Prof Tibaijuka lazima ajiuzulu

Prof Tibaijuka lazima ajiuzulu

Makosa yako ni haya.

1. Wewe wizara yako sio miongoni mwa mambo ya Muungano. Kwanini uliwasilisha wewe na sio waziri wa mambo ya nje?

2. Kwanini usihakikishe kuwa BLW lina taarifa za ongezeko hilo?

3. Je unaweza kuwaeleza wananchi kuwa umeomba eneo gani liongezwe (weka ramani) na sio kusema ukubwa tu (tuone uhalali wake)

4.Je hukuona wewe kuwasilisha kitu cha muungano kimataifa ni kuvunja sheria na katiba za Muungano? Wizara yako si wizara ya Muungano.

Je unajuwa kuwa mumeungana Kimkataba na sio kikatiba na Tz ni muungano wa nchi mbili huru tanganyika na Znz.
Barubaru, hoja zako ni dhaifu sana. Waziri Tibaijuka amesema alitumwa na Rais na wala hakuwakilisha ombi hilo kama waziri wa Ardhi na Makazi. Hivi unajua kuwa Rais ana mamlaka kikatiba kumchagua yeyote kuwa mjumbe wa Tanzania katika suala lolote kwenye Taasisi za Kimataifa? Kama hujui hata mambo madogo kama hayo, ni vigumu sana kujadiliana nawe. Ombi hili liliwakilishwa na timu ya Tanzania iliyoundwa na wajumbe wa kutoka sehemu zote mbili za mwungano, na kiongozi wa Timu hiyo alikuwa ni Prof. Tibaijuka.

Prof. Tibaijuka halazimiki kulitaarifu wala kuomba kibali cha BLW, hawajibiki huko. Kama Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar alihusika, waziri wa ardhi wa Zanzibar alihusika, na wajumbe wengine, kama kulikuwa na haja ya kuliaarifu au kuomba kibali cha BLW, hao ndiyo waliowajibika lakini siyo Prof. Tibaijuka. Hivi huko Zanzibar, BLW halina kazi nyingi? Maana kila kitu mnataka BLW lijadili, sasa kazi ya huyo Rais wenu na Mawaziri wenu ni nini?
 
Baadhi ya watu ni wavivu wa kutafuta taarifa, ninawawekeeni sehemu ya utangulizi wa muhutasari wa ripoti iliyowasilishwa
'UN Commission on the Limits of the Continental Shelf"

(Source: From Executive summary: URT-DOC-001_18-01-2012)

Preface
_____________________________________________________________________________________________________
This Submission by the United Republic of Tanzania ("Tanzania" or "URT") was prepared under the Tanzania Continental Shelf Delineation (TCSD) project.

The preparation of the Submission was undertaken under the guidance of National Steering and Technical Committees chaired by Permanent Secretary of the Ministry of Lands, Housing and Human Settlements Development (MLHHSD) and Director of Surveys and Mapping of Ministry of Lands, Housing and Energy (MLHE) of Zanzibar, respectively. The technical part of the project was carried out by a Technical Core Group (TCG). The following Ministries and Institutions were involved in the preparation of the Submission:

- Ministry of Lands, Housing and Human Settlements Development
- Ministry of Foreign Affairs and International Cooperation
- Ministry of Energy and Minerals
- Ministry of Communication, Science and Technology
- Ministry of Lands, Housing and Energy (Zanzibar)
- Attorney General's Chambers
- Tanzania Petroleum Development Corporation
- Institute of Marine Science - University of Dar es Salaam
- Ardhi University-Dar es Salaam

The above Ministries and Institutions provided experts who formed the Technical Core Group, which had the main responsibility of preparing the Submission. The following are the members of the TCG.

Professor Evelyne I. Mbede – Geologist,

Director of Science and Technology,
Ministry of Communication, Science and Technology
Chairperson TCG

Mr. Pandu S. Makame
– Lawyer,

State Attorney,
Zanzibar – Vice President's Office
Co - Chairperson TCG

Mr. Justo N. Lyamuya – Hydrographer,
Assistant Director - Hydrographic Surveys,
Ministry of Lands, Housing and Human Settlements Development
Secretary TCG

Mr. Abdon D. Makishe – Geophysicist,
Senior Principal Geophysicist,
Tanzania Petroleum Development Corporation,
Deputy Secretary TCG

Mr. John A. Msemwa – Geodesist,
Assistant Director – Topographic and Geodetic Surveys,
Ministry of Lands, Housing and Human Settlements Development,
Member TCG

Mr. Kelvin R. Komba – Geophysicist,
Senior Principal Geophysicist,
Tanzania Petroleum Development Corporation,
Member TCG

