Posho na Mishahara ya wabunge...

Posho na Mishahara ya wabunge...

Wanabodi,
Mjadala wa Posho za Wabunge, umerindima kwenye kipindi cha Baragumu ambacho kiko live Channel Ten wakati huu ninapoandika post hii. Mgeni mwalika ni Katibu Uenezi wa CCM, Nape Mnauye na mchokoza mada ni Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe aliyechokoza mada kwa njia ya simu.

Mtoa hoja ni Kiongozi wa Upinzani Bungeni, Freeman Mbowe, amefafanua vizuri sana msimamo wa Chadema na kujielekeza suala la posho za Wabunge, ni suala mtambuka zaidi ya posho za wabunge pekee bali ni posho za watumishi wote wa umma kwa ujumla wao, zikikatwa zitaokoa zaidi ya Shilingi Bilioni 900. Mhe. Mbowe, amekwenda mbali zaidi na kufafanua kwa nini Chadema inapigania kufutwa kwa posho hizo na sio kila posho lazima ifutwe, posho kama za kujikimu ni posho muhimu hivyo Mbowe amesema hana tatizo nazo.

Pia Mheshimiwa Mbowe ameweka bayana suala la posho lisionekana ni la Wabunge wa Chadema tuu, linapaswa kuwa ni suala la bunge lote kwa sababu linahusu maslahi ya taifa. Mbowe akasisitiza ukiweka maslahi ya taifa mbele badala ya maslahi binafsi.

Ilipofika zamu ya Nape, aliunga mkono hoja ya Mbowe kuwa kuna posho za lazima na zile ambazo sio za lazima. Amekubaliana na Mbowe kuwa posho ya kujikimu ni posho ya lazima, hivyo iendelee kuwepo. Mhe. Nape, amekwenda mbali zaidi kwa kueleza dhamira yake ya dhati kupunguza gap kati ya wenye nacho na wasio nacho. Amekiri wafaidika wa posho ndio wale wale wenye mishahara minono na marupurupu kibao. Amesisitiza hoja siyo ya Chadema, hoja iko kwenye ule mpango wa miaka 5. Amesema unaungana na hoja za kufutwa kwa posho ambazo sio za lazima, ila kwa vile posho hizo zipo kisheria, basi kuondolewa kwa posho hizo kufuate utaratibu.

Miongoni mwa wachangiaji kwa simu ni Mhe. Zarina Madabida, aliiweka wazi kuwa suala la posho liko kwenye hotuba ya bajeti. Naye alitetea msimamo wa kuwepo kwa posho muhimu na kutolea mfano posho za madakitari na uwepo wa per diem. Huyu mbunge Mama Madabida, aliwashutumu wabunge wa upinzani kwa kuuiba hoja ya posho baada ya kuikuta kwenye kamati, hivyo kuiteka hoja.

MY TAKE.
Mbowe amejieleza vizuri sana kwenye hili suala la posho. Nape pia is good, anasimamia maslahi ya taifa.
 
Wewe toka lini Nape akasimamia maslahi ya Taifa? Na kama ilikuwa sera yao mbona ilikuwa iko kimya kimya, iko mipango mizuri sana lakini huwa haitekelezwi hata ama ni agenda yao ilikuwa imeshakaa kapuni.
 
okay......kama ipo kwenye bajeti basi tuwait tuone hatua zipi zitachukuliwa
 
Nepi ni ganda la kufa

Siwezi kusikiliza huu upuuzi, nepi anatumia viungo vingine kufikilia sio brain
 
Ironically, two top CHADEMA leaders, who have been vocal and championed the debate to have MPs sitting allowances slashed, are among the biggest creditors. One has taken a 196m/- loan and another 100m/- both from CRDB Bank.

Records show that each MP (Daily News is in possession of the long list of the creditors) gets a 2,305,000/- monthly salary plus 5,115,000/- as constituency allowance, making the total deductible pay to 7,420,000,000/-.

The documents indicate that 883,000/- is deducted every month for five years to cover the 45m/- personal car loan each MP was advanced and a further 588,000/- paid as government taxes.
However, the package does not cover per diem and sitting allowances which are only paid if an MP has attended Bunge sessions.

