Popote ulipo wewe daktari, Mungu akulaani sana

Story
Story ya kutunga hii.. Kwa tabata hospitality ya mission siikumbuki zaidi ya pale Aroma ambayo ni binafsi kuna sanamu tu ya Mariamu ambaye ni Mama take na Yesu.. Na kupima wataandaliwa wanaopima na majibu wanapewa wahusika kwa kushauriwa ipasavyo bila sent yoyote..
Tabata Aroma ile hospital sio ya wakatoliki kweli?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Pole
Ila huwezi kujua pia ni nini Mola kakuepusha kutoka kwa huyo binti.
Au nae aliongwa?

Ungemtaja huyo daktari iliufurahie tu
 
Kama mwezi uliopita niliamua niende kanisani kuongea na mchungaji kumwambia nia yangu ya kuoa.

Mimi ni msabato mzuri sana. Mchungaji alinisaidia akanikutanisha na binti mmoja tuliyekuwa tunasali naye ambaye ambaye sisiti kumtaja jina lake anaitwa Winfilda Yusto Kingomile.

Mimi na huyo binti tukakubaliana kuwa wachumba kiukweli nilifurahi sana.

Sasa kama zilivyo taratibu zetu za kisabato. Mchungaji wetu akatuandikia barua ambayo tulipaswa kwenda mayo hospitali tukapime ili tujue afya zetu kwa ajili ya kujiandaa na harusi yetu.

Mimi na mchumba wangu tulienda mpaka hospitali moja ya misheni inayomilikiwa na kanisa la Roman Catholic kiukweli siwezi kuitaja jina kabisa iliyopo Tabata.

Tukamkabidhi daktari ile barua yetu tuliyotoka nayo kanisani kwetu, baada ya kuisoma daktari akatuelekeza kuelekea maabara kuchukuliwa damu kwa ajili ya vipimo.

Baada ya kama saa moja mimi nikaitwa chumba cha daktari nilipoingia cha kwanza daktari aliniuliza swali kwamba " una hela"?
Mimi nikamjibu "sina hela" huku nikiwa sijaelewa mantiki ya swali lile.

Basi daktari akaamuru na mchumba wangu aingie ndani. Alipoingia ndani daktari akatukabidhi majibu yetu yakiwa yapo kwenye bahasha na tulitakiwa tukampe mchungaji wetu kanisani bila ya kufungua bahasha hiyo.

Kwa sababu ya imani nzuri tuliyonayo ni kweli hatukufungua bahasha ile ya majibu yetu mpaka tukamkabidhi mchungaji wetu pale kanisani.

Baada ya mchungaji kusoma majibu Yale ghafla akawa mnyonge na akatuagiza tuwaite wazazi wetu waje pale kanisani. Ni kweli baada ya wazazi wetu kuja sisi tukatolewa wakabaki wazazi tu kwa mchungaji.

Baadaye wazazi wangu waliniambia kwamba majibu yanaonesha nimeathirika hivyo ndoa hakuna tena.

Kiukweli nilichanganyikiwa sana tena sana. Ila baba yangu mdogo alinishauri nikapime sehemu nyingine kwa kujiridhisha.

Nikaenda kupima Muhimbili, Amana, Mwananyamara, magomeni, Agakhan, kote huko nikaambiwa sina UKIMWI.

Nikajitosa kwenda kuchangia damu pia damu yangu ikaonekana ipo safi.

Nikarudi kumbembereza mchumba wangu na kumwambia kila kitu lakini yeye na ndugu zake hawataki kabisa kunisikia. Nikamwambia mchungaji wangu yaliyotokea naye amebaki kaduwaa tu.

MPAKA SASA SIJAJUA HUYU DAKTARI ALIKUWA ANAMAANA GANI?

ULAANIWE SANA WEWE DAKTARI.
Hili lilimtokea rafiki yangu na ilibaki kidogo tu ajiuwe.... Bahati nzuri habari hazikumfikia mchumba wake... Tukapundua majibu.... Baada ya ndoa tukafanya utaratibu akapima zaidi ya mara 4 hola... Huu ni mwaka wa 5 ndoa yake ana siha njema na vidume wawili walionona

Jr[emoji769]
 
Kama mwezi uliopita niliamua niende kanisani kuongea na mchungaji kumwambia nia yangu ya kuoa.

