Fatal5,
..Tanganyika ilipata uanachama wa UN mwaka 1961 au 1962 baada ya kupata uhuru wetu.
..kuna juhudi kubwa zinafanyika kuwapotosha Wazanzibari kwamba Tanganyika haikupata kuwa mwanachama wa UN.
..Zanzibar nayo ilipata uanachama wa UN mwaka 1963 kama ulivyoonyesha hapo kwenye picha.
..mwaka 1964 tulipoungana, Tanganyika, na Zanzibar, zili-surrender uanachama wao, na kuchukua uanachama mpya kwa jina la Tanzania.
..serikali ya Mapinduzi Zanzibar haitambuliki ndani ya UN, kwa msingi huo waziri wake wa Ardhi hawezi kwenda ktk vikao vya UN na kuwasilisha ombi la kuongeza eneo la mipaka ya Zanzibar.
..Waziri wa ardhi ktk serikali ya muungano naye hana mamlaka juu ya masuala ya ardhi yanayoihusu Zanzibar. Wazanzibari wanaweza kujenga hoja hiyo na wakawa sahihi.
..Ombi hili la kuongezewa mipaka ilipaswa lifanywe na WAZIRI WA MAMBO YA NJE wa serikali ya muungano kwasababu mamlaka yake yanamruhusu kuizungumzia Tanzania visiwani/Zanzibar ktk umoja wa mataifa. Mawaziri wa ardhi wa Tanzania bara na Zanzibar wangeweza kuwepo ktk ujumbe unaoongozwa na Waziri wetu wa mambo ya Nje.
..kwa hali ilipofikia sasa hivi njia muafaka ya kurekebisha tatizo hili dogo ni kusubiri majibu ya UN kuhusu maombi yetu ya kuongezewa mpaka. Baada ya hapo turejee kwenye mipaka ya Tanganyika na Zanzibar kabla ya muungano wa 1964 ili kuweza kujua kila upande utapata eneo kiasi gani.
?Ukiangalia katika masuala mbalimbali, picha tunayoipata ni kuwa wengi wa Wazanzibari ni Wabinafsi na Wachoyo. Hii hofu ya kufikiria kuwa eneo litakaloongezwa litakuwa la Tanganyika, na Wazanzibari watanyang'anywa eneo lao inatokana na nini? Hivi tangu mwungano huu uanzishwe ni kitu gani Wazanzibari wamenyang'anywa na Tanganyika? Hivi katika mambo haya ambayo tunayowafadhili Wazanzibari, Wazanzibari wanaweza kuwafanyia Watanganyika
Wengi wao wamesomeshwa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam bure, kwa kulipiwa na serikali ya Tanzania (Tanganyika); kwa muda mrefu wamepewa umeme bure; wabunge wao licha ya kuwakilisha watu wachache sana wanapewa haki zote sawa na wabunge wa bara ambao wanawakilisha maelfu ya watu ambao wanachangia bajeti ya mwungano karibu kwa 100%, Wazanzibari wamewahi kupewa uwaziri kuongoza wizara za serikali ya Tanzania zisizo za mwungano, Wazanzibari wanamiliki mashamba Tanzania bara, n.k. Hawa watu hawana hata shukrani, na upole wa Tanganyika unawafanya wadeke sana. Sidhani kama Tanganyika ina haja hata na bakuli moja ya maji ya bahari ya Zanzibar. Tanganyika ina Pwani ya bahari toka Tanga hadi Mtwara, ina maziwa: Ziwa Nyasa lenye dhoruba kubwa kuliko maziwa yote Duniani, ina Ziwa Tanganyika lenye kina kirefu kuliko yote, ina Ziwa Victoria ambalo ni kubwa kuliko yote; yapo na mengine kama Eyasi, Manyara n.k. Tanganyika ina mito mikubwa na mirefu inayotiririsha maji usiku na mchana, masika na kiangazi, halafu iende ikaipokonye Zanzibar bahari yake kwa lengo gani? Tangayika ina uwezo wa kuwachukua Wazanzibari wote na kuwapa wilaya moja ya Tanganyika, wakaishi kwa nafasi, na ardhi nyingine ikabakia. Wazanzibari, sisi tunawaona ninyi kuwa ni ndugu zetu, tuna-sacrifice mambo mengi kwaajili ya upendo wetu kwenu lakini hamna shukrani. Kuna siku tutawachoka, tutawaachia na ndipo mtajua thamani ya kile ambacho mmekuwa mkikichezea kwa miaka mingi.
