Rais ajaye ni lazima awe mkristo?

Rais ajaye ni lazima awe mkristo?

Udini ni pale tu mkristo akitajwa kuchukua nafasi ya juu?
Najua nyie ndo wale mnaopigia chapuo ishu ya uzanzibari na ujana kwa kuwa mtanufaika na hizo sifa.
Mnamuunga mkono January na Zitto kwenye ishu ya ujana kwa vile tu ni wenzenu ila hoja hii angeianzisha John ama Hosea ama mwingine mwenye kufanana kwayo mngeandamana kuwa hii ishu ni ya ubaguzi kupitiliza.
Tambueni kuwa hakuna mwenye hati miliki na nchi hii,si nyie wala wakristo
Heshimuni taratibu zinazoleta usawa baina ya watanzania.

Kipuyo,

Hapo ndio unapokosea usawa mnataka katika Urais tu mbona HAMTAKI USAWA KATIKA UTENDAJI AMBAPO ASILIMIA 90 MMEJAZANA WAKRISTO ???? Kama sio udini ni nini kinachowasumbua? Na nyote wafia udini hamlizungumzii hili mnalifumbia jicho ndio maana nikawaambia tuondoleeni uduwanzi wenu mtaliharibu taifa kwa propaganda zenu Za udini.
 
Mkuu umeandika maneno ya maana sana, lakini unfortunately, hali halisi haiko hivyo!

Labda kama unadhani tumepata marais wa dini za tofauti kila awamu kwa bahati mbaya?

Hilo hatuwezi kulikwepa mkuu!

It is an unwritten rule! Akija rais muislam awamu ijayo lazima kutakuwa na maneno!
NAUNGA MKONO HOJA..
MWANZO ALIKUWA BABU MZEE JULIUS.. MGALATIA TOKA BARA TANGANYIKA AMEKALIA 25YRS MJENGONI
AKAJA MZEE RUKHSA NI MUSLIM KUTOKA ZANZIBAR AMEKAA MJENGONI 10YRS
AKAMPISHA MZEE BEN MGALATIA PIA KUTOKA BARA, 10YRS MJENGONI.
hapa sasa ndio wakachemsha kidogo ila kidini style iliendelea vilevile.
WAMEMUWEKA MKUU WA KAYA (------) NI MUSLIM KUTOKA BARA MJENGONI 10YRS.
So anaefuatia lazima LAZIMA LAZIMA awe MGALATIA. PIGA GALAGAZA LAZIMA MGALATIA NDIO AKALIE MJENGONI.
Ila hapa mtihani wake unakuja hiviii... huyu MGALATIA ni lazima atoke ZANZIBAR ili kunusuru MUUNGANO FEKI HUU.
Hawa wabara wanaojinadi kuchukua nafasi ya MKUU WA KAYA wanapoteza muda tu.
kiukweli 2015 utakuwa ni mwaka mchungu sana kwa CCM hii ni kutokana na usanii mwingi walioachiwa na mzee JULIUS wa kuifanya tanganyika isiwepo tena na kuidanganya znz ijione kuwa na yenyewe ina srikali yake kumbe ni changa la macho hakuna serikali bali ni kikundi tu kwa ajili ya kupotezea wazanzibar lengo wasijitambue kuwa wamemezwa na tanganyika ndani ya TANZANIA.
MUUNGANO.jpg
 
Udini unapofusha sana, kwakuwa sina hakika kama mwanzisha mada alitegemea majibu haya kwa swali lake! Ukiwa huru na udini basi jibu hapa ni rahisi... tuendelee na utamaduni huo au tuhachane nao na kisha kujenga hoja kwa mtazamo wako.

Kwa mtazamo wangu utamaduni huu hautufai tena licha ya uzuri uliokuwa nao kwa kufanikisha kuondoa dhana ya haki-miliki ya uongozi wa juu wa nchi. Ni utamaduni uliojenga taswila ya pande mbili kuona "hiki ni chetu" badala la upande mmoja kukata tamaa na kuamua "liwalo na liwe". Lakini nyakati za ufia dini zinaenda tamati ambapo watu wanaanza kuelewa malengo ya uwepo wa dini. Katika zama hizi za utambuzi haiingii akilini kuona kwamba kwa kuwa ulizaliwa Tanzania na mzazi aitwae "Joseph" au "Bakari" basi unapoteza busara ya kuongoza katika wakati fulani licha ya kipaji chako. Na vipi tuking'ang'ana na utamaduni huu kisha ikatokea chama chenye sera na matumaini ya kuwakomboa Watanzania kikasimamisha mgombea asiye wa dini ya zamu ya wakati huo? Ndio kusema tutapiga kampeni kukinyima kura?

