Prof Tibaijuka lazima ajiuzulu

Prof Tibaijuka lazima ajiuzulu

Naomba nikuweke sawa kidogo kwani kuna mambo umeyasahau kidogo.

Tanganyika na Znz zimeungana kimkataba na sio kikatiba. Kuna mambo yamo katika mkataba huo nayo ndio mambo ya muungano. Suala la ardhi na makazi si suala la Muungano na ndio maana Znz kuna waziri wa wizara hiyo na Bara yupo.

Kumbuka kuwa Mamlaka ya Tibaijuka mwisho wake ni Chumbe akiwa Znz hana mamlaka yoyote ukilinganisha na waziri wa mambo ya nje au mambo ya ndani. hawa wana malka kote kote.

Kumbuka vile vile Znz ni nchi kamili yenye mamlaka kamili na hilo limebainishwa katika katiba ya Znz. Kwa msingi huo Katiba hiyo hiyo imeanisha eneo la Znz kiufasaha kabisa. sasa kwa ombi hilo la Tibaijuka ni lazima katiba ya Znz itabidi ibadilike kwa kuongeza eneo la milki yake au kupunguza miliki yake na hapo ili kubadilisha kipengele hicho cha katiba lazima BLW litahusika vilivyo kwani wao ndio wtunzi wa sheria za Znz na mambo yote yaliyo nje ya muungano.

Kumbuka kuwa katika Picha walopiga kule UN wakti wanawakilisha alikuweo Tibaijuka, balozi wa Tz katika UN, Mbunge wa Mafia na Katibu wa wizara kutoka Znz. Kwa mantiki hiyo inaonekana wazi Prof Tibaijuka alipata baraka zote za Bunge la Muungano dio maana akachukua muwakilishi wa Bunge.

Sasa upande wa BLW hawakuwa na taarifa zozote ongezeka hilo officially na aliku husishwa kwa lolote lile kitu ambacho Jussa amehoji. Ikumbukwe kuwa maombi haya yakifanikiwa lazima BLW litahusishwa katika kupitisha sheria za ongezeko la eneo la miliki la Znz.

sasa labda tujiulize.
Je Znz itaongezewa kiasi gani katika hicho kilicho ombwa? hilo ni suala ambalo limegubikwa na utata mkubwa na alijabainishwa katika mkataba au mbi hilo.

Lakini pia lazima ufahamu kuwa Tz na Znz zote zinaongozwa na Rules of Law. Na mihimili yote mikuu inajipambanua yaani Serikali, Bunge na Mahakama bila kuingilia katika utendaji kazi wake. Kila muhimili unajitegemea.

Limeanza baraza la wawakilishi kuhoji Serikali ya Znz kisha uzi utafuata. Kwani majibu ya Serikali ndio yatatoa mwangaza kwa sakata hilo. Lakin all in all Tibaijuka lazima ajiuzuru hapo.

Kwani mtiririko wa jambo hili unakuwa sawa kabisa na ule wa Tz kujiunga na OIC.

Labda wajumbe wa ZNZ waliopo kwenye huo msafara wawe hawajui hayo yote! Majungu ni tabia nayo!!
 
Ndio maana nikakwambia usome katiba kabla kuleta hoja zako.

Kumbuka kuwa katika mkataba wa muungano wa Tanganyika na Zanzibar suala la ardhi na makaazi halipo. Kwa maana nyingine suala hilo lipo nje ya Muungano na hili ndilo linalopelekea kuwe na waziri Znz wa Ardhi na makaazi ambaye ni Mh Ali Juma Shamuhuna na Waziri wa Ardhi wa makazi wa Muungano ni Prof Tibaijuka.

Sasa ni vizuri urejee kwenye katiba ya Muungano uone mipaka yao ya kazi.

Kwa kukusaidia kidogo imebainishwa wazi kutoka katika katiba ya muungano imesema hivi. Kuwa atashughulikia mambo yate ya Tanganyika (katiba wamesema Tz Bara) na yale yasiyokuwa ya muungano . Na wa Znz atashughulikia mambo yote ya Zanzibar.

Je wajua kuwa Znz ni nchi. Soma katiba ya Znz inayonena hivi.

