Posho na Mishahara ya wabunge...

Posho na Mishahara ya wabunge...

itawachukua mda kuelewa mantiki ya kufuta hizo posho. naamini CCM wataitumia hiyo km nguzo yao ya kutetea posho.
Ni kweli kabisa kwa wenye vichwa vya Panzi haiwezi kuwa rahisi kwao kuelewa huo wizi tunaofanyiwa. Imefika wakati masuala ya kuibiwa waziwazi kwa pamoja tuseme No. Kama wanaona dili basi raia wote wa tanzania tulipwe, kwani hata mkulima naye ni mfanyakazi wa kilimo
 
Siasa za kipuuzi kabisa. Hakuna mikopo kwa kutegemea posho za vikao maana mbunge hulipwa posho baada ya kuhudhuria kikao. Mkopo unatokana na mshahara na posho ya Ubunge ambayo inafikia tshs 5m kwa ajili ya mafuta 2m, kuendesha ofisi nk. Pia mshahara 2.3m! Hakuna mbunge anayeruhusiwa kukopa kwa kutumia posho za kujikimu au za vikao. Hizi ni propaganda za kitoto na zisizo na maana yeyote ambazo wala haziwezi kuzuia uzito wa hoja ya kufuta allowances za vikao.
CRDB nao ni wajinga tu kutoa taarifa kwa serikali au dailynews. Hata hivyo sishangai hata kidogo kwani crdb ndio benki iliyotumika kupitisha fedha za epa zaidi ya benki yeyote. Pia ndio benki inayoongoza kwenye wizi wa fedha za stimulus package.

Hapo kwenye Red, pungaza munkhari mkuu!! Wazo la kuondoa posho za vikao ni sawa, lakini tumewazingatia na wale wafanyakazi wa daraja la chini kabisa ambao mishahara yao haivuki mwezi kwenda mwezi mwingine? Kwa vigogo (na Wabunge mkiwemo) hii ni sawa maana mnapata posho zinazopita kiwango. Je mtapigania pia nyongeza ya mishahara kwa hao wafanyakazi wa daraja la chini? Maana angalau nao walikuwa wapata ahueni kutokana na posho hizo za vikao!
 
Hao unaowatetea wanaingia kwenye vikao venye posho?
 
Ni kweli kabisa kwa wenye vichwa vya Panzi haiwezi kuwa rahisi kwao kuelewa huo wizi tunaofanyiwa. Imefika wakati masuala ya kuibiwa waziwazi kwa pamoja tuseme No. Kama wanaona dili basi raia wote wa tanzania tulipwe, kwani hata mkulima naye ni mfanyakazi wa kilimo

Siyo kichwa cha panzi mimi nina kichwa cha binadamu. Nami sikatai posho za vikao sisiondolewe ila suala hili la posho hasa kwa wafanyakazi wa serikali linatakiwa liangaliwe kwa ujumla wake pamoja na maslahi mengine ya wafanyakazi. Hakuna mtu anayeongelea extra duty wala meal allowance, sijui hamzijui hizi nazo?
 
Tatizo la watu magamba akili,umeshaulizwa kama slaa halipi kodi mwenyekiti wako ccmagamba kodi yake ni ngapi????mshahara wake unaujua?????ota moto tuu mnasa matopeni.
 
Mwisho wa Siku Samwel Sitta ndo tutakayemlaumu, maana ktk kipindi chake nasikia aliongeza posho kwa wabunge. Na kama hilo litakuwa kweli, naye si mtaji wa kura kama alivyodai mwenyewe.
 
Umenena kweli kabisa, mtu yeyote mwenye uchungu wa kusaidia watumishi ktk nchi hii aanze na kuongelea Kupandishwa kwa mishahara halafu ndiyo ifuate posho...Wazo la kukata posho hii ni zuri lakini tunaomba tuipe serikali nafasi ipandishe mishahara halafu ikate hii posho..inawezekana na kwa kuanzia wabunge kweli kama wana nia nzuri waiambie serikali ianze na mshahara wa July 2011 uwe 315,000 (TUCTA) kinachofuata hapo ni kufuta posho hakuna atayelalamika mbona posho zenyewe wanaopata ni wateule tu!!!! Nimeona Daily news wanasema wabunge wanaolalamika zaidi ili posho iondolewe kumbe tayari walishaikopea mamilioni....ZITO KABWE uko wapi? kweli umekopa 200 milioni (kwa kutumia posho na mshahara wako?) JITETEE ili utupatie nguvu wafuasi wako ktk kutetea maslahi ya taifa
 