Na Mwinyi Sadallah
23rd January 2012
Chama cha Wananchi (CUF) kimesema kwamba kitapinga Umoja wa Mataifa (UN) kuiongezea Tanzania mipaka ya eneo la kiuchumi la bahari Kuu kabla ya kupatikana muafaka kati ya Serikali ya Muungano na Zanzibar.
Tamko hilo limetolewa na Naibu Katibu Mkuu na Mkurugenzi mambo ya nje wa Chama hicho, Ismail Jussa Ladhu, alipokuwa akihutubia mkutano wa hadhara uliyofanyika katika uwanja wa Gombani ya Kale huko kisiwani Pemba jana.
Alisema Serikali ya Muungano imefanya makosa kuandaa kupeleka maombi ya kutaka kuongezewa mipaka ya eneo tengefu la kiuchumi la bahari kuu (EEZ) bila ya kushirikisha Zanzibar.
Jussa alisema wananchi wa Zanzibar wapo tayari kupoteza maisha lakini hawatokubali eneo la bahari Kuu la Zanzibar kuongezwa na kuwa sehemu ya eneo la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Wananchi wa Pemba simameni kidete kutetea maslahi ya Zanzibar hata kama tutamalizika sote haiwezekani eneo la bahari Kuu la Zanzibar kuwa la muungano, alisema Jussa.
Alifafanua kuwa Januari 16 mwaka huu Waziri wa Ardhi nyumba na Maendeleo ya Makazi, Profesa Anna Tibaijuka, alitangaza mpango wa Tanzania kuomba UN kuiongezea maili 150 sawa na kilometa 241.5 kutoka usawa wa mwambao wa Tanzania.
Profesa Tibaijuka alisema kazi ya kukamilisha andiko hilo ilianza mwaka 2007 na kugharimu Sh. Bilioni 5.2 na kushilikisha wataalamu kutoka sekta ya mbalimbali, ili iweze kulifanyia utafiti zaidi kuhusu rasilimali zilizoko chini ya bahari kwa lengo la kuinua uchumi wa nchi.
Jussa alisema mpango huo umelenga kuiwezesha serikali ya Muungano kuongezewa eneo hilo ili kufanikisha mpango wake kufanya utafiti na uchimbaji wa mafuta wakati SMZ imekwishaliondoa kwenye orodha ya mambo ya muungano.
Hata hivyo, alisema mpango wa Tanzania kuongezewa eneo la maili 150 kutoka usawa wa bahari ya Hindi umefanyika bila ya kuishilikisha SMZ.
Jussa ambaye pia mwakilishi wa jimbo la Mji Mkongwe, alisema alipohoji suala hilo ndani ya Baraza la Wawakilishi Zanzibar (BLW) alitakiwa na serikali kuwa na subira na kutoa nafasi kwa serikali ya SMZ kulifuatilia.
Alisema suala la mafuta na gesi asilia tayari SMZ imeamua tangu mwaka 2009 kuliondoa katika orodha ya mambo ya muungano na haikuwa muafaka kwa serikali kupeleka maombi hayo bila ya kupata baraka ya Zanzibar.
Wenzetu wanataka kuchimba mafuta na gesi asilia ya Zanzibar kwa kutumia mlango wa nyuma hatukubali kwa maslahi ya Zanzibar na nchi yetu, alisema Jussa.
Kuhusu kufukuzwa kwa viongozi wanne wa CUF akiwemo Mbunge wa Wawi Hamad Rashid Mohammed, alisema viongozi hao wamekwenda kinyume na misingi ya kuanzishwa kwa chama hicho mwaka 1992.
Alisema CUF ilianzishwa kwa madhumuni makubwa ya kupingania haki za Zanzibar na wananchi wake ikiwemo mfumo wa Muungano.
Jussa alisema katika kupingania haki za Zanzibar ndiyo maana wapo watu wamepoteza maisha na wengine kupata ulemavu wa kudumu ndiyo maana chama kimeamua kuwafukuza viongozi hao baada ya kwenda kinyume na misingi ya kuanzishwa kwake.
Kwa upande wake, Mkurugenzi wa haki za Binadamu na mahusiano ya umma Salim Biman, alisema kwamba viongozi waliyofukuzwa ndani ya CUF waliweka maslahi binafsi mbele badala ya maslahi ya chama na wanachama wake.
