Nyie mmeinvest kwenye wizi na propaganda za kuwasifia wanasiasa lkn hiki kinchi kidogo masikini kinawatukana watu waliokizi maendeleo mpaka idadi ya watu mara mia.
Kuna siku East Afrika tutakuja kulia kisa kuifumbia macho hii migogoro ambayo inawakumba jirani zetu lkn hatuoneshi udhibiti zaidi ya kutegemea wageni wa ulaya watusaidie.
Nina imani hiki kinchi(Rwanda) hakifanyi mambo kwa kukurupuka wala kwa mihemko, bali ni uhalisia, pia nina uhakika kwa Rwanda ilipofika ina intelligence kubwa mpaka huku tusikofikiria, vile vile kina technologia ambazo baadhi yetu bado hatuna na hatuna mipango nazo kwa kujidanganya sisi taifa lenye amani
Ipo siku hii amani fake itawaliza watu na tutaumbuka vibaya sana, nguvu zetu tumeziwekeza ktk siasa chafu za kuuwana, kuchafuana na kupora mali za umma, lkn mambo ya msingi bado tuko nyuma.
Jeshi letu linaweza kuwa bora ktk uiamara wa kuwaandaa na kuwapa ukakamavu askari na wanajeshi lkn kwa technolojia hili tusidanganyane, technolojia haifichiki, bado tuko nyuma sana, nyuma saana.
Ushahidi mnao, kambi zetu si mnazijua? Maonesho ya siraha zetu si huwa tunayaona?, basi hata wakisema wanaficha baadhi ya siraha ushahidi mnao wenyewe kuwa Tanzania kitechnolojia bado tuko nyuma sana,
Tutafichwa vingine lakin nyenzo za kivita hasa ktk ulimwengu wa leo Tanzania bado hatujafika huko tumebaki ktk matumizi ya nyenzo za generation ya 3 huko ambayo ni outdated zingine zilitumika vita ya pili ya dunia na zingine kipindi cha akina Idd amin.
We need to improve, si tunajifunza vita za Ukraine+ Russia, Israel+ Iran kuwa vita vya sasa ni technolojia na kupunguza matumizi ya wanajeshi, yaani unapigwa nchini mwako kwa shambulio kubwa bila matumizi makubwa ya askari wa kijeshi, muda na fedha, na gharama za maandalizi ya plan.