Posho na Mishahara ya wabunge...

Posho na Mishahara ya wabunge...

Jamani kwani mkopo ni nini na posho ni nini? Kuna uhusiano gani gani ya mkono na posho? Mkopo ni mkopo na unautaratibu wake, nimeshangaa hata ktk Daily News (Monday, June 20th, 2011) the heading topic is "MP use allowances to get loans". Hivi hawa waandishi wanaakili timamu kweli za kuandika mambo? Tunalipia kununua hayo magazeti, tafadhari heshimuni professional yenu. Acheni ulimbukeni huo!
Kwani unafikiri hao waandishi hawako JF! Ndio baina yao unapata haya mawazo, inshort wao wanatoa humu vitu vingi na sisi humu ndani tuna tunavyotoa kwao.
 
Nkoi mambo ga poshoo bungeniii, mmhh Madimu sana!!
 
Mi nadhani muda wa kuwa waoga inabidi uishe!! coz bajeti ya upinzani ndio bajeti ambayo itakomboa mtanzania masikini!!!hivi kwanini tunashindwa kufanya maandamano ya kudai bajeti ya upinzani ipitishwe kama bajeti kuu kwa mwaka huu wa fedha????

Tukiacha shughuli zetu na kwenda Mnazi Mmoja kudai bajeti ya ya upinzani tutapewa!!! wananunua magari ya kifahari, wanataka posho. wanataka pesa ya jimbo, pesa ya mafuta ya gari bado mshahara!!!!

Mi nadhani sisi watanzania tusipojipanga na kulishikia kidete hili suala tutakuwa wajinga kuliko hata huyo Mijengo Iliyopinda!!!

Sante Wazee
hili wazo ni la msingi sana kwa sasabu kuna ushahidi wa kuhalalisha (justify) kuwa ajira serikarini zimekuwa za urasimu na kujuana ambapo wamerundika idadi kubwa ya watu ambao ni incompetent!
Sasa hivi wengi wanaamini (yaweza kuwa kweli) kuwa waajiriwa wa NGOs, na hata self employed (walioko mtaani) wana uwezo na uelewa mkubwa kuliko waajiriwa wa serikarini.
Kwa hiyo basi ndio maana budget ya upinzani (Mh. Zitto) inaonyesha uhalisia wa uchumi wa Tanzania badala ya takwimu za Mr. (Mh) Mkullo.
Wazo la kuikubali bajeti ambayo inatuelekeza kwenye matatizo zaidi wakati kuna alternative budget ikiwa imetengenezwa na Watanzania wenzetu (na sio wageni!!) ni uendawazimu.
Tuachane na ule mfumo wa zamani wa "Serikari imesema..." ili kuinusuru nchi yetu ambayo kama alivyosema Mh. Msigwa kulinganisha na mtoto mwanye miaka 10 akifanya mambo ya miaka 2.
Mimi kwa uwezo mdogo nilionao nawezo kushawishi watu kama 20 - 50 kuikataa.
 
It is so simple. Nimekopa benki na katibu wa Bunge kama Mwajiri ndiye mdhamini. Ila sijakopa kwa kutumia posho za vikao wala posho za kujikimu. Nimekopa kwenye mshahara wangu. Wala sioni aibu kusema hili popote. Kukopa hakuna mahusiano na hoja ya kuondoa posho za vikao.
Mkuu, nashukuru kwa majibu yako murua
 
Siasa za kipuuzi kabisa. Hakuna mikopo kwa kutegemea posho za vikao maana mbunge hulipwa posho baada ya kuhudhuria kikao. Mkopo unatokana na mshahara na posho ya Ubunge ambayo inafikia tshs 5m kwa ajili ya mafuta 2m, kuendesha ofisi nk. Pia mshahara 2.3m! Hakuna mbunge anayeruhusiwa kukopa kwa kutumia posho za kujikimu au za vikao. Hizi ni propaganda za kitoto na zisizo na maana yeyote ambazo wala haziwezi kuzuia uzito wa hoja ya kufuta allowances za vikao.
CRDB nao ni wajinga tu kutoa taarifa kwa serikali au dailynews. Hata hivyo sishangai hata kidogo kwani crdb ndio benki iliyotumika kupitisha fedha za epa zaidi ya benki yeyote. Pia ndio benki inayoongoza kwenye wizi wa fedha za stimulus package.