“
Source; Daily News

Wako wapi wale Pro-Chadema walikuwa wanapinga eti hakuna benki inayoweza kutoa mikopo kupitia posho, LAT na wenzako mpooo???

hapo kwenye red.........acha ushabiki , soma bandiko hilo vizuri au lugha haipandi
 
Wanabodi,
Mjadala wa Posho za Wabunge, umerindima kwenye kipindi cha Baragumu ambacho kiko live Channel Ten wakati huu ninapoandika post hii.

Mtoa hoja ni Kiongozi wa Upinzani Bungeni, Freeman Mbowe, amefafanua vizuri sana msimamo wa Chadema na kujielekeza suala la posho za Wabunge, ni suala mtambuka zaidi ya posho za wabunge tuu. Mhe. Mbowe, amekwenda mbali zaidi na kufafanua kwa nini Chadema inapigania kufutwa kwa posho hizo na sio kila posho ikiwemo kuunga mkono uwepo wa posho za kujikimu.

Pia Mheshimiwa Mbowe ameweka bayana suala la posho lisionekana ni la Wabunge wa Chadema tuu, linapaswa kuwa ni suala la bunge lote kwa sababu linahusu maslahi ya taifa. Mbowe akasisitiza ukiweka maslahi ya taifa mbele badala ya maslahi binafsi.

Ilipofika zamu ya Nape, aliunga mkono hoja ya Mbowe kuwa kuna posho za lazima na zile ambazo sio za lazima. Amekubaliana na Mbowe kuwa posho ya kujikimu ni posho ya lazima, hivyo iendelee kuwepo. Mhe. Nape, amekwenda mbali zaidi kwa kueleza dhamira yake ya dhati kupunguza gap kati ya wenye nacho na wasio nacho. Amekiri wafaidika wa posho ndio wale wale wenye mishahara minono na marupurupu kibao. Amesisitiza hoja siyo ya Chadema, hoja iko kwenye ule mpango wa miaka 5. Amesema unaungana na hoja za kufutwa kwa posho ambazo sio za lazima, ila kwa vile posho hizo zipo kisheria, basi kuondolewa kwa posho hizo kufuate utaratibu.

Miongoni mwa wachangiaji kwa simu ni Mhe. Zarina Madabida, aliiweka wazi kuwa suala la posho liko kwenye hotuba ya bajeti. Naye alitetea msimamo wa kuwepo kwa posho muhimu na kutolea mfano posho za madakitari na uwepo wa per diem. Huyu mbunge Mama Madabida, aliwashutumu wabunge wa upinzani kwa kuuiba hoja ya posho baada ya kuikuta kwenye kamati, hivyo kuiteka hoja.

MY TAKE.
Mbowe amejieleza vizuri sana kwenye hili suala la posho. Nape pia is good, anasimamia maslahi ya taifa.

Hapo ndipo wana magamba wanaposhangaza, eti wabunge wa upinzani wameiba hoja kwenye kamati?? mwizi siku zote humshuku mwenzake naye ni mwizi, kila mahali wanajishuku tu kwa kuwa wamezoea kuiba!!

Hata tukikubaliana naye kwamba hoja hiyo ilianzia kwenye kamati bado tunauona unafiki wao kwani hakuna mbunge mwingine wa magamba aliyesimama hadharani kutetea kuondolewa kwa posho zaidi ya january makamba, sasa kama waliizungumza kwenye kamati mbona tena wakija hadharani hawaitetei hoja yao??

Pamoja na yote safari hii wanamagamba hawatoki, posho lazima zifutwe, ili waache kuwa masultani majimboni na kuendelea kuwafanya wananchi omba omba!!
 