Kipato cha wabunge chahojiwa
Imeandikwa na Waandishi Wetu; Tarehe: 20th June 2011 @
HABARI LEO

KIPATO kikubwa cha Mbunge kwa mwezi, wakati anaingia bungeni na akimaliza muda wake,
kimetajwa kupunguza mchango wa wasomi na wataalamu katika ujenzi wa Taifa na kuzalisha wajasiriamali wengi wa kisiasa.

Akizungumza na gazeti hili wiki hii, Mhadhiri Mwandamizi wa Chuo Kikuu cha Mzumbe, Dk.
Prosper Ngowi alisema ukubwa wa kipato cha Mbunge umesababisha wataalamu ambao
wangetoa mchango mkubwa katika taaluma zao, kuzitelekeza na kukimbilia u bunge.

"Haina maana kuwa Bunge letu tukufu halihitaji wataalamu. Lakini ni ukweli kuwa pengine mtu mwenye taaluma kama ya utafiti na utabibu anaweza kutoa mchango mkubwa zaidi kwa umma kwa kufundisha, kutafiti na kutibu kuliko kukaa bungeni.

"Lakini kwa kuwa kifedha Bunge linalipa zaidi, watu wanashawishika na ni haki kushawishika kuacha taaluma na kazi ambazo mchango wao kwa Taifa ungekuwa mkubwa sana," alisema Dk. Ngowi.

Kwa sasa kipato cha Mbunge kinakadiriwa kufika Sh milioni 7 kwa mwezi, anapata mkopo wa Sh milioni 90 kwa ajili ya gari anapoingia bungeni na anapata kiinua mgongo wakati Bunge
linapovunjwa kwa ajili ya uchaguzi.

Hoja hiyo iliungwa mkono na Profesa wa Chuo Kikuu cha Mtakatifu Augustine, Mwesiga Baregu aliyesema mishahara mikubwa ya wabunge ni kichocheo kwa wataalamu kuacha fani zao wakiwa bado wanahitajika na jamii kwa utaalamu zaidi na kukimbilia kwenye ubunge.

Akitoa mfano wakati akiwa Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam na taarifa
alizonazo mpaka sasa, Baregu alisema, "mshahara wa Profesa anayefundisha Chuo Kikuu cha Dar es Salaam mwaka jana (2010) ulikuwa ni kati ya Sh milioni 2 hadi Sh milioni 2.5 na mwaka huu sidhani kama unazidi Sh milioni 2.9 na hapo ni kila kitu."

Dk. Ngowi kwa upande wake alisema pia si haki kwa mbunge kukopeshwa fedha za mlipa kodi wakati na wao ni watumishi wa umma na sehemu ya walipa kodi.

"Kwa kuwa Serikali haina fedha za kumkopesha kila mlipa kodi kama wabunge wanavyokopeshwa basi hakuna haki ya mgawanyo (distributive justice) kwa wachache kujipatia fedha hizi," alisema Dk. Ngowi.

Dk. Ngowi alipendekeza pia wabunge wasilipwe mishahara sawa bali mishahara
itofautiane kulingana na kiwango cha elimu, uzoefu, ujuzi na ufanisi wa mbunge
husika.

"Kama wafanyakazi katika sekta ya umma na binafsi wanalipwa kutokana na viwango vya elimu, uzoefu na ujuzi ni vema iwe hivyo pia bungeni," alisema Dk. Ngowi

Kutokana na hali hiyo, Dk. Ngowi alipendekeza kuundwe chombo huru kichunguze stahili halali za wabunge na kupinga marekebisho ya stahili hizo kufanywa na Bunge.

"Tatizo la ulipanaji huu mkubwa bungeni ni kuwa waheshimiwa ndiyo watunga
sheria. Unapokuwa mwamuzi (referee) na mchezaji kwa wakati huo huo hakuna
utawala bora. Ni bora kuwa na chombo huru kiamue stahili za waheshimiwa ni
zipi," alisema.

