Status
Not open for further replies.
Serikali semeni ukweli kuwa ni ugonjwa gani uliomua rais wetu? Siamini kama Afib ndiyo chanzo kikubwa kwa sababu hiyo inasababishwa (triggered) na underlying conditions. Kuna kitu kinafichwa hapa. Chronic Atrial fibrillation huwa unakuwa na chanzo. Tunataka ukweli
 
Kweli kabisa. Ukiwa Mkuu wa ngazi hiyo private is very minimal. Mimi ni mtumishi ujue. Najua wajibu wa wasaidizi wa Rais. Katika nchi zingine hawa wanastahili kuchukuliwa hatua kali za kinidhamu kwa uzembe huo Mkubwa. Huwezi kusema ajiamulie yeye kila kitu ambacho kingine ni hasara na hatari kwa Taifa.

Halafu nikwambie, Mfumo (system) ilichofanya ni kuwapenyezea Chadema taarifa za kilichopo na ndio maana walisema wazi kwamba wanataka serikali iseme nini kinaendelea kwa huyu ndugu. Pressure ilipozidi ndio wameona watangaze tu hakuna namna. Ndio uzuri wa kuwa na upinzani. Kuna mambo mengine system haiwezi lakini inakuwa na jukwaa la kusemea kupitia upinzani. Taifa likiua upinzani hakuna maendeleo.

Umeongea vyema nadhani inshu ya washauri makini imesababisha mengi! Doctor wa rais inabidi atuelezee kwa kweli! Magufuli wa true son of Africa legacy alioacha ni kubwa mno. Tutaanza kurudi kwy mambo ya michakato sasa na majizi umo umo yanapita! Sema “wanadai ivumayo haidumu sana”

Sio wote walikua wanamzunguka wanamkubali ndio hao wanatumika kutoa taarifa za siri kwa wqpinzani nk.
 
Si ya makumbusho hiyo? Something like that! Kwy qns why atoke JMKHI aende mzena sijawai hata kuwaza? Why not flying him to SA au hata Kenya apo baada ya kupata nafuu kwa uangalizi zaidi! Anyway yote tumuachie Mungu
Mkuu, it was too late.

Hata MOI waliona hiyo (worse condition) ndo ikaamuliwa aende Mzena kwa final analysis.
 
Kuna watu kwa kutomuelewa mheshimiwa rais wetu mpendwa, hayati JPM, wameendelea kumpaka matope hata ktk umauti wake!
Naomba niwasihi na kuwaonya, mtuache tumzike mpendwa wetu kwa aman! Bado hatujakubaliana na ukweli mchungu huu wa kifo ambacho pia hatujui kama kimetokea kiasili au kuna mkono wa mtu!

Tafadhari sana, naomba tupeane nafasi ya kumuomboleza kipenzi cha waafrica wote! Mungu tunakushukuru kwa kutupa JPM kutuongoza, tunakuomba uzidi kuiongoza na kuilinda nchi yetu Tanzania, na utupe rais mwingine ambaye ataiongoza kwa kulinda rasilimali zetu kwa wivu mkubwa zaidi hata ya JPM! Amen!
Macho yangu siyaelewi, maana yanatoa maji tiririka, sijui ni machozi! Hiki kipindi ni kigumu sana kwa watz wazalendo! Tupeni muda tumuomboleze mpendwa wetu!
 
Serikali semeni ukweli kuwa ni ugonjwa gani uliomua rais wetu? Siamini kama Afib ndiyo chanzo kikubwa kwa sababu hiyo inasababishwa (triggered) na underlying conditions. Kuna kitu kinafichwa hapa.....Chronic Atrial fibrillation huwa unakuwa na chanzo. Tunataka ukweli
Mkuu, huwezi kupata ukweli hapa.

Soma PM
 
View attachment 1724937

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Joseph Magufuli amefariki dunia.

