Rais ajaye ni lazima awe mkristo?

Rais ajaye ni lazima awe mkristo?

nakukumbuka malalamiko
ya udini serikalini yalishamiri sana wakati wa mwinyi. kinara wa agenda
ya kupromote uislam badala ya uzalendo wa nchi alikuwa kighoma malima.
anakumbukwa kufikia kugeuza misikiti baadhi ya vyumba vya majengo ya
wizara alizokuwa waziri. wakati wa mkapa hali ilitulia. kuja kikwete
uislam / ukristo imekuwa balaa, mpaka wachungaji wamechinjwa, makanisa
kulipuliwa, mihadhara ya kiislam ya kueneza chuki imeshamiri, nk. kwa
hiyo akifuata rais mwislam tutegemee mwendelezo wa haya?

mbona husemi na mashehe waliomwagiwa tindikali.? try to balance the story
 
kituru, hoja ya msingi ni kwamba uvunjifu wa amani unaotokana na hujuma mbalimbali dhidi ya ukristo umeshamiri sana wakati wa kikwete na haukemewi. hii inaleta picha kwamba yote haya yana baraka za wakubwa. kwamba kuna mashehe walimwagiwa tindikali je mlijua waliofanya hivyo na kwa nini?
 
Sielewi kwa nini mods wanaruhusu mijadala ya kipumbavu yenye kutaka kuchochea kuni kwenye ule moto ulioanza kufukuta 2010. Mleta mada cjui kam unajua madhara ya hiki ki2 ulicholeta au unadhani ni jambo la kawaida?? Kwani huyo Rais akiwa wa dini yako atakusaidia nn? Nambie waislam wanapata nn kwa Jk na wakristo walipata nn kw Mkapa. Acheni ujinga fanya kaz upate mahela cyo kutegemea kubebwa bebwa.
 
Mkuu uhuru niliokuwa ninauzungumzia uko ndani ya mipaka ya tamaduni zetu!

Ushoga si utamaduni wetu!Na pia si utamaduni wa mwafrika kwa ujumla!

Na ndiyo maana hata Obama amepoteza sana umaarufu miongoni mwa waafrika!

Kwenye thread hii, ninazungumzia utamaduni tulioko nao ambao umedumisha amani, mshikamano pamoja na umoja wetu, mambo ambayo nchi kedekede Africa na duniani kwa ujumla wanayaonea gere!

Mkuu soma kwa upole na utulivu kabisa bila hisia wala jazba!

Utamaduni unaousema hata kama upo ni mzuri hatutaki uwe sheria, kama upo aja uwepo kuanza kuujadili ni kuanza tupige kura kwa udini. Ushindwe
 
Baada ya dini tutaingia madhehebu, badae makabila tunamalizia na vita tunahamia ukimbizini basi. Mwenye huu uzi ana matatizo ya kidini. Aende kanisani/mskitini atatibiwa huko kisiasa hakuna tiba ya ugonjwa wake
 
Nashangaa mod sijui anasubiri nini kuacha posts za uchochezi namna hii
 
na sisi ambao tuna imani zetu za kimila mbona hatulalamiki? jaribuni kua wazalendo
 
Wala mimi siko huko isipokuwa hizi habari za kumchagua rais kwa sababu ni Kijana/Mzee au Mkristu/Muislaam inanipa mashaka sana na akili zetu.

Kiongozi kama rais ana sifa zake. Ni kiongozi ambaye anatambua tofauti zetu na umuhimu wa nila na tamaduni ambazo zimetuweka sisi kuwa wamoja kwa miaka 50 na Taifa gani tunataka kulijenga. Sasa unapopongeza utukufu unaotazama mtengano wa kiimani hizo tamaduni kuwa kigezo hapo ndipo naposhindwa kuelewa. Na ujue fika kwamba kuna tofauti baina ya Leadership na Management iwe kwa sifa ama malengo.

Hakuna adui mkubwa wa umoja wa watu kama kuendeleza tofauti zao na ndiomaana Nyerere alisisitiza kufuta Ukabila. Na pengine niseme tukitoka katika Ukristu kesho Hao hao wakristu watadai tunahitaji rais Lutherani au Protestant kwa sababu kila rais aliyepita alikuwa Mkatoliki, Na Shia nao watakuja na lao kuhusu Sunni, Bniani na kadhalika. Yanayotokea Iraq na nchi za Kiarabu leo sii ya bahati mbaya, hawa watu kabila zao sina define Imani zao, ni watu waloshindwa kuelewa mila na tamaduni zilizowaweka pamoja badala yake wakaweka imani zao kuwa msingi wa jamii.