Mkuu,

Ni kweli unayonena, na jinsi ninavyofahamu mie utaratibu wa kibenki ni vigumu kukopesha mtu kwa kutegemea posho kwani hakuna mkataba au kithibitisho cha kuwa posho hiyo itaendelea hadi atakapomaliza ubunge. Vile vile huo ni uzembe kwa upande wa benki kumkopesha mtu milioni 200 kwa kutumia mshahara wa 2.5 million akija kushindwa kulipa watarudisha vp pesa zao.

Hata hivyo hizi tuhuma za CRDB nilisikia tetesi tu, je unayosema yana uhakika, na kama ni hivyo niliwahi kusikia kuna kabenki kalikaribia kufa hela za stimulus zikaifufua isife je nazo ni kweli. Na tetesi hizo zinadai benki hiyo ni CRDB je ni kweli?? Mie nauliza kupata kujihakikishia tu.
 
It is so simple. Nimekopa benki na katibu wa Bunge kama Mwajiri ndiye mdhamini. Ila sijakopa kwa kutumia posho za vikao wala posho za kujikimu. Nimekopa kwenye mshahara wangu. Wala sioni aibu kusema hili popote. Kukopa hakuna mahusiano na hoja ya kuondoa posho za vikao.

Kuna makala nimezungumzia kuhusu ugiriki (na serikali yao kijamaa) ilivyofilisika sasa hivi kwasababu ya kukopa kwa kuendesha serikali. Hoja posho inawagusa watu wengi na wengi wametajirika kwa posho zisizokuwa na kichwa wala miguu. Ikiwa ni ngumu kuelewa waachie mkuu kawafahamishe wananchi watizame yanayoendelea ugiriki kwani serikali ya kijamaa iliyaruhusu hayo mambo watu wakaona maisha wameyapatia. Ilipokuja kufilisika nchi serikali imebidi ndio ianze kubana matumizi na kuongeza kodi na kukata mishahara na kufutilia mbali posho.
 
Nyie Pro-Chadema msiwe kama makinda ya bata yanamfata mama yao ata popote anapokwenda kama anavuka barabara. Hawo viongozi wenu wameishachukuwa mikopo benki kupitia hizo posho wanazozisema tena wa kwanza kuchukuwa ni Mbowe 200 milioni Zitto 150 milioni, mdhamini wao ni ofisi ya katibu wa bunge

I think you are talking nonsense, kwani wakichukuwa mkopo inakuhusu nini si wanajua wao namna ya kuilipa? unadhani wanalala kama wewe?
 
Kwa hiyo??? Unatetea posho za wabunge kwakuwa Mbowe na Zitto wamekopa?? Kweli wewe akili zako kama za Kiwete Mkwer.e






Ifahamike kuwa issue hapa siyo posho ya wabunge bali ni unafiki wa kutaka kujizolea umaarufu wa kisiasa kutokana na posho hizo. swali la kujiuliza ni "kwanini mbowe na kabwe wakope mil.200 na150 kwa kila mmoja?" bila shaka jibu linapatikana kwa wenye kuwaza.Labda kwa kuwasaidia wale wenye 'fixed mind' ni kwamba viongozi hao wanataka kujilimbikizia mali.
Evi kama kweli viongozi hao wanawaonea huruma wananchi waliodumbukia kwenye dimbwi la umasikini, kwanini wasitumie fedha hizo walizokopa na nyingine nyingi wanazokopa kuzipeleka majimboni mwao ilikwahayo waharakishe maendeleo kwa wananchi hao wanaodaiwa kuonewa huruma? na ndiomaana wachambuzi wa mambo wanawaona viongozi wanaoibua hoja hizo ni kama wanafiki tu walio kwenye mkakati wa kujinyakulia ushindi 2015 kwa kuwaghiribu akili wapiga kura.
Aidha,mwanahistoria maarufu alisema kuwa"Africans were colonised becouse of social atavism of Europeans" social atavism here is referred to as the desire of a person to control another.Hapa ndipo wanapodhiri viongozi hao wanafiki wa CHADEMA.Wanayafanya hayo si kwa ya kuwaonea huruma wananchi bali ni ile tamaa tu ya kutaka kuwatawala kama alivyosema mwanahistoria huo maaarufu.
Haya basi tukaneni maana ndio zenu pale mnapoelezwa ukweli huku ukiwagusa ukweli huo na mnatukana huku nafsi zenu zikijisemea "lakini kweli anayonena mtu huyu".
 
