Polisi, Madaktari na Mahakama wanavyoshughulikia kesi za kubaka watoto ni wazi Tanzania ni 'banana republic'. Inasikitisha, inatia hasira na aibu

Hebu fikiria. Mtoto wako wa miaka sita anatoka shule. Akiwa njiani mjinga fulani mwenye akili mbaya kuliko mnyama anamkamata na kumvutia porini, kisha anambaka na kumuumiza sana. Mtoto huyu wa miaka sita analia kwa maumivu, lakini mbakazi anamziba mdomo na kumtishia kumuua ikiwa ataendelea kupiga kelele au kumtaja kwa watu.

Mtoto wako huyu anarudi nyumbani analia na ametapakaa damu kwenye suruali yake. Unamwangalia kwa uchungu na kugundua mtoto wako mdogo kipenzi, miaka sita tu, darasa la kwanza, amebakwa na kuumizwa sana. Unamuuliza nani amefanya hivi anakutajia ni fulani, kwa kuwa anamfahamu aliyembaka.

Unamchukua mtoto na kumpeleka polisi. Polisi wanafungua jarida la kesi, lakini wala hawakuulizi nguo alizobakwa nazo ziko wapi. Mnampeleka mtoto hospitali, daktari anaemtibu wala hafanyi jitihada za kuchukua sampuli ndani ya mtoto na kuzihifadhi ili waje wafanye DNA test.

Kesi inapoenda mahakamani, mbakaji anafungwa kwa ushahidi wa kutambuliwa na mtoto. Lakini baadaye, jaji mtukuka wa mahakama ya rufaa anasema mbakaji aachiliwe huru kwa kuwa wakati wa kesi ile suruali yenye damu aliyokuwa amevaa mtoto haikuletwa mahakamani kama ushahidi. Mbakaji yuko huru.

Fikiria kama huyo mtoto wa miaka sita ni wa kwako, waangalie watoto wako, au watoto wa ndugu yako wa karibu, halafu piga picha wao ndio wamefanyiwa hivyo. Unajisikiaje?

Hii sio hadithi, ni tukio la kweli. Hawa ndio polisi wetu. Hawa ndio madaktari wetu. Hawa ndio majaji wetu. Hodari na makini sana katika kufuatilia kesi za siasa na kufunga watu kwa kesi za kubambikiwa, lakini sio kesi za watoto wa miaka sita kubakwa na kuumizwa.

Sasa niambie kama nikisema nchi yetu Tanzania ni banana republic, una sababu gani za kunibishia?

Reference: Suruali yenye damu ilivyotengua hukumu
kwa vile mahakama imemuachia. cha kufanya hapo unachukua bisu unamchinja.. unaondoka zako unahamia malawi.
 
Umenitonesha kidonda kilicho moyoni mwangu na mada yako.Chozi limenitoka hakika!Nitarudi baadaye
 
Wakifanya unavotaka wewe tutafungwa wengi kwa chuki tu za wabaya wetu mitaani
 
Daktari alipopelekewa mtoto wa kubakwa, yeye ndiye alitakiwa kufanywa swabs za sehemu za siri za mtoto na kuzihifadhi kama sample ambazo zinaweza kufanyiwa uchunguzi wa DNA. Kumbuka kwamba hata kama mtoto aliogeshwa, ndani ya mwili wake bado angekuwa na vitu kama shahawa za mbakaji. Madaktari wanaelewa utaratibu huu, sasa huyu kwa nini hakufanya?

Wote tunajadili kesi ambayo hatujui mazingira halisi ya huyu daktari. Je kesi ilipelekwa kwa daktari wa daraja lipi na ngazi gani?

Hospitali zinazokiosa urine na stool container ndo iwe na swab?
Kuna mengi yanatakiwa kufanywa mpaka vipimo kama:
1: hepatitis
2: syphilis
3: HIV
4: ujauzito /kwa wale wenye umri husika
5: nyoa nywele na zitunzwe.
6: chukua picha pia za ushahidi

Hii ni kazi si chini ya saa 1-2, hii inahitaji uelewa, motivation ya mazingira ya kazi, dedication etc
 
Inaumiza Sana ,,mzazi kwa Nini hakupeleka hiyo suruali iliyotapakaa ndamu Kama ushahidi huko polisi na mahakamani??
 