Hata huko India vile vile kabila ndizo zinajenga imani zao za dini na ndio maana wameishi kwa matabaka miaka yote. Pakistan, India na Bangladesh kugawanyika ilitokana na ubaguzi wa Kikabila = Dini. Hivyo nasi kuiga vitu kama hivi wakati tunaona athari zake ni kuonyesha wazi kwamba tunashindwa kusoma wakati. Kwa wenzetu wazungu Uislaam na dini nyinginezo ni wageni kwao hivyo mgeni analazimika kufuata mila na tamaduni zao japo wao ni wa makabila tofauti na imani tofauti ndani ya Ukristu.

ndio maana sisi wengine tunamwona Nyerere kama Genius kwa sababu alijaribu kuondoa Ukabila na Udini kutokana na mifano aloiona Ulaya. Mrusi aliyehamia Marekani leo anajisikia ni Mmarekani kuliko Mwafrika alozaliwa Marekani. Na ajabu Mrusi huyo huyo siku kuna mashindano baina ya Urusi na Marekani utamwona akibeba bendera vya Urusi. Tazama World cup hii jinsi Waamerika wenyewe walivyokuwa nyuma ya timu yao japo ikicheza na nchi ya asili yake anarudi kwao. Hakuna mtu alomshikia bango mwenzake wala uadui kwa sababu wanaelewa nini maana na haki za Uraia pamoja na fursa zake.

maendeleo ya watu hawa hayakuja kwa bahati mbaya bali ni kuelewa ruksa na fursa za Uraia. Kuelewa kwamba hakuna Ukabila ndani ya Marekani ila kuna taifa jipya lenye mkusanyiko wa Mataifa yote duniani na wenye vipaji na fursa ya kufikia ndoto ulokuwa nayo. Na tuseme ukweli bila woga Ujio wa Obama (sii mweusi tu bali ana asili ya Kenya, Afrika) ni ishara tosha ya Taifa waloweza kulijenga maana katoka ktk kundi la watu wachache na wanaodharauliwa kuliko mataifa yote.

Tuachane na fikra hizi za Ujana na Udini zitatupeleka pabaya zaidi..

Pongezi sana mkuuu watu wenye IQ kama zako tunawahitaji miaka800
 
Anayesema tusichague kutokana na dini nimsahihishe. Sema tusichague viongozi kutokana na majina yao waliyopewa na wazazi wao. Jina la mtu si Imani yake. Kwa maana ukisema dini, mwenye kusimama na dini anaujua wajibu wake. Kutenda haki. Tutahitaji kwanza kurudi nyuma na kurekebisha tulichokosea katika kuchagua kiongozi wa nchi.
 
Hivi Tanzania kuna udini? Au ushabiki tu, mbona kila nikiangalia list la uhalifu naona dini zinachanganyika, wizi wa mali za umma john na juma, wake za watu John na Juma. Kuuza sembe, John na Juma. Kubeba watoto wao serikalini, John na Juma. Kupokea rushwa za ngono, John na Juma. Hivi udini manake nini?
 
kituru, hoja ya msingi ni kwamba uvunjifu wa amani unaotokana na hujuma mbalimbali dhidi ya ukristo umeshamiri sana wakati wa kikwete na haukemewi. hii inaleta picha kwamba yote haya yana baraka za wakubwa. kwamba kuna mashehe walimwagiwa tindikali je mlijua waliofanya hivyo na kwa nini?

hadi tutakapokuwa 50/50 kwenye mawizara ya serikali ndo hali itatulia
 
Baada ya dini tutaingia madhehebu, badae makabila tunamalizia na vita tunahamia ukimbizini basi. Mwenye huu uzi ana matatizo ya kidini. Aende kanisani/mskitini atatibiwa huko kisiasa hakuna tiba ya ugonjwa wake

mbona madhehebu tayari! tafuta kuna uzi umeanzishwa na pasco utaona,
Rais wa Tanzania ajaye ni vema Mkristo wa
Dhehebu gani? (108) »(
 
kituru, hoja ya msingi
ni kwamba uvunjifu wa amani unaotokana na hujuma mbalimbali dhidi ya
ukristo umeshamiri sana wakati wa kikwete na haukemewi. hii inaleta
picha kwamba yote haya yana baraka za wakubwa. kwamba kuna mashehe
walimwagiwa tindikali je mlijua waliofanya hivyo na kwa nini?

mkuu haya masuala tuyadadavue kwa mapana zaidi ya kuendeshwa na msukumo wa imani zetu tutapata jawabu.
 
Jibu la swali ni "NDIYO", rais ajaye ni LAZIMA awe mkristo. Mambo ya dini, ukabila, uwezo wa kifedha nk havikutakiwa kuwa vigezo vya kumpata rais wa Tanzania. Lakini kama kumeanza kuwa na mahojiano ya kwamba rais anayefuata atatakiwa atoke Zanzibar, basi tukubali kwamba na udini utaingia tu.
 
udini ni mbaya sana kwenye utawala...hatutakiwi kupewa nafasi kabisa
 
Back
Top Bottom