Nakubaliana na Mushi kwamba utamaduni huu umesaidia kujenga na kudumisha amani na mshikamano wetu, lakini yatupasa kuanza kuupa kisogo kadri nyakati zinavyobadirika kwa mwongezeko wa watu wenye utambuzi wa mgawanyo wa keki ya Taifa. Tutumie njia nyingine kuhakikisha hakuna kundi litakaloona limehachwa hata kufikia kusema "liwalo na liwe" lakini sio lazima iwe uongozi wa juu wa nchi. Kumbuka Mungu alichagua manabii na wafalme pasipo kujali koo zao bali aliwajaza karama za utumishi.
 
Good point mkuu!

Ila hapo munaposema udini hautufai tena licha kuondoa dhana ya hati milki ya uongozi, halafu unasema utaratibu huo uachwe, basi ni muhimu uje na alternative solution Ili kuona kwamba amani bado inaendelea kuwepo!

Hatuwezi kusema kama watawala wote waliopita wangekuwa lets wakristo, kusingekuwa na amani, halafu bado tuwe na mawazo ya kuachana na utamaduni huo ambao pia tunakiri kwamba umetuletea hiyo amani bila kuwa na alternative!

Nina uhakika kabisa watu wenye sifa za uongozi wa nchi wanapatikana kutoka kwenye jamii yetu yenye watu wa dini tofauti na wasio na dini!
 
Nani nalosema Dr.Slaa alikuwa disqualified kwa sais aabu ya Upadre wake? au nimesema CCM walitumia sifa zake kumshusha! yaani hizo sifa ziwe mapungufu yake na ndivyo siasa zinavyochezwa. Na sii mara zote propaganda hizi humshusha mtu wengine ndio huongeza wafuasi kama Dr.Slaa kwa kila sifa mbaya walompaka CCM ndio kwanza alizoa Umaarufu zaidi.

Kesho Lowassa akigombea Urais atatazamwa sifa zake na mapungufu yake na pengine ilikuwa kosa ambalo hatukuliona ila tujifunze kesho tusimweke Sheikh wala Padre kugombea Urais pasipo kutazama mapungufu yake ktk sifa hizo.

January Makamba amekuja na Ujana kuwa sifa ya Ugombea wake na watu ama wanasiasa watamsakama ktk Ujana wake na pia zipo sifa zake ambaz wanasiasa wanajua mapungufu yake aidha iwe ktk ndoa yake ama usimamizi wake ktk madaraka alokuwa nayo. Swala hapa nalotaka kukuelewa wewe ni kwa nini umesisitiza rais ajaye lazima awe mkristu? Je ni ktk lugha za Pasco kutafuta kuwasikia wananchi watasemaje au kweli wewe unaamini Utamaduni wa kiimani lazima utumiwe ktk kupokezana Urais!.
Sifa ya kuwa expadre ikiwa ni upungufu machoni kwako, huo siyo udini?!

Maana hapo si unajaribu kuwa please wale wananchi wanaoona ukristo ama uexpadre ni jambo baya?

Sasa hao ukiwawekea rais mkristo mihula yote kutakuwa na amani?

Hivi kwanini hauwezi kabisa kuiona issue hii in many different dimensions?

Ama mnakuwa fixated kutokana na feelings?

Kiukweli ninatoa pendekezo na pia ni mada ya kuchokoza maoni for as there Is a question mark on the heading!

Ni baada ya kuona jinsi udini ulivyoongezeka, nikasema basi ni vyema tuangalie yale ambayo hayata endelea kuchochea huo moto ama cheche za udini!

Hili ni tatizo tena limekuwa sugu zaidi chini ya utawala huu wa ccm!

Mbali nakwamba ni vyema kuzingatia huo utamaduni kwa maoni yangu, pia ni vyema kuwapima wagombea hao kuhakikisha hawana sifa zitakazoleta malalimishi!

Wanapimwa kwa utendaji wao na si kihisia hisia kama ilivyotokea kwa Dr Slaa uchaguzi uliopita!

Tunadai hatuna hisia za kidini na wakati kuna viongozi waliokataliwa kwa hisia za kidini eti mukiita sifa mbaya yenye mapungufu?!

Na kama hujui mkuu, hisia za kidini ni rahisi sana kupofusha na kutokuona vilivyo wazi kabisa, just kwasababu havinasibiani na hisia zako za kiimani na machaguo yao!
 