Taarifa rasmi iliyotolewa kwa umma na Makamu wa Rais, Samia Suluhu Hassan kupitia Televisheni ya Taifa (TBC) leo usiku Machi 17, 2021 saa 5 usiku imeeleza kuwa Rais Magufuli amefariki dunia leo majira ya saa 12 jioni kwa maradhi ya Moyo akiwa katika Hospitali ya Mzena jijini Dar. Rais Magufuli alilazwa tarehe 6 Machi katika Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete kwa tatizo la moyo wa mfumo wa umeme ambalo limekuwa likimkabili kwa takirbani miaka 10.

Nchi itakuwa katika kipindi cha maombolezo kwa siku 14 na bendera zitapepea nusu mlingoti

View attachment 1728353




WASIFU:

Dkt, John Joseph Pombe Magufuli ni mwalimu na mtalaamu wa kemia akiwa na Shahada ya Uzamivu (PhD).

Kuzaliwa

Alizaliwa Oktoba 29 mwaka 1959 huko Chato mkoani Geita, Kaskazini magharibi mwa Tanzania.

Elimu

Magufuli alipata elimu ya msingi katika shule ya msingi Chato kuanzia mwaka 1967 hadi 1974.

Mwaka 1975 alijiunga na Seminary ya Katoke iliyo Biharamulo, Kagera kwa Elimu ya sekondari na kisha kujiunga na shule ya sekondari ya Lake iliyoko Mwanza hadi 1978 alipohitimu.

Mwaka 1979 alijiunga na shule ya Sekondari ya Upili ya Mkwawa, Iringa kwa ajili ya masomo ya kidato cha tano na sita na kuhitimu Mwaka 1981.

Mwaka 1981 hadi 1982 alisomea Stashahada (Diploma) ya Ualimu wa masomo ya Sayansi katika Chuo cha Ualimu cha Mkwawa, Iringa Masomo makuu yakiwa Kemia na Hisabati

Akiwa kazini, Magufuli aliamua kujiendeleza kwa kujiunga na Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) mwaka 1985 hadi 1988 alipotunukiwa Shahada ya Ualimu katika masomo ya Kemia na Hisabati.

Mwaka 1991 hadi 1994 alisomea Shahada ya Uzamili ya Kemia (Msc. Chemistry) katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam Tanzania na Chuo Kikuu cha Salford, Uingereza

Mwaka 2009 alitunukiwa Shahada ya Uzamivu (PhD) ya Kemia kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam

Mafunzo ya Kijeshi

Kati ya Mwaka 1983 na 1984, Magufuli alipitia mafunzo ya kijeshi kwa mujibu wa sheria kwenye Kambi za Jeshi la Kujenga Taifa Makutupora - Dodoma, Makuyuni - Arusha na Mpwapwa - Dodoma.

Kazi

Baada ya kufuzu Stashahada ya Ualimu, alifundisha masomo ya Hisabati (Mathematics) na Kemia (Chemistry) katika shule ya Sekondari Sengerema kuanzia mwaka 1983.

Baada ya hapo akafanya kazi kama Mkemia katika Chama cha Ushirika cha Nyanza huko Mwanza hadi mwaka 1995.

Siasa

Nyota ya Magufuli liana kung’aa katika siasa, alipogombea na kushinda ubunge eneo la Chato mwaka 1995. Mwaka huo huo aliteuliwa kuwa Naibu Waziri wa Ujenzi, nafasi aliyohudumu hadi Mwaka 2000.

Baada ya uchaguzi Mwaka 2000, aliteuliwa kura Waziri wa Ujenzi, nafasi aliyohudumu hadi Mwaka 2006 alipohamishwa kwenda Wizara ya Ardhi na Maendeleo ya Makazi alipokaa hadi Mwaka 2008.

Mwaka 2010, aliteuliwa kawa Waziri wa ujenzi kwa mara ya pili na kudumu kwenye nafasi hiyo hadi Mwaka 2015.

Urais

Mnamo Tarehe 12 Julai 2015, alichaguliwa kuwa mgombea Urais wa Tanzania kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM) Akiwa na Samia Suluhu Hassani kama mgombea mwenza.

Tarehe 29 Oktoba 2015 alitangazwa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi kuwa Rais wa Awamu ya Tano wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa ushindi wa kura 8,882,935 sawa na 58.46%.

