View: https://youtu.be/wUu2W2Mk3k0
General Paul Kagame amezungumzia mgogoro wake na Congo. Moja ya vitu alivyovisema ni kwamba wale wote ambao wanaamini kwamba wanaweza kuitishia Kigali wakiwa mbali anao uwezo wa kuwafuata hukohuko makwao.
Akaendelea kusema kwamba, wale waliokuwa wanaiunga mkono serikali ya Congo, Rwanda iliwasamehe na kuwaacha wapite nchini Rwanda na kurudi makwao. Katika watu ambao waliruhusiwa kupita Rwanda ni pamoja na askari wa JWTZ ambao kuna video inaonesha wanasachiwa ili kurudi nyumbani.
Paul Kagame amesema, kama wale wanajeshi wangethubutu kutunisha misuli bila kusalimu amri basi wangeangamizwa wote. Tena kama kuna wengine wataendelea kufikiria kwamba wataitishia Rwanda basi watafuatwa hukohuko makwao.
Maneno ya Dikteta Paul Kagame yameanzia dakika ya 14 ya hii video niliyoambatanisha hapa. Ni ujumbe wa vitisho kwa mataifa ya SADC, ikiwemo Tanzania, Malawi na Afrika Kusini.
Kuna msemo husema hivi, "Usipokuwa makini, hata mbwa atakucheka"
Povu Ruksa, Karibu Sana......
Ukweli ni kwamba Rwanda ni nchi pekee yenye uongozi kama taifa karika ukanda huu wa Afrika .
Wale wanajeshi wanaokwenda Kongo kujifanya kuwa wanalinda amani ni mamluki na wezi wa mali za Kongo .
Wengi kwa muda mrefu walikua wanakwenda Kongo kwa ufadhili wa UN na Majambazi wanaoiba madini Kongo na kupeleka silaha . Wanajeshi hao ikiwemo wa afrika Kusini wanapokua Kongo wanasiba sana dhahabu na madini mengine . Wakirudi makwao wanakua matajiri wakubwa . Hali inayopelekea kufurahia Vita ya Kongo na kuona kama ni dili.
Kuhusu Rwanda kufaidi madini ya Kongo hiyo ni dhana ya kijinga sana inayojengwa na hao hao watawala na wakuu wa vyombo vya majeshi hayo ya hizo nchi ambao wanasiasa wao ni wezi na wanashindwa kulipa wanajeshi wao vizuri hivyo huona kuwa fursa pekee ni ya kuwapeleka wanajeshi wao Kongo ,Dafuru n,k ili wapate mapesa mengi na kusahau siasa za kifisadi ndani ya nchi zao.
Mfano Tanzania wakati wa utawala wa awamu ya pili serikali ilikosa kabisa uwezo wa kulipa watumishi wake ikiwemo wanajeshi na polisi. Rushwa ikawa kubwa sana kwa polisi , ujambazi wa kuteka magari ya abiria ukawa juu sana mita chache karibu na kambi za jeshi na hata wizi wa mabenki na magari ya kubeba pesa .
Kambi za jeshi zikawa ni sehemu ya kuuza gongo na kupika gongo .Wanajeshi walikua na maisha magumu . Polisi rushwa ilikua juu sana hivyo wao walionekana kuwa na maisha mazuri kuliko wanajeshi . Chuki kati ya polisi , jwtz na askari magereza ilikua kubwa sana .
Baadae Mkapa aliuza kila kitu kwa Mabepari wa kizungu ,kiarabu na kihindi . Kisha akawaomba Hao mabwanyenye na wanyonyaji kuwa Wanajeshi wa Tanzania wapate nafasi za kwenda huko kwenye misheni zinazofadhiliwa na UN ili kushiriki kupinda amani. Lengo likiwa ni kuwasaidia kupata kipato huko maana UN wanalipa kwa viwango vya kimataifa . Lengo la pili ni kuwaondoa wanajeshi kwenye kufuatilia mambo ya siasa za ndani na kufuatilia siasa za nje . Ndio maana mambo yale yale yanayofanyika Kwenye setiksli za Kongo ,Somalia ,Sudani na kwengineko yanafanana sana sana na serikali nyinngine za Afrika lakini penye upenyo wa vurugu vita haiishi kwa sababu watawala wananufaika na vita za majirani na vurugu za ndani zinawapa jeuri ya kutawala kibabe huku wakiwa wanachota rasilimali za nchi zao wakati majeshi yao yakiwa bize kuruliza vurugu na vita za majirani.
Ndio maana ukiwaambia wafanye siasa za haki na sheria za haki wao wanakujibu kuwa amani itavurugika na watu watauana . Wao wanajua kitakachoendelea maana wapo tayari kutumia majeshi hata ya kukodi ili kuua watu na kisha kuyafanya majeshi kuwa bize huku wao wakiwa wanashirikiana na mabepari wa ndani na nje kuiba mali za umma .
Tangu lini uchaguzi wa haki ukaleta vita?
Ingekuwa uchaguzi unaleta vita Ulaya si ingekua kama Kongo ?
Vita za Afrika ni miradi ya Watawala na Mabepari wa nchi za magharibi .
Eti SADEC sijui vikundi gani vinapeleka majeshi kongo . Kwa nini wasipeleke majeshi na wasimamizi wa uchaguzi huru ili Wananchi wachague viongozi wao kwa haki na anayeshindwa akubali na kama kuna pingamizi lisimamie na kusikilizwa kwa haki . Mechi ikiisha kila mtu arudi nyumbani kwake kwa furaha .
Lakini hawa watawala wasanii wanachezea demokrasia na chaguzi zao halafu wanatumia silaha kuua watu wanaopinga udhalimu na wizi wa kura sasa nchi zikichafuka ndio wanapeleka majeshi kusaidiana ili kubakishana madarakani.
Kenya ,India , Tailand na Afrika kusini wanaongoza kwa kuuza Madini ya Tanzanite inayopatikana Tanzania .
Je, majeshi ya nchi hizo yanaikalia Tanzania ?
Waje wanijibu wale wapimbavu wanaoilaumu Rwanda kwa kuwa na akiba ya dhahabu kutoka Kongo .
Wachimbaji wadogo wadogo wanauza maduni yao kwenye nchi yenye soko zuri la kununua na kuwalipa kwa usalama bila makodi ya kukomoana na rushwa nyingi.