Mr. Omary S. Mtunguja – Geophysicist,
Senior Principal Geophysicist,
Tanzania Petroleum Development Corporation,
Member TCG

Professor Desiderius C. P. Masalu – Marine Geophysicist,
Institute of Marine Science - University of Dar es Salaam,
Member TCG

Mr. Adam I. Zuberi – Geologist,
Senior Principal Geologist,
Ministry of Energy and Minerals,
Member TCG

Mr. Issa A. Hemed
– Hydrographer,
Lecturer,
Ardhi University - Dar es Salaam,
Member TCG

Mr. Donald L. Chidowu – Lawyer,
Principal State Attorney,

Attorney General's Chambers,
Member TCG

Mr. Richard A. Maridadi
– Lawyer,
Legal Officer,
Ministry of Foreign Affairs and International Cooperation,
Member TCG

In preparing this Submission, Tanzania consulted with the Republics of Kenya and Seychelles on maritime boundary delimitation issues. The project received scientific data such as bathymetric, geological, geophysical and well data from the Tanzania Petroleum Development Corporation (TPDC), MHHLSD, MLHE, WesternGeco of UK and One Stop Data Shop (OSDS) of UNEP/GRID-Arendal. Technical support was received from UNEP/GRID-Arendal and Geocap AS of Norway, GX Technology of Houston Texas, USA and Bundesanstalt für Geowissenschaften und Rohstoffe (BGR) of Germany. The project received financing from the Government of Tanzania and financial support from the Royal Norwegian Government.

Professor Lawrence Awosika current member of the Commission on the Limits of the Continental Shelf (CLCS) provided technical advice. Mr. Oeivind Loenne from GRID-Arendal of Norway also provided technical advice as consultant. Mr. Harald Sund and Mr. Erlend Kvinnesland from Geocap AS of Norway provided all the necessary support on the usage of the Geocap software.
 
Barubaru, hoja zako ni dhaifu sana. Waziri Tibaijuka amesema alitumwa na Rais na wala hakuwakilisha ombi hilo kama waziri wa Ardhi na Makazi. Hivi unajua kuwa Rais ana mamlaka kikatiba kumchagua yeyote kuwa mjumbe wa Tanzania katika suala lolote kwenye Taasisi za Kimataifa? Kama hujui hata mambo madogo kama hayo, ni vigumu sana kujadiliana nawe. Ombi hili liliwakilishwa na timu ya Tanzania iliyoundwa na wajumbe wa kutoka sehemu zote mbili za mwungano, na kiongozi wa Timu hiyo alikuwa ni Prof. Tibaijuka.

Prof. Tibaijuka halazimiki kulitaarifu wala kuomba kibali cha BLW, hawajibiki huko. Kama Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar alihusika, waziri wa ardhi wa Zanzibar alihusika, na wajumbe wengine, kama kulikuwa na haja ya kuliaarifu au kuomba kibali cha BLW, hao ndiyo waliowajibika lakini siyo Prof. Tibaijuka. Hivi huko Zanzibar, BLW halina kazi nyingi? Maana kila kitu mnataka BLW lijadili, sasa kazi ya huyo Rais wenu na Mawaziri wenu ni nini?

ndugu yangu usitake kubatilisha maneno.

Kumbuka kuwa kuna kupewa rruhusa na kumwakilisha rais.

Kama umeipitia vizuri sana katiba ya muungano imejipambanua kuwa mwenye kazi ya kuiwakilisha Tz katika masuala ya kimataifa na mahusiano ya nje ni Waziri wa mambo ya nje. Kwa mantiki hiyo nasimamia kusema ulitakiwa useme kuwa Tibaijuka alimwakilisha Membe ambaye ni waziri wa mambo ya nje na sio rais.

Kwani issu hiyo haikuhitaji taasisi ya yais kuiwakilisha bali ni wizara ya mambo ya nje na mahusiano ya kimataifa.

Ndio maana nasema kuwa Tibaijuka amevunja sharia aliyetakiwa kuwasilisha alitakiwa kuwa Membe na sio yeye.

Vile vile Rais alimruhusu na sio kumwakilisha kwenye kuwasilisha suala hilo.

nasimama na kusema tena kwa kinywa kipana amevunja sheria za Muungano na lazima ajiengue tu kiungwana.Labda kama una utetezi mwingine

Hapa naona ni kumpigia mbuzi zeze...! Kukusaidia tu ...ni kwamba Prof. Tibaijuka hana kosa lolote na hang'oki ng'o.
 
ndugu yangu usitake kubatilisha maneno.

Kumbuka kuwa kuna kupewa rruhusa na kumwakilisha rais.