Na kwa mujibu wa Katiba ya Zanzibari ya Mwaka 1984 kama ilivyorekebishwa mwaka 2009:
ibara ya 3 na 4
1. "Zanzibar ni Nchi ambayo eneo la mipaka yake ni eneo lote la Visiwa
vya Unguja na Pemba pamoja na Visiwa vidogo vilivyoizunguka na bahari
yake ambayo kabla ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar ikiitwa Jamhuri ya Watu wa Zanzibar"

Hiki kitu ni batili Barubaru pamoja na utamu wake wa lugha ukikisoma. Sheria mama yaani katiba ya JMT inakibatilisha "ab initio"( sijui kama nimepatia). Hauwezi kuwa na Jamhuri mbili ndani ya moja. Soma sana Katiba ya JMT. Akina Jussa wanachezea akili za watu tu. Kwa akili yako ya kawaida kabisa nani angepeleka ombi lile UN?
 
Jamani, jamani - kwahiyo usemalo wewe zanzibar sio nchi? Ni kitu gani sasa - tafadhali naomba jina lake tu - kamkoa, kijiji, kitongoji? Maana kama tunauwezo wa kusema sio nchi basi tuwe na uwezo wa kusema inaitwaje?
Kwa KATIBA yetu ya JMT, Zanzibar ni SERIKALI tu. Kama ilivyo Scotland, Wales na Northern Ireland zinazounda UK.
 
Na Mwinyi Sadallah
23rd January 2012

My Take:

Kwa kosa alilolifanya kupeleka ombi Un Pasi na kupata baraka za baraza la wawakilishi Znz wakti anajua fika
suala la ardhi sio suala la muungano ni utovu mkubwa sana wa nidhamu na kutaka kufanya ubabe na kuvunja katiba ya Muungano na ile ya Zanzibar. Kiungwana anatakiwa ajiuzuru.

Mbona sasa hili ni suala la bahari a.k.a maji!!! Labda kama masuala ya ardhi yana include na bahari!!
 
nani akuchague wewe?hee!unafanya masihara na wazenj wewe!pata waka moto kama iraq!jussa yupo juu!tibaijuka ajiuzulu huko huko aliko!
natamani ningekuwa rais ningeifanya zenj mkoa na hao vimbelembele kama jusa ningewarudisha kwao uaharabuni, hawa ndio wanaotududisha nyuima. Tanahitaji raisi mbabe ndio tuendelee. La sivyo hatutafika mahali. Huyu jussa ni ni mtu hatari na si mzalendo kabisa ni mamluki
 
unataka kusema ni kama serikali ya mkoa wa TANGA au tofauti kidogo?
Hii ni serikali ambayo ipo KIKATIBA. Hakuna mahala kwenye katiba yetu ya JMT inataja serikali ya mkoa wa Tanga. Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar ipo. Ina Rais. Lipo pia Baraza la Mapinduzi. Lipo pia Baraza la Wawakilishi( Mwalimu aliwasaidia sana kulipata hili). Vipo pia vyombo vingine vingi tu.
 
Naamini Baraza la Wawakilishi ni baraza la watu wazima, watu makini na waliopo kwa mujibu wa Katiba yetu ya JMT. Waangalie na kupima yafuatayo:
-Walishajadili na kupitisha azimio zito juu ya mafuta. Nini kimefanyika?
-Walishajadili na kupitisha mabadiliko ya KATIBA ya Zanzibar. Wakachora na mipaka. Zanzibar ikawa "NCHI". Hali ikoje ndani ya katiba ya JMT?
-Katiba ya JMT bado inamtambua Waziri Kiongozi sio hawa makamu wawili bandia wa Rais wa Zanzibar. Barubaru na Jussa mnasemaje?
-Sasa mnalianzisha hili la mipaka ya bahari. Mtafika nalo wapi?

Suala la mafuta na gas asilia limeshaondolewa kwenye mkataba wa Muungano.

Labda nikuulize.

Anapokuja makamo wa kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim Seif shariff Hamad au Makamo wa Pili wa Rais wa Znz Balozi Idi huko Tanganyika kwanini wanapewa ulinzi mzito ikiwa pamoja na vingora vya polisi wanapotembea?

