Wanabodi,
Mjadala wa Posho za Wabunge, umerindima kwenye kipindi cha Baragumu ambacho kiko live Channel Ten wakati huu ninapoandika post hii. Mgeni mwalika ni Katibu Uenezi wa CCM, Nape Mnauye na mchokoza mada ni Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe aliyechokoza mada kwa njia ya simu.
Mtoa hoja ni Kiongozi wa Upinzani Bungeni, Freeman Mbowe, amefafanua vizuri sana msimamo wa Chadema na kujielekeza suala la posho za Wabunge, ni suala mtambuka zaidi ya posho za wabunge pekee bali ni posho za watumishi wote wa umma kwa ujumla wao, zikikatwa zitaokoa zaidi ya Shilingi Bilioni 900. Mhe. Mbowe, amekwenda mbali zaidi na kufafanua kwa nini Chadema inapigania kufutwa kwa posho hizo na sio kila posho lazima ifutwe, posho kama za kujikimu ni posho muhimu hivyo Mbowe amesema hana tatizo nazo.
Pia Mheshimiwa Mbowe ameweka bayana suala la posho lisionekana ni la Wabunge wa Chadema tuu, linapaswa kuwa ni suala la bunge lote kwa sababu linahusu maslahi ya taifa. Mbowe akasisitiza ukiweka maslahi ya taifa mbele badala ya maslahi binafsi.
Ilipofika zamu ya Nape, aliunga mkono hoja ya Mbowe kuwa kuna posho za lazima na zile ambazo sio za lazima. Amekubaliana na Mbowe kuwa posho ya kujikimu ni posho ya lazima, hivyo iendelee kuwepo. Mhe. Nape, amekwenda mbali zaidi kwa kueleza dhamira yake ya dhati kupunguza gap kati ya wenye nacho na wasio nacho. Amekiri wafaidika wa posho ndio wale wale wenye mishahara minono na marupurupu kibao. Amesisitiza hoja siyo ya Chadema, hoja iko kwenye ule mpango wa miaka 5. Amesema unaungana na hoja za kufutwa kwa posho ambazo sio za lazima, ila kwa vile posho hizo zipo kisheria, basi kuondolewa kwa posho hizo kufuate utaratibu.
Miongoni mwa wachangiaji kwa simu ni Mhe. Zarina Madabida, aliiweka wazi kuwa suala la posho liko kwenye hotuba ya bajeti. Naye alitetea msimamo wa kuwepo kwa posho muhimu na kutolea mfano posho za madakitari na uwepo wa per diem. Huyu mbunge Mama Madabida, aliwashutumu wabunge wa upinzani kwa kuuiba hoja ya posho baada ya kuikuta kwenye kamati, hivyo kuiteka hoja.
MY TAKE.
Mbowe amejieleza vizuri sana kwenye hili suala la posho. Nape pia is good, anasimamia maslahi ya taifa.