Awali akisoma risala ya mikoa miwili ya wanachama wa CUF Kisiwani Pemba, Ayoub Yussuf Mgeni, alisema wanachama wanaunga mkono maamuzi ya Baraza Kuu la Uongozi kwa kuwatimu viongozi hao.
Alisema viongozi hao ni wasaliti kutokana na kitendo chao cha kutetea maslahi binafsi na kuwapaka matope viongozi wa kitaifa kwa kutaka kuwagawanya kwa mtazamo wa Uunguja, Upemba na Utanzania Bara.
Alisema CUF kimefanya kazi kubwa kupingania misingi ya haki za binadamu na utawala bora hadi kufanikiwa kuundwa kwa serikali ya Umoja wa Kitaifa Novemba mwaka 2010.
Alisema tangu kundwa kwa serikali hiyo kesi za kisiasa, ubaguzi na ukikwaji haki za binadamu umeondoka kwa wananchi wa Zanzibar.
Aliongeza kuwa hatua kama hizo zinapaswa kuendelea kuchukuliwa kwa mwanachama yoyote anayetaka kuvuruga umoja wa kitaifa kwa wananchi wa Zanzibar.
Mapema Katibu Mkuu wa chama hicho, Maalim Seif Sharif Hamad, ambaye pia Makamu wa kwanza wa Rais, alipokea maadamano ya amani ambayo yalinzia huko Machomanne kupitia Mkanjuni huku wanachama wakiwa wamebeba mabango ya kumshutumu Mbunge wa Wawi aliyevuliwa uanachama Hamad Rashid Mohammed.
Baadhi ya mabango yalisomeka Tumekukuta Wawi na shuka kiunoni, tumekupeleka Dodoma na suti leo watusaliti; Tamaa imekuponza, siasa hukuweza rudi Wawi ukavue na lingine likisema Hamad umepanda upepo utavuna dhuruba
CHANZO: NIPASHE
My Take:
Kwa kosa alilolifanya kupeleka ombi Un Pasi na kupata baraka za baraza la wawakilishi Znz wakti anajua fika suala la ardhi sio suala la muungano ni utovu mkubwa sana wa nidhamu na kutaka kufanya ubabe na kuvunja katiba ya Muungano na ile ya Zanzibar. Kiungwana anatakiwa ajiuzuru.
Hakika Jusa wewe ni shujaa sana kwa kuliona hili kwani kuna dhulma kubwa sana ilitaka kufanyika hapa. Ikiwemo ile ya kumega eneo la bahari kwa Znz na kuitumbukiza katika Muungano.
Lazima kieleweke na Prof lazima aondolewe hapo. Kwani ubabe hauna nafasi kwenye sheria. lazima sheria zifuatwe.
Umeshatuambia kuwa muungano huu hauna katiba sasa unasimamiaje katiba ambayo haipo? Kajipange tena, muongo wewe!
zanzibar nchi?

Angalau walikuwa/ ni Watanzania. Huyu jamaa alijifanya MTANZANIA. Akatuibia kodi zetu kwa huruma ya Mwalimu kwa Wazanzibar. Sasa yuko Uarabuni anatufundisha democrasia. Waarabu na democrasia!Kuna wengi waliosoma Tanzania lakini kuona mambo mabaya wamehamia nchi za nje na kuchukuwa Uraia wa huko ama kuchukuwa "residence permit za huko" wanaishi huko na hawana habari za Tanzania. Ni wengi sana.
Ungekuwa umejaaliwa kusafiri safiri nje ya Tanzania (upeo wako unaonesha husafiri kabisa), ungejionea mwenyewe.
Hilo aliwezekani hata kidogo. Kwani Tanganyika na Znz zimeungana KIMKATABA na sio KIKATIBA. Kuna mambo apo nje ya mkataba wa Muungano likiwemo hili la ardhi na makazi.
Sasa unapozungumzia maslahi ya eneo la milki ya arrdhi ni lazima uziusishe pande zote mbili kwani hili si suala la muungano. Alichofanya Tibaijuka ni ubabe kitu ambacho hakikubaliki. Ni mawili tu yanatakiwa hapo ima a withdraw hayo maombi na kuanza mchakato mpya kama nchi zote mbili zitakubaliana au kuanisha kila nchi itanufaika vipi in terms of eneo hilo.
kama OIC ilizimwa na Muungano kwanini na hili lisizimwe.
Tibaijuka amechamke lazima ajiuzuru tu hakuna mjadala.
Nilifikiri serikali ya muungano inajumuisha na zanzibar kumbe hapana!!