Najiaandaaa kuelekea mkoani kwa ajili ya kutimiza majukumu ya kikazi,bahasha kubwa iko tayari hapa mezani kwangu,naambiwa niende kwa mhasibu kusaini upokeaji wa posho na masurufu mengine.Nimekataa kuchukua posho hii,mwajiri ananiona kama kichaa vile,ana wasiwasi kazi minayoenda kuifanya haitafanyika,namwakikishia niko makini,naendelea kumweleza hapa nilipo ndo sehemu ya kuonesha uzalendo,na siku nikishika ofisi ya umma,utakuwa mwendo mdundo.Sitaki posho!!!
 
imagine,ndo mtu aliyewahi kutamka kuwa anapiga stop mashangingi,na hata wakati fulani alithubutu kukataa alilonunuliwa,lakini wakati huo huo anadai posho haitoshi,dhamira ya kweli ipo hapo?
 
jizi tu lile li pinda ...hakuna mtoto wa mkulima wala nini.......mtu gani hana sauti yupo yupo tu?
 
Tarehe 24 mwezi huu kuanzia saa mbili asubuhi. kutakua na maandamano makubwa kwa mara ya kwanza kutokea tanzania. kupinga uozo wa viongozi wetu, tutakutana pale mnazi mmoja hivyo mnaombwa kuhudhuria ili tupiganie nchi yetu kutoka kwa mafisadi, wanyanganyi, wezi na matapeli. kufika kwako ndo kufanikisha hili.
 
Labda ingekuwa lugha ya kichangga hapo sina ujanja, kiingereza ata mbwa wangu nyumbani anajua, wewe ndio acha ushabiki kwa hiyo mpaka sasa bado utaki kukubali kama wabunge wako kina Mbowe wamekopa benki, labda nikuulize kwa nini Ofisi ya katibu wa bunge imewadhamini kwenye benki?

Kaka kuwa mwelewa, kama kweli mbwa wako nyumbani anaongea kiingereza, basi uelewa kuwa mkopo unazingatia kipato chako kwenye mshahara, na sio allowances ambazo hazina guarantee kama utapata au hautapata maana zinategemea sessions za Bunge, mara kadhaa bunge huwa linapunguza vikao kutokana na ufinyu wa bajeti na hivyo mbunge hapati hizo posho, lakini pia wakati mwingine wabunge huwa hawahudhurii vikao na hivyo hawezi pokea posho kama hajahudhuria kikao. Kipato kama hicho unawezaje kukopea benki yoyote haikubali maana siyo cha uhakika. Acha ushabiki wa Daily News. Chadema haitafuti umaarufu maana tayari ni maarufu. CCM ndo wanapambana na umaarufu wa Chadema.
 
imagine,ndo mtu aliyewahi kutamka kuwa anapiga stop mashangingi,na hata wakati fulani alithubutu kukataa alilonunuliwa,lakini wakati huo huo anadai posho haitoshi,dhamira ya kweli ipo hapo?

ndio maana nasema mnafiki sana yule...yeye anatumia gx akiwa na ziara ndani ya msafara wake kuna watu wana vx.....hana maana yule mnafiki tu...anakera sana....
 
