Popote ulipo wewe daktari, Mungu akulaani sana

Popote ulipo wewe daktari, Mungu akulaani sana

Mtoa mada ni muongo...hi ni chai isiyo na sukari kipimo Cha HIV kwa waliowahi kupimwa wanaelewa...Wala hakiendi maabara..na lazalima ufanyiwe counseling na upewe majibu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Msabato kaenda kupima kwenye hospitali inayomilikiwa na Roman Catholic kisha kaleta bandiko.

Nimeuliza mashehe na wachungaji na mapadre na maaskofu swali ; hivi pamoja na aina anuai za dini, madhehebu, masinagogi, misikiti na nyumba za ibada kwani kuna Mungu wangapi? wakanijibu Mungu ni mmoja tu.

Nikaconclude binafsi sioni haja ya kuwa na vita za kidini
Comment yako imenifikirisha Sana........ Nmepata kitu.
Nashukuru Sana mkuu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kama mwezi uliopita niliamua niende kanisani kuongea na mchungaji kumwambia nia yangu ya kuoa.

Mimi ni msabato mzuri sana. Mchungaji alinisaidia akanikutanisha na binti mmoja tuliyekuwa tunasali naye ambaye ambaye sisiti kumtaja jina lake anaitwa Winfilda Yusto Kingomile.

Mimi na huyo binti tukakubaliana kuwa wachumba kiukweli nilifurahi sana.

Sasa kama zilivyo taratibu zetu za kisabato. Mchungaji wetu akatuandikia barua ambayo tulipaswa kwenda mayo hospitali tukapime ili tujue afya zetu kwa ajili ya kujiandaa na harusi yetu.

Mimi na mchumba wangu tulienda mpaka hospitali moja ya misheni inayomilikiwa na kanisa la Roman Catholic kiukweli siwezi kuitaja jina kabisa iliyopo Tabata.

Tukamkabidhi daktari ile barua yetu tuliyotoka nayo kanisani kwetu, baada ya kuisoma daktari akatuelekeza kuelekea maabara kuchukuliwa damu kwa ajili ya vipimo.

Baada ya kama saa moja mimi nikaitwa chumba cha daktari nilipoingia cha kwanza daktari aliniuliza swali kwamba " una hela"?
Mimi nikamjibu "sina hela" huku nikiwa sijaelewa mantiki ya swali lile.

Basi daktari akaamuru na mchumba wangu aingie ndani. Alipoingia ndani daktari akatukabidhi majibu yetu yakiwa yapo kwenye bahasha na tulitakiwa tukampe mchungaji wetu kanisani bila ya kufungua bahasha hiyo.

Kwa sababu ya imani nzuri tuliyonayo ni kweli hatukufungua bahasha ile ya majibu yetu mpaka tukamkabidhi mchungaji wetu pale kanisani.

Baada ya mchungaji kusoma majibu Yale ghafla akawa mnyonge na akatuagiza tuwaite wazazi wetu waje pale kanisani. Ni kweli baada ya wazazi wetu kuja sisi tukatolewa wakabaki wazazi tu kwa mchungaji.

Baadaye wazazi wangu waliniambia kwamba majibu yanaonesha nimeathirika hivyo ndoa hakuna tena.

Kiukweli nilichanganyikiwa sana tena sana. Ila baba yangu mdogo alinishauri nikapime sehemu nyingine kwa kujiridhisha.

Nikaenda kupima Muhimbili, Amana, Mwananyamara, magomeni, Agakhan, kote huko nikaambiwa sina UKIMWI.

Nikajitosa kwenda kuchangia damu pia damu yangu ikaonekana ipo safi.

Nikarudi kumbembereza mchumba wangu na kumwambia kila kitu lakini yeye na ndugu zake hawataki kabisa kunisikia. Nikamwambia mchungaji wangu yaliyotokea naye amebaki kaduwaa tu.

MPAKA SASA SIJAJUA HUYU DAKTARI ALIKUWA ANAMAANA GANI?

ULAANIWE SANA WEWE DAKTARI.
Unamlaani daktari au mpimaji?
 
Kama ni story ya kweli nakupa pole,kitendo cha kuendelea kuficha jina la hospitali na la huyo doctor ni kuendelea kuuficha huo uchafu na uozo.
.
.
Funguka kama unataka mabadiriko ya hao wahusika

Sent using Jamii Forums mobile app
 
kama ulichoandika ni cha kweli ni muhimu kufungua mashtaka kukaa kimya ni kupoteza haki yako ya msingi na kusababisha wengine kudhulumiwa pia.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
UTATA
Nimesoma vizuri bandiko hili lakini nilichogundua ni yafuatayo
1: bado msabato anaendelea kumsakama mkatoliki
2: utaratibu wa ushauri nasaha na unasihi zimebadilika.mchungaji ndio mentor na sio examiner tena kama tulivyozoea
HITIMISHO
Hii habari ni ya uongo 100%. Bali msabato yupo kazini as usual. Ingekua ni kweli bhasi angethubutu hata kutaja hilo jina la hospitali. Bali ameweza kutaja Dhehebu tu. ROMAN CATHOLIC!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hadithi za kutungatunga hizi. Kisa wewe msabato huwapendi RC basi unaleta vijihathi vya ajabu. Tabata kuna hospitali nyingi why uende RC ambao mnawapinga kila siku.
 
Pole sana mkuu, tafuta kwingine wanawake wako wengi sana duniani.

Mwanza!!
 
Dini zinawapumbaza waafrika wengi,upumbavu wako ndio chanzo cha hayo matatizo yako.
 
Back
Top Bottom