Kipuyo,

Hapo ndio unapokosea usawa mnataka katika Urais tu mbona HAMTAKI USAWA KATIKA UTENDAJI AMBAPO ASILIMIA 90 MMEJAZANA WAKRISTO ???? Kama sio udini ni nini kinachowasumbua? Na nyote wafia udini hamlizungumzii hili mnalifumbia jicho ndio maana nikawaambia tuondoleeni uduwanzi wenu mtaliharibu taifa kwa propaganda zenu Za udini.
usawa gani katika utendaji haupo?

Acha utoto na udini.Kwahiyo rais akiendelea kuwa muislam ndo atasaidia kuwaondoa hao wakristu asilimia 90 kwenye utendaji? Wewe ndiyo duwanzi mdini mkubwa!
 
usawa gani katika utendaji haupo?

Acha utoto na udini.Kwahiyo rais akiendelea kuwa muislam ndo atasaidia kuwaondoa hao wakristu asilimia 90 kwenye utendaji? Wewe ndiyo duwanzi mdini mkubwa!

Simplicity,

Wewe si mzima? Naona unatoka mapovu pointless. Mdini mwenzio anadai kuna utaratibu wa kupokezana 50:50 . Yaani miaka kumi atawale mwislamu then ikisha aje mkristo. Kama utaratibu uko hivyo basi baraza la mawaziri liwe 50:50 badala ya iliyokuwa sasa na siku zote 75% wakristo asilimia 20% Muslim 5% wapagani.
Ikisha tuendelee na mgawanyiko huo huo katika taasisi za u mma 50:50 .

Kama hamlitaki hilo sasa mnalia lia nini kuleta hoja za kiduwanzi ati sasa zamu ya wakristo bila ya kujali a nasimamia misingi gani ya uongozi. Huo ni ujinga na uduwanzi wa hali ya juu.
 
wewe ni mdini.Ndo maana hutaki tupate viongozi kama utaratibu wetu wa kawaida ulivyo!

Sioni jambo la tofauti hap hadi utoe povu.Imekuwa hivyo toka awamu ya kwanza.Mdini mkubwa wewe!
 
wewe ni mdini.Ndo maana hutaki tupate viongozi kama utaratibu wetu wa kawaida ulivyo!

Sioni jambo la tofauti hap hadi utoe povu.Imekuwa hivyo toka awamu ya kwanza.Mdini mkubwa wewe!

Aha

Kwahiyo utaratibu upi unaodai wewe upo? Utaratibu wa kupishana baina ya wakristo na waislamu katika Urais haukuwapo uliokuwapo ulikuwa utaratibu wa kupishana baina ya bara na Zanzibar. Huo unaweza kuwa na mantik ni JK aliyekuja kuuharibu. Sasa mnaleta propaganda zenu Za kidini kudai ati sasa zamu ya wakristo.

Ndio maana nikawauliza kwa hoja ipi? Mmeshindwa kujibu kwasababu kama ni kupokezana basi kwenye utendaji pia tupokezane kama iliyokuwa katika Urais. Badala yake mmejazana wakristo na mnaona ni haki yenu hata kama Mmeshindwa kazi. Huo ndio udini wenyewe wadini wakubwa tunataka Rais mzalendo., msafi na mchapakazi na sio mdini mwenzenu. Tutoleeni pumba zenu hapa
 
Mkuu acha kuingiza hisia na hasira sasa unataka kuharibu thread ya kazi gani? Kwani huoni ni swali?

Hapa siyo pahala pa hoja za wakristo vs waislam, maana kwanza huo utamaduni nadhani ni mzuri kwasababu ya watu kama nyie?na hoja zenu kama hizi?
 
Mushi,

Huku ni kuishiwa hoja nimekuuliza swali kama unataka kupokezana vijiti basi mbona vijiti hatupokezani serikalini ktk utendaji? Mbona serikalini hakuna uwiano wa waislamu na wakristo? . Unakimbia kivuli chako mwenyewe wakati wewe ndio umeianzisha mada ukashindwa kuitetea? Na kwanini serikali inakigugumizi na madai ya mfumo kristo?

Acheni udini mkuu tujenge nchi. Tutafute kiongozi mwenye sifa nilizotaja katika post yangu iliyopita. Hivi ngoja nikuulize swali dogo akigombea Urais mfano kati Dr Salim Ahmed Salim na EL nani utamchagua?
 
Hilo la uwiano si mulishalianzishia threads sijui za mfumo kristo?

Sasa wewe unataka kureplace na mfumo kristo n mfumo gani? Two wrongs can not do one right! Soma sentensi yangu ya mwisho kabisa kwenye bandiko langu la kwanza!

I simply don't believe it was a coincidence ama sijui kubadilishana na Zanzibar.