Nianze tu kwa kusema Zanzibar kuna matatizo Mengi umeme unakatika kila siku Jusa yuko kimya,elimu mbovu yuko kimya,wazanzibar wanazidi kuteseka yeye analeta siasa.
Ulichoongea Jusa ni upumbavu maana Tanganyika ina eneo la Bahari toka TANGA mpaka LINDI unaweza kadiria ni kilometa ngapi hizo?kwanza unajua ni upande gani wanataka kuongeza,kama wanataka kuongeza upande wa Pwani zanzibar wawahusishe ya nini?kwanza kwa upande wa zanzibar hawawezi kuongeza maana ukitoka pemba unafika mombasa.
Hata kama wataongeza upande wenu ulitakiwa kukaa na viongozi wa serikali kujua mustakabathi wa hayo sio kupiga kelele kwa kitu ambacho kitafanyika miaka 20 au 30 ijayo.PEMBA ,MTWARA KUNA MAFUTA HAYAJACHIMBWA NDIO HAYO YA KATIKATI YA BAHARI YATACHIMBWA.
WASAIDIE WAZANZIBAR KUPATA ELIMU BORA,UMEME BORA,AFYA BORA ,BADO WANAKUNYWA MAJI MACHAFU,WANALALA PA CHAFU ALAFU UNAFANYA SIASA UNABOA SANA.
Mama Tibaijuka jana alilitolea ufafanuzi hili. Waliotaka kuelewa wameelewa. Wenye agenda nyingine nyuma ya hili waendelee tu na agenda zao. Watu wa Mungu hauwezi kuwazuia, kuwapimia au hata kukomalia hili wakiwa na maana ya lile.
Hakuna cha Prof. Tibaijuka kujiuzulu. Eneo hili kwa ajili ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambamo wewe na Jussa wako ni raia. Kama kuna kitu kingine si mseme tu. Achani kutumia uongo wa uani ili kutaka kuvunja muungano.
Ami yangu naona umewashika pabaya jamaa zangu,hivo hivo akiwachekea hawa ndugu zangu hata urais wa Tanzania mtausikia kwenye bomba tena,maana wameshaanza kupangana huku bara,wanasema safri ni zamu ya kaskazini,nyie wamewasahau kabisa!mkimaliza hilo wakomalieni na kwenye urais,tupo wabara tusiopenda dhulma tunawaunga mkono ili na sisi tupate pa kuanzia kuidai Tanganyika yetu irudishwe kwenye ramani ya dunia an kiti chetu UN kirudi vilevile!WC,,
Suala la ardhwi sio suala la kisiasa hilo ni rasilimali ya nchi hoyo. Ndio maana unasikia watu wanapigana na kuuwana kutokana na kugombea ardhi..
Labda nikuulize Je unajuwa kwanini suala la ardhi halimo katika hati ya makubaliano ya Muungano?
Kila nchi ina waziri wake wa Ardhi.
Kama suala hilo ni genuine halina shaka wala hila zozote kwanini lisiwasilishwe na Waziri wa mambo ya Nje na mawaziri wote wa ardhi wa nchi zote mbili kuwa wasindikizaji tu?
Kwani masuala ya mambo ya nje ni moja katika makubaliano katika hati ya muungano.
Kwanini asiwasilishe Membe au naibu wake Mahadhi Maalim. Tibaijuka amewasilisha kama nani?
Je wajua kuwa Rais wa Kwanza wa Znz na makamo wa kwanza wa rais wa Muungano , Amani Karume (Karume 1) taarih 16th Feb 1971 alisema alipohojiwa na waandishi wa habari uwanja wa ndege wa Znz akitokea Dar kuhusu Muungano alisema
" Muungano huu ni kama Koti, Likikuchosha unalitoa na kulivua "
Jambo usilolijua litakusumbua. Jussa na Baraza la Wawakilishi la Zanzibar wamezungumza kama majuha kwani hawajui kipi kimeombwa. JMK imeomba kuongezewa eneo zaidi ya lile Eneo Tengefu la Kiuchumi (ETK) au kwa Kiingereza Exclusive Economic Zone (EEZ). ETK haiombwi kwani hiyo ni haki ya nchi inayopakana na bahari. Tanzania ilikwisha tangaza eneo lake la ETK mwaka 1989 kwa mujibu wa Sheria ya Eneo la Bahari na Eneo Tengefu Namba 3 ya Mwaka 1989 ambayo ilisainiwa na Raisi Mzanzibari, Alhaji Ali Hassani Mwinyi na inatumika pande zote mbili za Muungano (soma kifungu 1(2). "This Act shall extend to Zanzibar".
