue jirani yako,ila ajabu operesheni yenyewe iko kule instagram na x,mitaani aionekani hapo ndio utajua sisi watanzania uzalendo ni sifuri,admin wa uhamiaji yy anapost tu,mwisho wa mwezi mshahara unaingia 😃utekelezaji hamna
Ila mkuu kwa dunia ya sasa kwenye suala la silaha hakuna usiriNdugu yangu! Usilo lijua ni Sawa na usiku kiza! TPDF si dhaifa kama unavyodhani, lipo more advance,kuna mengi yamefanyika na yanaendelea kufanyika kimyakimya, kama bado unamtazamo wa jeshi lileee lililopigana vita ya Kagera! Basi unakosea Sanaa,kuna Idadi kubwa ya vijana wenye uwezo wamekuwa walipelekwa urusi kwa mafunzo ya muda mrefu,takriban miaka 6 kwa bechi ya kozi moja,TPDF inafanya kazi zake kwa usiri na umakini mkubwa Sanaa,Tofauti na watu wanavyoifikiria.
View: https://youtu.be/wUu2W2Mk3k0
General Paul Kagame amezungumzia mgogoro wake na Congo. Moja ya vitu alivyovisema ni kwamba wale wote ambao wanaamini kwamba wanaweza kuitishia Kigali wakiwa mbali anao uwezo wa kuwafuata hukohuko makwao.
Akaendelea kusema kwamba, wale waliokuwa wanaiunga mkono serikali ya Congo, Rwanda iliwasamehe na kuwaacha wapite nchini Rwanda na kurudi makwao. Katika watu ambao waliruhusiwa kupita Rwanda ni pamoja na askari wa JWTZ ambao kuna video inaonesha wanasachiwa ili kurudi nyumbani.
Paul Kagame amesema, kama wale wanajeshi wangethubutu kutunisha misuli bila kusalimu amri basi wangeangamizwa wote. Tena kama kuna wengine wataendelea kufikiria kwamba wataitishia Rwanda basi watafuatwa hukohuko makwao.
Maneno ya Dikteta Paul Kagame yameanzia dakika ya 14 ya hii video niliyoambatanisha hapa. Ni ujumbe wa vitisho kwa mataifa ya SADC, ikiwemo Tanzania, Malawi na Afrika Kusini.
Kuna msemo husema hivi, "Usipokuwa makini, hata mbwa atakucheka"
Povu Ruksa, Karibu Sana......
Ishu inakuja wanyarwanda ni wengi sana Tz na wanazaliana sana na hata kama wamezaliwa na kukulia TZ, still wapo royal kwa nchi yao. Kama alivyosemaga mkuu wa majeshi wetu kwamba wapo raia wakigeni serikalini au kwenye taasisi zake na wengine wakiwa wameshika nafasi za kufanya maamuzi, basi hakika anachokisema PK kwamba anauwezo wa kukufata ulipo ni ukweli mtupu.Hii kauli inaonyesha jinsi gani wamejipanga. Vyombo vya Ulinzi na Usalama viwe macho muda wote
Ilikuwa wakati huo!Hiyo mikwara tu mkuu,kwa anayejua huyo hapati shida.
Kipindi cha Jakaya alipiga mikwara sana aisee,JAKAYA akampiga mkwara wa askari wa mpakani kwa paredi akaufyata.
Rwanda ni hype tu, reality itawaumbua siku moja.We una zalisha nini 😄
Au ndiyo top secret
Ova
Hawa ndio wajinga wanaotusumbua hapa TanzaniaWe una zalisha nini 😄
Au ndiyo top secret
Ova
Tatizo linalotusumbua Tz ni uccm.Hata jambazi akiwa CCM anakuwa Salama.Mkuu wa majeshi alishasema,TZ kuna wageni wengi mno serikalini na kwenye vyombo vya usalama,nadhani ndio uhamiaji ikaja na operesheni mjue jirani yako,ila ajabu operesheni yenyewe iko kule instagram na x,mitaani aionekani hapo ndio utajua sisi watanzania uzalendo ni sifuri,admin wa uhamiaji yy anapost tu,mwisho wa mwezi mshahara unaingia 😃utekelezaji hamna
Ndiyo hivyo mkuu..Kagame haogopi wamamaHii imenichekesha sana alooh🤣🤣
Wenzetu wanatumia pesa kuwekeza kwenye teknolojia ya kujilinda, sisi tunajilinda kwa kusisitizana kuwa eti tuendelee kuwa taifa la amani tu basi, huku pesa tukizepeleka kwenye mambo ya ovyo ovyo.Nyie mmeinvest kwenye wizi na propaganda za kuwasifia wanasiasa lkn hiki kinchi kidogo masikini kinawatukana watu waliokizi maendeleo mpaka idadi ya watu mara mia.
