Ni viongozi gani wakristo ambao unaona hawafai kuongoza taifa come 2015?
We sema tu bila kujali vyama.Maana mkuu si tunafahamu wewe pia ni muislam mwenye msimamo kabisa? Haya sasa, madhali unafahamu nimesema kwangu mimi hata akiwa mpagani sijali, wewe naona una prefer tuendelee kuwa na marais waislam bila ku alternate kama ilivyo utamaduni wetu?Maana sioni hoja yako hapa mkuu!
Ama kuna mahali umeona nimesema kuwa ninataka wakristo ndo watawale? Ama nyama ya binadamu ishakunogea mkuu?
Wapo viongozi wakristo ninaona hawafai kuongoza nchi 2015 kama walivyo viongozi waislamu wasiofaa kuongoza nchi 2015. Kukutajia kwa haraka:-
a. EL (Mkristo).
b. Mkono (Mkristo).
c. Dr Hussein (Mwislamu)
d. Kapuya (Mwislamu).
e. Mtoto wa mkulima (Mkristo).
f. Harrison (Mkristo).
g. January (Sijui dini yake).
h. Slaa (Mkristo).
i. Nyalandu (Mkristo).
j. Maembe (Mkristo).
k. Karume (Mwislamu).
Na wengineo wengi. Sasa wote hawa siwakubali sio kwasababu ya dini yao bali nimewakataa kwasababu mbali mbali either a. mafisadi, b. madikteta c. hawana vision na nchi wanataka either kuendeleza umalkia wao au ufalme wao d. hawataweza kuendana na mabadiliko ya nchi na changamoto zake.
Watu naowaona wanafaa ni mainly :-
a. Dr SAS (Mwislamu)(Amekataa lakini akifuatwa atakubali tu tunahitaji mtu ambaye atairejesha heshima jeshi, kupambana na ufisadi na kuwamudu wawekezaji na kuirudisha nchi katika ramani).
b. Dr Magufuli (Mkristo) (Ijapokuwa na kashfa ya nyumba ila ni mtendaji mzuri sana na mwenye vision).
c. Professor Muhongo (Mkristo) (Ijapokuwa amekaa muda mfupi ila huyu ni mtendaji na anaweza kuwamudu wazungu na pia atatumudu sie wazawa).
d. Dr Shein (Mwislamu) (Huyu ni msafi hana doa ila changamoto yake ni mkimya mno kiasi hata haujui vision yake ni nini hasa?)
e. Dr Gharib (Mwislamu) (Huyu ni kichwa kizuri na mfuatiliaji na mtendaji mzuri ila changamoto itakuwa ni sehemu ya uongozi uliopo na hivyo maadui wa uongozi huu wanaweza kumuhamishia yeye).
f. Balozi Kagasheki (Mwislamu) huyu ni kiongozi mzuri well organised mambo yake ila sio msafi sana ila anaweza kunyoosheka.
g. Warioba (Mkristo) Huyu ni kiongozi mwenye uzoefu muda mrefu ila kizazi kipya sidhani kama anaweza kukimudu pia hana interest na muungano sijui kama utadumu kwake.
h. Mangula (Mkristo) Huyu ni mjamaa na kiongozi muadilifu ila siku za karibuni naona misimamo yake imebadilika sijui kama anaelekea kule kule au keshabadili upepo.
i. Mengi (Mkristo) Ni mfanyabiashara mwenye uzoefu na exposure atatufaa ila shida ni fisadi na dalali mzuri sana atauza kila kitu hadi pumzi but tukiweka mfumo mzuri wa kuwadhibiti mafisadi but anaweza kutufaa kwa uzoefu wa biashara na anautaka urais.
Hao wanakutosha,
Ila the best choice kwa hali ilipofikia Tanzania believe it or not ni watu watatu tu wanafaa kuokoa hii nchi isipoteze mwelekeo nao ni
Dr SAS , Dr Shein na Magufuli (Ila magufuli kwanza tupate katiba mpya adhibitiwe asije kugeuka kuwa fisadi). Wengineo ni kama tunabahatisha. Uchaguzi wangu mainly ni kwasababu hawa ni viongozi ambao tunaweza kuwapa dhamana ya nchi yetu wakatupeleka tunakotarajia wengineo either hawana experience ya kutosha kama Professor Muhongo au wakabaji (wazee wa kupiga dili) na hivyo tunarudi kule kule hali ikawa mbaya zaidi.