Je unajuwa kwanini?

nasubiri jibu hapa. kabla kuendelea.

Mzee Barubaru nachelea kukuita mwongo kwa umri na elimu yako. Bunge letu la JMT limekaa lini likayaondoa mafuta na gas asilia. Unazijua taratibu za kuliondoa suala hili kwenye mambo ya Muungano?
Hili la ving'ora na ulinzi lisikupe shida. Hata harusi na misiba kuna ving'ora pia na ulinzi mkali. Jamaa hawa hawamo kwenye Katiba yetu ya JMT.
 
Barubaru, Katiba ya Zanzibar ipo kwa sababu Katiba ya Muungano imesema "kutakuwa na Katiba ya Zanzibar". Katiba ya Zanzibar haipo nje ya Katiba Ya Muungano. Kati ya Katiba hizo mbili linalotenguka ni lile linalopingana na Katiba ya Muungano linatenguka. Katiba ya Muungano ikipingana na ya Zanzibar, ya muungano haitenguki ni ya Zanzibar ndio inatenguka. Binafsi hata nikiona Katiba ya Zanzibar inasema "Zanzibar ni nchi" kwangu haina maana yoyote kwa sababu Katiba ya Muungano inasema "Tanzania ni nchi moja na ni Jamhuri ya Muungano!"! Hakuna nchi mbili ipo nchi moja!

Mwanakijiji.

Ni vizuri ukajuwa wazi Bila Zanzibar basi hakuna Katiba ya Muungano wala Muungano. Kwani ili kuwepo na Tanzania ni lazima ipatikane Tanganyika na Zanzibar. Na hakutakuwa na katiba yya muungano bila kuwa na Katiba ya Zanzibar. Kwani vyote vinategemeana.

Na katiba ya Zanzibar ndiyo inayoifanya Tanzania na katiba ya Tanzania kwani inatambua uwepo wa Rais wa Znz na BLW.

Wewe sio SHARIA hivyo kuitambua au kutoitambua sio tatizo kwa Znz wala muungano. Na sawa tu na maoni yako tu wala haiwashughulishi wa Znz kula chakula au kudai haki zao katika Muungano. Kumbuka huo ni muungano na sio Mvungano. wote mpo sawa mbele ya sheria za muungano.

Nakumbuka Raid Karume 1 aliwahi kusema wazi kabisa kuwa Muungano ni kama koti. Likikuchosha unalivua. Hivyo sio kosa kuuvunja kama kuna kudhulmiana au jamii moja kujiona bora kuliko wengine.

Katiba ya Znz inasema hivi.
Katiba ya Zanzibari ya Mwaka 1984 kama ilivyorekebishwa mwaka 2009:
ibara ya 3 na 4
1. "Zanzibar ni Nchi ambayo eneo la mipaka yake ni eneo lote la Visiwa
vya Unguja na Pemba pamoja na Visiwa vidogo vilivyoizunguka na bahari
yake ambayo kabla ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar ikiitwa Jamhuri ya Watu wa Zanzibar"

Kati ya watu ninaowashangaa na ntaendelea kuwa hivyo ni wazanzibar kwa kweli!
 
Hiki kitu ni batili Barubaru pamoja na utamu wake wa lugha ukikisoma. Sheria mama yaani katiba ya JMT inakibatilisha "ab initio"( sijui kama nimepatia). Hauwezi kuwa na Jamhuri mbili ndani ya moja. Soma sana Katiba ya JMT. Akina Jussa wanachezea akili za watu tu. Kwa akili yako ya kawaida kabisa nani angepeleka ombi lile UN?

usikurupuke WC,

Je unajuwa tofauti ya Jamhuri na Serikali?
tunaomba utupe darsa kidogo hapo la jamhuru ni nini na Serikali ni nini ili tuweze kuendelea na mujadila.

Kati ya watu ninaowashangaa na ntaendelea kuwa hivyo ni wazanzibar kwa kweli!

Utashangaa sana. Lakin ni lazima wadai haki zao ndani ya Muungano.

