Pombe ni dhambi, acha kuitumia

Pombe si dhambi.
Hapa duniani hakuna dhambi bali tafsiri.
Pombe ni dhambi. Dhambi ni kitu chochote chenye matokeo yanayoleta uharibifu wa akili, ufahamu na mwili kwa binadamu. Pombe inaleta uharibu wa akili, ufahamu na mwili.
 
Nuhu mtu safi mbele za Mola, alipiga maji mpaka akazima wewe ni nani mpaka useme pombe ni dhambi
 
Wanasema mwaka jana asilimia 30 ya ajali za barabarani zimesababishwa na pombe. Kwa maoni yangu hizi asilimia nyingine 70 zimesababishwa na watu wanaokunywa soda na juice
😁😁😁
 
Nuhu mtu safi mbele za Mola, alipiga maji mpaka akazima wewe ni nani mpaka useme pombe ni dhambi

Hoja yako ina makosa mawili. Kwanza, kuitwa mtu mwenye haki hakumaanishi mtu hawezi kufanya kosa. Pili, Biblia kusimulia kwamba Nuhu alilewa si sawa na kuidhinisha ulevi. Biblia yenyewe inakataza kulewa katika Waefeso 5:18. Kwa hiyo kusema ‘Nuhu alilewa, basi ulevi si dhambi’ ni sawa na kusema kila kosa lililosimuliwa kwenye Biblia limeruhusiwa jambo ambalo si kweli. Tofautisha kati ya Biblia kueleza tukio na Biblia kuamuru au kuhalalisha kitendo.
 
Harusi ya Kana maji yalibadilishwa kuwa divai au juice? Mpaka mkuu wa meza akaisifia
 
Hiyo nayo ni dhambi nyingine nawao wanahukumiwa kivyao. Katika dhambi hakuna aliye bora kuliko mwingine, wote wanatenda dhambi wamepungukiwa na utufu wa Mungu, wakisubiri ghadhabu ya Mungu.
Mungu anasemaje kuhusu raisi aliyeuwa watu hapo October 29 Kisha Leo anaimba maridhiano?
 
Pombe ni dhambi. Dhambi ni kitu chochote chenye matokeo yanayoleta uharibifu wa akili, ufahamu na mwili kwa binadamu. Pombe inaleta uharibu wa akili, ufahamu na mwili.
Ukila sana wali nyama ukawa na uzito mkuuuuubwa, then shinikizo la damu! Tutasema kuwa wali nyama ni dhambi?
 
Uzinzi, kuua ni dhambi, ila pombe inakuwa aje dhambi?
 
Ukila sana wali nyama ukawa na uzito mkuuuuubwa, then shinikizo la damu! Tutasema kuwa wali nyama ni dhambi?
Kwani kula kunaweza kuharibu uhusiano wa roho yako na Mungu. Yaani ukishiba unaweza kuona aibu mbele za Mungu? Vipi kama ukichepuka nje ya ndoa yako una kuwa na amani mbele za Mungu au unaona aibu? Tunacho zungumzia hapa ni vile vitu vinavyo haribu ufamu, akili na mwili wako kwa pamoj.
 
Hebu focus kwenye uharibifu wa akili tu, ukiweka mwili then mfano wangu hauepukiki.
 
Ni sawa na kusema chakula fulani ni haramu, mbona kinatumiwa na watu wanadunda tu. Kunyweni kwa ustaarabu bila kuzidisha. Ni kiburudisho ambaco hata Yesu alikibariki.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…