Kama umeipitia vizuri sana katiba ya muungano imejipambanua kuwa mwenye kazi ya kuiwakilisha Tz katika masuala ya kimataifa na mahusiano ya nje ni Waziri wa mambo ya nje. Kwa mantiki hiyo nasimamia kusema ulitakiwa useme kuwa Tibaijuka alimwakilisha Membe ambaye ni waziri wa mambo ya nje na sio rais.

Kwani issu hiyo haikuhitaji taasisi ya yais kuiwakilisha bali ni wizara ya mambo ya nje na mahusiano ya kimataifa.

Ndio maana nasema kuwa Tibaijuka amevunja sharia aliyetakiwa kuwasilisha alitakiwa kuwa Membe na sio yeye.

Vile vile Rais alimruhusu na sio kumwakilisha kwenye kuwasilisha suala hilo.

nasimama na kusema tena kwa kinywa kipana amevunja sheria za Muungano na lazima ajiengue tu kiungwana.Labda kama una utetezi mwingine

Barubaru,
Tafadhali sema ni sheria ipi imevunjwa? Ni kifungu gani cha KATIBA ya JMT kimekiukwa? Usiniambie nenda kasome. Umebaini sheria iliyovunjwa tuambie. Muulize hata Jussa atusaidie. Hili jambo sio SIASA. Tunaongelea MIPAKA ya JMT.
 
Umekosa hoja,

Sheria inayotumika kuwasilisha maombi ni sheria ya "Territorial Sea and Exclusive Economic Zone Act, Cap 238 R.E. 2002" iliyofanyiwa marekebisho kwa sheria "Act No.17 of 2009" ambayo pia inatumika kwa Zanzibar. Waziri mwenye jukumu la mambo ya bahari EEZ ni waziri husika na siyo waziri wa mambo ya nje. Kwa hiyo, Tibaijuka hajavunja sheria yoyote, isipokuwa wewe unakosa uelewa wa sheria zinazotumika. Kwenye kuwasilisha maombi alikuwepo pia balozi wa Tanzania kwenye umoja wa mataifa, na waziri ofisi ya makamu wa kwanza wa rais Zanzibar. Pia kwenye kamati ua UN ya mambo ya bahari, wanaoenda kutetea maombi ya Tanzania sio waziri wa mambo ya nje, bali ni waziri wa ardhi wa wizara iliyoratibu mchakato wa utayarishaji maombi.
 
suala la kujiuliza
Kama kweli Tanganyika ina utajili wote huo, Mbona masikini?

Out of point. Hiyo ni maada nyingine. Nenda kwa mtiririko. Ukweli unabaki pale pale kuwa Tanganyika ina rasilimali kubwa ya maji, kama haya maji mengi tuliyonayo hajatupa utajiri, maji kiduchu ya Zanzibar hayawezi kutupa utajiri.
 
Umekosa hoja,

Sheria inayotumika kuwasilisha maombi ni sheria ya "Territorial Sea and Exclusive Economic Zone Act, Cap 238 R.E. 2002" iliyofanyiwa marekebisho kwa sheria "Act No.17 of 2009" ambayo pia inatumika kwa Zanzibar. Waziri mwenye jukumu la mambo ya bahari EEZ ni waziri husika na siyo waziri wa mambo ya nje. Kwa hiyo, Tibaijuka hajavunja sheria yoyote, isipokuwa wewe unakosa uelewa wa sheria zinazotumika. Kwenye kuwasilisha maombi alikuwepo pia balozi wa Tanzania kwenye umoja wa mataifa, na waziri ofisi ya makamu wa kwanza wa rais Zanzibar. Pia kwenye kamati ua UN ya mambo ya bahari, wanaoenda kutetea maombi ya Tanzania sio waziri wa mambo ya nje, bali ni waziri wa ardhi wa wizara iliyoratibu mchakato wa utayarishaji maombi.

Suala dogo tu kwako. Je Tibaijuka au wizara yake ni wizara ya muungano? Pitia katiba uone suala la ardhi na makaazi kuona kama ni suala la Muungano?

Je Tibaijuka aliwakilisha kama suala la Tanganyyika au la muungano? Elewa mipaka yake ni bara tu na sio muungano kwa mujibu wa sharia zenu.

Naomba majibu yako hapo.

ndugu yangu usitake kubatilisha maneno.

Kumbuka kuwa kuna kupewa rruhusa na kumwakilisha rais.

