Salamu wana Jamii wenzangu!
Tanzania inaadhimisha miaka 50 ya Uhuru huku Taifa letu likiwa bado linaogolea kwenye wimbi kubwa la umaskini.Kumekuwa na juhudi za wazi kabisa za serikali za awamu zote toka awamu ya Kwanza hadi hiii ya nne kuapambana na Umaskini,naweza kusema juhudi hizi zimezaa matunda kwa kiasi Fulani lakini Ukweli umebaki pale pale kwamba nchi yetu na wanachi bado tu maskini sana.
Kwa majuma kadhaa sasa kumekuwa na mdadala mkali ndani ya Bunge la Bajeti la mwaka 2011,Wanasiasa na Vyama vya kijamii,kuhusiana na uhalali wa Posho wanazolipwa Wabunge na Watumishi wa Serikali na Taasisi za umma katika kipindi hiki cha mdororo wa Kiuchumi na unaoikumba Dunia na Taifa letu la Tanzania,kwa mtizamo wangu walioanzisha mjadala huu wana haki ya kutoa maoni yao kwakuwa nchi hii ni huru na tunaheshimu mawazo ya watu.Nasikitika sana kwa hoja nyepesi za kujibu hoja hii zinazotolewa na baadhi ya wanasiasa na viongozi wa andamamizi wa Serikali na mihimili ya Utawala wan chi yetu!
Baada ya kufuatilia kwa kina mjadala huu , mimi nimejiuliza swali moja tu,Ni kweli kwamba sisi watanzania Watanzania ya leo tunaoadhimisha miaka 50 ya Uhuru tukiwa Maskini tumegundua kwamba tatizo la Umaskini wetu ni Posho? Huu kweli si Mjadala wa Kipumbavu kwa Taifa maskini kama hili kuujadili wakati likiadhimisha miaka 50 ya Uhuru wake,huku sio kufilisika kisiasa na kifikra jamani!??
Tuwaambie watoto wetu kwamba Posho ndio suluhu ya matatizo linaikabili nchi yetu na tuwafundishe hivyo?
Mimi nasema,naomba mnisamehe mlio wakubwa kwangu,walimu wangu na wazee wangu,kama mnakaa kujadili Posho na mnasahau matatizo makubwa yanayowakabili Watanzani na sisi Vijana,mumefilisika sana kimawazo,mimi nasema Hasira ya Watanzania itawashukia muda si mrefu!!!Mbona mumeacha kujadili:
1.Wizi wa Rasilimali za Taifa Letu,Madini,Misamaha ya Kodi kwa Wawekezaji wababaishaji na Matapeli
Ninyi wabunge,kwanini Hamkatai Mikataba mibovu,kwanini mnanyamaza Kimya watu wanaiba Dhahabu zetu,wanachima Uranium Yetu,wanakula wanyamapori wetu,wanavuna Misitu yetu na kuuza magogo nchi zanje,wanavua Samaki wetu?wanatuacha sisi Maskini wa kutupwa na tunapiga miayoo na Maelfu ya Vijana wanakosa Ajira>>!!!! Hasira ya Vijana itawaka muda si mrefu!
Mbona HAMYAKATAI haya kwa nguvu zenu zote >?????Mnakataa Posho?Posho?What is Posho na watu wanachota Utajiri Mkubwa wa Taifa Letu mumenyamaza?mbona hamjakataa hilo?mnasema tu kwenye majukwaa siasa,onyesheni kwa vitendo,susieni Bunge siku moja mseme tunaenda kuangalia Dhahabu yetu inavyoibiwa na watu wetu wanavyoangamizwa migodini na kunyanganywa Utajiri wan chi yao,mnajadili Posho,Posho,Posho,What is Posho ni sawa tone tu la maji kwenye Mirahaba ya Dhahabu na Almasi inayoibiwa na mko Kimya?!!!!This is Non-Sense,naomba muondoe mijadala hii ya Kipumbavu,mjadili mambo ya maana ya kuliokoa Taifa Letu la Tanzania dhidi ya Umaskini baada ya Miaka 50 ya Uhuru.
