Rais ajaye ni lazima awe mkristo?

Rais ajaye ni lazima awe mkristo?

Hilo la kanisani hakuna aliyelidhibitisha zaidi ya maneno ya walioungana kutokana na dini zao(cuf na ccm) ila kampeni misikitini lilikuwa wazi na halihitaji proof kwa kuwa spika za sauti zilikuwa zinasikika kila kona pale penye misikiti na la pili Lipumba mwenyewe kadhibitisha alipokuwa akihubiri siasa misikitini na video yake ipo hapa hapa jf.Mbona hili hulisemi?au nyie mnataka kuligeuza taifa hili kuwa Iraq?

Nyie mlikuwa mnapiga kampeni kanisa hadi kanisa JK akataliwe kwa bahati mbaya waislamu na wasiokuwa waislamu but wenye nia njema na taifa letu wakastukizia mpango wenu mchafu wa kulazimisha kumuingiza padiri wenu ikulu sasa mmekuja kivingine ati ni zamu ya wakristo utadhani dini ndio kigezo kikuu cha uongozi hamna lolote zaidi ya UDINI TU UNAOWASUMBUA.

Wewe na wengineo hamna lengine zaidi ya udini unaowasumbua tu tuachieni taifa letu tuishi kwa amani!!!
 
Mkuu,

Nikuulize swali haya mabalaa ya Chadema ya usimamizi mbovu wa pesa, kujiuzia magari mitumba kwa bei juu, ufisadi wa fedha za wafadhili wa ndani na nje? kujilipa posho badala ya mshahara vyote hivyo hivyo unaona ni sahihi? Au kwa vile ni padiri ndio unaona huruhusiwi kuuliza mambo anayoyafanya mtendaji mkuu wa chama chenu? Maana wafuasi wa chadema ni wafuasi wa utopian leadership. Binafsi sioni tofauti kati yake na EL au Rostam. Sema fursa zinazidiana kama anakubali kulipwa posho isiyokatwa kodi wala kuulizwa na wanachama atakubali kwenda kula mihogo ikulu.

Tusidanganyane bana fumbo mfumbie mjinga mwerevu hustukia dili.
Dr Slaa siyo fisadi bana! Mbona ilibidi waingize udini 2010? Na tena kuna wanaoamini uchaguzi haukuwa huru na wa haki!

Huo ufisadi wake ungekuwepo wasingekuwa na haja ya kutumia udini 2010!

Na kwa utaratibu huu unaouzungumzia, ccm inastahili kutoa mgombea kweli? Maana kuhusu ufisadi wa ccm sijui tuanzie wapi tuishie wapi?
 
Kwani raisi huwa anapatikana kwa kuzingatia dini au wingi wa kura za wananchi? samahani lakin naomba kufahamishwa juu ya hilo wakuu
 
Nyie mlikuwa mnapiga kampeni kanisa hadi kanisa JK akataliwe kwa bahati mbaya waislamu na wasiokuwa waislamu but wenye nia njema na taifa letu wakastukizia mpango wenu mchafu wa kulazimisha kumuingiza padiri wenu ikulu sasa mmekuja kivingine ati ni zamu ya wakristo utadhani dini ndio kigezo kikuu cha uongozi hamna lolote zaidi ya UDINI TU UNAOWASUMBUA.

Wewe na wengineo hamna lengine zaidi ya udini unaowasumbua tu tuachieni taifa letu tuishi kwa amani!!!
Mkuu umejificha sana lakini imekuwa shida?

Walikuwa wakitaka kumuingiza padiri wao? Kumbe hayo ya kusema ufisadi ni kujificha nyuma ya udini!?Nani alikwambia anakwenda kuswalisha ikulu?

Ama hujui pia kuwa umeshaonyesha chuki za wazi kabisa za kidini halafu ndo unasema kusiwe na kupokezana?nimekuuliza endapo marais wote waliopita wangekuwa wakristo kungekalika?

acha utani bana.
 
Kwani raisi huwa anapatikana kwa kuzingatia dini au wingi wa kura za wananchi? samahani lakin naomba kufahamishwa juu ya hilo wakuu
Anategema kura za wananchi baada ya kuteuliwa ama kuchaguliwa na chama chake kukiwakilisha kwenye uchaguzi mkuu!

Other than that awe mgombea binafsi endapo inaruhusiwa!