Mkuu, unajua uzito wa ushahidi wa mtoto katika kesi? Katika kesi hii inawezekana kusiwe na collaborating evidence, lakini haiondoi uzito wa ushahidi wa mtoto. Hivyo jaji alitakiwa aangalie sana upande huu.

Mtoto wa miaka sita ukimwambia akadanganye ni fulani kambaka, ukimfanyia cross examination ya juu kutumia mtaalamu wa saikolojia, ataishia kusema baba alisema nimtaje fulani. Jaji anajua kabisa kwamba kama mtoto alisema ni fulani kanibaka uwezekano wa kuwa si kweli ni o.o1%, kwa hiyo hakupaswa kusimamia rufaa kwenye suruali, bali alipaswa kusimamia kwenye ukweli wa aliyosema mtoto.

Kama rufaa ingejenga shaka juu ya ushahidi wa mtoto hapo ningekubaliana na jaji. La sivyo huyu lazima ni jaji kihiyo tu, wale majaji wa Magufuli labda.

Jamhuri inatakiwa kukata rufaa ili hukumu ya huyu jaji mpuuzi itupiliwe mbali.
Wakati wanapanga kukata hiyo rufaa huyo mfungwa siatakuwa Kwanza kashaachiwa huru
 
Mimi sidhani kama tutapelekana polisi, shingo ya mbakaji itakuwa halali bora nifungwe kwa mauaji.

Inaumiza sana.
Mimi nampeleka mtoto wangu hospital mbakaji nampa miezi miwili tu ya kuvuta pumzi ya bure hapa duniani kisha namrudisha mavumbini bila kuacha alama yoyote kisha maisha yanaendelea
 
Inaumiza Sana ,,mzazi kwa Nini hakupeleka hiyo suruali iliyotapakaa ndamu Kama ushahidi huko polisi na mahakamani??
MKuu, kukusanya ushahidi ni kazi ya polisi, sio mzazi. Mzazi anatakiwa kuongozwa na Polisi kujua cha kufanya
 
Mkuu hisia hazijengi hukumu ingawa zinaletwa kwa kutengenezwa case theory kama hii yako.

Ila waza pia kama huyo anayeitwa mbakaji akawa si mbakaji alisia itakuwaje?
Mkuu, thread ipo ndani ya ushahidi uliotolewa, sio kukisia nini kilitokea
 
Kwanini ujisumbue kupeleka kesi mahakamani..wakati Kuna wahuni ukiwapa laki 5 wanamkata mbakaji kiungo chochote utakachotaka wanakuletea..ukitaka korodani zake,mkono,mguu hata macho wanayatoboa ukitaka
 
Utakaa mahabusu kwa miaka 3-5 afu utashinda kesi!! Kama ukifanya hivyo
 
Mkuu, unajua uzito wa ushahidi wa mtoto katika kesi? Katika kesi hii inawezekana kusiwe na collaborating evidence, lakini haiondoi uzito wa ushahidi wa mtoto. Hivyo jaji alitakiwa aangalie sana upande huu.

Mtoto wa miaka sita ukimwambia akadanganye ni fulani kambaka, ukimfanyia cross examination ya juu kutumia mtaalamu wa saikolojia, ataishia kusema baba alisema nimtaje fulani. Jaji anajua kabisa kwamba kama mtoto alisema ni fulani kanibaka uwezekano wa kuwa si kweli ni o.o1%, kwa hiyo hakupaswa kusimamia rufaa kwenye suruali, bali alipaswa kusimamia kwenye ukweli wa aliyosema mtoto.

Kama rufaa ingejenga shaka juu ya ushahidi wa mtoto hapo ningekubaliana na jaji. La sivyo huyu lazima ni jaji kihiyo tu, wale majaji wa Magufuli labda.

Jamhuri inatakiwa kukata rufaa ili hukumu ya huyu jaji mpuuzi itupiliwe mbali.
Unajua sheria za ushahidi mkuu ?
 
Najua uzito wa ushahidi wa mtoto; katika sheria watoto ni malaika
Kisheria ushahidi wa mtoto unahitaji kuongezewa nguvu na ushahidi wa ziada hata kama utakuwa na mashahidi mia tano ambao ni watoto kama huna ushahidi wa ziada utakuwa unapoteza muda tu except in special circumstances
 
Back
Top Bottom