Kama umeipitia vizuri sana katiba ya muungano imejipambanua kuwa mwenye kazi ya kuiwakilisha Tz katika masuala ya kimataifa na mahusiano ya nje ni Waziri wa mambo ya nje. Kwa mantiki hiyo nasimamia kusema ulitakiwa useme kuwa Tibaijuka alimwakilisha Membe ambaye ni waziri wa mambo ya nje na sio rais.

Kwani issu hiyo haikuhitaji taasisi ya yais kuiwakilisha bali ni wizara ya mambo ya nje na mahusiano ya kimataifa.

Ndio maana nasema kuwa Tibaijuka amevunja sharia aliyetakiwa kuwasilisha alitakiwa kuwa Membe na sio yeye.

Vile vile Rais alimruhusu na sio kumwakilisha kwenye kuwasilisha suala hilo.

nasimama na kusema tena kwa kinywa kipana amevunja sheria za Muungano na lazima ajiengue tu kiungwana.Labda kama una utetezi mwingine

Unaweza kutamka kwa kinywa kipana kama cha kiboko lakini kama kinachotoka katika kinywa hicho hakina mantiki inakuwa ni sawa na kutamka kwa kinywa kidogo kama cha kinyonga. Utamke usitamke hakuna kitakachobadilika. Kutamka unaweza kutamka chochote lakini kama hakina maana kitapuuzwa tu, kwani kuna wangapi wanatamka?
 
Suala dogo tu kwako. Je Tibaijuka au wizara yake ni wizara ya muungano? Pitia katiba uone suala la ardhi na makaazi kuona kama ni suala la Muungano?

Je Tibaijuka aliwakilisha kama suala la Tanganyyika au la muungano? Elewa mipaka yake ni bara tu na sio muungano kwa mujibu wa sharia zenu.

Naomba majibu yako hapo.

Sheria iliyotumika ina-apply na Zanzibar, na isitoshe anayewasilisha maombi ni lazima nchi yake iwe ni mwanachama wa UN. JMT ndiyo mwanachama wa UN, na mipaka ya JMT ni pamoja na visiwa vyote vya Zanzibar.

Pamoja na hayo. Prof. Tibaijuka keshatolea ufafanuzi, ikiwa hujaridhika, ni matatizo yako mwenyewe.
 
Barubaru,
Tafadhali sema ni sheria ipi imevunjwa? Ni kifungu gani cha KATIBA ya JMT kimekiukwa? Usiniambie nenda kasome. Umebaini sheria iliyovunjwa tuambie. Muulize hata Jussa atusaidie. Hili jambo sio SIASA. Tunaongelea MIPAKA ya JMT.

Nafikiri ni vizuri ujue wizara za muungano na mamlaka yake na wizara zisizo za muungano na mamlaka yake. zimepambanuliwa vizuri katika katiba zipitie kisha utaona tupo wapi na nasimamia wapi.

Lakin Hata ukisoma majibu ya Tibaijuka utaona kabisa hamna kitu.

Jusa ameongelea suala hili Barazani (kwenye BLW) na kuomba majibu kutoka SUK Zanzibar. yeye kama waziri wa tanganyika alitakiwa akae kimya kama amesoma mambo ya kidiplomasia. Kwani suala lipo katika muhimili wa BLW na SUK na litakapo iva basi na kukiwa na budi ya kuulizwa basi watafanya hivyo kwa kufuata itifaki.

nachelea kusema enzi zetu tupo Tz kwa madaraka kama waziri au kiongozi wa Serikali tulikuwa tunapelekwa pale chuo cha Diplamasia opposite Mgulani JKT kupata mafunzo kwa wiki tatu ndio uanze kazi. Sijui kama utaratibu huo bado upo siku hizi.

Naona tumekwenda kwenye ififaki sasa...teh teh teh. Kweli kuishi ni kuona mengi.
 
Na Mwinyi Sadallah
23rd January 2012

Chama cha Wananchi (CUF) kimesema kwamba kitapinga Umoja wa Mataifa (UN) kuiongezea Tanzania mipaka ya eneo la kiuchumi la bahari Kuu kabla ya kupatikana muafaka kati ya Serikali ya Muungano na Zanzibar.

Tamko hilo limetolewa na Naibu Katibu Mkuu na Mkurugenzi mambo ya nje wa Chama hicho, Ismail Jussa Ladhu, alipokuwa akihutubia mkutano wa hadhara uliyofanyika katika uwanja wa Gombani ya Kale huko kisiwani Pemba jana.

Alisema Serikali ya Muungano imefanya makosa kuandaa kupeleka maombi ya kutaka kuongezewa mipaka ya eneo tengefu la kiuchumi la bahari kuu (EEZ) bila ya kushirikisha Zanzibar.