Na kama wewe una wagombea wako, samahani sana mimi sina mgombea! Ofcourse nitamchaguwa Dr Salim btn him and EL!

Hapa siyo ubishani wa kidini, ni mjadala tu ambao umebeba maoni na masuali, pamoja na tafakuri kuhusiana na mfumo na utamaduni ama desturi zinazotupatia viongozi.

Sasa hii ni hoja tu halafu hisia hivi? As if mimi ndo pekee ninayechaguwa rais?

Halafu unasema eti nakimbia? Wewe unaweza kunikimbiza kwa lipi? Hapa jf wewe unikimbize? Please mkuu!
 
Si lengo la thread hii kusema kuwa dini flani ndo kigezo cha urais kama vile wale wa kigezo cha ujana wanavyofanya.

Mbali na hayo, chini ya taratibu zetu ndani ya awamu nne, hatujawahi kuwa na marais wawili mfululizo wenye imani moja!

Kwa utaratibu huo, ni wazi kuwa sasa ni muhimu tukapata kiongozi mwenye imani ya tofauti, inaweza ikawa hata mpagani!

Kwa maoni yangu, hypothetically, si vyema kureplace malalamishi ya mfumo wa imani moja kwa kuupachika mfumo wa imani nyengine.
Mkuu jmushi, japo ni kweli, ila hili lilitokea by a chance tuu, hakuna utaratibu huo!.

Kwenye mada yangu Sumu ya Siasa za Udini, Ukanda na Ukabila, "Is It Real?,

nilisema hivi
Wanabodi nauliza, hii sumu ya siasa za udini, ukabila na ukanda are they real au ni dhana tuu?!.

Jee Watanzania si wana dini zao?, jee kuna ubishi kuwa alipoanza rais Mkristu, JK Nyerere, alipoondoka Mwinyi aliingia tuu by chance?. No miongoni mwa sababu za Mwinyi kuingia ni pamoja na dini yake, this is a fact!. Alipoondoka Mwinyi sialiingia Ben, inamaana aliingia tuu by a mare chance and by chance akawa ni Mkiristu na alipotoka JK nae akaingia by mare chance, na by chance akawa ni Mwislam?. Tutake tusitake, kuna kupokezana hata kama ni by chance, then tuendelee ku play by chance?. Kwenye uchaguzi uliopita kuna vyama vilipata kura nyingi maeneo ya dini fulani, and this is a fact!. Kuna taasisi na makundi ya watu wali waendorse wagombea fulani kutokana na dini zao!. This is fact!. Jee hii ni dhana ya udini tuu au ndio ukweli wenyewe?

Jee mbegu hii ya sumu kaipanda nani?, jee tunaweza kuipiga vita kwa kuikanusha tuu (denial) au tunatakiwa kuubali ukweli mchungu na kukabiliana nao (facing the problem)!.

Nauliza tuu?

Pasco

Na kwenye mada yangu hiiKete ya Dhana ya 'Zamu za Kupokezana' ina turufu yoyote Katika Urais wa JMT?!.

nilisema hivi

Vivyo hivyo kwenye hili la udini, Tanzania ni secular state, serikali haina dini, ila watu wake wana dini zao!. Rais nchi hachaguliwi na serikali isodini, bali huchaguliwa na watu wenye dini zao!. Jee kuna uwezekano, wa dini ya mgombea urais kuwa ni moja ya vigezo, vitakavyomfanya achaguliwe?!.

Japo haijaandikwa popote kuwa urais unapatikana kwa kupokezana kwa zamu, kati ya Wakristu na Waislamu, ila ni ukweli halisi kuwa by coincidence tuu Nyerere alikuwa Mkristo, akafuatiwa na Mwinyi, Muislamu, then Ben, Mkiristo, akaja JK Muislamu, hivyo 2015 coincidence inapaswa ku play in favour ya ni zamu ya Mkristo? If we don't break it!.

Vivyo hivyo hata kama imetokea rais wa kwanza akawa ni Mkristu, akafuatiwa na Muislamu, then akaja Mkristu, na sasa aliyepo ni Muislamu, kwa vile hakuna utaratibu rasmi wa kupokezana, ili kuundoa mfuatano huo wa coincidence tuu, mnaonaje kama rais ajaye awe Muislamu tena, na tena this time atoke Zanzibar, ili kupunguza marais wa kutoka bara tuu ndio wafuatane, yaani Mkapa alitoka bara, JK ametoka bara, na 2015 mnataka kutuletea tena rais wa kutoka bara?!, huu utakua kweli ni muungano wenye haki na usawa?!.

