Press za Polepole kwa sasa hazina tija

Press za Polepole kwa sasa hazina tija

Power yoyote inamuda sahihi ili ilete ufanisi. Muda na sehemu/mahali sahihi ni muhimu katika kurusha vyuma
Muda huo bado, pahara hatujafika bado, ngoja bi mkubwa aingie uwanjani. Atashinda? sijui ila akiwa amechakaa sana, Avae bukta mana si kwa mieleka tegemewa
 
Hamjambo!

Katika vita ya mtandaoni, hasa vita maneno. Kuna kanuni zake.

Unapotupiana maneno na mtu kama unakombora kubwa kuliko haupaswi kulichelewesha sana kama vile katika vita vya silaha mfano Nyukilia ambazo hutolewa kidogo kidogo na kutokea yenye uwezo mdogo kufuatia yenye uwezo Mkubwa

Vita ya maneno ili ushinde lazima uangalie tension, shauku, hamu kubwa ya watazamaji, vita ya maneno watazamaji hutaka kusikia kombora kubwa kuliko hasa likitolewa dakika za mapema kabisa ili kumaliza kazi.

Vita ya maneno hasimu huwa na hofu ya kusemwa zile tabia zake mbaya za siri, usipomsema katika dakika za mwanzo, ukasema mambo ya kawaida. Tayari unampa mazingira ya kuzoea hofu na kisaikolojia ukishazoea hofu ya kile unachotarajia inapunguza uzito wa kombora lenyewe hata likitupwa.

Ikiwa unamchelewesha mtu katika vita ya Maneno jitahidi uwe na taarifa kubwa ya kutisha ambayo yeye(hasimu wako) anajua taarifa hiyo hauna. So inakuwa suprise sio tuu kwa Mashabiki bali hata kwa adui. Na hilo linakuwa pigo moja takatifu ambalo lazima liitwe Knock out.

Sasa Polepole press ya kwanza watu walijua atatuma vyuma vya uhakika, kisha awamu ya pili kutuma ushahidi, yeye watu wanamsubiri wakijua atakuwa na jambo zito. Akaboronga.

Watu wakasema huenda anavuta kasi, kapanga shambulizi la Pili, akaboronga.

Mpaka hasimu zake wamemdharau.
Alafu mbaya zaidi mlengwa Mkuu ambaye ni Rais yupo Kimya.
Na hili nilishaeleza kuhusu mpambano unavyokuwa.

Rais hawezi kujibu shambulizi lililopoa. Na nilimwambia kuwa ukimya wa Rais kwake auhesabu kama ishara ya hatari.

Kikawaida mtu ambaye unajua siri zake ukianzisha vita naye. Kama atakupiga shambulizi lililopoa huwezi mjibu kwani unajua hajamaliza risasi zake. Kwamba kuna risasi anayoitegemea.

Ni tofauti na Gwajima Vs Makonda. Gwajima alipokuwa katika vita vya Maneno na Makonda, Gwajima alianzia moja kwa moja kwenye kiini. Kisha akaacha ngoma imehang huku ushahidi ukiwa unafuata kwa shambulizi alilofanya.

Gwajima Vs Serikali ambao ni kivuli cha watekaji kwa Mujibu wake.

Shambulizi lake alianzia juu na hakuwa na risasi nyingine. Vita ilianza kwa tensioni kubwa.

Rais alimjibu kwa sababu alijua Gwajima amemaliza risasi zake na hana tegemeo jingine tena. Hana kipya atakachoongea.

Polepole yeye katoa shambulio lililopoa Sana. Madhara yake sio makubwa.
Hata kuzima mitandao ni hofu tuu.

Lakini ni kiashiria kuwa Polepole anataarifa nyingi na nyeti sana.

Polepole angerusha mawe mazito hata vipande nusu ambavyo vitamfanya awaabishe adui zake na awapagawishe. Kisha hatua inayofuata aseme anakuja na ushahidi ambao utawashangaza, na aseme atauweke hadharani na kila mtu atauona.

Huku akisema amebakisha vyuma vingine ambavyo vitaitetemesha nchi.

Ukishatoa madai ya kumdhalilisha hasimu wako utakuwa upo nusu ya ushindi. Kuthibitisha utakuwa umemaliza kazi.

Kadiri Polepole anavyochelewa ndivyo mashambulizi yake yanakosa nguvu.
Yaani leo hata aje aseme kitu gani hakitakuwa na nguvu ya maana kama angeshambulia mwanzoni.

Tayari watu wameshazoea, watu wameshapredict, hasimu kashazoea tension jambo ambalo kwenye vita ya maneno sio zuri.

Soma >> GE2025 - Polepole: Kuongea na watanzania Agost 6, saa 2:00 kuhusu mustakabali wa taifa

Polepole hata zile trick za majigambo na mikwala ya kusema yeye yupo tayari kufa lakini lazima hasimu wake alale nao mbele hatilii mikazo katika laini hizo.