Nyie Pro-Chadema msiwe kama makinda ya bata yanamfata mama yao ata popote anapokwenda kama anavuka barabara. Hawo viongozi wenu wameishachukuwa mikopo benki kupitia hizo posho wanazozisema tena wa kwanza kuchukuwa ni Mbowe 200 milioni Zitto 150 milioni, mdhamini wao ni ofisi ya katibu wa bunge
Sijawahi kuona mkopo unaotolewa kwa kutegemea malipo ya posho..hyo mikopo unayosema inalipwa na mishahara yao..acha kupotosha watu.
 
lazima wakubaliane na CDM maana ndo wameshika remote control ya CCM ni kubofya tu angaliwa watu wanavyogongana vichwa leleleeeee weee wewe heeeeee kazi ipo...
 
  • Thanks
Reactions: FJM
yaan Nape anageuka kinamna namna awafurahishe wanainchi na mafisadi at the same time
Mpuuzi Nape
 
Kwa hiyo, Rais kupitia mpango wa taifa wa maendeleo anataka posho ziondolowe, chama tawala (ccm) kupitia kwa katibu wake mwenezi nacho kinakubaliana na hoja ya kuondoa posho. Lakini Waziri mkuu ambaye anayesimamia shughuli za serikali kama anavyoagizwa na Rais anapingana na hoja ya posho kuondolewa. Tena anafanya hivyo mbele ya chombo cha kutunga sheria sehemu ambapo sheria ya kufuta posho ingeweza kupitishwa. Sasa, Waziri mkuu anamuakilisha nani? How can he lead when he does not agree with the government policy. His position as Prime Minister in my view is unattainable. Anatakiwa ajiuzulu maana hana dhamira ya kweli ya kusimamia utekelezaji wa mipango ya serikali.
 
hapo kwenye red.........acha ushabiki , soma bandiko hilo vizuri au lugha haipandi
Labda ingekuwa lugha ya kichangga hapo sina ujanja, kiingereza ata mbwa wangu nyumbani anajua, wewe ndio acha ushabiki kwa hiyo mpaka sasa bado utaki kukubali kama wabunge wako kina Mbowe wamekopa benki, labda nikuulize kwa nini Ofisi ya katibu wa bunge imewadhamini kwenye benki?
 
Labda ingekuwa lugha ya kichangga hapo sina ujanja, kiingereza ata mbwa wangu nyumbani anajua, wewe ndio acha ushabiki kwa hiyo mpaka sasa bado utaki kukubali kama wabunge wako kina Mbowe wamekopa benki

not my caliber ..... enjoy your foolishness

bye
 
[Miongoni mwa wachangiaji kwa simu ni Mhe. Zarina Madabida, aliiweka wazi kuwa suala la posho liko kwenye hotuba ya bajeti. Naye alitetea msimamo wa kuwepo kwa posho muhimu na kutolea mfano posho za madakitari na uwepo wa per diem. Huyu mbunge Mama Madabida, aliwashutumu wabunge wa upinzani kwa kuuiba hoja ya posho baada ya kuikuta kwenye kamati, hivyo kuiteka hoja.]

Kwani hiyo Kamati inawajumbe wa CCM tu? Si inawezekana kwamba wajumbe wa upinzani (hata kama ni mmoja) akalipeleka kwenye hiyo kamati. Kama chadema ilidhamilia hili hata kuwa kwenye ilani ya uchaguzi 2010 kwa nini tusiseme ni hoja yao? Huko kweye hotuba ya budget anayosema kuna maneno tu kwambwa serikali itaangalia posho zinazotolewa na kuziondoa zisizo na tija, hakutaja kiasi gani wataokoa. Waziri mkuu kadai hiyo posho inatija. Ulitegemea nini?

Wapinzani wameshitukia mchezo wa kuweka mambo kwenye maandishi na kukaa kimya. Ndo maana CCM sasa wanajikanyaga kanyaga tu, hawaelewani kama wajenzi wa mnara wa baberi.
 
Mh.Pinda kasema posho inawasaidia wabunge 'kuwatoa' 'wapiga mizinga'. utata mtupu!
 
nape ni mpuuzi sana.........hana lolote ...ila pinda ndo kazid sana....
 
Sioni uhusiano wa posho inayolalamikiwa na mikopo ya bank. Hawa wabunge wanavyanzo vingine vya mapato kama miradi binafsi
Hivyo sioni tatizo wakakopo bank
 
Back
Top Bottom