Rafiki wa Mume wangu............

Rafiki wa Mume wangu............

realMamy

JF-Expert Member
Joined
Apr 28, 2024
Posts
7,587
Reaction score
19,374
Nimeolewa, ndoa yangu ina miaka 12 sasa hivi. Changamoto kubwa kwenye ndoa yangu ni kwamba mume wangu ni mtu wa kununa, kukasirika na kusikiliza sana marafiki. Ana rafiki yake mmoja ambaye tangu tuoane amekuwa akimsikiliza kuliko hata mimi mke wake.

Mara nyingi tukigombana, hata tukikaa na kukubaliana jambo, akienda kuongea na rafiki yake anarudi na kubadilisha maamuzi. Mwanzoni nilikuwa nakasirika, lakini baadaye nikagundua kwamba nikitaka kitu kutoka kwa mume wangu, ni bora niongee na rafiki yake. Akimshawishi, mume wangu anakubali.

Hali hiyo ilitengeneza mazoea kati yangu na huyo rafiki yake, mpaka tukajikuta tumeingia kwenye mahusiano ya kimapenzi.
Sasa mume wangu ana tabia moja, tukigombana ananifukuza nyumbani. Ananiambia, "Rudi kwenu, chukua vitu vyako!"

Mwanzoni alikuwa akinifukuza, namtafuta rafiki yake amshawishi anisamehe. Wakati mwingine naenda kwetu, nakaa siku chache, halafu narudi.

Lakini baada ya kuanza mahusiano na rafiki yake, mambo yakabadilika. Mume wangu akinifukuza, naenda moja kwa moja kwa rafiki yake. Nakaa naye hata wiki nzima, halafu tukichokana, anamtafuta mume wangu na kumwambia, "Mrudishe mke wako, sasa hivi atakuwa ameshajifunza."

Mume wangu ananikubali na mimi narudi nyumbani kama hakuna kilichotokea.
Hali hiyo imeendelea kwa miaka mingi mpaka sasa tuna watoto. Wakati mwingine hata bila kugombana, tukimissiana na huyo rafiki yake, tunapanga mpango. Mimi nafanya kakituko kidogo, mume wangu anakasirika na kumtafuta rafiki yake.
Rafiki yake anamwambia, "Huyu bado hajajifunza, mrudishe kwao kwanza!"

Mume wangu ananifukuza, mimi najifanya nimeenda kwa ndugu zangu, kumbe naenda kukaa kwa rafiki yake. Tukimaliza mambo yetu, ananishawishi nirudi kwenye ndoa yangu.

Lakini sasa hivi kumetokea changamoto ambayo imenichanganya sana!

Huyo rafiki yake anataka kuoa. Ana watoto na wanawake mbalimbali, lakini hajawahi kuoa. Mwezi ujao anafunga ndoa, kila kitu kimekamilika na matangazo ya kanisani yameshatolewa.
Sasa ameniambia kwamba kabla hajaoa, anataka nimzalie mtoto wa kumbukumbu!

Anasema akishaingia kwenye ndoa atakuwa bize, hatutakuwa tena na uhuru wa kukutana kama zamani. Kwa hiyo anataka nibebe mimba yake ili tubaki na kitu cha kutukumbusha mahusiano yetu.

Ukweli ni kwamba mimi pia natamani sana kumzalia, lakini nina wasiwasi. Hivi nikikubali kubeba mimba ya rafiki wa mume wangu, kweli haitaleta matatizo baadaye?

👇👇👇👇👇👇👇👇

(Copied and pasted)
 
loh binti safi sana wewe umenikumbusha miaka mingi nyuma... ujanani nilipenda sana wanawake makurumbembe..sikupenda watulivu.. niliwezana sana na makurumbembe... unanifaa wewe,, ndo michezo yngu hiyo... mpaka uzeeni mimi napenda makurumbembe yale ya town... nipo hivyo ingawa nimezeeka sana na busara zinapiga hodi... mzalie huyo jamaa,, utakuja kunishukuru
 
Huyo mwanamke hajui maana ya ndoa!

Amechukua maisha na ukanjanja wa usingle amepeleka kwa ucouple/ndoa!

Afanye yafuatayo

1. Aache ukaribu na huyo mwanamme anayetaka kuoa!

2. Ndoa ni kuipambania, anatakiwa kusimama kama mwanamke.

3. Anatakiwa kutafuta usuluhishi kwa wazazi wa mme wake og pind anapokumbana na matatizo katika ndoa

4. Aache umalaya wa kutamani waume za watu.

5. Asitumie k yake kama honey trap ya kutatua matatizo.

6. Ngono na umalaya ni roho chafu, unavyozidi kuitumikia ndivyo unafungwa kuzimu kuanzia maisha ya kiroho hadi kimwili, mwisho wake ni mafarakano yasiyoisha kwenye familia.

7. Avunje mawasiliano na majikedume yasiyojua ndoa na yaliyoshindwa kujenga ndoa

8. Asipeleke uanaharakati kwenye ndoa.
 
Team "Kataa Ndoa" wanachelewa wapi pale kuleta mashambulizi golini?

Naona kuna mshambuliaji mmoja kakaa mbele palee, anaviziavizia mpira kabla purukushani hazijaanza 😂😂😂

Ah, tayari wawili wanapigiana pasi za karibu.
Point nyingi kwao 😝
 
Huyo mwanamke hajui maana ya ndoa!

Amechukua maisha na ukanjanja wa usingle amepeleka kwa ucouple/ndoa!

Afanye yafuatayo

1. Aache ukaribu na huyo mwanamme anayetaka kuoa!

2. Ndoa ni kuipambania, anatakiwa kusimama kama mwanamke.

3. Anatakiwa kutafuta usuluhishi kwa wazazi wa mme wake og pind anapokumbana na matatizo katika ndoa

4. Aache umalaya wa kutamani waume za watu.

5. Asitumie k yake kama honey trap ya kutatua matatizo.

6. Ngono na umalaya ni roho chafu, unavyozidi kuitumikia ndivyo unafungwa kuzimu kuanzia maisha ya kiroho hadi kimwili, mwisho wake ni mafarakano yasiyoisha kwenye familia.

7. Avunje mawasiliano na majikedume yasiyojua ndoa na yaliyoshindwa kujenga ndoa

8. Asipeleke uanaharakati kwenye ndoa.
Kabisa
 
Back
Top Bottom