Jussa alisema wananchi wa Zanzibar wapo tayari kupoteza maisha lakini hawatokubali eneo la bahari Kuu la Zanzibar kuongezwa na kuwa sehemu ya eneo la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

"Wananchi wa Pemba simameni kidete kutetea maslahi ya Zanzibar hata kama tutamalizika sote haiwezekani eneo la bahari Kuu la Zanzibar kuwa la muungano," alisema Jussa.

Alifafanua kuwa Januari 16 mwaka huu Waziri wa Ardhi nyumba na Maendeleo ya Makazi, Profesa Anna Tibaijuka, alitangaza mpango wa Tanzania kuomba UN kuiongezea maili 150 sawa na kilometa 241.5 kutoka usawa wa mwambao wa Tanzania.

Profesa Tibaijuka alisema kazi ya kukamilisha andiko hilo ilianza mwaka 2007 na kugharimu Sh. Bilioni 5.2 na kushilikisha wataalamu kutoka sekta ya mbalimbali, ili iweze kulifanyia utafiti zaidi kuhusu rasilimali zilizoko chini ya bahari kwa lengo la kuinua uchumi wa nchi.

Jussa alisema mpango huo umelenga kuiwezesha serikali ya Muungano kuongezewa eneo hilo ili kufanikisha mpango wake kufanya utafiti na uchimbaji wa mafuta wakati SMZ imekwishaliondoa kwenye orodha ya mambo ya muungano.

Hata hivyo, alisema mpango wa Tanzania kuongezewa eneo la maili 150 kutoka usawa wa bahari ya Hindi umefanyika bila ya kuishilikisha SMZ.

Jussa ambaye pia mwakilishi wa jimbo la Mji Mkongwe, alisema alipohoji suala hilo ndani ya Baraza la Wawakilishi Zanzibar (BLW) alitakiwa na serikali kuwa na subira na kutoa nafasi kwa serikali ya SMZ kulifuatilia.

Alisema suala la mafuta na gesi asilia tayari SMZ imeamua tangu mwaka 2009 kuliondoa katika orodha ya mambo ya muungano na haikuwa muafaka kwa serikali kupeleka maombi hayo bila ya kupata baraka ya Zanzibar.

"Wenzetu wanataka kuchimba mafuta na gesi asilia ya Zanzibar kwa kutumia mlango wa nyuma hatukubali kwa maslahi ya Zanzibar na nchi yetu," alisema Jussa.

Kuhusu kufukuzwa kwa viongozi wanne wa CUF akiwemo Mbunge wa Wawi Hamad Rashid Mohammed, alisema viongozi hao wamekwenda kinyume na misingi ya kuanzishwa kwa chama hicho mwaka 1992.

Alisema CUF ilianzishwa kwa madhumuni makubwa ya kupingania haki za Zanzibar na wananchi wake ikiwemo mfumo wa Muungano.

Jussa alisema katika kupingania haki za Zanzibar ndiyo maana wapo watu wamepoteza maisha na wengine kupata ulemavu wa kudumu ndiyo maana chama kimeamua kuwafukuza viongozi hao baada ya kwenda kinyume na misingi ya kuanzishwa kwake.

Kwa upande wake, Mkurugenzi wa haki za Binadamu na mahusiano ya umma Salim Biman, alisema kwamba viongozi waliyofukuzwa ndani ya CUF waliweka maslahi binafsi mbele badala ya maslahi ya chama na wanachama wake.

Awali akisoma risala ya mikoa miwili ya wanachama wa CUF Kisiwani Pemba, Ayoub Yussuf Mgeni, alisema wanachama wanaunga mkono maamuzi ya Baraza Kuu la Uongozi kwa kuwatimu viongozi hao.

Alisema viongozi hao ni wasaliti kutokana na kitendo chao cha kutetea maslahi binafsi na kuwapaka matope viongozi wa kitaifa kwa kutaka kuwagawanya kwa mtazamo wa Uunguja, Upemba na Utanzania Bara.

Alisema CUF kimefanya kazi kubwa kupingania misingi ya haki za binadamu na utawala bora hadi kufanikiwa kuundwa kwa serikali ya Umoja wa Kitaifa Novemba mwaka 2010.

Alisema tangu kundwa kwa serikali hiyo kesi za kisiasa, ubaguzi na ukikwaji haki za binadamu umeondoka kwa wananchi wa Zanzibar.

Aliongeza kuwa hatua kama hizo zinapaswa kuendelea kuchukuliwa kwa mwanachama yoyote anayetaka kuvuruga umoja wa kitaifa kwa wananchi wa Zanzibar.