[TABLE="class: contentpaneopen"]
[TR]
[TD="class: contentheading, width: 100%"]Sakata la Posho:Chadema wamkaba koo Waziri Mkuu [/TD]
[TD="class: buttonheading, width: 100%, align: right"] Send to a friend [/TD]
[/TR]
[/TABLE]
[TABLE="class: contentpaneopen"]
[TR]
[TD="class: createdate"] Sunday, 19 June 2011 21:04 [/TD]
[/TR]
[TR]
[TD]

14pindaa.jpg
Waandishi Wetu, Dodoma na Dar
SUALA la kufutwa kwa posho za wabunge na watumishi wengine wa umma bado ni mwiba kwa Serikali, baada ya Chadema kuzidi kumbana Waziri Mkuu, Mizengo Pinda na safari hii wakimtaka afute kauli yake kwamba posho hizo zipo kisheria kwa kuwa si kweli vinginevyo watachukua hatua kali zaidi.
Chama hicho pia kimemtaka Waziri Mkuu, kuueleza umma kwamba kauli yake ya kuwa Wabunge wa Chadema wanazimezea mate posho hizo, si kweli kwani msimamo wa kuzipinga upo kwenye Ilani ya chama hicho ya mwaka 2010.

Katibu wa Wabunge wa Chadema na Kambi ya Upinzani bungeni, John Mnyika aliwaambia waandishi wa habari jana mjini Dodoma kuwa Pinda anapaswa kufanya hivyo kabla ya mwisho wa mkutano huo wa bajeti, vinginevyo wabunge wa chama hicho watakaa na kujadili cha kufanya.

Alisema kauli ya kuhalalisha posho za wabunge kwa hoja ya kwamba zinahitajika kwa ajili ya kuwapa watu wanaoomba fedha nje ya Ukumbi wa Bunge siyo sahihi kwani ni kinyume na misingi ya Bunge na maadili yake.

“Waziri Mkuu, Pinda anapaswa kufuta kauli yake kwani inapotosha majukumu ya Bunge na wabunge wake yaliyotajwa kwenye ibara ya 63 kifungu cha (2) na (3) ya kuisimamia Serikali, kuwakilisha wananchi, kupitisha mipango na kutunga sheria,” alisema na kuongeza:

“Kauli ya Waziri Mkuu Pinda inahamasisha siasa za fadhila katika taifa, ambazo zimetumika na CCM kupandikiza mbegu za rushwa katika uchaguzi kwa kisingizio cha takrima."

Mnyika alisema kauli hiyo ya Pinda inadhihirisha kuwa hana dhamira ya dhati kutekeleza kwa ukamilifu na kwa haraka maagizo ya Rais Jakaya Kikwete kinyume na Katiba ibara ya 52 (3) inayomtaka atekeleze au asababishe utekelezaji wa jambo lolote ambalo Rais ataagiza kwamba litekelezwe.

Alisema akiwa Katibu wa wabunge wa Chadema anamtaka Waziri Mkuu, Pinda kuelewa kuwa suala la kutaka mabadiliko ya mfumo wa posho ni la pamoja kwa Chadema na hivyo kumtaka Waziri Mkuu huyo kusoma ilani ya chama hicho kupata msingi wa msimamo huo.

“Kama sehemu ya kuimarisha uchumi kwa kuondoa ubadhirifu ilani ya Chadema ya Agosti 2010 kifungu cha 5.5.1 kipengele cha 5 imeeleza bayana kuwa Serikali ya CCM imekuwa ikitenga kiwango kikubwa cha fedha kwa ajili ya posho,” alisema Mnyika huku akitolea mfano wa posho za Ofisi ya Rais na Bunge kwa mwaka 2009/10

Aliendelea, "Kipengele cha 6 kwenye ilani ya Chadema ya mwaka 2010 kimeeleza bayana kwamba Serikali ya Chadema itaweka utaratibu ili semina, warsha, mafunzo na vikao katika taasisi mbalimbali za umma zifanyike kama sehemu ya kazi bila uwepo wa posho maalumu za vikao kwa siku.”

Zitto asema Pinda anapingana na Mpango wa Taifa wa Maendeleo

Mbunge wa Kigoma Kaskazini (Chadema), Zitto Kabwe amemtaka Pinda ajiuzulu au afukuzwe kazi mara moja kutokana na kutetea posho hizo kuwa zipo kwa mujibu wa sheria zilizoanishwa kikatiba na kudai wapo Wabunge wa Chadema wanaozimezea mate.

Akizungumza na gazeti hili jana, Zitto alisema, " Mimi nina mambo mawili kwa Waziri Mkuu, anapaswa kuchukua uamuzi ama ku resign (kujiuzulu) au afukuzwe kazi mara moja kwa kutetea posho."