Yupo katika vita kubwa lakini anapambana kwa namna laini sana. Jambo ambalo unagundua kuna kitu hakipo sawasawa.

Anyway! Sisi tupo!
Na tutakuwepo!

TaikonMaster
Kwa sasa Dar es salaam
Zinatija sana ila kama unaona hazina tija pita pembeni ukale ugali wako na mandondo ulale!!!
 
Mkuu uchaguzi upo
Ndugu Robert Heriel Mtibeli UCHAGUZI MKUU 2025 HAUPO unless uwe huna macho makali ya ndani kuona hili..

It completely doesn't matter what preparations are going on now...

Haijalishi ni viapo na majigambo gani yanafanyika sasa kwa hawa wanaosema TUTAFANYA...

Na sio kwamba, hatutaufanya, la hasha. Uchaguzi utafanyika lakini sio Oktaba 2025 bali inaweza kuwa mwakani pending kufanyika kwa electoral reforms..

Wenye mamlaka wakikaidi (wasipotii maelekezo ya Mungu) kwa kutotumia hekima ya akili zao kufanya maamuzi sahihi, Mungu Jehovah ataamua yeye kwa njia yake katika namna ambayo italeta maumivu makubwa sana kwao hawa wenye mamlaka...

Atasababisha matukio kadhaa yenye ku - block chochote kisiendelee. Sitashangaa tukishuhudia hata vifo au kifo cha mtu ambaye atasababisha kila kitu kusimama na ku - rejuvenate akili na ufahamu wa watu na kuanza kuuona uhalisia wa mambo na kinachotakiwa kufanyika...

Rejea utawala wa serikali ya mfalme Sauli vs Daudi mchunga kondoo au utawala wa mfalme Farao ya Misri ya kale na falme nyingine nyingi ktk historia ya binadamu ulimwenguni...

I am optimistic 100% kuwa, uchaguzi mkuu haufanyiki na hauwezekaniki mwaka huu 2025 bila kujali maandalizi gani yanafanyika sasa...

Ni katika mazingira ya namna hii ya jeuri na kiburi cha mwadamu Mungu - Yahwe hujipatia utukufu wake ktk wakati ambapo mwanadamu huyu hufikiri kuwa ameshinda au ametoboa na hakuna mwingine tena na mwenye uwezo wa kuzuia haja ya tamaa yake..

Ndugu Robert Heriel Mtibeli, huyu mama (Bi Samia) na kundi/genge lake la utekaji, utesaji na mauaji ya raia ni jeuri na ana kiburi sana aisee. Haoni haya kumwaga damu za watu hadharani ili kupata atakacho na haoni kuwa hiyo ni shida na ni mauti yake pia....

Hajifunzi na hajajifunza kwa mtangulizi wake John P. Magufuli. Hajui kuwa AUAE KWA UPANGA, NAYE ATAKUFA KWA UPANGA siyo...?

Haya bhana...

Let's wait and see the end of this saga..
 
Hamjambo!

Katika vita ya mtandaoni, hasa vita maneno. Kuna kanuni zake.

Unapotupiana maneno na mtu kama unakombora kubwa kuliko haupaswi kulichelewesha sana kama vile katika vita vya silaha mfano Nyukilia ambazo hutolewa kidogo kidogo na kutokea yenye uwezo mdogo kufuatia yenye uwezo Mkubwa

Vita ya maneno ili ushinde lazima uangalie tension, shauku, hamu kubwa ya watazamaji, vita ya maneno watazamaji hutaka kusikia kombora kubwa kuliko hasa likitolewa dakika za mapema kabisa ili kumaliza kazi.

Vita ya maneno hasimu huwa na hofu ya kusemwa zile tabia zake mbaya za siri, usipomsema katika dakika za mwanzo, ukasema mambo ya kawaida. Tayari unampa mazingira ya kuzoea hofu na kisaikolojia ukishazoea hofu ya kile unachotarajia inapunguza uzito wa kombora lenyewe hata likitupwa.

Ikiwa unamchelewesha mtu katika vita ya Maneno jitahidi uwe na taarifa kubwa ya kutisha ambayo yeye(hasimu wako) anajua taarifa hiyo hauna. So inakuwa suprise sio tuu kwa Mashabiki bali hata kwa adui. Na hilo linakuwa pigo moja takatifu ambalo lazima liitwe Knock out.

Sasa Polepole press ya kwanza watu walijua atatuma vyuma vya uhakika, kisha awamu ya pili kutuma ushahidi, yeye watu wanamsubiri wakijua atakuwa na jambo zito. Akaboronga.

Watu wakasema huenda anavuta kasi, kapanga shambulizi la Pili, akaboronga.

Mpaka hasimu zake wamemdharau.
Alafu mbaya zaidi mlengwa Mkuu ambaye ni Rais yupo Kimya.
Na hili nilishaeleza kuhusu mpambano unavyokuwa.

Rais hawezi kujibu shambulizi lililopoa. Na nilimwambia kuwa ukimya wa Rais kwake auhesabu kama ishara ya hatari.