Kifungu cha 7 cha sheria hiyo kinasema.
7.-(I) There is established contiguous to the territorial waters, an Exclusive Economic marine zone to be known as the Exclusive Economic Zone.
(2) Subject to subsection (3), the exclusive economic zone shall not extend beyond 200 nautical miles from the baselines from which the breadth of the territorial water is measured.
Hivyo eneo la ETK ndilo hilo na hapo hakuna na nchi yetu ina haki nalo na ndiyo maana Waziri Magufuli alifanikiwa kuishika ile meli ya iliyokuwa inavua samaki katika eneo hilo. Kwa mujibu wa Makubaliano ya Umoja wa Mataifa ya Sheria za Baharini ya Mwaka 1982 United Nations Convention on the Law of the Sea (UNCLOS), nchi inayopakana na bahari inaweza kuomba kuongezewa eneo nje ya ETK lenye ukubwa wa maili za kinutikali 350.Ikumbukwe kuwa Maili 1 ya kinutikali= Mita 1,852 (Kilomita 1 na mita 852). Eneo hili la ziada linaitwa Eneo Tengefu la Kibara (Continental Shelf(CZ)).
Ibara ya 76 ya Makubaliano hayo ya Sheriza za Bahari inasema:
1. The continental shelf of a coastal State comprises the seabed and subsoil of the submarine areas that extend beyond its territorial sea throughout the natural prolongation of its land territory to the outer edge of the continental margin, or to a distance of 200 nautical miles from the baselines from which the breadth of the territorial sea is measured where the outer edge of the continental margin does not extend up to that distance.
4. (a) For the purposes of this Convention, the coastal State shall establish the outer edge of the continental margin wherever the
margin extends beyond 200 nautical miles from the baselines from which the breadth of the territorial sea is measured, by
either:
----
5. The fixed points comprising the line of the outer limits of the continental shelf on the seabed, drawn in accordance with paragraph 4 (a)(i) and (ii), either shall not exceed 350 nautical miles from the baselines from which the breadth of the territorial sea is measured or shall not exceed 100 nautical miles from the 2,500 metre isobath, which is a line connecting the depth of 2,500 metres.
6. Notwithstanding the provisions of paragraph 5, on submarine ridges, the outer limit of the continental shelf shall not exceed 350 nautical miles from the baselines from which the breadth of the territorial sea is measured. This paragraph does not apply to submarine elevations that are natural Article 76.The outer limit of the continental shelf shall not exceed 350 nautical miles
from the baselines from which the breadth of the territorial sea is measured. This paragraph does not apply to submarine elevations that are natural components of the continental margin, such as its plateaux, rises, caps, banks and spurs.
----
8. Information on the limits of the continental shelf beyond 200 nautical miles from the baselines from which the breadth of the territorial sea is measured shall be submitted by the coastal State to the Commission on the Limits of the Continental Shelf set up under Annex II on the basis of equitable geographical representation. The Commission shall make recommendations to coastal States on matters related to the establishment of the outer limits of their continental shelf. The limits of the shelf established by a coastal State on the basis of these recommendations shall be final and binding.
Kazi ya Tume za Ukomo wa Eneo Tengefu la Kibara ni kama zilivyoanishwa na Kiambatanisho cha Pili cha Makubaliano hayo:
Article 3
1. The functions of the Commission shall be:
(a) to consider the data and other material submitted by coastal States concerning the outer limits of the continental shelf in
areas where those limits extend beyond 200 nautical miles, and to make recommendations in accordance with article 76 and the
Statement of Understanding adopted on 29 August 1980 by the Third United Nations Conference on the Law of the Sea;
(b) to provide scientific and technical advice, if requested by the coastal State concerned during the preparation of the data
referred to in subparagraph (a).
2. The Commission may cooperate, to the extent considered necessary and useful, with the Intergovernmental Oceanographic Commission of UNESCO, the International Hydrographic Organization and other competent international organizations with a view to exchanging scientific and technical information which might be of assistance in discharging the Commission's
responsibilities.
Article 4
Where a coastal State intends to establish, in accordance with article 76, the outer limits of its continental shelf beyond 200 nautical miles, it shall submit particulars of such limits to the Commission along with supporting scientific and technical data as soon as possible but in any case within 10 years of the entry into force of this Convention for that State. The coastal State shall at the same time give the names of any Commission members who have provided it with scientific and technical advice. (Mkazo umeongezwa).
