Mi nataka kuuliza.
Prof. Tibaijuka sasa hivi anatambua mipaka ya Jamhuri ya Muungano, kuna suala la kupanua hizo miles baharini, primarily kwa kuangalia mambo ya rasilimali.
Ikiwa nchi sovereign yenye uanachama UN inaruhusiwa kufanya hivyo, na Zanzibar si nchi hivyo, na siku yoyote Zanzibar ikitoka kwenye muungano nayo inaweza kudai kufanya hivyo hivyo (angalau kwa pwani yake ya mashariki), kelele nyiingi kuhusu hili swala za nini?
Au ni njia moja tu ya kuusema muungano vibaya? Maandamano ya kutaka kura ya maoni 2015 yako wapi nijiunge?
Au itabidi nianzishe mwenyewe Dar-es-salaam December hii kwenye sherehe za Uhuru wa Tanganyika ?
Mimi nafikiri kama kweli Wazanzibari wanajivunia nchi yao, wajitoe kwenye muungano kwanza, wawe na nchi yao, wawe na uanachama UN na uhakika wote wa ku deal na "Tanganyika" kama a sovereign state, tutamaliza hizi nyepesi nyepesi zote.
Ya nini kutaka kutibu TB kwa Cofta? Deal na tatizo la msingi, tibu ugonjwa, kata mzizi wa fitina, sio unadeal na vi symptoms na vijani vya mti wa fitina.
Hivyo vijani kama hujakata mzizi kila siku vitaota vipya, matokeo hata wanaofanya kazi zao kama Tibaijuka mtawaona maadui wa Waanzibari.
Vunjeni muungano tujue moja, then mnaweza kuongea kama watu wenye nchi yenu. Sasa hivi mnapalilia dhana tu kwamba Wazanzibari wabishi
.