Posho na Mishahara ya wabunge...

Posho na Mishahara ya wabunge...

Hivi wewe umewahi kujiuliza inakuwaje mtumishi wa serikali wa kima cha chini anayepata shs. 130,000.00 anaweza kuishi DSM? Hata upige hesabu ukiwa huna nguo huwezi ku ibalance hiyo hela ili aweze kuishi DSM hata akiwa peke yake. Huytu ni mtu mdogo kwa hiyo hawezi kuiba wala kula rushwa: Siri yake ni POSHO. Posho zinatunza watu hapa mjini. POSHO POSHO
Mimi nasema kwa experience yangu posho hizo hazina tija. Bajeti ya Zitto imeeleza vizuri kima cha chini kiwe 315000/= ili posho zifutwe. hii ni hoja ya msingi lakini serikali haitaki kuongeza mshahara ila posho inang'ang'ania ziwepo
 
Wana JF,
Naomba kwa wale wenye kuweza kuwasiliana na Waziri Mkuu wanifikishie ujumbe wangu kuwa wabunge wetu hawatugawii hizo hela za posho kama anavyofikiri.
Mtakumbuka wakati anajibu swali la kuhusu posho Bungeni,waziri mkuu alisema kuwa,posho kwa wabunge ipo kwa mujibu wa sheria,na moja ya kazi zake ni Mbunge kuzitumia kusaidia wapiga kura wake,kwahiyo ni wajibu wa Mbunge kunigawia hela kwani mimi ndo mpiga kura wake.
Sasa tunaomba pia ufafanuzi kwenye hili,tuache kushirikiana au kuwachagua wabunge ambao hawatugawii fedha?
Na atatuambia nini kuhusu ule mfuko wa jimbo?
 
Kweleakwelea mimi siwezi kutumwa na mtu yeyote najituma mimi mwenyewe na nasema ambacho nikiona na kukisikia. Unaona sasa hapo kwenye post yako yanongelewa mambo mengi ikiwepo usafiri wa ndege. Kwa hiyo suala la posho linatakiwa liangaliwe kwa ujumla wake. Nakuambia zaidi ya posho za vikao kuna meal allowance na extra duty allowance; hizi zina umuhimu gani? Ukiziondoa hizi bila kuongeza mishahara kwa wafanyakazi wa serikali utaelewana nao kweli? Najua posho ni zinalipwa kwa discretion ya mwajiri na siyo statutory kama ulivyo mshahara na posho hazichangii kwenye terminal benefits. Hapa wafanyakazi wana enjoy posho lakini uzeeni kiinua migongo hakitakuwa kizuri. Tatizo ni kwamba ukizigusa bila kuongeza mishahara yao kweli nakuambia wafanyakazi wa serikali watakuchukia. Nimewasikia wenyewe wakisema siyo wawili wala watatu ni makumi!

Hawa Wafanyakazi wa Serikali ndio ni watu waliozoea kuonekana kwamba wao ndio serikali. Wamekuwa wakipata upendeleo mwingi sana wakati sisi wengine tunaofanya sehemu binafsi hatupati pendeleo hizo. Kama vile exemption katika manunuzi yao n.k. Katika hili Serikali ilishajenga ubaguzi miongoni mwa raia wake.

Tunachosema ni Posho (Seating allowance) ziondolewe, maana hata wanaolipwa ni aina fulani ya ubaguzi, na si kila mwajiriwa wa ofisi husika anafaidika nazo bali ni wajanja tu wanaojua kuzitengenezea dili ya jinsi ya kuzihalalisha. Kuna vikao vingine havina kichwa wala miguu vinaitishwa na wakubwa kwa minajiri ya kuhalalisha matumizi ya pesa zilizotengwa kama sitting allowance.

Sitting allowance zimekuwa dili kiasi kwamba zinawafanya hata Mabosi wasio na maadili kuwarubuni wake za watu wanaofanya nao ofisini na kutembea nao na hata wengine kuwaambukiza ukimwi kwa kuwashawishi kama wakiwakataa basi hawataorodheshwa miongoni mwa wajumbe watakaoshiriki kwenye vikao vinavyotoa sitting allowance.
 
Sichochei wala sina mtimanyongo na mtu yeyote. Sipingi posho za vikao kuondolewa kwa wabunge na wafanyakazi wengine wa serikali. Ila sasa kusema kweli wafanyakazi wengi wa serikali wananufaika sana na hizi posho za vikao. Kuna viongozi (wakubwa), kuna wahudumu na kuna wataalamu (sekretariat) wote hawa kukiwa na vikao nao wanapata posho kusupliment mishahara yao. Pia kuna meal allowance na extra duty (siyo overtime) allowance; sijui kuna mtu anajua zinalipwalipwaje. Wafanyakazi kwa sasa wana chuki na mtu aliyeanzisha hili suala kabla ya kuhakikisha kuwa mishahara yao inapanda kabla ya kuondoa posho za vikao ambazo wanasema huenda zikafuatiwa na kuondolewa kwa posho zingine kama meal allowance na extra duty allowance.
Hata ubadilishe ID yako mara mia,na wanaokutuma nahisi hawa elewi kwamba wengi unaowakuta hapa hawajacheza chipukizi kama wewe,we JUHA hivi, POSHO zilizo lalamikiwa ni wizi wa mchana kutwa.Na niwazi wewe unataka kuchochea hasira zaidi ya tulizo nazo hili watu wapigwe BAN,wizi huu kupitia POSHO(jasho la wananchi) auna tofauti na EPA,nk hata kama mnatuibia kutumia sheria zilizopo kama enzi za sheria ya TAKRIMA
 
POSHO zitaibua mengi!! POSHO Zinatugawa!!
 