Tukiangalia kwa makini ni kuwa maombi ya JMT yamechelewa kwani yalitakiwa yatolewe ndani ya kipindi cha miaka kumi tangu sheria hiyo kuanza kufanya kazi yaani mwaka (1994-2004). Kwa hiyo maombi ya JMT ni lazima yawe na sababu zilizoifanya Tanzania ichelewe kupeleka maombi yake. Kupewa eneo kunaipa miliki nchi ya kipwani haki ya kutafuta na kutumia rasilimali zilizomo. Sasa akina Jussa na wajumbe wa BLW walitakiwa kuelewa kuwa haki zote ambazo JMT inapata katika eneo hili ni zao pia na hata kama muungano huu ulio mahututi utakufa basi kutafanyika mgawo wa mali na madeni kama ambavyo ilifanyika mwaka 1977 baada ya kuvunjika kwa Jumuia ya Afrika Mashariki. Bahati mbaya tunazungumza na watu walio mtero au kwa Kiingereza "jumpy" ambao wanakurupukia mambo wakijifanya wanajua kumbe hawajui kitu na wanawapotosha watu wengi. Ni vema wakumbuke maneno ya wahenga "Simba mwenda pole ndiye mla nyama.
************************Tibaijuka amshangaa Jussa kupinga mradi wa kiuchumi
Aziza Masoud
WAZIRI wa Ardhi,Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Profesa Anna Tibaijuka, ameshangazwa na kauli iliyotolewa na Mwakilishi wa Mji Mkongwe, Ismail Jussa (CUF), kuhusu mradi wa kuongeza eneo la ziada nje ya ukanda wa uchumi baharini.Akizungumza Dar es Salaam jana, Profesa Tibaijuka alisema haoni sababu ya kugombana wakati ombi hilo liliwasilishwa kama Serikali ya Jamhuri ya Muungano na wakati wa mchakato wa kuandaa, wananchi wa Zanzibar walishirikishwa.
Profesa Tibaijuka alitoa kauli hiyo baada ya Jussa kusema mbele ya Baraza la Wawakilishi Zanzibar kwamba, ongezeko hilo halihusu Serikali ya Jamhuri, bali Serikali ya Tanzania Bara na kitendo kilichofanyika kinaonekana kuhujumu eneo la bahari ya Zanzibar.Sioni sababu ya kugombania fito wakati nyumba tunayoijenga ni moja, siku zote tukipima mipaka huwa tunapima kati ya Jamhuri ya Muungano na nchi husika, hakuna siku tuliyopima mipaka ya Tanzania Bara wala visiwani peke yake kwenye suala hili, alisema Profesa Tibaijuka.
Alisema ni muhimu watu kujua suala la ongezeko ukanda wa uchumi katika eneo la bahari, kwani ni suala nyeti na litakuwa jambo la kusikitisha kama wataanza kuvutana wenyewe kabla halijamalizika.
Hivi inakuingia akilini, mimi niliyepewa kazi ya uwaziri na Rais niende Marekani kudai ardhi bila watu kujua, ni suala la kusikitisha siwezi kukurupuka kwenda kudai eneo la nchi bila ruhusa ya viongozi, watu wanadai nijiuzulu nitakuwa wa kwanza kuondoka madarakani kama nikijua kosa nililolitenda, alisema.
Alisema madai ya Jussa kwamba Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ) haikushirikishwa katika mchakato huo, hayaendani na yaliyojiri kutokana na wajumbe na viongozi wa SMZ kushiriki na kufanya kazi kwa bidii katika mchakato wa kudai eneo hilo. Mwisho.
Ni kweli kabisa usemayo na ndiko tunakoelekea lakini nitasikitka sana kuona "somalia" mpya ikitengenezwa baada ya ''kuvua" hilo koti.... Nikuulize swali jepesi tu na tafadhali kuwa objective katika jibu lako ... Unadhani kati ya wabara na wazanzibari ni wapi wanaofaidika na muungano? na je ukivunjiaka na kila mtu arudi kwake nani ataathirika?? tatu eneo analopigia kelele jusa na wenzake wenye upeo finyu kwa sasa linamsaidia nin? kwanini hakuwahi yeye kuwasilisha hilo ombi? je Ikipewa Tanzania yeye (ninyi) ataadhirika kivipi au ndo yale mambo yetu ya joka la mdimu???