Kumbuka kuwa tanganyika kujivika koti la Tanzania sio sababu ya kudhulumu haki za Zanzibar. Kumbuka kuwa Znz ni nchi kamili inayotambulika na Muungano wa Tanganyika na Zanzibar.
Katiba ya Zanzibari ya Mwaka 1984 kama ilivyorekebishwa mwaka 2009:
ibara ya 3 na 4
1. "Zanzibar ni Nchi ambayo eneo la mipaka yake ni eneo lote la Visiwa
vya Unguja na Pemba pamoja na Visiwa vidogo vilivyoizunguka na bahari
yake ambayo kabla ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar ikiitwa Jamhuri ya Watu wa Zanzibar"

Tatizo huyu Kikwete amekuwa legelege mno! Ingekuwa enzi za Mwalimu "hawa wote" wangeitwa Magogoni na baadaye kuwekwa 'kizuizuni' Kigamboni. Muulizeni Aboud Jumbe Mwinyi. Kama ZNZ ni nchi Rais gani angekubali kufanywa hivyo?

Pinda aliwaambia bila kumung'unya maneno ZNZ sio nchi, Mahakama kuu ilishasema ZNZ sio nchi. Kikwete legelege akarikoroga eti ZNZ ni nchi ndani ya mipaka JMT na ZNZ sio nchi nje ya mipaka JMT.

BLW limeondoa suala la mafuta na gasi asilia kwenye mambo ya Muungano. Khatibu akawaambia hicho wanachofanya BLW ni utoto, chombo chenye mamlaka ya kuliondoa hilo suala ni Bunge la JMT. Kikwete anaona haya yote lakini anayanyamazia. Matokea yake ZNZ wamefanya mabadiliko haramu kwenye katiba yao, yanayokinzana na katiba ya JMT ambayo ndiyo mama.

Historia inatufundisha kwamba hakuna nchi yoyote dunia iliyotoakipande cha ardhi yake in a siliver plate, Tangia East Timor, Sudan ya Kasikazini, mpaka leo N. Ireand, Taiwan wanapigania, Nchi zilizokuwa Jamhuri za Yugoslavia, Russia etc.

Kama wanzazibari wanataka kuirudisha nchi yao kutoka Tangayika, Jussa na wenzake waende msituni waone kilichomnyoa kanga manyoa. Au wamesahau yaliyompata Nduli Idd Amin Dada.

SMZ ni sawa serikali za Kijiji, wilaya, mkoa kama ilivyo huku Tanzania bara, tofauti ni kwamba wao wanaye ceremonial president. Rais gani wa nchi ambaye hata akienda Burundi hawezi kupigiwa mizinga 21? Sasa huyu ana tofauti gani na Rais wa TFF? Tuwaambie ukweli hawa wazanzibari ili wafahamu status quo yao, mambo ya kulembalemba ya JK hayana nafasi kwenye masuala ya kisheria.
 
Mwanakijiji.

Ni vizuri ukajuwa wazi Bila Zanzibar basi hakuna Katiba ya Muungano wala Muungano. Kwani ili kuwepo na Tanzania ni lazima ipatikane Tanganyika na Zanzibar. Na hakutakuwa na katiba yya muungano bila kuwa na Katiba ya Zanzibar. Kwani vyote vinategemeana.

Na katiba ya Zanzibar ndiyo inayoifanya Tanzania na katiba ya Tanzania kwani inatambua uwepo wa Rais wa Znz na BLW.

Wewe sio SHARIA hivyo kuitambua au kutoitambua sio tatizo kwa Znz wala muungano. Na sawa tu na maoni yako tu wala haiwashughulishi wa Znz kula chakula au kudai haki zao katika Muungano. Kumbuka huo ni muungano na sio Mvungano. wote mpo sawa mbele ya sheria za muungano.

Nakumbuka Raid Karume 1 aliwahi kusema wazi kabisa kuwa Muungano ni kama koti. Likikuchosha unalivua. Hivyo sio kosa kuuvunja kama kuna kudhulmiana au jamii moja kujiona bora kuliko wengine.

