wamesema ni posho zisizo za lazima tuuuuuuuuuuuu........
utakuwa umetumwa na wanamagamba!!!!
[h=3]Askofu KKKT ajitosa mjadala wa posho[/h]
*Ataka wabunge wanaozikataa waungwe mkono
*Mbowe azifananisha na wizi wa kutisha
Na Martha Fataely, Hai
ASKOFU wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Dayosisi Kaskazini, Dkt. Martin Shao, ameunga mkono hoja ya
wanaotaka kufutwa kwa posho zisizokuwa za msingi kwa watumishi wote wa umma na wabunge kwa maslahi ya taifa.
Msimamo huo ulitolewa mjini hapa juzi ikiwa ni siku chache tangu Kambi ya Upinzani Bungeni iwasilishe mapendekezo ya kutaka posho zisizo za lazima kwa watumishi na wabunge ziondolewe kwa kuwa ni mzigo kwa taifa.
Asjkofu Shao alitangaza msimamo huo wakati wa mahafali ya 40 ya Chuo cha Uganga Machame kinachomilikiwa na kanisa hilo, ambapo wanafunzi 48 walihitimu masomo ya stashahada ya utabibu.
Alisema hoja hiyo ni ya msingi hasa kwa kuzingatia kuwa Tanzania ni nchi maskini, ambayo inahitaji uangalizi wa fedha, na siyo kila mmoja kuangalia maslahi yake binafsi.
"Taifa limekuwa likikumbwa na matukio ya wizi, ubadhirifu na ufisadi wa kutisha, hivyo wanapotokea watu wachache ambao wanaonekana kutafuta kupunguza matumizi yasiyo ya lazima, sisi kama taifa tunapaswa kuwaunga mkono na kukemea pale inapobidi," alisema Askofu Shao na kuongeza kuwa;
"Nchi hii kuna uozo wa watu kuangalia maslahi yao, yaani wao kwanza, tabia hii twapaswa kuiepuka, kila mtu asiangalie mambo yake mwenyewe, bali aangalie na ya wengine," alisema.
Kwa mujibu wa askofu huyo, baadhi ya watumishi wamekuwa wakilipwa posho ambazo zingeweza kusaidia kuboresha huduma za afya kwa kuwapa motisha wale wanaofanyakazi katika mazingira magumu ili wananchi wanaoishi katika maeneo hayo waweze kupata huduma bora.
Alisema ni vyema kwa serikali kuona umuhimu wa kubadili sera hizo ili kuwawezesha watumishi wake kuongezewa mishahara na kupata kipato kutokana na mishahara yao halali na siyo kujilundikia posho.
Askofu Shao alitoa mwito kwa serikali kuona umuhimu wa kuboresha huduma maeneo ya vijijini, hasa kwa upande wa sekta ya afya na kutilia mkazo utaratibu wa kuwapangia vituo vya kazi wataalamu kuanzia ngazi ya zahanati, vituo vya afya na hospitali
Alisema zaidi ya asilimia 80 ya wakazi nchini wanaishi vijijini na hukumbwa na tatizo la upungufu wa huduma hizo, lakini serikali imekuwa ikitoa asilimia 60 ya huduma hizo huku ikichangiwa na mashirika ya dini kwa asilimia 40.
Dk. Shao alisema kanisa limekuwa likijikita zaidi kutoa huduma hizo vijijini, hivyo serikali inapaswa kuunga mkono jitihada hizo kwa lengo kuwaondolea wananchi kero ya kutumia gharama kubwa kupata matibabu.
Awali, akizungumza wakati wa mahafali hayo, Mbunge wa Jimbo la Hai, Bw. Freeman Mbowe alielezea masikitiko yake juu ya taarifa mbalimbali zinazotolewa na vyombo vya habari zikipotosha ukweli wa suala la posho.
Bw. Mbowe alisema anashangazwa na vyombo vya habari kuripoti kuwa ugomvi wa posho ni miongoni mwa wabunge, jambo ambalo alisema siyo kweli, kwani wamekuwa wakipinga posho zisizokuwa na umuhimu kwa watumishi wa kada za manejimeti na wabunge.
Alisema kambi ya upinzani imekuwa ikipinga posho nyingi zinazotolewa au kuchukuliwa na baadhi ya watumishi wa kada za juu ambao kwa siku huweza kuandikiwa au kujiandikia posho zaidi ya mara tatu.
"Jamani nilichokuwa napinga ni hiki, unakuta mbunge analipwa posho ya kujikimu yaani malazi, chakula na mawasiliano sh. 80,000, hii hatuna ugomvi nayo, lakini akihudhuria bungeni hata kama anaumwa yaani hatakaa siku nzima, analipwa pesa ya kukaa sh. 70,000, jamani huu ni wizi wa kutisha," alisema Bw. Mbowe.
Alisema kwa upande wa menejimenti za utumishi wa umma, pia kuna posho zisizohesabika kwani kila mwezi hujikuta wanalipwa mshahara sh. milioni moja na posho sh. milioni tano. - NI UKWELI KABISA
"Watu ambao wamekuwa wakifaidi posho hizi ni wale mawaziri, makatibu wakuu, wakurugenzi, wakuu wa idara lakini wale wafanyakazi wa kawaida wala hawapati chochote na ndiyo maana kunakuwa na tofauti kubwa kati ya walionacho na wale wasiokuwa nacho ilihali wote wanalipwa mshahara," alisema.- NA HIZI POST NI KWA AJILI YA WANAMAGAMBA TUUUUU
"Unakuta mtu haonekani ofisini, kazi yake ni kuvizia vikao vya posho, anaingia cha kwanza anasaini na kuondoka, vile vile kama ni ofisa elimu anakwenda kukagua miradi ya elimu analipwa posho na wakati huo ametumia gari la serikali lenye mafuta lakini pia mshahara upo pale pale," alisema.
Bw. Mbowe aliwataka Watanzania kuwaombea kwa kukataa posho kwani kuna hatari ya wao kutolewa roho, kwa kuwa wamegusa maslahi ya wakubwa zaidi. Hata hivyo alisema hawahofii hilo.
Alisema matumizi mabaya ya fedha za walipa kodi ni makubwa. Alitoa mfano akisema wabunge wanapotaka kusafiri badala ya kutumia usafiri wenye nafuu kwa manufaa ya taifa, wanatumia gharama kubwa bila msingi.
"Kwa mfano, ukishakuwa mbunge tu ujue umeula, kwani kwenye ndege ukipanda unakaa First Class (daraja la kwanza) kwenda Marekani nauli yake ni dola 8,000 (sh milioni 12) wakati ndege hiyo hiyo, ina vipengele vya Business Class dola 5,000 (sh milioni 7.5) na Economy Class sh. milioni 1.8, haya ni matumizi mabaya," alisema.
Alisema kutokana na hali ya umaskini hapa nchini viongozi wanapaswa kuona umuhimu wa kupunguza matumizi yasiyokuwa ya lazima ili kutatua kero mbalimbali zinazowakabili wananchi wake. WEWE UNASEMAJE??
Awali Kaimu Mkurugenzi wa Hospitali ya Machame, Dkt. Elisinya Masawe aliwashukuru washirika wa maendeleo wa hospitali hiyo kutoa shirika la Alegent Health la Marekani hususani mwakilishi wake, Bw. Robert Cassworn kwa moyo wa kujitolea kuisadia hospitali hiyo.