Mapema Katibu Mkuu wa chama hicho, Maalim Seif Sharif Hamad, ambaye pia Makamu wa kwanza wa Rais, alipokea maadamano ya amani ambayo yalinzia huko Machomanne kupitia Mkanjuni huku wanachama wakiwa wamebeba mabango ya kumshutumu Mbunge wa Wawi aliyevuliwa uanachama Hamad Rashid Mohammed.

Baadhi ya mabango yalisomeka ‘Tumekukuta Wawi na shuka kiunoni, tumekupeleka Dodoma na suti leo watusaliti'; ‘Tamaa imekuponza, siasa hukuweza rudi Wawi ukavue' na lingine likisema ‘Hamad umepanda upepo utavuna dhuruba'

CHANZO: NIPASHE

My Take:

Kwa kosa alilolifanya kupeleka ombi Un Pasi na kupata baraka za baraza la wawakilishi Znz wakti anajua fika suala la ardhi sio suala la muungano ni utovu mkubwa sana wa nidhamu na kutaka kufanya ubabe na kuvunja katiba ya Muungano na ile ya Zanzibar. Kiungwana anatakiwa ajiuzuru.
Hivi kwani Zanzibar inatambulika huko UNO? mi nafikiri Zanzibar ni kama Tabora au mikoa mingine ya bara tu.Hata FIFA haiwajui jamani,inayojulikana ni Tanzania tu,hizo kelele za chura hazimzuii tembo kunywa maji kwenye dimbwilake bana
 
Sheria iliyotumika ina-apply na Zanzibar, na isitoshe anayewasilisha maombi ni lazima nchi yake iwe ni mwanachama wa UN. JMT ndiyo mwanachama wa UN, na mipaka ya JMT ni pamoja na visiwa vyote vya Zanzibar.

Pamoja na hayo. Prof. Tibaijuka keshatolea ufafanuzi, ikiwa hujaridhika, ni matatizo yako mwenyewe.

Labda nikuulize ni nchi gani hiyo?

Kwani mamlaka ya Tibaijuka kwa mujibu wa sharia zenu ni mambo yote ya ardhi na makaazi kwa Tz bara (tanganyika tu) na Mh Shamhuna ni mamlaka yake ni kwa Znz tu.

Kumbuka kuwa Wizara ya Ardhi sio wizara ya muungano. Kwa msingi huo Tibaijuka hana uwezo wowote kisheria kuwakilisha Tanzania kwa lolote lile (unaposema Tz maana yake ni Tanganyika na Zanzibar).

Ukiangalia vizuri na kuipitia vizuri katiba yenu utaona mwenye mamlaka ya kuwasilisha ombi hilo ambalo ni la muungano ni waziri wa mambo ya nje na mahusiano ya kimataifa.

Je unajuwa kwanini Membe ni waziri wa mambo ya nje na uhusiano wa kimataifa? je unajuwa kwanini akaongezewa kipengele hicho cha uhusiano wa kimataifa?

Soma katiba vizuri sio kubababisha.

Hivi kwani Zanzibar inatambulika huko UNO? mi nafikiri Zanzibar ni kama Tabora au mikoa mingine ya bara tu.Hata FIFA haiwajui jamani,inayojulikana ni Tanzania tu,hizo kelele za chura hazimzuii tembo kunywa maji kwenye dimbwilake bana

Wewe sio sheria.

Kuitambua au kutoitambua hakuongezi au kupunguza kitu kwa Zanzibar na waZanzibar.

Ukweli utasimama daima. Na sharia lazima ifuatwe na kusimamiwa bila kuogopana wala kudhulumiana. wote mpo sawa mbele ya muungano na sharia.

Nafikiri ni vizuri ujue wizara za muungano na mamlaka yake na wizara zisizo za muungano na mamlaka yake. zimepambanuliwa vizuri katika katiba zipitie kisha utaona tupo wapi na nasimamia wapi.

Lakin Hata ukisoma majibu ya Tibaijuka utaona kabisa hamna kitu.

Jusa ameongelea suala hili Barazani (kwenye BLW) na kuomba majibu kutoka SUK Zanzibar. yeye kama waziri wa tanganyika alitakiwa akae kimya kama amesoma mambo ya kidiplomasia. Kwani suala lipo katika muhimili wa BLW na SUK na litakapo iva basi na kukiwa na budi ya kuulizwa basi watafanya hivyo kwa kufuata itifaki.

nachelea kusema enzi zetu tupo Tz kwa madaraka kama waziri au kiongozi wa Serikali tulikuwa tunapelekwa pale chuo cha Diplamasia opposite Mgulani JKT kupata mafunzo kwa wiki tatu ndio uanze kazi. Sijui kama utaratibu huo bado upo siku hizi.