Katiba ya Znz inasema hivi.
Katiba ya Zanzibari ya Mwaka 1984 kama ilivyorekebishwa mwaka 2009:
ibara ya 3 na 4
1. "Zanzibar ni Nchi ambayo eneo la mipaka yake ni eneo lote la Visiwa
vya Unguja na Pemba pamoja na Visiwa vidogo vilivyoizunguka na bahari
yake ambayo kabla ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar ikiitwa Jamhuri ya Watu wa Zanzibar"

Katiba ya JMT imo humu. Isome ikusaidie. Nchi ina Katiba moja tu. Katiba nyingine zote zinatokana na katiba hii. Inapotokea kuna mgongano kati ya katiba ya JMT na hizo nyingine inayofuatwa ni katiba ya JMT. Hili nalo ni gumu kuelewa kweli? Au ni kwa kuwa Uarabuni mambo ni ya kifalme na kisultani?
 
Mzee Barubaru nachelea kukuita mwongo kwa umri na elimu yako. Bunge letu la JMT limekaa lini likayaondoa mafuta na gas asilia. Unazijua taratibu za kuliondoa suala hili kwenye mambo ya Muungano?
Hili la ving'ora na ulinzi lisikupe shida. Hata harusi na misiba kuna ving'ora pia na ulinzi mkali. Jamaa hawa hawamo kwenye Katiba yetu ya JMT.

Kumbuka kuwa ninaposema ving'ora ninamaanisha msafara.

Na msafara wowote kisheria ni ule unao ongozwa Polisi. Ambao kwa Tanganyika ni watu watatu tu ki protocal wanapata hiyo nao ni waziri mkuu, Rais na Makamo wa Rais wa Muungano. Na maalim Seif na Balozi Iddi wanapewa sawa nao pasi na kumsahau Rais wa Znz. wakiwa tanganyika.

je unasemaje hapo? je hawatambuliwi? kama hawatambuliwi kwanini wapewe status ya juu namna hiyo kwene mapokezi na misafara yao?
Pitia sheria vizuri utambue msafara ni nini?
 
usikurupuke WC,

Je unajuwa tofauti ya Jamhuri na Serikali?
tunaomba utupe darsa kidogo hapo la jamhuru ni nini na Serikali ni nini ili tuweze kuendelea na mujadila.

Mfano rahisi kabisa: Zanzibar sio Jamhuri ni Serikali.
 
Kumbuka kuwa ninaposema ving'ora ninamaanisha msafara.

Na msafara wowote kisheria ni ule unao ongozwa Polisi. Ambao kwa Tanganyika ni watu watatu tu ki protocal wanapata hiyo nao ni waziri mkuu, Rais na Makamo wa Rais wa Muungano. Na maalim Seif na Balozi Iddi wanapewa sawa nao pasi na kumsahau Rais wa Znz. wakiwa tanganyika.

je unasemaje hapo? je hawatambuliwi? kama hawatambuliwi kwanini wapewe status ya juu namna hiyo kwene mapokezi na misafara yao?
Pitia sheria vizuri utambue msafara ni nini?
KATIBA ya JMT inawatambua Maalim na Balozi Seif? Hata Mama Asha Rose Migiro akija hapa anasindikizwa na polisi!
 
Mamlaka ya JMT ni kamili. Eneo la jamhuri ya Muungano ni eneo zima la bara na visiwani. Hakuna eneo lolote la 'nchi ya Zanzibar' ambalo si eneo la JMT. Kama lipo niambie. Katiba ya ZNZ inaweza kusema lolote lakini ikipingana na ile ya Muungano vipengele vyake ni batili. Zanzibar ni nchi kwa Wazanzibari tu; siyo nchi inayotambulika mahal popote duniani. Kuwa na jeshi, mahakama, na rais (mihimili mitatu ya dola) hakuifanyi ZNZ kuwa nchi vinginevyo miye ningetamba niko "nchi" ya Michigan! Kuongeza eneo la bahari kutakuwa na manufaa kwa Zanzibar na kwa Tanzania nzima. Wananchi wa ZNZ yawapasa wafurahi na kuunga mkono uamuzi huu wa serikali ya JMT.

This is very clear, zaidi ya hapo ni ubishi tu. No more.
 
Back
Top Bottom