Rais Kagame anailenga Tanzania katika ujumbe huu?

Rais Kagame anailenga Tanzania katika ujumbe huu?

Hii sasa ni dharau, hivi kagame anaweza kuvuka mpaka na kuja kupigana na tanzania? Hebu aambiwe ukweli tanzania si congo na asijaribu kuvuka mpaka hata sentimeta moja. SADC haikutaka kuichakaza rwanda afahamu hilo
Unajua uwezo wake? Israel yenye watu 8mln imempiga Iran yenye watu zaidi ya million 100 kwa siku 12 mpaka rais wao hajaonekana mpaka leo akiogopa kuuliwa🤣🤣🤣🤣
 
Ataanza vipi kumuogopa bibi chaudere kama hata kipindi cha mzee wa msoga alijaribu kupiga mikwara, na nikufahamishe tuu hayo maneno haongei bure ana watu wengi kwenye mfumo wa serikali za afrika mashariki, anawajua vizuri sana
 
In reality Tanzania umoja ule haupo alafu vita ni science Israel imempiga Iran kwa siku 12 tuuu
Ni kweli Mkuu!Ila siasa zetu zinavyoenda unaweza Sema ukiwa nje kuwa kuwa Umoja haupo lakini inside Umoja upo.Kagame sio mjinga Kuna jambo katonya kuwa hayuko salama ndio maana kaamua kuchimba mkwara.Na hiyo ni message kwa Ramaphosa.
 
View: https://youtu.be/wUu2W2Mk3k0

General Paul Kagame amezungumzia mgogoro wake na Congo. Moja ya vitu alivyovisema ni kwamba wale wote ambao wanaamini kwamba wanaweza kuitishia Kigali wakiwa mbali anao uwezo wa kuwafuata hukohuko makwao.

Akaendelea kusema kwamba, wale waliokuwa wanaiunga mkono serikali ya Congo, Rwanda iliwasamehe na kuwaacha wapite nchini Rwanda na kurudi makwao. Katika watu ambao waliruhusiwa kupita Rwanda ni pamoja na askari wa JWTZ ambao kuna video inaonesha wanasachiwa ili kurudi nyumbani.

Paul Kagame amesema, kama wale wanajeshi wangethubutu kutunisha misuli bila kusalimu amri basi wangeangamizwa wote. Tena kama kuna wengine wataendelea kufikiria kwamba wataitishia Rwanda basi watafuatwa hukohuko makwao.

Maneno ya Dikteta Paul Kagame yameanzia dakika ya 14 ya hii video niliyoambatanisha hapa. Ni ujumbe wa vitisho kwa mataifa ya SADC, ikiwemo Tanzania, Malawi na Afrika Kusini.

Kuna msemo husema hivi, "Usipokuwa makini, hata mbwa atakucheka"

Povu Ruksa, Karibu Sana......

Yeye anatoaga vitisho wenzake wapo kimya hata hawamjibu.Kama anajiamini sana si avamie awashikishe adabu. Siyo kila siku anatoa vitisho kisa anawasumbua wakongo ambao nao wamegawanyika na hwana umoja.
 
Ni kweli Mkuu!Ila siasa zetu zinavyoenda unaweza Sema ukiwa nje kuwa kuwa Umoja haupo lakini inside Umoja upo.Kagame sio mjinga Kuna jambo katonya kuwa hayuko salama ndio maana kaamua kuchimba mkwara.Na hiyo ni message kwa Ramaphosa.
Umoja Gani upo wewe Hilo la kwenu kama mmemchokoza kagame acha awashugulikie wananchi hatutaiunga mkono jwtz hata siku moja
 
Ni kweli Mkuu!Ila siasa zetu zinavyoenda unaweza Sema ukiwa nje kuwa kuwa Umoja haupo lakini inside Umoja upo.Kagame sio mjinga Kuna jambo katonya kuwa hayuko salama ndio maana kaamua kuchimba mkwara.Na hiyo ni message kwa Ramaphosa.
Wanyarwanda kwa ticket ya ukimbizi wamejaa Tanzania kila idara. Na pia sisi vyombo vyetu wakiona upo kwenye ccm huwa hawana muda. Chunguza sana, kingine Rwanda na Uganda ni marafiki, ushahidi ninao kuna course iliendeshwa kule TMA huwezi amini ma cadet waliokuwa wametoka Rwanda na waliotoka Uganda walikuwa wanafahamiana vizuri🤣🤣🤣🤣
 
Hii sasa ni dharau, hivi kagame anaweza kuvuka mpaka na kuja kupigana na tanzania? Hebu aambiwe ukweli tanzania si congo na asijaribu kuvuka mpaka hata sentimeta moja. SADC haikutaka kuichakaza rwanda afahamu hilo
Mi naona SADC imefeli tu, hakua kujificha kwenye kulinda amani wala SADC haikuichokoza Rwanda...
Kilichopaswa kufanywa pale ni ubabe ubabe kuilinda DRC, hata US kuna muda anafaya ubabe ulio wazi kama juzi alipotuma B2 Iran japo hakufanikiwa ...

SADC ilipaswa kufanya ubabe na iwe onyo kwa M23 kuleta ghasia kusini mwa bara la Africa... tuseme tu SADC wamefeli..
 
Wanyarwanda kwa ticket ya ukimbizi wamejaa Tanzania kila idara. Na pia sisi vyombo vyetu wakiona upo kwenye ccm huwa hawana muda. Chunguza sana, kingine Rwanda na Uganda ni marafiki, ushahidi ninao kuna course iliendeshwa kule TMA huwezi amini ma cadet waliokuwa wametoka Rwanda na waliotoka Uganda walikuwa wanafahamiana vizuri🤣🤣🤣🤣
Kwa hiyo unafikiri Tz ni kubwa jinga? Iko wazi naona kisura Cha mke wa Museveni kama ni Dada wa Kagame.Tuko vizuri Mkuu.
 
Back
Top Bottom