Bottomline ni uwingi wa kura za wananchi, lakini wenye chama wanaangalia maoni ya wananchi kabla ya kuchaguwa mwakilishi wao.Hili linawasaidia kwenye kuwanadi kwa wananchi.
 
Umesema "siasa ni mchezo mchafu, Slaa alikuwa Padri, ccm wakatumia hilo kwenye kampeni dhidi yake"

Nikakuuliza hukuona kuwa huo ulikuwa udini?Maana ulikuwa ukiipinga hoja ya GODLOVEME kwamba huo ulikuwa udini, wewe ukasema ni kwasababu ilitokea Slaa alikuwa padri ndo maana ccm waliweza kuitumia hiyo hoja!

Si unaona jinsi watanzania tulivyo?

Ndo nikashangazwa na hao ccm na wenye kuamini hivyo,, nikauliza tena anaenda Ikulu kusalisha?
Nashindwa kukuelewa tena maana unavyosema ktk mada hii ni kama ungetaka Dr.Slaa achaguliwe ili aende Ikulu kusalisha (kutumia itikadi na sera ziwe za kidini kusisitiza ya imani yake maana ndio utamaduni wake). Na kama hukubalini na hili, kwa nini unataka dini itumike kumchagua rais ajaye ikiwa hukuyaona hayo kwa Dr.Slaa? Na kama hutaki rais atumie utamaduni wake wa kiimani kwa nini iwe sifa ya wewe unasisitiza kwa mada hii rais ajaye lazima awe Mkristu!
Sijakuelewa bado...
 
Mods nyuzi kama hizi ni za kufutilia mbali bana, mambo gani haya tunataka viongozi bora , mambo ya udini udini ni upuuzi tu, Mods hata kama hamuzi kuifuta hii nyuzi ihamishieni jukwaa la dini humu haistahili kuwepo.

duh unatoa mapovu, we muislam nini?
 
Nashindwa kukuelewa tena maana unavyosema ktk mada hii ni kama ungetaka Dr.Slaa achaguliwe ili aende Ikulu kusalisha (kutumia itikadi na sera ziwe za kidini kusisitiza ya imani yake maana ndio utamaduni wake). Na kama hukubalini na hili, kwa nini unataka dini itumike kumchagua rais ajaye ikiwa hukuyaona hayo kwa Dr.Slaa? Na kama hutaki rais atumie utamaduni wake wa kiimani kwa nini iwe sifa ya wewe unasisitiza kwa mada hii rais ajaye lazima awe Mkristu!
Sijakuelewa bado...
Mkuu hilo ni suali nililowauliza wale mlosema kuwa kwasababu alikuwa padri, basi alikuwa dissqualified!

Pia katika mada hii, sijataja popote kuwa nataka fulani ama fulani ndo awe rais!Ni udadisi wangu tu uliopeleka kutoa maoni haya kutokana historia ya taifa letu!

Nikazi gatia kabisa utamaduni wetu ninaoamini umetusadia kuipreserve amani tuliyo nayo! Tena cha msingi kabisa, heading ya thread nimeweka kama suali tu!

Wenye wagombea wao, wamejitia upofu na kuanza kupanic! Sasa visi gio vikishaisha, watajidai hawaelewi.
 
Sisi wapagani ni zamu yetu kutoa rais..
Wapagani huwa hawana shida kama hizo! Utakuwa mpagani feki wewe!

Mpagani namfahamu humu ni Kiranga! Wewe unazungumza kuharibu mjadala tu!
 
Last edited by a moderator:
Wapagani huwa hawana shida kama hizo! Utakuwa mpagani feki wewe!

Mpagani namfahamu humu ni Kiranga! Wewe unazungumza kuharibu mjadala tu!

kwani unanijua mkuu? mimi ni mpagani original
 
Last edited by a moderator:
Mkuu hilo ni suali nililowauliza wale mlosema kuwa kwasababu alikuwa padri, basi alikuwa dissqualified!

Pia katika mada hii, sijataja popote kuwa nataka fulani ama fulani ndo awe rais!Ni udadisi wangu tu uliopeleka kutoa maoni haya kutokana historia ya taifa letu!

Nikazi gatia kabisa utamaduni wetu ninaoamini umetusadia kuipreserve amani tuliyo nayo! Tena cha msingi kabisa, heading ya thread nimeweka kama suali tu!