Kuna siku East Afrika tutakuja kulia kisa kuifumbia macho hii migogoro ambayo inawakumba jirani zetu lkn hatuoneshi udhibiti zaidi ya kutegemea wageni wa ulaya watusaidie.
Nina imani hiki kinchi(Rwanda) hakifanyi mambo kwa kukurupuka wala kwa mihemko, bali ni uhalisia, pia nina uhakika kwa Rwanda ilipofika ina intelligence kubwa mpaka huku tusikofikiria, vile vile kina technologia ambazo baadhi yetu bado hatuna na hatuna mipango nazo kwa kujidanganya sisi taifa lenye amani
Ipo siku hii amani fake itawaliza watu na tutaumbuka vibaya sana, nguvu zetu tumeziwekeza ktk siasa chafu za kuuwana, kuchafuana na kupora mali za umma, lkn mambo ya msingi bado tuko nyuma.
Jeshi letu linaweza kuwa bora ktk uiamara wa kuwaandaa na kuwapa ukakamavu askari na wanajeshi lkn kwa technolojia hili tusidanganyane, technolojia haifichiki, bado tuko nyuma sana, nyuma saana.
Ushahidi mnao, kambi zetu si mnazijua? Maonesho ya siraha zetu si huwa tunayaona?, basi hata wakisema wanaficha baadhi ya siraha ushahidi mnao wenyewe kuwa Tanzania kitechnolojia bado tuko nyuma sana,
Tutafichwa vingine lakin nyenzo za kivita hasa ktk ulimwengu wa leo Tanzania bado hatujafika huko tumebaki ktk matumizi ya nyenzo za generation ya 3 huko ambayo ni outdated zingine zilitumika vita ya pili ya dunia na zingine kipindi cha akina Idd amin.
We need to improve, si tunajifunza vita za Ukraine+ Russia, Israel+ Iran kuwa vita vya sasa ni technolojia na kupunguza matumizi ya wanajeshi, yaani unapigwa nchini mwako kwa shambulio kubwa bila matumizi makubwa ya askari wa kijeshi, muda na fedha, na gharama za maandalizi ya plan.
Wanaongozwa na watu wanaojitambuaWarwanda wako well organised
Ova
Kila mwaka mnazika ila hamjielewi
Habari ya miaka 12 ndiyo unaileta leo unafikiri watu watakuwa hawajajifunza tuKila mwaka mnazika ila hamjielewi kama nyumbu.
![]()
Askari JWTZ mwenye asili ya Rwanda atoroka jeshini!
Askari wa JWTZ mwenye asili ya Rwanda adaiwa kutoroka Tanzania! Jeshi limesema litatoa taarifa zaidi kuhusu mwanajeshi huyo anayedaiwa kutoroka na nyaraka muhimu za jeshi!! Source: Mtanzania Jumapili ====== OFISA wa cheo cha juu katika Jeshi la Wananchi (JWTZ), anayeaminika kuwa na asili...www.jamiiforums.com
Kwani Watanzania sio wengi Rwanda?Ishu inakuja wanyarwanda ni wengi sana Tz na wanazaliana sana na hata kama wamezaliwa na kukulia TZ, still wapo royal kwa nchi yao. Kama alivyosemaga mkuu wa majeshi wetu kwamba wapo raia wakigeni serikalini au kwenye taasisi zake na wengine wakiwa wameshika nafasi za kufanya maamuzi, basi hakika anachokisema PK kwamba anauwezo wa kukufata ulipo ni ukweli mtupu.
Lakini naiamini sana Nchi yangu TZ
View: https://youtu.be/wUu2W2Mk3k0
General Paul Kagame amezungumzia mgogoro wake na Congo. Moja ya vitu alivyovisema ni kwamba wale wote ambao wanaamini kwamba wanaweza kuitishia Kigali wakiwa mbali anao uwezo wa kuwafuata hukohuko makwao.
Akaendelea kusema kwamba, wale waliokuwa wanaiunga mkono serikali ya Congo, Rwanda iliwasamehe na kuwaacha wapite nchini Rwanda na kurudi makwao. Katika watu ambao waliruhusiwa kupita Rwanda ni pamoja na askari wa JWTZ ambao kuna video inaonesha wanasachiwa ili kurudi nyumbani.
Paul Kagame amesema, kama wale wanajeshi wangethubutu kutunisha misuli bila kusalimu amri basi wangeangamizwa wote. Tena kama kuna wengine wataendelea kufikiria kwamba wataitishia Rwanda basi watafuatwa hukohuko makwao.
Maneno ya Dikteta Paul Kagame yameanzia dakika ya 14 ya hii video niliyoambatanisha hapa. Ni ujumbe wa vitisho kwa mataifa ya SADC, ikiwemo Tanzania, Malawi na Afrika Kusini.
Kuna msemo husema hivi, "Usipokuwa makini, hata mbwa atakucheka"
Povu Ruksa, Karibu Sana......