Kwanini Rais Samia anatumia ndege za ATCL kwa safari zake hata fupi badala ya ndege ya Rais?

Synthesizer

JF-Expert Member
Feb 15, 2010
11,141
18,769
1629273322390.png

Nimeona katika picha Rais Samia alitumia ndege ya ATCL Airbus 220 5H-TCH (Dodoma - Hapa Kazi Tu) kwenda Malawi kwenye mkutano wa SADC. Ndege hii ina uwezo wa kubeba abiria kama 120 hivi.

Sio kwamba ninataka tu kumkosoa Rais Samia, lakini najiuliza sana, kwamba ni kwa nini anapofanya safari kama hizi fupi za kwenda hapa karibu Malawi anatumia ndege kubwa ya ATCL badala ya ndege ya Raisi ambayo iliponunuliwa tuliambiwa hata kama ni kula nyasi ili inunuliwe basi tungekula?

Nina uhakika ndege kama Airbus 220 ina gharama kubwa zaidi kumpeleka Samia na ujumbe wake Malawi kuliko angetumia ndege ya Raisi. Na kama watasema walihitaji Airbus 220 kwa sababu ya kuwa na ujumbe mkubwa, ni kwa nini waende na ujumbe mkubwa katika mkutano huu wa SADC wa siku mbili sijui?

Mie nadhani wakati Watanzania tunaambiwa tuvumilie tozo ili kuendeleza miundo mbinu na uchumi kwa ujumla, basi na watu kama Rais Samia wawe na ufikirio wa matumizi ya fedha za serikali kwa kuwa na busara katika vitu kama hivi. Mie sioni sababu ya Rais kutumia ndege za ATCL wakati kuna ndege ya Rais iliyonunuliwa mahsusi kwa ajili ya safari za Rais, na ina uwezo wa kwenda hadi USA.

Na sitegemei watatuambia kwamba hawakuitumia hii Airbus 220 bure bali waliikodi toka ATCL na kulipia, kwa sababu hizo fedha za kukodi pia ni fedha zetu za tozo na zinatuuma.
 
Mwache mama ale maisha na ndege mpya aina ya Airbus!! Ile ya Rais imechoka bhana!! Tangu enzi hizo!!

Viti vyenyewe tu vya kukalia, unaweza ukakuta ni zaidi ya vile vya ile TATA ya Simba.
Kwani ina miaka mingapi hadi sasa? Basi si wangeiuza ili tujue hatuna ndege ya Raisi na tozo ziongezwe au tule nyasi ili kununua ndege ya Raisi mpya? Serikali hii inaweza kuamua chochote, waamue hivyo.
 
Mama hajui kabisa kubana matumizi. Hapo akipanda hiyo ndege ikipiga rout moja ya kwenda malawi na kurudi si chini ya bilion 1
 
Lakini mimi ninawaza tofauti:

Labda, maafisa wengi wa awamu ile walipanda Ndege ya Rais(Miongoni mwao walishapatwa na UVIKO 19! Sasa waliopo wanaweza wasiwe na haraka ya kutumia ndege ya Rais.
 
Back
Top Bottom