Wenye wagombea wao, wamejitia upofu na kuanza kupanic! Sasa visi gio vikishaisha, watajidai hawaelewi.
Nani alosema Dr.Slaa alikuwa disqualified kwa sababu ya Upadre wake? au nimesema CCM walitumia sifa zake kumshusha! yaani hizo sifa ziwe mapungufu yake na ndivyo siasa zinavyochezwa. Na sii mara zote propaganda hizi humshusha mtu wengine ndio huongeza wafuasi kama Dr.Slaa kwa kila sifa mbaya walompaka CCM ndio kwanza alizoa Umaarufu zaidi.

Kesho Lowassa akigombea Urais atatazamwa sifa zake na mapungufu yake na pengine ilikuwa kosa ambalo hatukuliona ila tujifunze kesho tusimweke Sheikh wala Padre kugombea Urais pasipo kutazama mapungufu yake ktk sifa hizo.

January Makamba amekuja na Ujana kuwa sifa ya Ugombea wake na watu ama wanasiasa watamsakama ktk Ujana wake na pia zipo sifa zake ambaz wanasiasa wanajua mapungufu yake aidha iwe ktk ndoa yake ama usimamizi wake ktk madaraka alokuwa nayo. Swala hapa nalotaka kukuelewa wewe ni kwa nini umesisitiza rais ajaye lazima awe mkristu? Je ni ktk lugha za Pasco kutafuta kuwasikia wananchi watasemaje au kweli wewe unaamini Utamaduni wa kiimani lazima utumiwe ktk kupokezana Urais!.
 
Sijawahi kuwa na dhana hii kichwani.siku zote nimekuwa na mtazamo mwingine tofauti na dini.ni baada ya kusoma thread hii ndio nimekumbuka kumbe marais wetu waliopita ni wakatoliki na waislam.aisee,hivi mnatujenga au mnatubomoa?manake mie si wa dini hizo ila sijawahi kuwaona "wao wakatoliki na waislam" ila Pasco umenitia sumu aisee,sijui nimeingilia nini huku jukwaani aaargh,ngoja nilog off!
 
Mkuu umejificha sana lakini imekuwa shida?

Walikuwa wakitaka kumuingiza padiri wao? Kumbe hayo ya kusema ufisadi ni kujificha nyuma ya udini!?Nani alikwambia anakwenda kuswalisha ikulu?

Ama hujui pia kuwa umeshaonyesha chuki za wazi kabisa za kidini halafu ndo unasema kusiwe na kupokezana?nimekuuliza endapo marais wote waliopita wangekuwa wakristo kungekalika?

acha utani bana.

Mushi,

Hoja yako ni mfu na sasa unataka kudeviate attention kwa vile umeshindwa kutetea hoja yako. Nimekuambia kuwa dini sio kigezo cha msingi na kama itatumika 2015 italeta changamoto kwasababu hadi sasa Serikali imeshindwa kujibu hoja ya waislamu kuhusu mfumo kristo. Na hii imetokana na kwamba katika serikali na mataasisi yake watendaji na viongozi wake wengi ni wakristo kuanzia cabinet hadi kwenye mashirika na taasisi nyenginezo. Ilihali wasomi wa kiislamu wapo ila kuna nepotism ya hali ya juu inaendelea.

Pili ni ukweli usiopingika kanisa lilikuwa linataka Padiri Slaa aingie Magogoni kama unakumbuka kulikuwa na kampeni kila jumapili makanisani yakitolewa matamko ya kuwataka waumini wasimwangalie mtu tabia zake bali waangalie misingi anayoisimamia. Wakilenga kwamba wasiangalia Slaa anaishi na mke wa mtu bali waangalia anapigania maswala gani ya msingi kwa jamii. Vile vile kuna kanisa mmoja kama sikosei liliwafukuza waumini wake kwa kupinga amri ya kasisi ya kuwataka wakipigie kura chama cha padiri ikawa mzozo mkubwa.

Mushi usijifiche bana mbona watendaji wakuu kuanzia Serikali 1,2 3 4 wote karibia 80% wamekuwa wakristo na tumeendelea kuishi bila ya matatizo sembuse rais? Au unadhani urais ni mtu mmoja? Sasa kama 90% ya Serikali imejaa wakristo na waislamu wameishi na kuvumilia watashindwa kuongozwa na rais mkristo?

Acha Propaganda zako mkuu. Tujenge taifa letu na sio kuamsha vitu visivyo na msingi.
 
Dr Slaa siyo fisadi bana! Mbona ilibidi waingize udini 2010? Na tena kuna wanaoamini uchaguzi haukuwa huru na wa haki!