Tukikubali to break the circle, ya urais hakuna kupokezana, wala hakuna zamu, pia tunaweza ku break kale ka secret code kuwa amkiwa Mkristo basi ni lazima awe wa dhehebu fulani!, yaani tujiaminishe kuwa kuwa rais alipokuwa Juliasi, it just happened kuwa pia alikuwa ni Mkatoliki, na alipokuja Bunyamini, pia it just happened alikuwa Mkatoliki, hivyo hata akija Membe ambaye ni Mkatoliki, it will be "just happened!", can't we break the "just happened!", kwa kuhakikisha wengine wenye uwezo nao pia wanakuwepo kwa kuthamiria to break the circles za just happened?!.

Yaani Tanzania tuendelee kuchagua rais kwamare coincidence kuwa it just "happened" au tudhamirie kumchagua rais kwa sababu?!.
Kwa vile hizi ni dhana tuu ila pia ndicho kilichotokea, ili kusimamisha dhana hii isiendelee na kugeuka "grund norm" haujafika wakati sasa, lazima tufike mahali tuamue by affirmative actions against dhana hizi kwa kuchagua the contrary ?!.

Pasco
 
Swala hapa nalotaka kukuelewa wewe ni kwa nini umesisitiza rais ajaye lazima awe mkristu? Je ni ktk lugha za Pasco kutafuta kuwasikia wananchi watasemaje au kweli wewe unaamini Utamaduni wa kiimani lazima utumiwe ktk kupokezana Urais!.
Lile swali langu kule lilikuwa valid, niliuliza a very simple questions kuwa Ikiwa ni kweli kuna wakati rais wa Tanzania ni lazima awe Mkristo, jee Mkristo huyo ni lazima awe ni Mkatoliki?!, hii ni kufuatia marais Wakristo wote waliotangulia walikuwa Wakatoliki. Japo Mode wameifuta ile thread!, lakini concern yangu was genuine na itakapotokea 2015 atakayepita ni Mkatoliki tena for whatever reasons, tutaamini hiyo ndio grund nome ya urais wa JMT and this time around, hatutakubali!, kama ni zamu ziwe zamu za haki kwa pande na sio zamu za upande fulani tuu! ndio maana nimeshauri hizi zamu tuzifutilie mbali!.
Pasco
 
Kipuyo,

Hapo ndio unapokosea usawa mnataka katika Urais tu mbona HAMTAKI USAWA KATIKA UTENDAJI AMBAPO ASILIMIA 90 MMEJAZANA WAKRISTO ???? Kama sio udini ni nini kinachowasumbua? Na nyote wafia udini hamlizungumzii hili mnalifumbia jicho ndio maana nikawaambia tuondoleeni uduwanzi wenu mtaliharibu taifa kwa propaganda zenu Za udini.

Utendaji unaendana na Elimu.Umeshafanya Tathmini ya shule za Sekondari na Vyuo ambavyo wakristo wanavyo ukilinganisha na Waislamu?.Umeshafanya Tathmini ya kuona ni Wakristo na waislamu wangapi wako kwenye Mashirika Makini ya kimataifa na yale ya Kibinafsi ambayo Udini hauna nafasi?.Nyie endeleeni na Kampeni za Kisiasa Misikitini ila mwisho wa Siku mtajikuta mmejaa kwenye Siasa lakini Vichwani Zero.
 
Mkuu jmushi, japo ni kweli, ila hili lilitokea by a chance tuu, hakuna utaratibu huo!.

Kwenye mada yangu [h=3]Sumu ya Siasa za Udini, Ukanda na Ukabila, "Is It Real?,[/h]nilisema hivi

Na kwenye mada yangu hii[h=3]Kete ya Dhana ya 'Zamu za Kupokezana' ina turufu yoyote Katika Urais wa JMT?!.[/h]
nilisema hivi

Kwa vile hizi ni dhana tuu ila pia ndicho kilichotokea, ili kusimamisha dhana hii isiendelee na kugeuka "grand nome" haujafika wakati sasa, lazima tufike mahali tuamue by affirmative actions against dhana hizi kwa kuchagua the contrary ?!.

Pasco

Pasco,

That is my point as well tukiyaacha haya makitu yakaendelea wallah maendeleo nchi kamwe hayatakuja. Na sio tu udini hata kuamini kiongozi bora anatokana na ccm au chadema au cuf. Kwasababu ukiniambia mie kama Wapo wengi nje wanaweza kutufaa mfano mbatia au mengi au hata mufuruki. But tunapofushwa na vyama na tukiendeleza hizi desturi zitageuka kuwa grund norm na itakuwa imekula kwetu.
 
Back
Top Bottom