Posho na Mishahara ya wabunge...

Posho na Mishahara ya wabunge...

elimu yangu ya mikopo ni ndogo saaaaana ila ninachojua ni kwamba collateral ya mkopo bank kama si mali isiyohamishika basi ni prove ya mshahara (sio posho) wako ambao wao wana-centre kwenye Pension yako ndio maana hata ukiwa mfanyakazi unapata mshahara wa 100Million/month kama hukatwi pension hukopeshwi (NMB na CRDB) so nakataa kwamba posho inayozungumziwa na wapinzani (sio CDM pekee) eti ndio collateral ya mikopo yao benki.


Kwanza nimpongeze Zito kwa michango yake huko ndani ya mjengo na kwa kupata muda kuwa nasi ndani ya jamiiforums. CRDB wamekuwa mamluki sasa wa kuibia nchi. Ni kweli wao ndio walikuwa kinara wa kupitisha pesa za EPA. Kukopa benki kwa mategemeo utapata posho ndio ulipie mkopo naona hilo ni ndoto za mchana. Pengine CRDB wamefanya hivyo kama walivyofanya EPA. Siwezi nikaamini hata punje walioandika Daily News maana naona imekaa kisiasa zaidi. Bw Zito kongomelea na hili. Tufafanulie zaidi, hata kama ni wewe umekopa (kukopa sio dhambi hata mara moja), tueleze ni kweli ulikopa against Posho, hata kama ni mwenzio kule CDM, tufafanulie kabla ya magamba hawajamwaga sumu kwa watu wetu.
 
Nimeikuta kwenye facebook status ya Dr W.slaa.
"suala la Posho serikali haina la kujitetea maslahi ya Taifa kwanza kwa maendeleo ya watanzania wote"
 
Mh. Zitto na kundi lako mjue mmegusa ulaji wa watu. Kuna kundi kubwa sana linategemea hizo posho na kunufaika nazo. Vita yenu siyo ndogo na mtakutana na vikwazo vingi. Jipeni moyo maana Mungu wa kweli yuko nanyi. Hakuna dhambi kukopa na wala kukopa kwa kudhaminiwa na Bunge hakumaanishi kuwa pato lako lote linatokana na Bunge tu. Wenye akili tunaelewa..... wenye kamasi kichwani wanashabikia uozo wa Daily News, Habari Leo na Watawala walioko madarakani.

NAWAOMBEA SANA MSHINDE VITA HII
 
Mama Madabida ni Kihiyo. Hajui ni Lini ILANI ya CHADEMA iliandikwa na ni lini MPANGO wa MAENDELEO UMEANDIKWA ndio maana siwapendi Wabunge wa CCM kwa sababu hawapendi kujisomea
Mkuu unafikili hawapendi kusoma wanasoma sana ila tatizo wanasoma nini!?
Unawakuta bize na magazeti ya udaku tuuuu!
 
Kwa hiyo, Rais kupitia mpango wa taifa wa maendeleo anataka posho ziondolowe, chama tawala (ccm) kupitia kwa katibu wake mwenezi nacho kinakubaliana na hoja ya kuondoa posho. Lakini Waziri mkuu ambaye anayesimamia shughuli za serikali kama anavyoagizwa na Rais anapingana na hoja ya posho kuondolewa. Tena anafanya hivyo mbele ya chombo cha kutunga sheria sehemu ambapo sheria ya kufuta posho ingeweza kupitishwa. Sasa, Waziri mkuu anamuakilisha nani? How can he lead when he does not agree with the government policy. His position as Prime Minister in my view is unattainable. Anatakiwa ajiuzulu maana hana dhamira ya kweli ya kusimamia utekelezaji wa mipango ya serikali.

CCM ni watata ba hapo wamekwama .Hawana nia njema at all . Nape anaanza kupata akili baada ya kuona JF wanampa ushauri kila mara . Huenda ameanza kuona sasa na kusikia .
 
Nape ni mpiga propaganda,kesho tena utasijkia anafafanua kwamba hakusema hivyo.Yetu macho.
 
Nimeikuta kwenye facebook status ya Dr W.slaa.
"suala la Posho serikali haina la kujitetea maslahi ya Taifa kwanza kwa maendeleo ya watanzania wote"

Hiyo ndio Official statement ya Katibu Mkuu wa CHADEMA?
 
nape nnauye A.K.A ACHEBE.........hana lolote
 
Wako wapi wale Pro-Chadema walikuwa wanapinga eti hakuna benki inayoweza kutoa mikopo kupitia posho, LAT na wenzako mpooo???
Propagada za CCM nyingi hazina mantiki WAPINZANI WANANUFAIKA POSHO NA CCM WASIONUFAIKA NA POSHO HIZO WANAZIUNGA MKONO!!Na wanadai WAPINZANI wameiba hoja Yao ,Kama iliku ni hoja Yao na walikua na nia ya kuitimiza ingalikua na mantiki kuwashukuru na kuwaunga mkono kuitekeleza.VINGINEVYO NI USANII.
 
Mi nashangaa sana, kuna watu wanafanya sie wananchi ni mazuzu kabisa. Hebu mwana JF mmoja anipe uhusiano wa posho ya kikao na mkopo benki! Namshangaa sana mhariri wa DN kwani kwa namna moja au nyingine anajionyesha ni kwa kiwango gani asivyotumia akili kuliendesha gazeti hilo la Serikali. Kwanini asiende kuwa mhariri wa gazeti la Uhuru?

