Rafiki wa Mume wangu............

Rafiki wa Mume wangu............

Nimeolewa, ndoa yangu ina miaka 12 sasa hivi. Changamoto kubwa kwenye ndoa yangu ni kwamba mume wangu ni mtu wa kununa, kukasirika na kusikiliza sana marafiki. Ana rafiki yake mmoja ambaye tangu tuoane amekuwa akimsikiliza kuliko hata mimi mke wake.

Mara nyingi tukigombana, hata tukikaa na kukubaliana jambo, akienda kuongea na rafiki yake anarudi na kubadilisha maamuzi. Mwanzoni nilikuwa nakasirika, lakini baadaye nikagundua kwamba nikitaka kitu kutoka kwa mume wangu, ni bora niongee na rafiki yake. Akimshawishi, mume wangu anakubali.

Hali hiyo ilitengeneza mazoea kati yangu na huyo rafiki yake, mpaka tukajikuta tumeingia kwenye mahusiano ya kimapenzi.
Sasa mume wangu ana tabia moja, tukigombana ananifukuza nyumbani. Ananiambia, "Rudi kwenu, chukua vitu vyako!"

Mwanzoni alikuwa akinifukuza, namtafuta rafiki yake amshawishi anisamehe. Wakati mwingine naenda kwetu, nakaa siku chache, halafu narudi.

Lakini baada ya kuanza mahusiano na rafiki yake, mambo yakabadilika. Mume wangu akinifukuza, naenda moja kwa moja kwa rafiki yake. Nakaa naye hata wiki nzima, halafu tukichokana, anamtafuta mume wangu na kumwambia, "Mrudishe mke wako, sasa hivi atakuwa ameshajifunza."

Mume wangu ananikubali na mimi narudi nyumbani kama hakuna kilichotokea.
Hali hiyo imeendelea kwa miaka mingi mpaka sasa tuna watoto. Wakati mwingine hata bila kugombana, tukimissiana na huyo rafiki yake, tunapanga mpango. Mimi nafanya kakituko kidogo, mume wangu anakasirika na kumtafuta rafiki yake.
Rafiki yake anamwambia, "Huyu bado hajajifunza, mrudishe kwao kwanza!"

Mume wangu ananifukuza, mimi najifanya nimeenda kwa ndugu zangu, kumbe naenda kukaa kwa rafiki yake. Tukimaliza mambo yetu, ananishawishi nirudi kwenye ndoa yangu.

Lakini sasa hivi kumetokea changamoto ambayo imenichanganya sana!

Huyo rafiki yake anataka kuoa. Ana watoto na wanawake mbalimbali, lakini hajawahi kuoa. Mwezi ujao anafunga ndoa, kila kitu kimekamilika na matangazo ya kanisani yameshatolewa.
Sasa ameniambia kwamba kabla hajaoa, anataka nimzalie mtoto wa kumbukumbu!

Anasema akishaingia kwenye ndoa atakuwa bize, hatutakuwa tena na uhuru wa kukutana kama zamani. Kwa hiyo anataka nibebe mimba yake ili tubaki na kitu cha kutukumbusha mahusiano yetu.

Ukweli ni kwamba mimi pia natamani sana kumzalia, lakini nina wasiwasi. Hivi nikikubali kubeba mimba ya rafiki wa mume wangu, kweli haitaleta matatizo baadaye?

👇👇👇👇👇👇👇👇

(Copied and pasted)
Okoya
 
Tukitumia maarifa tutagundua kuwa;
Kuna post nyingine hata tukikutana nazo kwenye magroup mengine, hazina haja ya kuendelea kuzisambaza...
KUZIPUUZIA KUNAFAIDA KULIKO KUSAMBAZA!!!
 
Tukitumia maarifa tutagundua kuwa;
Kuna post nyingine hata tukikutana nazo kwenye magroup mengine, hazina haja ya kuendelea kuzisambaza...
KUZIPUUZIA KUNAFAIDA KULIKO KUSAMBAZA!!!
Ukipuuzia wewe inatosha.
Mimi na Baadhi ya wenzangu tunajifunza kitu.
Pole sana kama umekwazika.
 
Huyo Rafiki huwa haendi/hawatembeleani nyumbani kwa rafiki yake hadi mkewe aishi wiki nzima? Au urafiki wa baa za mbege?
 
Team "Kataa Ndoa" wanachelewa wapi pale kuleta mashambulizi golini?

Naona kuna mshambuliaji mmoja kakaa mbele palee, anaviziavizia mpira kabla purukushani hazijaanza 😂😂😂

Ah, tayari wawili wanapigiana pasi za karibu.
Wanapita Hapa Wakijoki Tu Halafu Wanatema Mate Kando Pwaa !😂😂😅😅😅😆😆😁😄😄😃😀😀😄😁😁😁😁😆😆😆😁😁😅😅😅😂😂🤣
 
Back
Top Bottom