Kwa heshima na taadhima tunakuomba mheshimiwa Rais wa nchi yetu idhinisha malipo ya madai ya wastaafu wa ATCL. Kumekuwa na dana dana juu ya kulipwa hawa wastaafu toka Katibu Mkuu Kiongozi alipo iandikia wizara Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano kushughulikia malipo ya madai ya wastaafu wa ATCL.
Wizara haijafanya lo lote kwa madai kuwa Hazina ndio wanatakiwa kupeleka pesa PSSSF. Mheshimiwa raisi, wastaafu hawa wanaelezwa na maafisa wa PSSSF kuwa pesa iliyolipwa toka serikalini kipindi chote kilicho pita hakuna malipo kwa ajili ya wastaafu wa ATCL.
Ombi maalum kwa mheshimiwa raisi, wasaidie wastaafu hawa wanyonge kulipwa mapungufu ya pension zao maana uhakiki ulifanyika zaidi ya mara mbili.
Tumeshuhudia wengine wakifariki bila kupata haki zao.