Mfanyabiashara ndogo wa Mbezi Luis, Nassor Abdallah alielezea kushangaa wabunge wanaoshabikia posho kwa madai kuwa wanaweka mbele maslahi yao na si ya wananchi.

Kwa upande wake, Gema Mmari, mkazi wa Sinza, Dar es Salaam aliiomba Serikali kuchukua hatua mara moja kupunguza kama si kuondoa kabisa posho za wabunge kwa kuwa wanaendelea kuweka pengo kati ya walionacho na wasionacho nchini.

Mjadala wa kipato cha wabunge umeibuka baada ya mjadala wa posho ulioamshwa na Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Kabwe Zitto aliyekataa kulipwa posho za vikao huku Mbunge wa Bumbuli, January Makamba akisema ni suala la kitaifa na lipo katika Mpango wa Taifa wa
miaka mitano.

Kwa wafuatiliaji wa siasa za Tz tunaufahamu vizuri msimamo wa Dr(PhD). Slaa. Amekuwa mtu wa kwanza kulalamikia ukubwa wa malipo na posho za wabunge tangu akiwa Mbunge. It is very clear kwamba hakubaliani na hizo posho.
Baada ya kuacha ubunge akataka alipwe kama yuko bungeni!
 
Tumekwishaaa watz! kwa hili sioni uhalali wa CCM kuwepo Tz, yani mi sioni umhimu wa kuwaacha waishi dunia hii, yani wapo pale kutetea na kuunga hoja mkono suala la kumuibia mtu mnyonge na maskini wa Tz, Shame on you CCem, vionee! nyoooooo! yan nina hasira. Shangingi moja ni sawa na Zahanati mbili nzuri tena zenye ubora! jamani.
Peleka taarabu yako huko kwa mabwana zako wa CDM
 
Umenena kweli kabisa, mtu yeyote mwenye uchungu wa kusaidia watumishi ktk nchi hii aanze na kuongelea Kupandishwa kwa mishahara halafu ndiyo ifuate posho...Wazo la kukata posho hii ni zuri lakini tunaomba tuipe serikali nafasi ipandishe mishahara halafu ikate hii posho..inawezekana na kwa kuanzia wabunge kweli kama wana nia nzuri waiambie serikali ianze na mshahara wa July 2011 uwe 315,000 (TUCTA) kinachofuata hapo ni kufuta posho hakuna atayelalamika mbona posho zenyewe wanaopata ni wateule tu!!!! Nimeona Daily news wanasema wabunge wanaolalamika zaidi ili posho iondolewe kumbe tayari walishaikopea mamilioni....ZITO KABWE uko wapi? kweli umekopa 200 milioni (kwa kutumia posho na mshahara wako?) JITETEE ili utupatie nguvu wafuasi wako ktk kutetea maslahi ya taifa
Hata mimi nimesoma Uhuru, Jambo Leo na habari Leo, nikasikiliza na kuangalia TBC1 na TBC Taifa wanasema hivyohivyo. Hivi unawezaje kukopa posho ya kiako ambacho huna uhakika kama utahudhuria au la? Kama ndivyo basi nchi hii ina wajinga wengi mno. Binafsi naunga mkono posho ziondolewe instantly kwa sababu zinawasaidia wakubwa tu. Hata hao wanaozungumzia meals and extra duty wajiulize kila mtu analipwa? Au ni kwa wakubwa wachache waliopo Dar?
 
Kweleakwelea mimi siwezi kutumwa na mtu yeyote najituma mimi mwenyewe na nasema ambacho nikiona na kukisikia. Unaona sasa hapo kwenye post yako yanongelewa mambo mengi ikiwepo usafiri wa ndege. Kwa hiyo suala la posho linatakiwa liangaliwe kwa ujumla wake. Nakuambia zaidi ya posho za vikao kuna meal allowance na extra duty allowance; hizi zina umuhimu gani? Ukiziondoa hizi bila kuongeza mishahara kwa wafanyakazi wa serikali utaelewana nao kweli? Najua posho ni zinalipwa kwa discretion ya mwajiri na siyo statutory kama ulivyo mshahara na posho hazichangii kwenye terminal benefits. Hapa wafanyakazi wana enjoy posho lakini uzeeni kiinua migongo hakitakuwa kizuri. Tatizo ni kwamba ukizigusa bila kuongeza mishahara yao kweli nakuambia wafanyakazi wa serikali watakuchukia. Nimewasikia wenyewe wakisema siyo wawili wala watatu ni makumi!

