Ukiangalia katika masuala mbalimbali, picha tunayoipata ni kuwa wengi wa Wazanzibari ni Wabinafsi na Wachoyo. Hii hofu ya kufikiria kuwa eneo litakaloongezwa litakuwa la Tanganyika, na Wazanzibari watanyang'anywa eneo lao inatokana na nini? Hivi tangu mwungano huu uanzishwe ni kitu gani Wazanzibari wamenyang'anywa na Tanganyika? Hivi katika mambo haya ambayo tunayowafadhili Wazanzibari, Wazanzibari wanaweza kuwafanyia Watanganyika?
Wengi wao wamesomeshwa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam bure, kwa kulipiwa na serikali ya Tanzania (Tanganyika); kwa muda mrefu wamepewa umeme bure; wabunge wao licha ya kuwakilisha watu wachache sana wanapewa haki zote sawa na wabunge wa bara ambao wanawakilisha maelfu ya watu ambao wanachangia bajeti ya mwungano karibu kwa 100%, Wazanzibari wamewahi kupewa uwaziri kuongoza wizara za serikali ya Tanzania zisizo za mwungano, Wazanzibari wanamiliki mashamba Tanzania bara, n.k. Hawa watu hawana hata shukrani, na upole wa Tanganyika unawafanya wadeke sana. Sidhani kama Tanganyika ina haja hata na bakuli moja ya maji ya bahari ya Zanzibar. Tanganyika ina Pwani ya bahari toka Tanga hadi Mtwara, ina maziwa: Ziwa Nyasa lenye dhoruba kubwa kuliko maziwa yote Duniani, ina Ziwa Tanganyika lenye kina kirefu kuliko yote, ina Ziwa Victoria ambalo ni kubwa kuliko yote; yapo na mengine kama Eyasi, Manyara n.k. Tanganyika ina mito mikubwa na mirefu inayotiririsha maji usiku na mchana, masika na kiangazi, halafu iende ikaipokonye Zanzibar bahari yake kwa lengo gani? Tangayika ina uwezo wa kuwachukua Wazanzibari wote na kuwapa wilaya moja ya Tanganyika, wakaishi kwa nafasi, na ardhi nyingine ikabakia. Wazanzibari, sisi tunawaona ninyi kuwa ni ndugu zetu, tuna-sacrifice mambo mengi kwaajili ya upendo wetu kwenu lakini hamna shukrani. Kuna siku tutawachoka, tutawaachia na ndipo mtajua thamani ya kile ambacho mmekuwa mkikichezea kwa miaka mingi.