Kumbe wewe Mzee mtupu sana kwa mambo ya Tanzania. Katiba yetu ina wizara za Muungano? Ibara ipi hiyo? Acha kuhangaika na SIASA za TANZANIA. Ngumu. Hauziwezi. Vinginevyo nitashindwa kukutofautisha na Jussa aliyelelewa na Maalim Seif pale Starlight.
 
Kwenye katiba yenu imepambua wazi kuwa kuna wizara zenye sura na muundo wa muungano. Mfano wizara ya mambo ya nje, Ndani, afrika mashariki n.k Na ukizitizama wizara hizi kama waziri wake akitoka upande mmoja wa muungano basi naibu wake atatoka upande mwingine wa Muungano.

Kuna wizara zisizo kuwa na sura ya muungano. Mfano wizara ya Afya, elimu, biashara, fedha ,katiba n.k.

Ukitaka kujua wizara zenye muundo na sura ya kimuungano zimetokea wapi pitia mkataba wa Muungano baina ya tanganyika na zanzibar. na kuona mambo mliyokubalina kushirikiana.

Ndio maana ninasema kikatiba Tibaijuka hana mandate yoyote kuiwakilisha Tz kwa maana ya tanganyyika na Zanzibar kwa sabbabu katiba hiyo haimruhusu.

Atakuwa amevunja katiba. na lazima kama muungwana ajiuzuru.

Unazungumza mambo meeeeengi lakini inaelekea hujui eneo gani lililo ombwa.

Je unaweza kutujuza ni eneo gani lililo ombwa.

Ikiwezekana tuwekee ramani ili tuanze kuzichambua sheria na kuona nani ana uhalali wa kuomba.

Lakini pia Tz ni muungano wa nchi mbili na zimeungana kimkataba. Je mkataba huo ukivunjika nani atamiliki nini kutoka katika eneo hilo?

Vile vile kwanini ombi hilo amewasilisha Tibaijuka waziri wa ardhi wa Muungano (tanganyika) na sio waziri wa mambo ya nje B Membe? Kwani ardhi halimo katika hati ya mkataba ya muungano wa nchi hizo?

Hayo ni masuala ya msingi kuyajua kabla kuvamia mada hii. na kama una majibu basi tuwekee ili tukuone una upeo kiasi gani nasi tutakujuza pale usipopajua katokana na sakata hili.

naomba upitie kisha tuanze kuzichambua sheria tuone nani ana haki zaidi hapo.

Nimeonyesha eneo liliombwa na inaelekea huelewi Kiingereza soma hapo utaona nimezungumzia "Continental Shelf" wewe hilo hulifahamu. Usiwe mbishi kama mshipa.
 
Kwenye katiba yenu imepambua wazi kuwa kuna wizara zenye sura na muundo wa muungano. Mfano wizara ya mambo ya nje, Ndani, afrika mashariki n.k Na ukizitizama wizara hizi kama waziri wake akitoka upande mmoja wa muungano basi naibu wake atatoka upande mwingine wa Muungano.

Kuna wizara zisizo kuwa na sura ya muungano. Mfano wizara ya Afya, elimu, biashara, fedha ,katiba n.k.

Ukitaka kujua wizara zenye muundo na sura ya kimuungano zimetokea wapi pitia mkataba wa Muungano baina ya tanganyika na zanzibar. na kuona mambo mliyokubalina kushirikiana.

Ndio maana ninasema kikatiba Tibaijuka hana mandate yoyote kuiwakilisha Tz kwa maana ya tanganyyika na Zanzibar kwa sabbabu katiba hiyo haimruhusu.

Atakuwa amevunja katiba. na lazima kama muungwana ajiuzuru.

Kwa maneno yako ina maana Tanzania hakuna wizara za mwungano bali zipo zenye sura na muundo waa mwungano. Kwenye katiba ya Tanzania hakuna mahali popote ambapo Rais anazuiwa kumchagua mtu kutoka upande wowote wa mwungano kuongoza wizara zisizo na sura ya mwungano. Kukosekana kwa ukomo huo, ndiyo kulikomfanya Rais Mwinyi kumchagua Mzanzibari kuongoza Wizara ya Mali ya Asili na Utalii ambayo huimamia mambo ya bara tu. Hata hiyo unayodai kuwa kwenye wizara za mwungano, kama Waziri akitoka Bara, naibu hutoka visiwani na kinyume chake, ni maamuzi tu ya Rais, lakini hakuna sheria inayomlazimisha kufanya hivyo.