Huo ufisadi wake ungekuwepo wasingekuwa na haja ya kutumia udini 2010!

Na kwa utaratibu huu unaouzungumzia, ccm inastahili kutoa mgombea kweli? Maana kuhusu ufisadi wa ccm sijui tuanzie wapi tuishie wapi?

Dr Slaa sio fisadi basi arudishe posho za milioni 7 anazopokea na badala yake apokee mshahara kama watu wengine na alipe kodi. Vile vile arudishe stahiki zote ili ajitofautishe na mafisadi wengine kwa kuwa mfano akiishi maisha ambayo sisi watanzania wengine tunaishi.

Pili arudishe hela zote zilizotafunwa kwenye ruzuku na pia chama kiwe na account yake badala ya kuwa ruzuku inapitia katika account ya mtu binafsi.

Tatu atuambie ni vp mbowe ameweza kumdanganya yeye kama mtendaji mkuu akauziwa migari mtumba bei ya mara mbili ya gari mpya na kwanini wanaendelea kukodi nyumba ya muasisi hadi leo badala ya kujenga nyumba yao.

Ndio maana narudia ni fisadi hamna tofauti na wengineo ila tofauti ni kuzidiana kwa fursa na kama wanayafanya haya kwenye chama wakifika magogoni si ndio watauza hadi fanicha???

Tafuteni mwengine but sio Slaa na kwakweli sijamuona bado Chadema labda Mnyika kama mmeishiwa kabisa.....
 
Wapagani huwa hawana shida kama hizo! Utakuwa mpagani feki wewe!

Mpagani namfahamu humu ni Kiranga! Wewe unazungumza kuharibu mjadala tu!

Enzi hizi za elimu mpagani ni yule anayetumia neno "mpagani" rejareja.
 
Last edited by a moderator:
Mkristo Pombe Magufuli mimi naona atatufaa sana ninaan dika hivi kama muislam ninayeoona mbali sana,huyu jamaa mbali na dini au kabila yake naamini atakuja tufikisha mbali sana watanzania hawa wengine sijui akina Makamba na wengineo ni wababaishaji watupu wanaweza kutuletea sokomoko moja baya sana hapa nchini ila kuna suala la kiongozi kuwa mtu tough sana hilo nalo ni lazima tulitupie macho sana kwani hivi sasa katika maeneo yetu ya hapa afrika mashariki maadui zetu wanazidi kujipanga na wote dua zao kubwa ni kuona tanzania inasambaratika kwa namna yeyote ile kwa hiyo tunahitaji tumpate rais ambaye ataweza kuja pambana na hizi changamoto za namna hii na pia awe mbabe wa aina fulani hivi asije chezewa na vimtu kama vile akina kagame na kundi lao zima huyo ajaye ni lazima awe mtu makini sana hii amani tuliyonayo ndio sababu kubwa ya kuchukiwa na majirani zetu wengi makwao wenzetu wanauana ka kuku kwa visababu vidogo vidogo tuu.Amani yetu ni lazima tuilinde kwa nguvu zote.
 
Nyie mlikuwa mnapiga kampeni kanisa hadi kanisa JK akataliwe kwa bahati mbaya waislamu na wasiokuwa waislamu but wenye nia njema na taifa letu wakastukizia mpango wenu mchafu wa kulazimisha kumuingiza padiri wenu ikulu sasa mmekuja kivingine ati ni zamu ya wakristo utadhani dini ndio kigezo kikuu cha uongozi hamna lolote zaidi ya UDINI TU UNAOWASUMBUA.

Wewe na wengineo hamna lengine zaidi ya udini unaowasumbua tu tuachieni taifa letu tuishi kwa amani!!!

Udini ni pale tu mkristo akitajwa kuchukua nafasi ya juu?
Najua nyie ndo wale mnaopigia chapuo ishu ya uzanzibari na ujana kwa kuwa mtanufaika na hizo sifa.
Mnamuunga mkono January na Zitto kwenye ishu ya ujana kwa vile tu ni wenzenu ila hoja hii angeianzisha John ama Hosea ama mwingine mwenye kufanana kwayo mngeandamana kuwa hii ishu ni ya ubaguzi kupitiliza.
Tambueni kuwa hakuna mwenye hati miliki na nchi hii,si nyie wala wakristo
Heshimuni taratibu zinazoleta usawa baina ya watanzania.
 
Back
Top Bottom