Wewe toa hoja mambo ya ujuha hayapo hapa. Nani kakuambia nabadilisha ID. Nibadilishe ili iweje. Kama unataka kutukana tukana tu lakini penye ukweli nitasema wala sitaogopa kutukanwa na mtu. Ukitukana nitajua tu kwamba huna hoja basi. Mimi nakuambia siwezi kutumwa labda wewe ndio umetumwa. Mimi sipingi posho kuondolewa napinga unafiki unaofanywa na wabunge wa CHADEMA kwa kutomuunga mkono Zitto wanamwacha peke yake. Majukwaani baadhi wanapiga kelele lakini bungeni wanasign. Zitto anapiga kelele na hasaini. Huyu ndio anaonyesha mfano na si MNAFIKI laki wengine wote ni WANAFIKI narudia tena kwamba ni WANAFIKI na waache UNAFIKI
 
POSHO zitaibua mengi!! POSHO Zinatugawa!!
Lazima zitugawe kama kuna sababu ya kufanya hivyo. Unaogopa kugawanyika ambako kuna maslahi? Hata bungeni kumeshagawanyika so na sisi tumegawanyika. Hata posho zenyewe zinatolewa kimatabaka. Hivi karani, mtunza kumbukumbu na mhudumu wa ofisi wanazijua posho hizo? Hata baadhi ya Maafisa wa ngazi za chini hawazijui posho hizo unazozitetea hapa
 
Shilingi Trilioni moja ambazo ni sawa kabisa na bajeti ya Wizara mbili au hata tatu ni pesa nyingi sana kugawana kama posho ni lazima zipigiwe kelele hizi mpaka ziondolewe.
 
Tafadhali sana Wabunge wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo(CHADEMA) chukueni posho zenu.Ni heri nusu shari kuliko shari kamili.Ni afadhali kwa sasa twajua kuwa kuna pesa wanapewa Waheshimiwa wetu Wabunge kuliko tusijue zinapotumika.Niliwahi kumuuliza mwalimu wa Kemia shuleni kwangu:Mwalimu,eti mshumaa unapozimwa moto wake waenda wapi? Mwalimu akanijibu:unabakia hewani lakini hauonekani! Ndio kitakachotokea kwenye posho pindi zitakapofutwa.Ni heri sana hata walalahoi wenzetu wa Upinzani mnazionja kidogo.Mkiziacha,zitagaiwa kizota............zitabaki hewani.Tafakari....chukua hatua!
 
Mwisho wa Siku Samwel Sitta ndo tutakayemlaumu, maana ktk kipindi chake nasikia aliongeza posho kwa wabunge. Na kama hilo litakuwa kweli, naye si mtaji wa kura kama alivyodai mwenyewe.
Suala la posho tuanzie kwa CDM kwa nini mmemrundikia posho Dr. Slaa wakati ambapo TEMEKE ofisi yenu imewekwa bar?
 
Sichochei wala sina mtimanyongo na mtu yeyote. Sipingi posho za vikao kuondolewa kwa wabunge na wafanyakazi wengine wa serikali. Ila sasa kusema kweli wafanyakazi wengi wa serikali wananufaika sana na hizi posho za vikao. Kuna viongozi (wakubwa), kuna wahudumu na kuna wataalamu (sekretariat) wote hawa kukiwa na vikao nao wanapata posho kusupliment mishahara yao. Pia kuna meal allowance na extra duty (siyo overtime) allowance; sijui kuna mtu anajua zinalipwalipwaje. Wafanyakazi kwa sasa wana chuki na mtu aliyeanzisha hili suala kabla ya kuhakikisha kuwa mishahara yao inapanda kabla ya kuondoa posho za vikao ambazo wanasema huenda zikafuatiwa na kuondolewa kwa posho zingine kama meal allowance na extra duty allowance.

Have you ever heard TWISTED THINKING!

This remind me to "PUT THE CART BEFORE THE HORSE" I real love Jamiiforums a home of greater thinker!

