Yoote haya uliyo eleza humu, yote yanaanzia ndani ya nchi husika; nchi kujitambua na viongozi wao kujuwa kuwa hatma ya nchi hiyo ni ya wananchi wenyewe na viongozi wao; haya mengine ya marafiki, amoja na kuwa ni muhimu, lakini yote yanategemea nchi inavyo jisimamia yenyewe.
Tuchukue mfano mgumu sana wa nchi, kama ninavyo ihisi hii hoja.
Israel. Pamoja na kuwategemea sana wamarekani na nchi za magharibi kwa ujumla; hasa katika mambo ya ulinzi wao, viongozi na wananchi wa nchi hiyo hawakujikabidhi moja kwa moja kwa hao watoa misaada kwao. Nimesema huu ni mfano mgumu sana, lakini sioni mfano mwingine ulio rahisi kukielezea ninacho kifikiria kama wajibu wa viongozi na wananchi wa nchi kama mfano sahihi wa kueleza hoja.
Nikisema Korea Kaskazini, najuwa 'roaganda' zimewachukua na kuwazoa watu wengi kuona kuwa nchi hiyo ni karibu kabisa na jehenamu; lakini, kiukweli; amoja na maungufu mengi ya mfumo wao; hawa huwezi kusema ni watu waliojikabidhi kwa wengine, kama tunavyotafuta sisi kujikabidhi.
Tuseme ukweli, Korea Kaskazini inaizidi nini Tanzania ambacho kinawazungusha akili hata akina Trum?
Nazitaja hizi nchi mbili mahsusi, hasa katika hili tunalolijadili kwenye mada hii; bila ya kusisitiza hayo mengine ya kiuchumi, n.k..