Prof. Mussa Assad: Katiba Mpya ni Muhumu, itamjenga Rais na haitampunguzia chochote

Quinine

JF-Expert Member
Jul 26, 2010
21,271
47,271

Profesa Assad akihojiwa, amesema kuwa katiba mpya ni jambo la muhimu sana
Akasema somo tulilolipata katika utawala uliopita limetuonyesha umuhimu wa kuwa na katiba nzuri.

Profesa Assad amemuambia rais Samia kuwa, yeye kuleta katiba mpya hakutampunguzua chochote bali kutamuongezea credit

MY TAKE:
Samia asiipoteze nafasi hii ya adhimu ya kuwa kiongozi aliyefanya reforms za msingi za kisiasa na kiutawala katika nchi hii.
Samia afahamu tu kuwa Uchumi uko linked na nasuala ya utawala biea na Siasa nzuri na haki katika nchi na mifumo bora na Imara. Msingi wa huvyo vyote ni Katiba bora.

Samia kama anadhani anataka kujenga uchumi chini ya katiba hii, badi atambue tu ni rahisi kweli kwa mtu ajaye kubomoabomoa uchumi alioujenga kwa sababu katiba hii i ampa haki ya kufanya hivyo bila consequences zozote.
 
Katiba mpya haitaleta maendeleo kwa mtu bali uongozi thabiti wa kusimamia katiba iliyopo ndio chachu ya maendeleo.

Nikichukua mfano wa Kenya Katiba mpya haijaleta Ugali mezani mwa mwanakibera bali niliona vurugu zile zile za kisiasa kabla na baada ya katiba mpya.
Tusiwe kasuku wa kuimba umagharibi.

KWA HISANI YA MTU WA TANZANIA
 
Katiba mpya haitaleta maendeleo kwa mtu bali uongozi thabiti wa kusimamia katiba iliyopo.
Nikichukua mfano wa Kenya Katiba mpya haijaleta Ugali mezani mwa mwanakibera bali niliona vurugu zile zile za kisiasa kabla ya katiba mpya.
Tusiwe kasuku wa kuimba umagharibi
Hoja ya ajabu sana
 
Katiba mpya haitaleta maendeleo kwa mtu bali uongozi thabiti wa kusimamia katiba iliyopo ndio chachu ya maendeleo...
Katibu mkuu wa chama cha CCM alikuwa anaamrisha mwenyekiti wa tume ya uchaguzi,msajiri wa vyama vya siasa nk.Sasa najiuliza kama anaweza kuwakemea na kuwaambia ukifanya jambo fulan huna kazi anashindwaje kuwaamrisha kufuta wagombea wa vyama vingine?
KATIBA mpya ni sasa sio baadaye
 
Kwa hiyo unataka kipengele cha katiba chenye kumtaka katibu mkuu asiamrishe??
 
Itaepusha na hayo matamko kila kiongozi anatamka Kama wao ndio katiba.

Na iingizwe kwenye mtaala Kama masomo mengine. Mbona tulisoma dini? Tunaomba katiba mpya inayoenda na wakati uliopo na unaoendelea. Na iwe na muda wa expare date ili isiwasumbue wajukuu zetu.
 
Katiba mpya haitaleta maendeleo kwa mtu bali uongozi thabiti wa kusimamia katiba iliyopo ndio chachu ya maendeleo.

Nikichukua mfano wa Kenya Katiba mpya haijaleta Ugali mezani mwa mwanakibera bali niliona vurugu zile zile za kisiasa kabla na baada ya katiba mpya.
Tusiwe kasuku wa kuimba umagharibi.

KWA HISANI YA MTU WA TANZANIA
Usiiangalie katiba kwa angle ndogo ya kisiasa, iangalie kwa mapama yake kiuchumi, ustawi wa jamii nk.

Katiba ya Kenya inamuwajibisha rais juzi Mahakama ya Kenya ilikataa mapendekezo ya rais ya BBI, Kenya wamezindua satellite yao, juzi wamezindua bandari ya Mombasa, wamezindua SGR sisi bado tunakimbizana kujenga sanamu la mwendazake sijui hilo ndilo litakalokuletea ugali mezani.

Ingekuwa kenya hili sanamu lisingejengwa lingepingwa mahakamani.
 
Katiba mpya haitaleta maendeleo kwa mtu bali uongozi thabiti wa kusimamia katiba iliyopo ndio chachu ya maendeleo.

Nikichukua mfano wa Kenya Katiba mpya haijaleta Ugali mezani mwa mwanakibera bali niliona vurugu zile zile za kisiasa kabla na baada ya katiba mpya.
Tusiwe kasuku wa kuimba umagharibi.

KWA HISANI YA MTU WA TANZANIA
Futeni katiba nchi iongozwe kwa "Matamko ya Rais" kama mnaona si muhimu.
 
Usiiangalie katiba kwa angle ndogo ya kisiasa, iangalie kwa mapama yake kiuchumi, ustawi wa jamii nk.

Katiba ya Kenya inamuwajibisha rais juzi Mahakama ya Kenya ilikataa mapendekezo ya rais ya BBI, Kenya wamezindua satellite yao, juzi wamezindua bandari ya Mombasa, wamezindua SGR sisi bado tunakimbizana kujenga sanamu la mwendazake sijui hilo ndilo litakalokuletea ugali mezani.
SISI TUNA NYERERE DAM,SGR,BOMBA LA MAFUTA.

RWANDA INASONGA MBELE BILA KATIBA MPYA MNAYOITAKA

CHINA IPO VIZURI BILA KATIBA MNAYOITAKA

NAKUSHAURI USIANGALIE MATATIZO KWA ANGLE NDOGO YA KATIBA
 
SISI TUNA NYERERE DAM,SGR,BOMBA LA MAFUTA.

RWANDA INASONGA MBELE BILA KATIBA MPYA MNAYOITAKA

CHINA IPO VIZURI BILA KATIBA MNAYOITAKA

NAKUSHAURI USIANGALIE MATATIZO KWA ANGLE NDOGO YA KATIBA
Kama katiba ni angle ndogo kwako pole, nchi inaendeshwa na katiba, katiba ni kama injini ya nchi.

Miradi yetu mikubwa bado ipo kwenye michakato hakuna hata mmoja uliokamilika wao Kenya wanazindua get the difference.
 
Nchi lazima iongozwe na kiongozi katiba ni mbwembwe tu.
Hata umasaini kuna uongozi na discpline.hawana katiba mnayoitaka
CCM ina Katiba na inaihuisha mara kwa mara, lakini wafuasi wake wanaona hakuna umuhimu wa kuhuisha katiba ya nchi.
 
Nchi lazima iongozwe na kiongozi katiba ni mbwembwe tu.
Hata umasaini kuna uongozi na discpline.hawana katiba mnayoitaka
Kwa akili hizi No wonder why, kwa Tanzania rais ndio anaiongoza katiba badala ya katiba imuongoze yeye.
 
Kama katiba ni angle ndogo kwako pole, nchi inaendeshwa na katiba, katiba ni kama injini ya nchi.

Miradi yetu mikubwa bado ipo kwenye michakato hakuna hata mmoja uliokamilika wao Kenya wanazindua get the difference.
Wewe uliona maendeleo ni angle ndogo mimi naona katiba si lolote si chochote.Uwe na katiba yenye kila kitu hutasaidika iwapo usimamizi hautakuwepo period.

Watu hawaogopi msahafu/biblia wataogopaje Katiba??Think
 
Back
Top Bottom