Hebu tuone basi kama ikiwa ni sahihi, kwanini wasiziondoe ili hao wabunge wa CDM wenye mikopo mikubwa benki washindwe kuilipa? Kama hivyo ni kweli basi wao ndo wangekuwa mstari wa mbele kuzitetea ziendelee. Sasa wahariri kama hawa sioni ni kwa nini wanaendele kuwepo huku wakilipwa mishahara na posho za vikao kwa fedha za walalahoi.

Msitufanye sie wajinga, tunajua katika hili nani anasema kweli, kwahiyo msipoteze muda wenu bure kutuhadaa......!
 
Mkuu naomba nikurekebishe kidogo,

Sheria ya benki ya mwaka 1961, 1991, na duniani kote duty of confidentiality ends if the information inquiry is of the matter of national interest, judicial inquiry or tax purposes (with authorisation from the commissioner). Hivyo basi Daily News hawajafanya kosa lolote. Ila mie najiuliza kama mshahara wako ni kidogo kwanini ukope hela nyingi hivyo milioni 200 kwa mshahara wa 2.5 na posho ya milioni 5???? Kweli Tanzania hakuna mkombozi wala mzalendo wamejaa walafi na watu wenye njaa tu.

Sasa Daily News ni mahakama au TRA?......What national interest?
 
Jamani kwani mkopo ni nini na posho ni nini? Kuna uhusiano gani gani ya mkono na posho? Mkopo ni mkopo na unautaratibu wake, nimeshangaa hata ktk Daily News (Monday, June 20th, 2011) the heading topic is "MP use allowances to get loans". Hivi hawa waandishi wanaakili timamu kweli za kuandika mambo? Tunalipia kununua hayo magazeti, tafadhari heshimuni professional yenu. Acheni ulimbukeni huo!
 
Zitto, Wewe kweli umechukuwa mkopo benki na ofisi ya katibu wa bunge ndio mdhamini wako? Tunaomba utuweke sawa kwenye hili swala
It is so simple. Nimekopa benki na katibu wa Bunge kama Mwajiri ndiye mdhamini. Ila sijakopa kwa kutumia posho za vikao wala posho za kujikimu. Nimekopa kwenye mshahara wangu. Wala sioni aibu kusema hili popote. Kukopa hakuna mahusiano na hoja ya kuondoa posho za vikao.
 
Kwa wafuatiliaji wa siasa za Tz tunaufahamu vizuri msimamo wa Dr(PhD). Slaa. Amekuwa mtu wa kwanza kulalamikia ukubwa wa malipo na posho za wabunge tangu akiwa Mbunge. It is very clear kwamba hakubaliani na hizo posho.
 
#9 Beano 2011-06-20 09:09 Mimi naamini kama Watanzania hatutalimaliza hili la posho kwa wakati huu, basi upo uwezekano likabadilishwa sura na hawa waheshimiwa kujilipa kwa namna nyingine. Kila tunapolisikia suala la posho, tuweke akilini kinachozungumzi wa hapo ni around 930bn kila mwaka. Jamani hizi ni fedha nyingi sana. Juzi wakati bunge linajisifia kuwa litanunua bajaj kwa ajili ya kubebea wagonjwa vijijini, wengi tulishangilia kwa kuona huo ni ukombozi. Hata mimi sikatai kuwa zitasaidia lkn hapo kwenye kauli zao utaona jinsi hawa watu walivyo wabinafsi na wenye kujijali. Narejea kauli zao za nyuma kuhusu mashangingi wanayotumia kuunguzia mafuta ya kodi zetu. Magari haya mazito ya kifahari wanayotumia viongozi yalitetewa uwepo wake na mabunge yaliyopita kuwa yana ulazima wa kuwepo kutokana na miundombinu dhaifu ya barabara za vijijini wanapoenda kwenye shughuli za maendeleo. Ikiwa waziri hawezi kufika kijijini na TOYOTA HILUX PICK-UP 4x4 mpaka akahitaji shangingi la 240ml, Bajaj inawezaje kufanya kazi ya kubeba wagonjwa huko huko vijijini? Huu ni ubinafsi na uropokaji wa mazoea ya kuongea na watu wasiofuatilia mambo. Sasa leo waziri mkuu wa nchi anasema 931bn si jambo kubwa ilhali zingeweza kununua AMBULANCE 3720 ambazo ni zaidi ya mahitaji ya magari hayo kwa nchi yetu na bado kuna baadhi yetu tunamsapoti na kumpigia makofi! Na hiyo ni posho ya mwaka mmoja tu, mwaka mwingine ungetatua kero nyingine. Tunafikia kukodi mitambo ya umeme ya dowans ambayo gharama yake ya ununuzi ni robo ya hizi posho, tumeshindiwa nini kununua mitambo yetu? Mimi nafikiri huu hiki kiburi kinaletwa na wingi wao bungeni na hili ni kosa letu wakati tulipopata nafasi ya kufanya mabadiliko. Sasa uzembe wetu wa kutokwenda kupiga kura au kuchagua kwa mazoea unatutafuna na cha ajabu wapo baadhi yetu wanaoshangilia utetezi wa hoja hii inayoligharimu taifa kuishi na maradhi ya uchumi miaka nenda rudi

mtanzania maoni
 
Back
Top Bottom