Polisi waonya mikusanyiko ya kumpokea Lissu, na maandamano ya wanafunzi

Analogia Malenga

JF-Expert Member
Feb 24, 2012
5,079
10,034
Jeshi la polisi limesema limeona baadhi ya viongozi wa CHADEMA wakihamasisha kukusanyika ili kumpokea mmoja wa kiongozi wanayetarajia kurejea nchini Julai 27, 2020.

Polisi wamesema hawana taarifa rasmi ya mikusanyiko hiyo inayohamasishwa mitandaoni. Wamesema ni haki yao kukusanyika lakini hakuna haki bila wajibu, hivyo wamewataka viongozi hao kufuata sheria.

Aidha jeshi la polisi limesema linafuatilia wanaosambaza ujumbe wa kuhamasisha wanafunzikugoma kwa kutoingia madarasani ili kushinikiza Bodi ya Mikopo kurejea masharti ya mkataba ya fedha ya kujikimu.

Polisi wamesema hawatasita kuwachukulia hatua wanaokiuka sheria, kwa kuitisha mikusanyiko na maandamano yasiyo na Baraka za kisheria, hivyo wamewataka wanafunzi wafuate njia stahiki za kufikisha malalamiko yao na sio kukiuka sheria.1595686686274.png

1595686721002.png
 
Ndio maana tunasema huko CDM hakuna weledi tena, yaani fujo za threads kwenye mitandao zimejaa, kumbe hata ruhusa hawajaomba!!
Kuna watu wanataka kuwatanguliza wenzao kichwa kichwa kwa ajili ya kupata Kiki
Kwanza kuna kuomba ruhusa kumpokea mtu? Mapokezi ya Simba na Yanga uwanja wa ndege yanakuwaga na maombi kwa polisi???

Mapokezi ya Hussein Mwinyi Zanzibar juzi waliomba ruhusa polisi?
 
Ushauri wangu polis na chadema kaeni meza moja mjadili njia atakazotumia lissu kupita, viongozi Wa chadema nendeni kwa mambosasa mjadiliane, muda, Massa yatakayotumika kumpokea lissu ili shughuli zingine ziendelee.

Kwa polis litakuwa jambo la ajabu na aibu sana kukamata RAIA au kupiga kisa kumpokea Mtu uwanja Wa ndege ambayo Ni haki yake. Chondechonde polis msitusababishie ya Zanzibar 2001 ambapo rais mstaafu mpaka anaondoka anajutia.

Hili la Chadema wakikaa mezani inawezekana.
 
Polisi wa Tanzania wanaenda kuingia kwenye rekodi chafu sana. Wasipoangalia wanaenda kuiingiza hii nchi kwenye matatizo makubwa sana.

Hakujawai kuwa na kibali cha mapokezi ya mtu hapa Tanzania kila siku tunawapokea Simba na Yanga na wala hakuna kibali chochote cha kuwapokea polisi wanahitaji
Una uhakika? Au kwakua unaona tu watu wapo mitaani na kombe. Kamati husika huwa zinaomba kibali kwa polisi na ndio Mana unaona kunakuwa na ulinzi wa polisi.
 
Kwanza kuna kuomba ruhusa kumpokea mtu??? Mapokezi ya Simba na Yanga uwanja wa ndege yanakuwaga na maombi kwa polisi???

Mapokezi ya Hussein Mwinyi Zanzibar juzi waliomba ruhusa polisi???
Ndio wameomba ruhusa! Hakuna mkusanyiko mkubwa wa watu unaoruhusiwa bila kibali cha polisi
 
Tatizo huna shule in mjinga tangu lini unapopokea mgeni uombe kibali ndio maana tunasema muende shule
Usiye soma ni we we, na Kama ulisoma basi ujinga haujakutoka kichwani! Dada nenda kampokee Lisu bila kibali cha kukusanyika then utatupa mrejesho hapa
 
Ngoja wapeleke barua usikie ramli zitakazopigwa
Sio barua tu, viongozi wakuu miongoni mwao waende kwa mambosasa wakapangane, muda utakaotumika, Massa, pia njia zitakazotumika kumpokea lissu.

Hili jambo halihitaji RAIA kuumizwa, watakuwa polis Wa ajabu sana, polis watoe muda maalumu Wa kumpokea lissu, pia wao waangalie usalama...mawaziri wetu Wa mambo ya ndani Ni mizigo wanashindwa kutoa dira kwa jeshi LA polis.
 
Back
Top Bottom