Mimi sishangai kwa wenzetu Wazanzibari, wao ni wazuri sana katika kupiga porojo, na wanafurahia. Tabia hiyo ya kufurahia porojo, majungu na mikwaruzano ndiyo iliyoiweka Zanzibar mahali ilipo leo. Naambiwa nyumba zile alizowajengea marehemu Karume hawataki kulipa hata kodi ya pango, hawataki kulipia maji lakini bomba lilikipasuka tu, kesho yake wapo kwenye ofisi za maji kutoa taarifa kuwa, 'mfereji umepasuka yakhe, mwende mkazibe'. Kazaneni kupiga maneno labda yatawasaidia lakini kama mngeacha kuendekeza maneno, Zanzibar leo hii isingekuwa ilipo. Chini ya ukoloni, Zanzibar ilikuwa juu sana kuliko mji wowote wa bara lakini leo Zanzibar inafanana na baadhi ya makao makuu ya wilaya za bara. Wenzenu wanachapa kazi, ninyi mmekalia maneno na porojo zisizo na msingi.
 
Naomba nikuweke sawa kidogo kwani kuna mambo umeyasahau kidogo.

Tanganyika na Znz zimeungana kimkataba na sio kikatiba. Kuna mambo yamo katika mkataba huo nayo ndio mambo ya muungano. Suala la ardhi na makazi si suala la Muungano na ndio maana Znz kuna waziri wa wizara hiyo na Bara yupo.

Kumbuka kuwa Mamlaka ya Tibaijuka mwisho wake ni Chumbe akiwa Znz hana mamlaka yoyote ukilinganisha na waziri wa mambo ya nje au mambo ya ndani. hawa wana malka kote kote.

Kumbuka vile vile Znz ni nchi kamili yenye mamlaka kamili na hilo limebainishwa katika katiba ya Znz. Kwa msingi huo Katiba hiyo hiyo imeanisha eneo la Znz kiufasaha kabisa. sasa kwa ombi hilo la Tibaijuka ni lazima katiba ya Znz itabidi ibadilike kwa kuongeza eneo la milki yake au kupunguza miliki yake na hapo ili kubadilisha kipengele hicho cha katiba lazima BLW litahusika vilivyo kwani wao ndio wtunzi wa sheria za Znz na mambo yote yaliyo nje ya muungano.

Kumbuka kuwa katika Picha walopiga kule UN wakti wanawakilisha alikuweo Tibaijuka, balozi wa Tz katika UN, Mbunge wa Mafia na Katibu wa wizara kutoka Znz. Kwa mantiki hiyo inaonekana wazi Prof Tibaijuka alipata baraka zote za Bunge la Muungano dio maana akachukua muwakilishi wa Bunge.

Sasa upande wa BLW hawakuwa na taarifa zozote ongezeka hilo officially na aliku husishwa kwa lolote lile kitu ambacho Jussa amehoji. Ikumbukwe kuwa maombi haya yakifanikiwa lazima BLW litahusishwa katika kupitisha sheria za ongezeko la eneo la miliki la Znz.

sasa labda tujiulize.
Je Znz itaongezewa kiasi gani katika hicho kilicho ombwa? hilo ni suala ambalo limegubikwa na utata mkubwa na alijabainishwa katika mkataba au mbi hilo.

Lakini pia lazima ufahamu kuwa Tz na Znz zote zinaongozwa na Rules of Law. Na mihimili yote mikuu inajipambanua yaani Serikali, Bunge na Mahakama bila kuingilia katika utendaji kazi wake. Kila muhimili unajitegemea.

Limeanza baraza la wawakilishi kuhoji Serikali ya Znz kisha uzi utafuata. Kwani majibu ya Serikali ndio yatatoa mwangaza kwa sakata hilo. Lakin all in all Tibaijuka lazima ajiuzuru hapo.

Kwani mtiririko wa jambo hili unakuwa sawa kabisa na ule wa Tz kujiunga na OIC.

Pamoja na kujitahidi kutoa maelezo marefu lakini umesahahu suala moja tu kwamba Zanzibar ni nchi kwa mujibu wa wazanzibar, lakini nchi hiyo haiko kwenye ramani ya dunia. Sisi tuanaifahamu Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, na hii nchi ndiyo yenye kiti UN. Sasa huu uroho wenu watu wa design ya Jusa utawapeleka pabaya. Mimi nafikiri dont hit around the bush, mje wazi na kusema hatuutaki huu muungano. Na kwa kweli kwetu sisi tusio ijua vizuri CUF sasa inathibitika wazi kuwa agenda yao na Zenji na Zenji alone. Wale wana CUF mlioko bara tafuteni muelekeo mwingine kabla hamjachelewa, wenzenu kule wameamua kufa na kupona.
 
Back
Top Bottom