Mimi ni msabato mzuri sana. Mchungaji alinisaidia akanikutanisha na binti mmoja tuliyekuwa tunasali naye ambaye ambaye sisiti kumtaja jina lake anaitwa Winfilda Yusto Kingomile.

Mimi na huyo binti tukakubaliana kuwa wachumba kiukweli nilifurahi sana.

Sasa kama zilivyo taratibu zetu za kisabato. Mchungaji wetu akatuandikia barua ambayo tulipaswa kwenda mayo hospitali tukapime ili tujue afya zetu kwa ajili ya kujiandaa na harusi yetu.

Mimi na mchumba wangu tulienda mpaka hospitali moja ya misheni inayomilikiwa na kanisa la Roman Catholic kiukweli siwezi kuitaja jina kabisa iliyopo Tabata.

Tukamkabidhi daktari ile barua yetu tuliyotoka nayo kanisani kwetu, baada ya kuisoma daktari akatuelekeza kuelekea maabara kuchukuliwa damu kwa ajili ya vipimo.

Baada ya kama saa moja mimi nikaitwa chumba cha daktari nilipoingia cha kwanza daktari aliniuliza swali kwamba " una hela"?
Mimi nikamjibu "sina hela" huku nikiwa sijaelewa mantiki ya swali lile.

Basi daktari akaamuru na mchumba wangu aingie ndani. Alipoingia ndani daktari akatukabidhi majibu yetu yakiwa yapo kwenye bahasha na tulitakiwa tukampe mchungaji wetu kanisani bila ya kufungua bahasha hiyo.

Kwa sababu ya imani nzuri tuliyonayo ni kweli hatukufungua bahasha ile ya majibu yetu mpaka tukamkabidhi mchungaji wetu pale kanisani.

Baada ya mchungaji kusoma majibu Yale ghafla akawa mnyonge na akatuagiza tuwaite wazazi wetu waje pale kanisani. Ni kweli baada ya wazazi wetu kuja sisi tukatolewa wakabaki wazazi tu kwa mchungaji.

Baadaye wazazi wangu waliniambia kwamba majibu yanaonesha nimeathirika hivyo ndoa hakuna tena.

Kiukweli nilichanganyikiwa sana tena sana. Ila baba yangu mdogo alinishauri nikapime sehemu nyingine kwa kujiridhisha.

Nikaenda kupima Muhimbili, Amana, Mwananyamara, magomeni, Agakhan, kote huko nikaambiwa sina UKIMWI.

Nikajitosa kwenda kuchangia damu pia damu yangu ikaonekana ipo safi.

Nikarudi kumbembereza mchumba wangu na kumwambia kila kitu lakini yeye na ndugu zake hawataki kabisa kunisikia. Nikamwambia mchungaji wangu yaliyotokea naye amebaki kaduwaa tu.

MPAKA SASA SIJAJUA HUYU DAKTARI ALIKUWA ANAMAANA GANI?

ULAANIWE SANA WEWE DAKTARI.
MTAJE KWA MAJINA ANAAIBISHA TAALUMA YA UDAKTARI
 
WATU WANACHANGIA BILA KUJUA IMANI NA TARATIBU ZA IMANI ZINGINE, WANASHANGAA MAJIBU KUPEWA MCHUNGAJI? KWANI ALIYEWAAMBIA WAKAPIME NI NANI???

KUNA BAADHI YA NCHI ILI KUPATA VIZA LAZIMA UPIMWE UKIMWI, JE MAJIBU UNAKAA NAYO WEWE AU ALIYEKUAMBIA UKAPIME??

KUNA MAKANJANJA WENGI SAAAAANA HUMU HALLAFU WOTE WAJUAJI.
 
Hujataja jina lako, jina la hospitali uliyoenda, jina la Dr, jina la mchungaji, jina la mahala kanisa lako lilipo ila umetaja jina la aliyekua mchumba wako kwanini? Huku ni kukiuka miiko.
 
