Polisi Moshi wamekataa kupeleka kesi hii mahakamani na wanasisitiza dhamana iwe hapo kituoni

Mwanatheologia

New Member
Oct 20, 2019
4
5
Mimi ni mfanyakazi katika taasisi ya Kikristo iliyoko Moshi. Taasisi hii Ina shule ya Msingi na ya Secondari.

Taasisi hii pamoja na kuwa na watoto wanaotoka kwenye familia za kawaida shuleni, pia huwasaidia watoto walioko kwenye mazingira magumu pia yatima na waliotelekezwa. Mwanafunzi mmoja wa form two katika shule hii amekuwa akishawishiwa na vijana wanaojohisisha na wizi walioko jirani na eneo la shule.

Pikipiki iliibiwa shuleni na baadae kupatikana kwa mmoja wa vijana jirani Hawa.

Aliyekamatwa na Pikipiki akamtaja mwanafunzi wa kidato cha pili kwamba ndiye aliyemuuzia. Wote wakikamatwa na kupelekwa POLISI Moshi.

Mwanafunzi ana umri chini ya miaka 18 kwa hiyo tulomba kesi iende mahakamani Ili tumdhamini mwanafunzi na tuweze kuwapata wale watuhumiwa wengine.

Tulijua mazingira ya kituo cha Moshi kati yamejaa rushwa na ukosefu wa uadilifu. Waliruhusu dhamana (ambayo ni haki ya kila mtu) kwa mtuhumiwa na kutaka mwanafunzi naye adhaminiwe hapo kituoni. Kwa kuwa tulijua kuwa kwa Sheria mwanafunzi hawezi kuendelea kukaa hapo zaidi ya masaa 48 tuliomba tumdhamini mahakamani.

Kwa kujua wale watuhumiwa walikuwa wametoa rushwa tuliomba wapeleke kesi mahakamani Ili mwanafunzi tumdhamini mahakamani.

Tulimshirikisha kiongozi wetu. (Mtu anayeheshimika katika jamii na mwanafunzi huyu anamchukulia kama baba) alifika kituoni na akakubaliana na mawazo yetu ya kuomba kesi ipelekwe mahakamani Ili amdhamini mwanafunzi huyu huko.

Kuanzia tarehe 29 January hadi leo POLISI MOSHI wamekataa kupeleka kesi mahakamani na wanasisitiza dhamani iwe hapo kituoni.

Kwa kuwa tunajua nia yao na sisi tumebakia na msimamo wetu. Kiongozi wetu akajitahidi kuwasiliana na ngazi mbalimbali za uongozi lakini bado hadi leo February 10 mwanafunzi yuko rumande kituoni na kesi haijapelekwa mahakamani na hawaonyeshi nia ya kuipeleka.

Walipoona kiongozi wetu (Askofu) amekubaliana na wazo letu wameenda kujaribu kumchonganisha na mwanafunzi na kumwambia baba amekukataa. POLISI sasa wanampigia mke wa Askofu kumwambia yeye akamdhamini mtoto.

Lakini naye ameomba akamdhamini pale mahakamani Ili tuwapate wanaomshawishi mwanafunzi huyu
Wanasheria na watetezi wa haki tusaidieni. Kiongozi wetu amesafiri kumpeleka mkewe Hospital nje ya Kilimanjaro na Sasa anaanza kuona labda tumdhamini tu Ili mwanafunzi asiendelee kuteseka.

Sisi tumemuomba atuachie Ili POLISI na watuhumiwa tutafute namna ya kuwafikisha kwenye mkono wa Sheria
 
Kuna polisi hapo mtu wa singida, ana nyota mbili au Moja. Ni mpokea rushwa 100%, amekaa kituo hapo tangu akiwa koplo hadi Sasa na manyota.
Ni mweupe mnene .
Amedumu Moshi mjini kama polisi miaka 27.
 
Back
Top Bottom