2.Elimu duni na mifumo mibovu ya Elimu
Mbona Elimu imepewa Kisogo?Mnakaa Kimya,mnashabikia Kilimo Kwanza ?Kilimo kwanzaaa ehhee?Cha kutegemea mvua?Etii yee,ma power Tila yaKilima Hekta 1000 na mvua hainyeshi,Mbolea Hakuna na Mkulima mwenyewe Mumemnyima Elimu na Mtaji wa Kulimia hana!!! This is Non-Sense!!! Huu ni Upumbavu wa Wanaotudanganya mabo ni Mabeberu wan chi za Magharibi!Hakuna Maendeleo ya Taifa lolote bila ELIMU!!! Ndio maana namuunga mkono kwa nguvu zote Mheshimiwa EL kwamba ELIMU KABLA NA KILOMO KWANZA hii ndio sera mbadala wake Hakuna.Mkulima apewe Elimu kabla ndipo afundishwe Kilimo cha Kisasa!!!!
-Mbona Wanafunzi wa Vyuo Vikuu mnawafukuza wakidai Haki yao?
-Mbona Mikopo haitoshi kuwawezesha kusoma bila shida?
-Mbona shule za Kata zimetelekezwa bila maabara na Vifaa
-Mbona Hakuna Nyumba za Walimu
-Mbona Walimu hawalipwi Posho zao na Mishahara ili kuwaongezea Tija ya kazi
-Mbona Shule hazina Maabara za Kutosha?
3.Huduma Duni za Jamii kama Maji,Hospitali ,Mafoleni ya Dsm.Usafiri wa Reli,Ndege Mbovu nk
4.Miundombinu Hafifu,Barabara na Umeme kama Mshumaa,kidogo umewaka mara umweiziam
5.Mfumuko wa Bei za Bidhaa masokoni,wala Pesa haina thamani tena!
6.Ukosefu Mkubwa wa Ajira kwa Vijana na Maslahi duni ya Watumishi walio katika Ajira katika Sekta Rasmi na Zisizo Rasmi
7.Rushwa na Ufisadi
8.Ukosefu wa Usalama wa Raia,Wizi na Unyanganyi wa kutumia Silaha,Mabomu yanalipuka katika maghala ya Silaha za Majeshi yetu
9.Uchafuzi Mkubwa wa Mazingira unafanywa na wamwekezaji wababaishaji wanachimba Dhahabu yetu na kutuachia mashimo makubwa,vumbi kutapakaa angani,Misitu inavyunwa na watu wanakula hadi nyama za Swala na walisahau siku nyingi kula ngombe.
10.Umaskini mkubwa wa Kipato miongoni mwa Mamilioni ya Watanzania waishio Mijini na Vijijini
11.Makazi duni na Mipango Miji mibovu na unyaanyi wa Adhi yetu na Wageni
13.Kuongezeka kwa Kasi kwa Deni la Taifa na hivyo kutishia nchi yetu kufilisika kama nchi za Ugiriki na Hispania zinakoelekea sasa
14.Ukabila,Udini na Ubaguzi wa kila namna Vinashamiri kila kukucha
15.Muungano usio Imara,kila leo kurushiana maneno na tumesahau umoja na mshikamano wa Taifa letu
16.Haki za Bindamu zinadharauriwa,Msongamano wa Wafungwa Magerezana,Rushwa katika Mahakama,Udharirishaji watoto na Wanawake,watu kujichukulia madaraka mkononi
17.Katiba ya Kizamani na Sheria Kandamizi
Na mengine Meengii!
Haya na mengine meengi ndiyo yanasababisha Taifa letu liendelee kuwa Maskini kwa wakati tukiadhimisha Miaka 50 ya Uhuru,Wanasiasa/Asasi za kijamii na Wabunge wetu,tujadiri haya ???na tuwafundishe watoto wetu haya na tuache kujadili mambo madogo madogo kama Posho huku tukiacha Taifa letu likiangamia kwa Umaskini.Kujadiri Posho na Kuacha haya ni KUFILISIKA KWA MAWAZO.
Natoa hoja ya kufunga Mjadala wa Posho kuanzia leo!