Wingi wa wafanyakazi hautupiti sisi wakulima ambao ni wapiga kura, siku za kula huwa ni mapumziko kwa wafanyakazi wakati wakulima ndio siku ya kwenda kupiga kula.
 
Hiyo habari ya gazeti iko sawa. Unajua watu wanaongelea kipato cha wabunge kwa ujumla wake ndio maana hiyo million 7 inaonekana sana. Kumbe suala si posho ya vikao tu: Kuna mikopo, kiinua mgongo, fuel allowance, n.k. Inapokuja kwa wfanyakazi wa serikali inabidi pia tuongelee posho za vikao, extra duty allowance, meal allowance, sitting allowance na mishahara. Hata hao wahadhiri wameongelea tu gross pay hawajaongelea makandokando mengine yanayopatikana kwenye posho. Bila kuongelea masuala hayo kwa ujumla wake sijui kama wafanyakazi wa serikali watakuelewa.

Tusipoangalia posho zitaligawa taifa.
 
Hata mimi nimesoma Uhuru, Jambo Leo na habari Leo, nikasikiliza na kuangalia TBC1 na TBC Taifa wanasema hivyohivyo. Hivi unawezaje kukopa posho ya kiako ambacho huna uhakika kama utahudhuria au la? Kama ndivyo basi nchi hii ina wajinga wengi mno. Binafsi naunga mkono posho ziondolewe instantly kwa sababu zinawasaidia wakubwa tu. Hata hao wanaozungumzia meals and extra duty wajiulize kila mtu analipwa? Au ni kwa wakubwa wachache waliopo Dar?

Hivi wewe umewahi kujiuliza inakuwaje mtumishi wa serikali wa kima cha chini anayepata shs. 130,000.00 anaweza kuishi DSM? Hata upige hesabu ukiwa huna nguo huwezi ku ibalance hiyo hela ili aweze kuishi DSM hata akiwa peke yake. Huytu ni mtu mdogo kwa hiyo hawezi kuiba wala kula rushwa: Siri yake ni POSHO. Posho zinatunza watu hapa mjini. POSHO POSHO
 
Zifutwe zote kabisa, kila mtu ategemee mshahara wake, kama hawezi aache kazi, hii ni kwa sababu zinaleta matatizo mengi kwa wafanyakazi kuliko faida. Si kweli kwamba wafanyakazi wengi wanapata posho hizo ni wachache mno wanaojilipa posho hizo.
 
I concur with what Dr(Phd) Slaa said. Kama hawa Mambulula wa CCM waliona kuwa Hilux Pick up haziwezi kufika kwa Wapiga kura, na hao hao wanaona huko walipo wapiga kura Bajaj zinaweza kufika, basi wanapaswa wakapimwe akili!
 
Siyo kichwa cha panzi mimi nina kichwa cha binadamu. Nami sikatai posho za vikao sisiondolewe ila suala hili la posho hasa kwa wafanyakazi wa serikali linatakiwa liangaliwe kwa ujumla wake pamoja na maslahi mengine ya wafanyakazi. Hakuna mtu anayeongelea extra duty wala meal allowance, sijui hamzijui hizi nazo?
Mkuu Kimbunga wewe ni mwajiriwa Serikalini ee?
 
kwa nini alikuwa akizipokea siku zote? mbona hata sasa hivi nasikia analipwa mamilioni ya hela za kodi zetu bila hata ya kukatwa kodi?
siungi mkono suala la posho hasa zisizo za lazima kama siting allowances za wabunge etc.
Then what?
 
Labda ingekuwa lugha ya kichangga hapo sina ujanja, kiingereza ata mbwa wangu nyumbani anajua, wewe ndio acha ushabiki kwa hiyo mpaka sasa bado utaki kukubali kama wabunge wako kina Mbowe wamekopa benki, labda nikuulize kwa nini Ofisi ya katibu wa bunge imewadhamini kwenye benki?

UUUUUUUUUUUUUU...sit down!!!
 
Back
Top Bottom