Magufuli aliapishwa kama Rais wa Tano wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania tarehe 5 November 2015.

Muhula wa Pili

Mnamo tarehe 30 Oktoba 2020, Tume ya Uchaguzi Tanzania ilimtangaza John Pombe Magufuli kama rais kwa muhula wa pili kwa kupata kura milioni 12.5 hiyo ikiwa ni sawa na asilimia 84 akiwa amemshinda mshindani wake wa karibu, Tundu Lissu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) aliyepata kura milioni 1.9.

Baadhi ya Nukuu zake:

"Ni nafuu wakuchukie... uonekane wewe sio Mwanasiasa mzuri (Unpopular) kwasababu sikuja kutafuta Mchumba. Nimekuja Kufanya kazi za Watanzania." - Septemba 7, 2017


Soma pia:

1) Nukuu toka kwa Rais Magufuli (QUOTES)

2) Magufuli: Kila atakayetaka kuiokoa nafsi yake atapoteza...


VIDEO:



Baadhi ya Hotuba zake:

Hotuba ya Rais Magufuli kufungua Bunge la 12: Utumbuaji majipu utaendelea ili kuhakikisha Watumishi wanatenda kazi kwa mujibu wa Sheria na Kanuni - Novemba 13, 2020

Bungeni Dodoma: Rais Magufuli avunja Bunge la 11. Asema ajira 6,032,299 zimetengenezwa, Viwanda vipya 8,477 vimeanzishwa - Juni 16, 2020
Mlolongo wa nyadhifa za uwaziri, umeruka waziri wa mambo ya uvuvi/kilimo pia kama vilikuwa pamoja.
 
Mliosema Mh rais Magufuli yupo anapiga kazi. DHAMBI HII MTAIBEBA NA AIBU HAITAONDOKA KWENYE NYUSO ZENU.MMEWAKOSEA SANA WATANZANIA WAOMBAJI. MNGESEMA UKWELI MZEE ANAUMWA WAOMBAJI WANGEMUOMBEA SANA TENA KWA MCHOZI MENGI.NANI AJUAYE LABDA MUNGU ANGEFANYA REHEMA KAMA KWA MFALME EZIKIA ALIEAMBIWA NA NABII ISAYA UTAKUFA NA BAADA YA MAOMBI MUNGU AKAMREHEMU NA KUMUONGEZEA MIAKA 15. Rip Mh Rais MAGUFULI. UMEACHA ALAMA NYUMA YAKO. IPO RELI kila atakayepanda treni utakumbukwa.Lipo BWAWA la umeme. Nenda ila umeacha ambayo yatanenwa daima.
NDIO NA HILI FUNZO;LILILO TUGARIMU KWELI, UONGO NI DHAMBI
 
R.I.P mambo mengi mno. Mungu tusaidie tuanze upya. Amani, upendo na mshikamano. Utengano kwa udini, ukabila, ukanda, uvyama tuuzike tuanze kurasa mpya. Mungu Ibariki Tanzania.
 
Wamemuua, lini tukasikia hospitali ya Mzena, so did they deny him proper care at Muhimbili? Account zao za nje zilikuwa haziingizi hela kwa sababu JPM alikuwa amekata pa kuchota hela zetu.

Those leaders have a lot to answer. Heart problems are a long term ailment and at his level death can be avoided. Tanzania leaders, tell us the truth what went wrong. If you have heart problems and you contact Covid-19, of course it becomes very complicated to treat, and this causes death!
 
Umeongea vyema nadhani inshu ya washauri makini imesababisha mengi! Doctor wa rais inabidi atuelezee kwa kweli! Magufuli wa true son of Africa legacy alioacha ni kubwa mno. Tutaanza kurudi kwy mambo ya michakato sasa na majizi umo umo yanapita! Sema “wanadai ivumayo haidumu sana”
Sio wote walikua wanamzunguka wanamkubali ndio hao wanatumika kutoa taarifa za siri kwa wqpinzani nk
Hao watu ndumilakuwili, watapata lijala yao!
 
Raha ya milele umpe eebwana na mwanga wa milele umuangazie apumzike kwa amani Amina.

Nimeumia sana.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom