ATCL kulipa madeni ya wastaafu ya Gratuity, na Long Service Awards na kuto lipa PSSSF (PPF) ni dhihaka kwa Wastaafu.

kisingi

JF-Expert Member
Apr 9, 2014
516
377
Nimesoma waraka wa management ya ATCL kuwa inalipa wastaafu na wafanyakazi wengine wa kampuni hiyo ya serekali madeni ya Long service awards na Gratuity tu na hawalipi madai ya wastaafu ya PSSSF zamani PPF.

Hili ni suala ambalo ATCL inabidi ili angalie upya na kuchukua hatua stahiki za kulipa madeni ya PSSSF. Nasema haya kwa sababu zifuatazo

1. Wastaafu wa ATCL walikuwa wanakatwa michango ya PSSSF kutoka katika mishahara yao kila mwezi bali management ya ATCL ilikuwa haiwakilishi michango hiyo kunako husika kwa miezi kadha kitendo ambacho kimeadhiri wastaafu kujikuta wanapata mafao kidogo wakati walipo staafu.

Kwa kuwa uhakiki ulisha fanywa na taasisi husila kama CAG na wakaguzi waliyoteuliwa na serikali ni wajibu wa management ya ATCL kuwalipa wastaafu wa kampuni hiyo madai yao ya PSSSF ambayo haya kuwakilishwa ofisi za PSSSF.

Stahiki walizo lipa za Long service awards na Gratuity zina husu watu wachache sana na kuacha kundi kubwa lililoadhirika na mafao ya kustaafu. ATCL Management lipeni madai ya PSSSF ya wastaafu ambayo kosa la kuto wakilisha michango lilifanywa na uwongozi wa kampuni.

2. Suala la kusema madai hayo yalipwe na wizara Ukenzi, Uchukuzi na Mawasiliano halina mantiki kwa sababu tayari management ya ATCL imeshaamua kulipa baadhi ya madeni ya wastaafu ni wajibu wao kulipa yote ambayo yametokana na kutojali mfumo wa uwajibikaji kiutendaji watu wanapo kabidhiwa madaraka.

3. Kuna wastaafu amba bado wapo kwenye ajira za mikataba na ATCL huwa hawawezi kulisemea hili lakini wale ambao wapo nyumbani na mitaani baada ya kutumikia ATCL kwa uwaminifu hadi kustaafu ndio wanao umia zaidi.

4. Serikali isilifumbie macho suala hili. Wastaafu wana watu wana wategemea kukosa kwao haki waliyoitumikia kwa unyenyekevu ni kuumiza utitiri wa wanao wategemea. Mafao kidogo yanawaathiri mno kimaisha ili hali haki yao bado ipo mikononi mwa kampuni ya ATCL.
 
Back
Top Bottom