Akitetea hoja yake, Zitto alisema kitendo cha Pinda kutetea posho kimemfanya ashindwe kutekeleza uamuzi wa kisera wa Baraza la Mawaziri ambao pia ulipitishwa na Bunge, hivyo anapaswa kujiuzulu.

"Kwanza, nasikitika kuwa Waziri Mkuu amerejesha suala la posho za vikao kwenye mjadala ilhali lilimalizwa baada ya Bunge kupitisha Mpango wa Maendeleo wa miaka mitano. Kitendo cha Waziri Mkuu kulilia posho kinaonyesha jinsi asivyo tayari kusimamia na kutetea sera za Serikali yake anayoiongoza," alisema na kuongeza:

"Anapaswa kuchukua hatua mbili, ama afukuzwe kazi mara moja kwa kwenda kinyume na maamuzi ya kisera ya Serikali yaliyopitishwa na Baraza la Mawaziri kisha Bunge au, ajiuzulu. Hatuwezi kuvumilia viongozi wanaokwenda kinyume na sera za Serikali."

Zitto alisema uamuzi huo wa Baraza la Mawaziri ambao ni wa Serikali uliomo katika Mpango wa Taifa wa Maendeleo kwa miaka mitano, umeanisha maeneo ya vipaumbele na namna ya Serikali kudhibiti matumizi yakiwamo kukata posho na kupunguza misafara ya safari za viongozi.

Naibu Kiongozi huyo wa upinzani bungeni alifafanua kwamba, baada ya uamuzi huo kujadiliwa ulipitishwa na wawakilishi hao na kuonyeshwa kushangazwa na kauli hiyo ya Waziri Mkuu.

"Kauli ya Waziri Mkuu haiwezi kupita hivi hivi bila kuhojiwa. Waziri Lukuvi (Sera, Uratibu na Bunge), alisema kuondolewa kwa posho za vikao ni msimamo wa Serikali katika Mpango wa Maendeleo wa Miaka Mitano. Then (kisha ukaletwa na Serikali na Bunge likaujadili na kuupitisha," alisema Zitto na kuongeza,

"Sasa leo hii, wiki moja baada ya kupitishwa na Bunge, Waziri Mkuu anakuja kusema posho ni suala la kikatiba, hivyo anakwenda kinyume na uamuzi wa kisera wa Serikali, kimsingi, anapaswa ku resign ua kufukuzwa."

Aliongeza kwamba, tayari uamuzi huo uliotokana na Baraza la Mawaziri na kisha kupitishwa na Bunge umeanishwa katika mpango huo ukurasa wa 17, hivyo kitendo cha mkuu huyo wa shughuli za kiserikali bungeni ni kuupingana nao.

Zitto alisema akiwa waziri Kivuli wa Fedha, leo anatarajia kuwasilisha hoja bungeni akimtaka Waziri Mkuu ajiuzulu kutokana na mapungufu hayo ya kiutendaji.

"Natarajia kuwasilisha hoja hiyo bungeni kutaka Waziri Mkuu ajiuzulu wakati nikichangia. Haiwezekani Waziri Mkuu apingane na maamuzi ya kisera ya Serikali ambayo pia yamepitishwa na Bunge."

Mapema mwezi huu Zitto alimwandikia Spika wa bunge barua akielezea kusudio lake la kukataa posho ya vikao vya wabunge bungeni, akijenga hoja kwamba hiyo ni sehemu ya kazi yake, hivyo kulipwa ni makosa akitaka fedha hizo zielekezwe jimboni kwake.

Hata hivyo, hoja hiyo ambayo imetekwa na chama chake cha Chadema inaonekana kuitikisa nchi huku viongozi wa dini, wasomi na watu wa kada tofauti wakijadili kwa mitazamo tofauti.

Askofu awalipua wabunge kuhusu posho

Askofu wa Dayosisi ya Kaskazini ya Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Dk Martin Shao juzi alitema cheche akiwataka wabunge kuacha kutanguliza ubinafsi katika kung’ang’ania kulipwa posho za vikao vya Bunge.