Kikawaida mtu ambaye unajua siri zake ukianzisha vita naye. Kama atakupiga shambulizi lililopoa huwezi mjibu kwani unajua hajamaliza risasi zake. Kwamba kuna risasi anayoitegemea.

Ni tofauti na Gwajima Vs Makonda. Gwajima alipokuwa katika vita vya Maneno na Makonda, Gwajima alianzia moja kwa moja kwenye kiini. Kisha akaacha ngoma imehang huku ushahidi ukiwa unafuata kwa shambulizi alilofanya.

Gwajima Vs Serikali ambao ni kivuli cha watekaji kwa Mujibu wake.

Shambulizi lake alianzia juu na hakuwa na risasi nyingine. Vita ilianza kwa tensioni kubwa.

Rais alimjibu kwa sababu alijua Gwajima amemaliza risasi zake na hana tegemeo jingine tena. Hana kipya atakachoongea.

Polepole yeye katoa shambulio lililopoa Sana. Madhara yake sio makubwa.
Hata kuzima mitandao ni hofu tuu.

Lakini ni kiashiria kuwa Polepole anataarifa nyingi na nyeti sana.

Polepole angerusha mawe mazito hata vipande nusu ambavyo vitamfanya awaabishe adui zake na awapagawishe. Kisha hatua inayofuata aseme anakuja na ushahidi ambao utawashangaza, na aseme atauweke hadharani na kila mtu atauona.

Huku akisema amebakisha vyuma vingine ambavyo vitaitetemesha nchi.

Ukishatoa madai ya kumdhalilisha hasimu wako utakuwa upo nusu ya ushindi. Kuthibitisha utakuwa umemaliza kazi.

Kadiri Polepole anavyochelewa ndivyo mashambulizi yake yanakosa nguvu.
Yaani leo hata aje aseme kitu gani hakitakuwa na nguvu ya maana kama angeshambulia mwanzoni.

Tayari watu wameshazoea, watu wameshapredict, hasimu kashazoea tension jambo ambalo kwenye vita ya maneno sio zuri.

Soma >> GE2025 - Polepole: Kuongea na watanzania Agost 6, saa 2:00 kuhusu mustakabali wa taifa

Polepole hata zile trick za majigambo na mikwala ya kusema yeye yupo tayari kufa lakini lazima hasimu wake alale nao mbele hatilii mikazo katika laini hizo.

Yupo katika vita kubwa lakini anapambana kwa namna laini sana. Jambo ambalo unagundua kuna kitu hakipo sawasawa.

Anyway! Sisi tupo!
Na tutakuwepo!

TaikonMaster
Kwa sasa Dar es salaam
Inahitajika Utangulize kwanza Akili kumuelewa Polepole na Sio Hisia

Kumbuka huyu MTU anajua Taarifa nyingi nyeti ambazo amezijua Kwa kutumia Nafasi alizokua nazo.
 
Huyo katumwa na sisiemu ili kuua ajenda ya NRNE na amefanikiwa kwa 70% mpaka sasa .

Na Lissu soon watu watamsahau Tanzania ni nchi ya watu wajinga
Hivi kama asingejitokeza Polepole ni nini kingetokea kwenye hiyo ajenda? CHADEMA imefungiwa kufanya chochote, Lissu yuko gerezani. Nadhani unajisemea tu. Polepole yeye anazungumzia suala la ndani ya CCM na yuko serious halafu eti mnasema katumwa!!
 
Objective ya polepole sio kuumiza chama chake.
 
Saikolojia anayoitumia PP ni wachache wenye uwezo wa kumuelewa kiundani. Kama jina lake ililivyo hiyo inaitwa slow burn psychology...yaani walengwa wanaungua pole pole

Shambulizi lilipoteza target linakosa maana.
 
Kalaghabaho!

Grand finale in essence, signifies the climactic ending that leaves a lasting impression.

Grand finale...the last and most exciting, spectacular and impressive part of a series.

Grand finale...what everybody in the crowd waits for.
 
Lakini ni kiashiria kuwa Polepole anataarifa nyingi na nyeti sana.

aseme anakuja na ushahidi ambao utawashangaza, na aseme atauweke hadharani na kila mtu atauona.
Kumbuka ana viapo vya kutunza siri za mambo aliyoyajua akiwa ndani ya serikali, hivyo usitarajie kuwa atapiga kombora mchana kweupe. ( anasema kufanya hivyo kunaweza kupelekea kifungo cha atmost 25 years). Kama ni mtu wa code naona anaeleweka tu vizuri hizo hints zinatosha.
 
Kalaghabaho!

Grand finale in essence, signifies the climactic ending that leaves a lasting impression.

Grand finale...the last and most exciting, spectacular and impressive part of a series.

Grand finale...what everybody in the crowd waits for.

Polepole kashapoteza Target za muhimu. Risasi alizobakiwa nazo hazitamsaidia.

Sasa hivi hawatazima mitandao
 
Back
Top Bottom