WATU WANACHANGIA BILA KUJUA IMANI NA TARATIBU ZA IMANI ZINGINE, WANASHANGAA MAJIBU KUPEWA MCHUNGAJI? KWANI ALIYEWAAMBIA WAKAPIME NI NANI???

KUNA BAADHI YA NCHI ILI KUPATA VIZA LAZIMA UPIMWE UKIMWI, JE MAJIBU UNAKAA NAYO WEWE AU ALIYEKUAMBIA UKAPIME??

KUNA MAKANJANJA WENGI SAAAAANA HUMU HALLAFU WOTE WAJUAJI.
Imani yake inaruhusu kutaja jina la mpenzi wake, Tena majina yote matatu. Kafanya kosa
 
Kuna madaktari nadhani hii kazi sio wito kabisaa kwao, nmekumbuka iliwahi nitokea lkn kwa kesi tofauti, nlkuwa mjamzito mimba ya miezi nane (R.I.P mwanang), nlkuwa naumwa nkaenda hospitalini nikamwambia Dokta naumwa, hakunipima akaniandikia dawa nkanywa, siku ya kesho yake nkashinda vzr ya tatu nkazidiwa kufika hospitalini Dr yule yule akanibadilishia dawa bila kunipima , kufika usiku nkazidiwa kumbe ni uchungu nkajifungua , lkn mwanang alitoka upande mmoja ameoza , ikabidi nikimbizwe hosp nyingine yule Dokta wa pili alishangaa akasema toka lini mjamzito akatibiwa bila kupimwa na huruhusiwi kunywa dawa ovyo, akasema hawa ndio wanaotufanya tuonekane wajinga, mtoto dawa zimemuua, sijawahi kuumwa roho kama ile siku, nlivyopona nkamfata nkamwambia unanikumbuka akajidai sijui nini nkamwambia subiri nkakushtaki kwa ulichonifanyia maana ushahidi nnao, aliniomba msamaha hadi machozi, lkn sijasahau hilo tukio hadi leo.
 
Imani yake inaruhusu kutaja jina la mpenzi wake, Tena majina yote matatu. Kafanya kosa

KWANI KWA WEWE KUJUA MAJINA YA HUYO CHUMBA UMEMJUA?? NA HATA KAMA WAPO WANAOMJUA BILA SHAKA HABARI HII WANAYO MAANA IMETOKEA KANISANI NA MNAJUA MAMBO YA KANISANI YAVOVUMA.
NYI KUFICHA ID ZENU HAIMAANISHI HUMU KUTAJA JINA LA MTU NI JINAI..
MNAFICHA ID ZENU ILI MCHANGIE MATUSI NA MAMBO AMBAYO HAMTAKI KUFAHAMIKA KAMA MNACHANGAMANA NAYO
 
Unatetea lkn sio sawa. Kutaja jina lako ni sawa, ila la mwenzake bila idhini yake haipendezi. Anyway ni mawazo yangu binafsi
 
HAPA LA MSINGI ANGEMTAJA HUYO DAKTARI KANJANJA NA HOSPITALI ANAYOFANYIA IKIENEA (VIRAL) ANACHUKULIWA HATUA TU HATA ZA KIUTAWALA. MAANA KESHAHARIBU MAISHA YA MTU, JAMAA ANGEJINYONGA JE??
 
Kupima wapimwe wengine majibu apewe mwingine hiki ni kitu ambacho hakiwezekani.
 
SDA V'S RC
shetani katulia pembeni anaangalia mtanange, ila hizi imani hizi sometimes muwe mnafikiria nje ya box, yaani majibu ya afya yako badala ya kuangalia wewe kwanza unampelekea third-party,
 
Kwa hiyo huyo demu alikuwa anasubiri mchumba kwa mchungaji?? nauliza ili na mimi nitumie njia hiyo
 
Tafuta chaguo lako,Hilo ni chaguo la Mchungaji,Je kama Mchungaji nae kakupiga cha uwani (Kwenye barua)..........
Mtazamo tu!
Nimehisi hivyo sijui kwanini! Kafungue mashtaka utapata ukweli ni Dr au mchungaji!?!
 
Back
Top Bottom