Badala yake, Dk Shao alisema posho hizo na zile wanazolipwa watumishi wa umma waliofikia ngazi ya menejimenti zielekezwe kuboresha maslahi ya watumishi wa umma wanaofanya kazi katika mazingira magumu vijijini.

Kauli hiyo ya Askofu Shao imekuja siku chache baada ya Waziri Mkuu, Pinda kutetea malipo hayo ya posho ambayo yamezua malumbano makubwa bungeni kati Wabunge wa Upinzani , CCM na Spika, Anne Makinda.

“Nchi hii kuna uozo huko kwa wakubwa kutanguliza mambo binafsi…mimi kwanza…na hili limesumbua sana kwenye Bunge wiki hii, wakubwa kwanza, waheshimiwa wabunge kwanza,”alisema Dk Shao.

Askofu Shao alisema yeye anaungana na wale wanaopinga kulipwa kwa posho hizo akisisitiza kuwa si haki wabunge kutanguliza umimi na kuwataka wabunge na vigogo serikalini wasiingie katika dhambi ya umimi.

"Posho hizo ziende zikaboreshe matabibu vijijini, ziende kwa walimu wetu wanaofundisha katika mazingira magumu, kutanguliza umimi siyo haki, tunaomba sana wabunge msiangalie mambo yenu wenyewe,"alisisitiza Askofu Shao.

Dk Shao alisema ni vyema Serikali ikawa na mpango mahsusi wa kuendesha sekta ya afya kwa kushirikiana na mashirika ya dini, ili kuhakikisha hospitali na zahanati vijijini zinakuwa na madaktari na wauguzi mahiri.

Habari hii imeandikwa na Daniel Mjema, Hai, Kizitto Noya na Masoud Masasi, Dodoma, Ramadhan Semtawa, Dar.
[/TD]
[/TR]
[/TABLE]
 
It is so simple. Nimekopa benki na katibu wa Bunge kama Mwajiri ndiye mdhamini. Ila sijakopa kwa kutumia posho za vikao wala posho za kujikimu. Nimekopa kwenye mshahara wangu. Wala sioni aibu kusema hili popote. Kukopa hakuna mahusiano na hoja ya kuondoa posho za vikao.

Kukopa ni njia mojawapo ya kujiongezea kipapo kwa uhalali na hii haina uhusiano na hoja ya kufuta posho za watumishi wa serikali pamoja na wabunge maarufu kama (Sitting Allowances). Zito na Chadema Muwe na Moyo mkuu, tayari tumeshawashinda hawa, wanatapatapa tu.
 
Nyie Pro-Chadema msiwe kama makinda ya bata yanamfata mama yao ata popote anapokwenda kama anavuka barabara. Hawo viongozi wenu wameishachukuwa mikopo benki kupitia hizo posho wanazozisema tena wa kwanza kuchukuwa ni Mbowe 200 milioni Zitto 150 milioni, mdhamini wao ni ofisi ya katibu wa bunge
Acha kua na akili kama ya NEPI wewe, suala sio nani kakopa, tsh ngapi, na nani hajakopa,Suala ni kua unapokea mshahara kila mwezi, halafu kila siku unayoenda kazini hapohapo unapolipwa huo mshahara tena unadai posho ya kila siku, inakujaje hii?kwanin basi kama ni utaratibu mzuri usiwekwe kwa taasis zingine za serikali kama walimu, madaktari, wauguzi n.k?Tumia kichwa kufikiri, sio Tumbo
 
lkn yanapokuja kufuta kodi kwa makanisa na vifaa vya dini huwa wakali sana. hii ndio viongozi wetu wa dini bana. wamesahau wamewateteavya kutosha

Mashirika ya dini yanajenga shule, Hospitali, vyuo vikuu n.k kazi ambazo zilipaswa kufanywa na serikali kwa vifaa ambavyo serikali isingelipia kodi. Hivi huoni wanaisadia serikali kuboresha huduma za jamii na kama mashirika ya dini yanafanya kwa niaba ya serikali kuna ubaya gani vifaa kama hivyo kuwa na tax exemption?

Ninakuheshimu MS na ili ku-maintain status yako usifanye analysis za kishabiki au za kichovu kwani pia ni ruksa kuwa kimya na kumeza mate kama jambo limekukuna.
 
Back
Top Bottom