Polisi, Madaktari na Mahakama wanavyoshughulikia kesi za kubaka watoto ni wazi Tanzania ni 'banana republic'. Inasikitisha, inatia hasira na aibu

MKuu, kukusanya ushahidi ni kazi ya polisi, sio mzazi. Mzazi anatakiwa kuongozwa na Polisi kujua cha kufanya
Lakini office ya DPP si ndiyo inatowa maelekezo ya Upelelezi kwa police Kama kuna mapungufu yarekebishwe ndiyo kesi ipelekwe Mahakamani!? Kwa hiyo hapa aliefeli ni DPP!!
 
Kuna kitengo cha Polisi cha Forensic Investigations hapa Dar es Salaam, tena kinaongozwa na injinia. Wanafanya nini?
Hebu fikiria. Mtoto wako wa miaka sita anatoka shule. Akiwa njiani mjinga fulani mwenye akili mbaya kuliko mnyama anamkamata na kumvutia porini, kisha anambaka na kumuumiza sana. Mtoto huyu wa miaka sita analia kwa maumivu, lakini mbakazi anamziba mdomo na kumtishia kumuua ikiwa ataendelea kupiga kelele au kumtaja kwa watu.

Mtoto wako huyu anarudi nyumbani analia na ametapakaa damu kwenye suruali yake. Unamwangalia kwa uchungu na kugundua mtoto wako mdogo kipenzi, miaka sita tu, darasa la kwanza, amebakwa na kuumizwa sana. Unamuuliza nani amefanya hivi anakutajia ni fulani, kwa kuwa anamfahamu aliyembaka.

Unamchukua mtoto na kumpeleka polisi. Polisi wanafungua jarida la kesi, lakini wala hawakuulizi nguo alizobakwa nazo ziko wapi. Mnampeleka mtoto hospitali, daktari anaemtibu wala hafanyi jitihada za kuchukua sampuli ndani ya mtoto na kuzihifadhi ili waje wafanye DNA test.

Kesi inapoenda mahakamani, mbakaji anafungwa kwa ushahidi wa kutambuliwa na mtoto. Lakini baadaye, jaji mtukuka wa mahakama ya rufaa anasema mbakaji aachiliwe huru kwa kuwa wakati wa kesi ile suruali yenye damu aliyokuwa amevaa mtoto haikuletwa mahakamani kama ushahidi. Mbakaji yuko huru.

Fikiria kama huyo mtoto wa miaka sita ni wa kwako, waangalie watoto wako, au watoto wa ndugu yako wa karibu, halafu piga picha wao ndio wamefanyiwa hivyo. Unajisikiaje?

Hii sio hadithi, ni tukio la kweli. Hawa ndio polisi wetu. Hawa ndio madaktari wetu. Hawa ndio majaji wetu. Hodari na makini sana katika kufuatilia kesi za siasa na kufunga watu kwa kesi za kubambikiwa, lakini sio kesi za watoto wa miaka sita kubakwa na kuumizwa.

Sasa niambie kama nikisema nchi yetu Tanzania ni banana republic, una sababu gani za kunibishia?

Reference: Suruali yenye damu ilivyotengua hukumu
Inauma sana
 
Mtoto wa mdogo wangu wa kike miaka 8,darasa la pili amebakwa majuzi tu na mbaba ambaye mdogo wangu wa 1978 ni mdogo kwa huyo baba!Alafu ametolewa kwa dhamana!Hii imetokea mombasa maana mdogo wangu ameolewa huko!Nimeumia saaana sana sana
 
Sitamuua mbakaji lakini nitafanya kitu ambacho jamii ma mbakaji hatasahau
 
Mtoto wa mdogo wangu wa kike miaka 8,darasa la pili amebakwa majuzi tu na mbaba ambaye mdogo wangu wa 1978 ni mdogo kwa huyo baba!Alafu ametolewa kwa dhamana!Hii imetokea mombasa maana mdogo wangu ameolewa huko!Nimeumia saaana sana sana
Kesi si inaendelea?dhamana isikutishe
 
Hapo ni Mungu tu asaidie. Binafsi Kwa hii scenario ningeshitakiwa Mimi Kwa Mauaji..
 
Mtoto wa mdogo wangu wa kike miaka 8,darasa la pili amebakwa majuzi tu na mbaba ambaye mdogo wangu wa 1978 ni mdogo kwa huyo baba!Alafu ametolewa kwa dhamana!Hii imetokea mombasa maana mdogo wangu ameolewa huko!Nimeumia saaana sana sana
POle sana Mkuu. Natumaini huyo jamaa atahukumiwa inavyostahili, japo haitaondoa maumivy ya mtoto wa mdogo wako na nyie wanafamilia
 
Achana na mambo ya Polisi Wala mahakamani.Huyo unamuua kimya kimya kwa siri kuu hata mkeo usimwambie.Ukishindwa Kodi watu wafanye kazi hiyo .
 
Back
Top Bottom