If your among of the greater thinker, no wonder we're among of HIPC (Highly Indepted Poor Country)
 
Zifutwe zote kabisa, kila mtu ategemee mshahara wake, kama hawezi aache kazi, hii ni kwa sababu zinaleta matatizo mengi kwa wafanyakazi kuliko faida. Si kweli kwamba wafanyakazi wengi wanapata posho hizo ni wachache mno wanaojilipa posho hizo.

bro/sis hujui utamu wa posho serikalini hasa kwa wafanyakazi wa chini, ivi umemaliza kadigrii kako afu unalipwa 315,000 kwa mwezi utaweza ishi? posho ndio zinazo wanyanyua asikwambie mtu, unakuta ukiotea dili la kwenda nje unalipwa 65,000 per diem na siting ya hivho kikao kama 20 hivi so jumla unalamba 85 kwa siku ukipiga siku kumi tu una laki 8, sasa anaesema zifutwe namshangaa...

hao wabunge ndo wapunguziwe na sio kufutiwa kabisa, mimi ni mwanachama mtiifu wa chadema lakini kwa hili wenzangu wanakosea kidogo, ndo nimeanza kuona sasa.
 
Lazima zitugawe kama kuna sababu ya kufanya hivyo. Unaogopa kugawanyika ambako kuna maslahi? Hata bungeni kumeshagawanyika so na sisi tumegawanyika. Hata posho zenyewe zinatolewa kimatabaka. Hivi karani, mtunza kumbukumbu na mhudumu wa ofisi wanazijua posho hizo? Hata baadhi ya Maafisa wa ngazi za chini hawazijui posho hizo unazozitetea hapa

Mkuu sitetei posho za vikao. Naongelea posho ambazo hazina mashiko na zinawahusu wafanyakazi wote wa serikalini japo kwa viwango tofauti. Nielewe: Hivi meal allowance na extra duty allowance zinalipwa kwa kazi gani? Hizi pia kwa maoni yangu zinatakiwa ziondoke. Kwa wafanyakazi wa serikali uikiondoa posho inabidi uongeze mishahara. Kwa hiyo inabidi serikali iongeze mishahara ili iende sambamba na kuondolewa kwa posho zisizo na mashiko. Au tunajikita kuondoa posho za vikao tu?
 
bro/sis hujui utamu wa posho serikalini hasa kwa wafanyakazi wa chini, ivi umemaliza kadigrii kako afu unalipwa 315,000 kwa mwezi utaweza ishi? posho ndio zinazo wanyanyua asikwambie mtu, unakuta ukiotea dili la kwenda nje unalipwa 65,000 per diem na siting ya hivho kikao kama 20 hivi so jumla unalamba 85 kwa siku ukipiga siku kumi tu una laki 8, sasa anaesema zifutwe namshangaa...

hao wabunge ndo wapunguziwe na sio kufutiwa kabisa, mimi ni mwanachama mtiifu wa chadema lakini kwa hili wenzangu wanakosea kidogo, ndo nimeanza kuona sasa.

Afadhali umeona kama kweli umeona.
 
Have you ever heard TWISTED THINKING!

This remind me to "PUT THE CART BEFORE THE HORSE" I real love Jamiiforums a home of greater thinker!

If your among of the greater thinker, no wonder we're among of HIPC (Highly Indepted Poor Country)

Hapo sijui kwa kuwa sina weledi.
 
Siyo kichwa cha panzi mimi nina kichwa cha binadamu. Nami sikatai posho za vikao sisiondolewe ila suala hili la posho hasa kwa wafanyakazi wa serikali linatakiwa liangaliwe kwa ujumla wake pamoja na maslahi mengine ya wafanyakazi. Hakuna mtu anayeongelea extra duty wala meal allowance, sijui hamzijui hizi nazo?

Sasa Mh. Mtu akama afisa mtendaji wa Tanroads unahitaji kurekebisha mshahara wake ili kufuta posho ya vikao? Mshahara wa mwezi si anaweza kununua gari lililotumika hapa Tanzania wakati mtumishi mwingine kununua redio lazima adundulize au acheze kibati?
 
Nakubaliana kabisa na wewe. Lakini pia huko tanroads kuna watumishi wa chini ambao wanapokea hizo posho. Mimi hapa naongelea kurekebisha vima vya chini si kwa watu kama hao ambao nasikia wanalipwa mamilioni.
 
Tupe information inayojitoshereza

Mkuu nimetembelea kwenye FB page yake hakuna cha zaidi ya hicho kilichoandikwa. Yule bwana ni PhD na ameandika kifupi bila kufafanua. Sentensi mbili haziwezi kuwa tamko la chama. Atoe tamko tena kwa waandishi wa habari ili kuwachagiza wabunge wa CHADEMA wamuunge mkono Zitto.
 
Nakubaliana kabisa na wewe. Lakini pia huko tanroads kuna watumishi wa chini ambao wanapokea hizo posho. Mimi hapa naongelea kurekebisha vima vya chini si kwa watu kama hao ambao nasikia wanalipwa mamilioni.
Zitto aliongelea hili kwenye bajeti akasema kima cha chini kiwe 315000/= kama suluhu ya kuondoa posho. Wewe unaonaje?
 
Back
Top Bottom